Gerrardgerry
Member
- Oct 2, 2024
- 30
- 15
Umetisha singano mpk linii tenaa????
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukran sana mkuu. Tutashukuru kwa mwendelezo zaidiSHETANI RDISHA AKILI ZETU MTUNZI:SINGANOJR.
SEHEMU YA 180.
Barua kutoka kwa Yonesi
Ni gari aina ya pickup iliochakaa , ilionekana ikipita maeneo ya Kiwangwa-Msata kwa spidi kubwa. Dereva wa pickup hio alikuwa ni mwanaume alievalia jacketi lenye kofia pamoja na kepu kichwani na kumfanya asionekane sura yake moja kwa moja.
Pembeni ya dereva huyo alikuwepo mwanamke alievalia nguo nyeusi huku nywele zake zilikuwa zimechanguka.
“Master tunaondoka kweli?”Aliuliza yule mwanamke kwa sauti ya kuonekana hakuridhishwa na safari hio.
“Kwahio hutaki kuondoka . Upo t tayari kupoteza maisha?”Aliuliza yule mwanaume katika sauti iliojaa usiriasi.
“Lakini….”
“Hakuna cha lakini. Mpango wangu haujafeli kabisa , hivyo ni swala la muda tu nitarudi tena”Aliongea yule mwanaume.
Lakini muda ule alijikuta akikanyaga breki ghafla mara baada ya kuona kivuli cheusi kinachotoa miale ya mwanga wa bluu kikishuka kutoka juu angani na kutua mbele ya barabara.
Dereva yule haraka sana baada ya kukanyaga breki aliongeza mwangaza wa taa za gari na ndipo alipoweza kuona kivuli kile kilikuwa ni cha mtu na miale ile ni kutoka kwenye Suti ya chuma aliovaa mwilini mwake na kumfanya aonekane kama roboti.
Dereva wa gari ile haraka sana na kwa wasiwasi mkubwa alishuka kutoka kwenye gari.
“Wewe ni nani?”Aliuliza kwa sauti ya juu.
“It is not important who I am, what is important is…We have a common purpose and a common goal.”Aliongea kwa kingereza akimaanisha kwamba sio muhimu kumfahamu yeye ni nani lakini swala muhimu ni kwamba wote pamoja wana malengo na makusudio yanayofanana.
“Una maanisha nini… Acha kuongea kwa mafumbo”Aliuliza na kumfanya lile Damisi kucheka.
“Haha... You don't even know what kind of existence the enemy you face is. You can't win against that man.”(Haha.. Hata hujui ni adui wa aina gani una pambana nae . Huwezi kumshinda yule mtu).
“Unamjua adui yangu ni nani?”Aliuliza.
“Bila shaka namjua, nakujua pia na wewe na ukiburi wako na kutokuwa tayari kukubali kushindwa , lakini naona upo katika hali ya kukata tamaa kwasababu ya kukosa uwezo na pesa, matokeo yake umegeuka na kuwa panya wa mtaa na hakuna ambae yupo tayari kukusaidia na hakuna ambae atakuamini , huna unapoweza kwenda zaidi ya kukisubiria kifo chako pekee”Aliongea yule Damisi kwa sauti ya uchokozi kabisa.
“Kama unajua hilo kwanini umekuja kunitafuta?”
“Ni rahisi sana , nimependezwa na kipaji chako na nipo tayari kukusaidia kulipiza kisasi na kuondoka Tanzania”
“Vipi kama sitaki na zaidi kwanini niamini unao uwezo wa kufanya hivyo?”Aliuliza yule bwana katika sauti yenye hisia ambazo hazikusomeka.
“Hutakiwi kuuliza maswali , unapaswa kuchagua tu”Aliongea yule Damisi na kumfanya yule bwana kusaga meno yake kwa sekunde kadhaa
“Nimekubali, niambie unataka nifanye nini?”Aliongea na kufanya yule Damisi kuanza kutoa cheko kubwa lililosababisha sauti ya kuumiza masikio kama maiki mbovu katikati ya kichaka hicho.
*****
Ni ndani ya moja ya ghala la kuhifadhia nondo, alionekana Tresha Noah, akiwa ameshikilia kishikwambi na kupangusa taratibu taratibu na kutoa tbasamu ambalo lilijaa kejeli .
Mbele yake kulikuwa na wanaume kama kumi hivi waliojazia misuli kwenye mikono na kulikuwa na mwanaume ambae alikuwa amefungwa na kamba zito akiwa amekalishwa kwenye kiti.
“Ndaro, kazi nzuri”Aliongea Tresha na bwana ambae alikuwa karibu yake aliishia kutingisha kichwa akipokea sifa hizo kutoka kwa bosi wake.
Muda huo simu ya Tresha ilianza kuita na alitoa ishara itolewe kwenye mkoba wake apatiwe huku akimpatia Ndaro kile kishikwambi.
“Dastani umeziona picha?”Aliongea Tresha mara tu baada ya kupokea simu ile.
“Nimeziona , ila bado sijapata maana yake kamili. Ulikuwa ukimfuatilia Amosi kimya kimya?”
“Unakumbuka uliniambia kwamba nilihusika kumteka Amosi mara baada ya kupotea?. Siku chache zilizopita niliweza kuonana na Carlos” “Unamaanisha Carlos muuaji wa BINAMU!”
“Ndio, Nilitaka kuthibitisha sababu ya Amosi juu ya kutekwa na nilimhoji Carlos na aliniambia hakufanya hivyo na hakuagiza mtu yoyote kuhusika na Amosi”
“Tresha kwanini hukuniambia kuhusu hilo?”
“Amosi alikwambia alitekwa na akakurushia mzigo wewe kwasababu ya picha zetu za pamoja , sikuwahi kupenda kila tunachofanya kinamfikia ndio maana niliamua kufanya uchunguzi wa kimya kimya kwa kumuwekewa watu kumfuatilia”
“Kwahio unataka kusema nini juu ya hizi picha ulizonitumia?”
“Huyo mwanaume anaonekana kukutana na
Amosi unamfahamu fika ni Jasusi wa Kanisa la
Wabrazili ,Ajent Alonzo. Unadhani kwanini Amosi akutane na Alonzo?”
“Kuna sababu mbili zinawezekana , Amosi ni Liason Agent wa Malibu na TISA , pengine yupo kwenye misheni .Pili inawezekana kutekwa kwake kuna uhusiano na kukutana na Alonzo?”Aliongea Kanali.
“Hio ni kazi yako Dastani kupata majibu , unashirikiana na Amosi kwasababu unaamini anafanya kazi ya Serikali , lakini vipi kama ni zaidi ya unavyomfahamu? Maana yake kazi zetu zote tunazofanya zinavuja na hiki ni kikwazo cha mpango wetu”Aliongea Dina
“Kuhusu hilo nitalifanyia kazi?”
“Vipi kuhusu faili la Mshua, umepiga hatua?”.
“Kuna mpango nimeusuka na unaanza kufanya kazi , nafanya ufuatiliaji kwasasa, nitajua kama nimepiga hatua au lah baada ya matokeo”Aliongea Dastani.
“Unapaswa kuharakisha hilo. Alex yupo kwenye mikono yangu na nina uhakika mpaka sasa hivi pengine watu wa BINAMU washapata taarifa”Aliongea Tresha huku akiangalia mbele yake kumchunguza mwanaume ambae alionekana kufungwa kwenye kiti akiwa hana fahamu.
“Tresha unafanya makosa makubwa sana na yanaweza kunifikia na mimi. Nadhani hujapata
taarifa ila Alex ni moja kati ya watu wanaochunguzwa juu ya kifo cha Dokta Frida Franklin wa taasisi ya Haliz”Aliongea na kumfanya Tresha macho yake kucheza.
“Frida Franklin! Nakumbuka nishawahi kusikia jina lake mahali”Aliongea Tresha huku akionekana kuvuta kumbukumbu.
“Ndio mwanasayansi aliegundua teknolojia ya Kurekodi ndoto katika mjongeo wa picha . Taarifa ya mafanikio yake imetoka juzi baada ya kukutwa nyumbani kwake akiwa hana uhai. Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na kati ya watu ambao walionekana kuwa na ukaribu na Dokta Frida mmoja wapo ni Alex, kwa taarifa nilizokuwa nazo uelekeo wa kesi upo upande mwingine lakini ni swala la muda tu na Alex atafikiwa na kuhojiwa”Aliongea Kanali na kumfanya Tresha kufikiria kidogo.
“Ninachotaka kutoka kwa Alex ni taarifa juu ya biashara yake ya vyungu , akileta ushirikiano nitamuacha hai , ila akileta ubishi sina namna zaidi ya kumuua”
“Tresha acha kukurupuka. Usije kuthubutu kumuua Alex , Kumteka ni kosa la kwanza lakini kumuua ni kosa lingine na moja kwa moja utajenga uhasama na watu wa Binamu”Aliongea kanali akionekana katika hali ya kupaniki.
“Najua ninachokifanya Dastani”Aliongea Tresha na kisha palepale alikata simu na kuikabidhi kwa mabaunsa na kuzipita hatua kumsogelea Alex.
“Mwamsheni!”Aliongea kwa sauti na palepale mmoja ya watu wale alichukua kindoo cha maji na kumwagia Alex ambae alishituka palepale.
“Alex!”Aliita Tresha.
*****
Hamza alikuwa bize kuwaza namna ya kumpata Saidi na hakuweza hata kupata muda wa kuelezea kinachoendelea kwa wanawake wake wengine hususani Eliza ambae alikuwa hotelini baada ya nyumba yake kuungua.
Baada ya kutoka kwa Yulia alikuwa amefanikisha kuingia dili na mrembo huyo kumuazima jumba moja ambalo lilikuwa karibu zaidi na mtaa wa Egret Kigamboni.
Nia yake kufanya hivyo ni kutaka kumuweka Eliza karibu na Regina ili iwe rahisi kuwalinda lakini vilevile asisafiri umbali mrefu kufuata Kitumbua.
Familia ya Yulia ilikuwa na nyumba nyingi karibia jiji zima na wala hakujali Hamza kuchukua nyumba yake na hata hakumuuliza anataka ya nini zaidi ya kumpatia , huku yeye akiwa bize kuangalia taarifa za tafiti za Saidi ambazo Hamza alifika nazo.
Hamza alienda hotelini na kumchukua Eliza na kwenda kumuonyesha makazi hayo mpya , Ijapokuwa Eliza alishangaa kutokana na kuwa na nyumba iliokuwa chini ya Kampuni lakini mara baada ya Hamza kumwelezea sababu alijikuta akikubali kwa furaha lakini kwa wasiwasi pia baada ya kuona kile ambacho kinaendelea.
Mara baada ya kumalizana na swala la Eliza Hamza alirudi nyumbani , Ingawa ilikuwa ni asubuhi tayari lakini taa za nje na ukumbini badi zilikuwa zinawaka.
Regina na Shangazi walikuwa sebuleni wamekaa na kulikuwa na mwanamke wa kizungu aliekuwa amesimama pembeni , alikuwa amevalia suruali nyeusi ya ngozi, alikuwa mrefu mno mwenye mwili uliojengeka na nywele zake zilikuwa nyeusi.
Mara baada ya kumuona Hamza amerudi Regina na Shangazi walisimama. Yule mwanamke wa kizungu mara baada ya kumuona Hamza mwonekano wake ulibadilika mara moja na palepale alipiga goti kutoa heshima lakini Hamza alimpa ishara ya kumzuia.
Yule mwanamke alishangaa lakini alielewa nini ambacho Hamza anamaanisha na palepale alisimama.
Lakini sasa kitendo chake hicho kilionekana kumuogopesha Regina mno hasa namna ya tembea yake ilivyokuwa nyepesi kiasi kwamba ilikuwa ngumu kwa Regina na Shangazi kuizoea.
“Hamza nini kimetokea? Imekuwaje Saidi akarudi kuwa hai?”Aliuliza Regina.
“Ni stori ndefu , Crow umejitahidi sana leo unaweza kwenda sasa”Aliongea Hamza kwa kingereza.
“Its my honor”Alijiibu yule mzungu na palepale aligeuka na kuwa kivuli na kupotelea nje na haikujulikana alikuwa amepitia dirishani , mlango wa nyuma au wa mbele.
“Hii mbinu ya mafunzo ya nishati sijawahi kuiona , Inaitwaje?”Aliuliza Shangazi na kumfanya Hamza kutingisha mabega kukataa.
“Hayo sio mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
Ni uwezo wa asili kwa kila Strigoi”Aliongea Hamza.
“Strigoi?!” Regina alijikuta akibung’aa, “Kwahio
unamaanisha huyu mwanadada ni
Vampire?”Aliuliza Regina kwa mshangao mkubwa. “Strigoi hawapendi kuitwa Vampire ni kama ilivyo kwa watu weusi wasivyopenda kuitwa Nigga, ni vizuri ukajizuia kuongea hilo neno kirahisi rahisi , isitoshe nina marafiki wengi kutoka Strigoi”Aliongea Hamza huku akicheka.
“Hamza umetushangaza mno , umewezaje kuwafanya Strigoi kufanya kazi chini yako?”Aliuliza Shangazi kwa mshangao mkubwa na Hamza alimimina chai kwanza kwenye kikombe na kisha akakaa chini na kuwapa ishara na wao kukaa waongee.
“Kwanza kabisa Crow na wenzake sio watu wangu, wanafanya kazi chini ya rafiki yangu , pili hawa Strigoi ni wa damu mchanganyiko nikimaanisha wana damu ya ubinadamu, hivyo hawawezi kuitwa Vampire kamili”Aliongea Hamza.
“Ndio maana ametoka nje bila ya kuwa na wasiwasi wa mwanga wa jua na pili ana kivuli”Aliongea Regina akiwa hana hofu bali alionekana kuvutiwa sana na utambuzi huo. “Unaonekana umeangalia sana filamu za Vampire si ndio? Hawa Strigoi wana nguvu kubwa kuliko binadamu , kama jua lingekuwa na madhara kwao wangekwisha kupotea , Kusema jua lina madhara kwao ni ishara feki tu kuwapumbaza binadamu kuamini kama wanao uwezo wa kuwamaliza . Watu pekee ambao wanaweza kuwazidi nguvu hawa Strigoi ukiachana na nguvu ya ukuu ni watu wa Baraza Takatifu.Wamekuwa wakipambana na jamii ya hawa viumbe wanywa damu kwa miaka mingi sana , wakitegemea Nuru yenye uwezo wa kuwazuru”Aliongea Hamza.
“Baraza takatifu! Unamaanisha nini au unazungumzuia watu wa dini?”Aliuliza Regina katika hali ya mshangao na kuchanganyikiwa.
“Baraza takatifu haihusiani kabisa na mambo ya Holy See ama Imani za kidini , kuhusu hili Wife inabidi nitafute mtu wa ulimwengu wa chini akutafutie baadhi ya taarifa uweze kujionea mwenyewe maana ni ngumu kukuelezea hapa hapa na ukaelewa mara moja , kwasasa nitaongea kuhusu Saidi”Aliongea Hamza na kisha palepale alianza kuwaambia kuhusu matukio ya Saidi m huku akiacha kumtaja Yulia kabisa . Isitoshe uhusika kamili wa Yulia ni siri ya taifa.
Regina mara baada ya kusikia kuhusu habari hio sura ilijikumja huku akiwa katika mwonekano usiokuwa ukielzeka.
“Wife usiwe na wasiwasi kabisa , mimi nikiwepo sitomruhusu akuguse”Aliongea Hamza akimfariji Regina ambae alikuwa na wasiwasi.
“Ni kweli Regina, Hamza ni muwajibikaji na makini sana. Ndio maana Madam alionekana kumthamini sana kabla ya kuondoka , inaonekana alimkadiria vyema”
Aliongea Shangazi , akishindwa kujizuia kuhusu wasifu halisi wa Hamza na ilionekana Bibi yake Regina alionekana kufahamu mara baada tu ya kumwona.
“Mimi sina wasiwasi kuhusu Saidi , wasiwasi wangu ni kuhusu Lamla , anaonekana kutia huruma mno”Aliongea Regina na kauli yake ilimshangaza Hamza.
“Wife usiniambie unamuonea huruma Lamla! Ndie mtu aliesababisha kifo cha baba yako”
“Ni kweli lakini kama ni adhabu amekwisha ipata tayari, tuliwahi kuwa ndugu kwa zaidi ya miaka kumi na najua anachopitia anastahili lakini .. kumuacha katika hali aliokuwa nayo nahisi sio..”
“Regina una moyo mwepesi mno , Lamla ni ngumu kubadilika. Moyo wake umejaa uovu tayari na ukimtendea wema ataishia kukulipa mabaya, ni sawa tu na kufuga nyoka”Aliongea Shangazi
akijitahidi kumpoza Regina aachane na anachowaza
.
Regina alionekana kuwa katika hali ya hisia mchanganyiko na alikosa maamuzi ya moja kwa moja na aliishia kumwangalia Hamza.
“Niambie wewe , unadhani ni vizuri kuachana nae?”Aliuliza na Hamza aliishia kuhema kwa nguvu huku akishindwa kujiuliza kwanini Regina ana mawazo ya namna hio isitoshe hakuwa na undugu wowote na Lamla licha ya kuishi pamoja. Kuhusu Lamla kuteseka ni sahihi kusema adhabu aliopata inamtosha na ni kawaida kwa Regina hasira yake kupotea.
“Wife maamuzi yoyote utakayofanya mimi nitakusapoti”Aliongea Hamza, huku akiamini kwa hali aliokuwa nayo Lamla hawezi kuleta shida mbeleni.
“Basi naomba unisaidie niweze kumpata”Aliongea Regina.
“Sasa hivi?”
“Haiwezekani?”
Hamza alijikuta akishindwa hata kujibu , hakudhania Regina angekuwa siriasi sana na jambo hilo.
“Hakuna shida , itakuwa hajaondoka mahali nilipomuacha , ngoja niongee na mtu anisaidie kumtafuta na kumleta”Aliongea Hamza.
Mtu ambae Hamza alitaka kumuomba msaada ni Dina , mtu mdhaifu tu kama Lamla hakuhitaji msaada wa Yulia au wa Strigoi.
Hamza hakuficha chochote na alimpigia Dina mbele ya Regina na alidhania simu yake ingechelewa kupokelewa kutokana na mwanamke huyo kuchelewa kuamka lakini alipokea sekunde hio hio.
Dina hakujua kidogo tu ashambuliwe na roboti la Saidi , hivyo hakujua chochote kinachoendelea kuhusu Saidi.
“Hamza kuna tatizo , mbona asubuhi asubuhi?”Aliuliza Dina kivivu.
“Mbona kushakucha , inamaana mpaka sasa umelala?”
“Nilichelewa kulala , jana nilikuwa na kikao kilichoisha usiku wa manane, ndio najiandaa kulala”Aliongea Dina.
“Nimekupigia kwasababu nahitaji msaada wako , nataka unisaidie kumtafuta Lamla , aliekuwa Mama wa kambo kwa mke wangu”Aliongea Hamza.
“Kwani si alikwisha fariki?”
“Yupo hai”
“Kwahio unataka nidili nae baada ya kumpata au?”
“Hapana nataka tu umtafute . nilimuacha jana maeneo ya Mapinga , waambie vijana wako waanzie hapo”Aliongea Hamza.
Ingawa Dina aliona maelekezo ya Hamza sio ya kawaida kutokana na historia ya Lamla na Regina lakini hakuuliza sana.
“Vipi lakini upo free asubuhi hii tukutane? Kuna kitu nataka tuongee”Aliongea Dina.
“Sawa nitakuja muda si mrefu”Alijibu Hamza na kisha alikata simu.
Baada ya kukata simu Hamza alimwambia Regina watu wa Dina wangesaidia kujua alipo Lamla.
Upande wa Regina hakuwa mjinga , kwa muda mfupi alioishi pamoja na Hamza asingeshindwa kujua kuhusu mahusiano yake na Dina.
“Sawa wakimpata waniambie nitawashukuru kwa kazi yao”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutabasamu.
“Nilijua tu mke wangu wewe ni mwelewa. Ukweli nilipanga kukuambia kwanza mimi na Dina tunafahamiana kwa muda mrefu sana”Aliongea Regina.Ilikuwa ni ngumu kwa Regina kutokumfahamu Dina hasa kwa mfanyabiashara kama yeye ambae kwake taarifa ni mtaji.
Regina asingechukia Hamza kuwa na ukaribu na Dina kutokana na kwamba walianza kufahamiana kabla na hata namna ambavyo yeye na Hamza walikutana ilikuwa ni kwa kazi ambayo iligeuka na kuwa mahusiano. Mtu ambae Regina hakutaka Hamza kuwa nae karibu ni Yulia pekee.
“Acha kunisifia , nimekubali msaada kutoka kwake kwasababu namtegemea kunisaidia kumpata Lamla”Aliongea Regina akiwa siriasi.
Hamza hata hivyo hakujali sana , alipanga kwenda taratibu sana na Regina kumwandaa kisaikolojia ili ikitokea akiwa nao wote kusitokee ugomvi.
Regina alikuwa amechoka na hakuwa na mpango wa kutoka nyumbani siku hio , baada ya kuona Hamza amerudi akiwa salama alipanga kwenda kupumzika ila hakusahau kumwagiza amtafutie taarifa zinazohusiana na ulimwengu wa siri ili na yeye ajifunze, alikuwa na shauku ya kutaka kujua mambo yaliokuwa yakiendelea gizani.
Upande wa Hamza alienda chumbani kwake na kuoga kwanza kisha ajiandae kwa safari ya kwenda kumsalimia Dina, lakini sasa ile anamaliza tu kuoga na kuvaa nguo safi simu yake ilianza kuita na alipoangalia anaepiga alikuwa ni Sally.
“Sally kuna tatizo?”Aliuliza Hamza akiwa katika hali ya mshangao .
“Sir, Linksi aliekuwa akimchunguza Serena amekufa”Aliongea Sally huku akionekana kama vile alikuwa akishindana na hisia zake za hasira.
Hamza mara baada ya kusikia taarifa hio macho yake yalichanua kwa mshangao.
“Nitaenda kuangalia , usikurupuke”Aliongea Hamza. Alijua vyema watu hao walikuwa wakithaminiwa mno na Sally . Ijapokuwa walikuwa kama wanamfanyia kazi lakini mahusiano yao yalikuwa ni kama yale ya undugu.
Hivyo yoyote akifa ni lazima Sally kukasirika mno na mwanamke huyo mwenye muonekano wa
kiuungwana akikasirika inatisha mno kwa kile ambacho anaweza kufanya.
“Nitafanya uchunguzi kujua nani kamuuwa Linksi”Aliongea Sally na kisha alikata simu palepale.
Hamza ilibidi aghairishe safari ya kwenda kwa Dina kwanza na moja kwa moja alienda kwenye Apartment ambako Prisila na Serena walikuwa wakiishi.
Nusu saa mbele mara baada ya kufika ndani ya jengo hilo na kuingia ndani , ile anatoka katika floo ya vyumba vyao aliweza kugundua milango ya kuingilia yote ilikuwa wazi.
“Hamza!”
Aliita Prisila ambae alikuwa akitoka kwenye Apartment ya Serena akiwa na mwonekano wa kupaniki.
“Prisila upo sawa?”
Hamza alishindwa kujizuia kuwa na wasiwasi kwa namna ambavyo Prisila alionekana.
“Yule kaka , Pakamwitu amefariki ..”Aliongea na Hamza aliishia kukunja sura tu huku akiongozana na Prisila kuingia katika nyumba ya Serena. Ilikuwa ni kweli waliweza kukuta maiti ya Liksi ikiwa chini sakafuni eneo la sebuleni huku eneo la moyo wake likiwa na shimo.
Hamza aliishia kukunja ngumi yake , ilionekana wazi aliemuua Pakamwitu alikuwa akijua udhaifu wao ulipo.
Machotara wa kistrigoi ni ngumu sana kufa kwa majeraha ya kawaida , labda tu waharibiwe vichwa au moyo wao unyofolewe , kingine ni ngumu sana kutumia kitu cha ncha kuweza kuwaumiza na yote hayo ni kwasababu miili yao ilikuwa migumu, walichokuwa wakiogopa ni moto tu pekee.
“Prisila , Yupo wapi Serena?”
“Hata sijui , nilikuwa nikijiandaa kutoka , ila baada ya kuona mlango wa kuingilia ndani kwake upo wazi ndio nikaingia kuangalia n na ndio nikakuta maiti ya Linksi lakini Serena hakuwepo.
Nimejaribu kumpigia simu pia hapatikani”Aliongea na Hamza alionekana kufikiria kwa sekunde kadhaa na palepale alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Nilimchukulia poa Serena , ila amewezaje kufanya hivi?”
“Hamza unataka kusema Serena ndio kamuua Liksi?”Aliuliza Prisila kwa mshangao na Hamza alitingisha kichwa.
“Ukweli tu kwa muda mrefu nilikuwa nikimshuku Serena kwa kusema amekuja Tanzania kwasababu amemkumbuka mume wake .. Kingine kwa uzoefu wangu wa kuishi nje ya nchi hasa na hawa wazungu nawajua vizuri , ingawa Serena hakuonyesha kuwa na dosari yoyote , lakini bado nilihisi kuna kitu hakipo sawa ndio maana nikamuweka Liksi kumchunguza kwa siri wakati huo akikulinda na Liksi alifanya kazi yake vizuri , lakini awamu hii nadhani Serena amegundua namtilia shaka na hakutaka nikimkamata ndio maana akaamua kukimbia na Liksi akajaribu kumzuia ndio akaishia kumuua”
“Inamaana..!!”Prisila alijikuta akiziba mdomo akishindwa kuamini , alikumbuka namna alivyokuwa na ukaribu na Serena kwa kipindi chote alichofikia hapo kwenye Apartment yao , hata kupika na kula pamoja , ilikuwa ngumu kukubali Serena alikuwa muuaji.
“Prisila najua hii imekushitua na kukufanya kuwa na huzuni , hata mimi nilitamani kuona Serena ni mtu mzuri ambae ameamua tu kuja kuishi Tanzania lakini uwezo wake wa akili hatuwezi kuuchukulia kwa wepesi . Sio mwanamke wa kawaida”aliongea Hamza na Prisila alitingisha kichwa huku machozi yakimtoka.
“Mimi siamini , mpaka nishuhudie kwa macho yangu Da-Serena akimuua mtu , alikuwa mtu mkarimu sana , amenisaidia kwenye vitu vingi mno , sijawahi kuwa na ukaribu na mtu kama ilivyo kwa Serena”Aliongea na Hamza alijikuta akishangazwa na kauli ile ya Prisila kumtetea Serena,lakini wakati huo huo Hamza alijiuliza kwanini Serena
hakufanya chochote kibaya kwa Prisila baada ya kumuua Liksi.
Maana kama kweli amegundua alikuwa akimtilia shaka na amefanikisha kumuua Liksi angemteka na ingempa nafasi ya juu kufanya mazungumzo na yeye, lakini Serena aliamua tu kumwacha Prisila.
“Mpaka sasa bado nashindwa kujua sababu ya Serena kuweka ukaribu wake kwako na mimi lakini unapaswa kukumbuka hivi Prisila , ikitokea amejitokeza mbele yako tena usije ukamwamini”Alionya Hamza.
“Hamza nimechoka kweli , nataka nirudi nyumbani tu nikapumzike , siwezi kuendelea kukaa hapa”Aliongea Prisila akiwa na mwonekano wa kuchoka.
“Sawa wewe nenda kapumzika na niachie hili suala nitadili nalo”Aliongea Hamza akimshika Prisila bega kumfariji.
Baada ya Prisila kuondoka palepale kivuli kilijitokeza kutoka kwenye kona ya chumba hicho na alikuwa ni Crow.
"My Prince, how should I handle this?"Aliuliza.
Crow mara baada ya kukosa mawasiliano na Linksi haraka sana alichukua nafasi hio kuja kumtafuta na ndio alikuta amekwisha kupoteza uhai na ndio alietoa taarifa kwenda kwa Sally.
“Chukua mwili wake na urudishe kisiwani , hakikisha anazikwa vizuri . Mwambie Sally aweke umakini wake kwa Serena na aendelee kufanya mchakato wa ki upembuzi ili kujua taarifa alizozipata kutoka Marekani ni sahihi , hisia zangu zinaniambia kufa kwa Dokta Genesha na kifo cha Frida kuna uhusiano na Serena, kama ndio basi anaweza kuwa na nguvu kuliko vile tunavyomdhania. Hata kama ikitokea mmepata msipigane nae kizembe”Aliongea Hamza akitoa maelekezo na Crow aliitikia.
Crow macho yake yalikuwa yamejawa na hisia za kisasi , lakini licha ya hivyo alikubali maelekezo ya Hamza kwa kuweka mkono kifuani na kisha palepale aliubeba mwili wa Liuksi na kuondoka.
SEHEMU YA 173.
Saa tatu kamili za asubuhi siku iliofuata Hamza alitoka nyumbani kwa Dina akipanga kuelekea moja kwa moja kazini. Siku ya jana yake alisafiri kwenda Mtwara pamoja na Dina na haikueleweka walienda kufanya nini lakini walirudi usiku sana na kumlazimu Hamza kulala hapo hapo.
Saa nne kamili za asubuhi mara baada ya Hamza kufika nje ya jengo la kampuni simu yake iliita na alipoangalia anaempigia alikuwa ni Yulia na alipokea na hapo ndio Yulia alimwelezea kuhusu maendeleo ya kumtafuta Saidi.
Ukweli wakati anaona simu hio alijua labda Yulia alikuwa amempata Saidi kupitia teknolojia yake kama alivyosema , lakini matokeo yake Yulia alimwambia Hamza Saidi amepotea.
Yulia upande wake pia aliona ni jambo la kushangaza . Mwanzoni aliamini kupitia teknolojia yake ingekuwa rahisi sana kumtafuta Saidi ili mradi yupo Tanzania hata kama iwe amejificha ndani ya handaki lakini hakuona viashiria vyovyote vya uwepo wa Saidi Tanzania.
Alijikuta akikosa namna nyingine kwani iliokuwa kete yake muhimu ya kumpata Saidi haikufanya kazi.
Hamza mara baada ya kusikia hivyo alimwambia aendelee kumtafuta huku akijiambia katika moyo wake anapaswa kuongeza umakini sana , kwani kupotea kwa Saidi na Serena kwa wakati mmoja ilileta ukakasi mwingi sana. Kingine pia juu ya swala la Frida kupoteza maisha nyumbani kwake. Ijapokuwa ni taarifa ambayo hakuifuatilia kwa kina sana kuhusu Frida lakini ilimfanya kuhisi kuna muunganiko wa matukio hayo yote.
Hamza mara baada ya kuegesha gari yake , palepale aliingia kwenye lift iliomchukua moja kwa moja mpaka ghorofa ya juu kabisa na ile anataka kuingia katika ofisi yake alisogelewa na Linda alievalia suti ya rangi nyeusi juu hadi chini akiwa siriasi kama kawaida yake.
“Hamza Mkurugenzi ana mgeni ambae anahitaji kuonana na wewe katika ofisi yake”Aliongea Linda.
“Mgeni gani?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.
“Nenda utamuona mwenyewe”Aliongea Linda kikauzu.
“Dada Linda kwani ukiniambia kuna tatizo”Aliongea Hamza.
“Mimi sio dada yako”Aliongea Linda akimkodolea macho Hamza.
“Sawa dada , ila ngoja nikuambie sio vizuri kuwa kauzu muda wote , wewe sio kama bosi wetu hata kama awe kauzu vipi lakini bado ni mrembo. Sawa wewe rafiki yangu bado ni wa kawaida lakini unajinunisha muda wote , utapataje mpenzi kwa staili hio?”Aliongea Hamza.
“Sorry to disappoint you , Nina mpenzi tayari na ananipenda mno huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi”Aliongea Linda huku akivuta mdomo na kauli hio ilimshangaza kidogo Hamza.
“Haha kama ni hivyo hongera. Ila mpenzi wako atakuwa ni kijana jasiri mno namtakia kila la kheri”
“Unamaanisha nini wewe?”Aliuliza Linda , alikuwa na hasira kiasi cha kutaka kumrukia Hamza na kumrarua.
Hamza aliishia kucheka tu na kuingia ndani ya ofisi ya Regina. Ile anaingia tu aliweza kuona mwanaume mwenye mwonekano wa kitanashati wa umri wa makamo alievalia suti na alionekana kuwa tulivu.
Regina pia hakuwa amekaa katika kiti chake cha kazi bali alikuwa amekaa kwa upole kwenye sofa akimsabahi mgeni.
“Jenerali!?” Hamza alijikuta akiwa katika hali ya mshangao mara baada ya kugundua mtu ambae alikuwa akimsubiria ni baba yake Yonesi, Meja Jenerali Daudi Mazengo.
Afande Daudi mara baada ya kumuona Hamza alitabasamu huku akisimama na kumpatia mkono kumsalimia.
“Hamza! Umefika”Aliongea huku akiwa mpole kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza wanakutana.
“Kaa chini Hamza , Jenerali alikuwa akikusubiria”Aliongea Regina akihama sofa kumpa nafasi Hamza.
Regina alijua Mjeshi huyo alikuwa akijua yeye na Hamza ni wanandoa ndio maana alimuonyeshea heshima Hamza mbele ya Afande.
Hamza hakutegemea Regina kuwa mnyenyekevu mbele yake na aliishia kutingisha kichwa na kukaa chini.
“Jenerali naona umenishtukiza. Vipi hali ya Mama yake Yonesi?”
“Shukrani kwa upasuaji uliomfanyia , mke wangu alisharuhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri kabisa”
“Nimefurahi kusikia anaendelea vizuri”.
“Ujio wangu hapa ukiachana na kukushukuru kwa kumsaidia mke wangu lakini vilevile nipo kwa ajili ya kukushukuru kwa niaba ya familia nzima”Aliongea na Hamza alijua nini anashukuru.
Mpango wa mwanzo wa Hamza ni kuunganisha Kambi ya Nyoka na familia ya Wanyika lakini alighairi na kuona ingeleta tija zaidi kama angeiunganisha na familia ya Chifu Mazengo, aliona familia ya Yulia ilikuwa na nguvu tayari.
“Tumekwisha kusaini mkataba na Wazee wa
Kambi ya nyoka na makubaliano yetu ni kwamba Kambi ya Nyoka itatoa sapoti ya ki ulinzi kwa familia yetu . Kwa muda mrefu tumekuwa dhaifu kutokana na kukosa ufunuo wa kimafunzo na kujenga kambi lakini chini ya mkataba huu hadhi yetu ya kifamilia imepanda”Aliongea.
“Usiwe na wasiwasi kabisa Afande , kama nilivyoahidi kuifanya familia yako kuwa yenye nguvu ndio ninachokwenda kutekeleza. Ijapokuwa kwasasa Kambi ya Nyoka inaweza isiwe na nguvu kama zilivyokambi nyingine ambazo zina msingi mzuri wa kimafunzo , lakini kuwa na ushirika ni swala linalowaweka katika meza moja ya hadhi”Aliongea Hamza.
“Ni wewe ulieshambulia kambi ya nyoka siku ziliozopita?”Aliuliza Regina kwa mshangao , aliweza kuona habari ya kambi ya nyoka kushambuliwa katika runinga.
“Ilikuwa ni swala la kufanyika ili kuwa katika hali ya usalama. Kwasasa mimi ni Chifu wa heshima ndani ya Kambi ya Nyoka. Nimeamua kuifanya kambi ya Nyoka kusaidia familia ya Chifu Mazengo katika kuibua vipaji vya wavuna nishati.”
“Si ulisema unaenda kuyamaliza na kiongozi wa kambi hio , Imekuwaje ukageuka kuwa mtu wa heshima?”Aliuliza Regina akiwa kama haamini. “Ni stori ndefu , ila nitakuelezea baadae”
“Haina haja ya kuelezea , isitoshe sipendi sana kuuliza maswali mengi”Aliongea Regina.
Regina hakuwa akivutiwa sana na mambo ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi , pia hakujali Hamza staili yake ya kudili na matatizo ili mradi matokeo yawe mazuri ndio alichotaka.
Mara baada ya kuona namna Hamza na Regina wanavyoongea kirafiki kama wanandoa aliishia kutoa tabasamu tu.
“Hamza umenifanya nikukubali kwa mara nyingine. Siku nyingine ukifika Dodoma familia yetu ipo tayari kukupokea kwa tafrija. Baba pia amefurahi kwa kuona hatima ya familia yetu imebadilika. Umekuwa msaada sana kwa familia yetu ya kichifu kwa kuipa hadhi tuliokosa kwa miaka mingi”
“Usiwe na shaka kabisa Afande . Nimefanya haya yote sio tu kwa ajili ya familia yenu lakini vilevile kwa ajili ya Yonesi kupata utulivu. Halafu kama Mama anaendelea vizuri imekuwaje Yonesi mpaka sasa hajarudi?”Aliuliza Hamza
Ingawa Regina alikuwa pembeni yake . Hamza hakutaka kushikwa na wasiwasi wa kumzungumzia Yonesi. Pili Hamza hakutaka kuonyesha hajiamini mbele ya Regina.
“Kuhusu Yonesi ndio kitu kingine kilichonileta hapa na kukutaarifu kwamba Yonesi hana mpango wa kurudi tena”
“Nini! Hana mpango wa kurudi tena hapa?”Aliuliza na Baba yake Yonesi aliishia kutingisha kichwa na kisha alitoa bahasha ya khaki na kumpatia Hamza.
“Amekuandikia barua na ameniambia nikufikishie . Ukishaisoma utaelewa”Aliongea Afande huyo akiwa na mwonekano usioelezeka.
Hamza aliishia kupokea bahasha ile na kufungua ndani na kutoa karatasi ilioandikwa kwa mkono. Ulikuwa ni mwandiko wa Yonesi.
Hamza hakuona shida kuisoma hapo hapo hivyo alianza kusoma kimya kimya.
****
Kwako Hamza,
Unaposoma barua hii, mimi sipo tena Dar es Salaam. Pia, nimeondoka nyumbani na pengine kwa sasa nipo nje ya nchi. Najua ni ghafla sana, lakini ukweli ni kwamba moyo wangu umekuwa ukikuwazia kwa muda mrefu. Kilichotokea hivi karibuni ndicho kimenifanya kufikia uamuzi huu.
Tangu siku tulipokutana mpaka sasa, umenishangaza sana na uwezo wako wa mapigano na koneksheni ulizonazo. Hali hii imenifanya nione kwamba kuna pengo kubwa kati yetu. Ingawa hatujafahamiana kwa muda mrefu, kwa kipindi kifupi nilichokuona ndani ya kampuni, nimejikuta nikiwa na shauku kubwa sana kuhusu wewe.
Mwanamke anapokuwa na shauku na mwanaume, mara nyingi hayuko mbali na kupenda. Nimefurahishwa kuona kuwa unataka kunipenda, lakini mimi ni sehemu ndogo sana kwako. Mimi si mpole, wala sina busara kama Dada Eliza. Kitu pekee ninachojua ni kupigana, na kwako uwezo wangu huo hauna maana.
Safari hii umefanikisha ushirikiano kati ya familia yetu na Kambi ya Nyoka. Wazee wa familia wamefurahi mno na wamenisifia kwa kuwaletea
mwanaume kama wewe, lakini kwangu mimi
haijalishi. Sijali kile unacholetea familia yetu wala mawazo ya wazee kuhusu uhusiano wetu.
Ninachojali ni kuwa na hadhi ya kuendana na wewe. Sikujui vizuri wewe ni nani au wasifu wako ni
upi, lakini najua mwanamke kama mimi hakosekani kwa wale waliokuzunguka. Hivyo, naamini kuondoka kwangu hakutokufanya uhuzunike.
Napanga kujifunza na kupata nguvu, angalau nisiwe najiona mdogo mbele yako. Mpaka siku nitakayoweza kusimama mbele yako kwa kujiamini, natumaini hutakuwa umenisahau.
Tafadhali mpe shukrani zangu za dhati Mkurugenzi Regina kwa ukarimu wote alionionyesha wakati nilipokuwa mpweke bila msaada.
Take care,
Ni mimi,
Yonesi Daudi
*****
Hamza hakufunika barua na Regina aliekuwa pembeni aliweza kusoma pia na mara baada ya kusoma macho yake yalijawa na huzuni. “Afande Daudi ni wapi alipo Yonesi?”Aliuliza Regina.
“Niwe tu mkweli sijui kabisa alipoenda. Ninachojua ni kwamba kutokana na kupungua kwa wanajeshi wengi wa kitengo cha Malibu , Jeshi lipo kwenye mpango wa kukusanya vijana wapya watakaojiunga na programu maalumu ya mafunzo . Yonesi alikuwa mwanajeshi hivyo lazima atakuwa amefanikiwa kuchaguliwa lakini kuhusu wapi mafunzo yake yatafanyikia au misheni gani anapewa katika nafasi yangu siwezi kufahamu”Aliongea
“Hata kama unajua naamini
usiongeongea?”Aliongea Hamza ambae alikwisha ikunja barua ile.
“Nimefanikisha kuileta barua kwako tayari na hilo ndio muhimu . Kama unamheshimu Yonesi nadhani itakuwa vizuri ukiyaheshimu maamuzi yake”.
“Sina chakufanya kwasasa. Hata kama niseme nimtafute nitaendelea kumpa presha tu. Sijawahi kuwaza ninachofanya kitamfanya kujisikia vibaya”
“Namjua binti yangu vizuri. Akiamua kitu hawezi kubadili mawazo. Haikuwa rahisi kuja Dar es salaam na kuishi peke yake bila ya msaada wa ndugu kwa zaidi ya miaka mitatu”
Hamza pia alikuwa akielewa hivyo, hata kama hakuwa tayari kukubali maamuzi yake lakini asingefanya chochote.
“Hamza, Mkurugenzi Regina . Nina vikao ya vya kuhudhuria hivyo muda wangu hapa umeisha. Kama nitapata nafasi nitakuja kuwatembelea nyumbani”
Mara baada ya kuongea hivyo aliaga bila kuwapa nafasi Regina na Hamza kumsindikiza.
Baada ya kuondoka ni Hamza na Regina waliobakia ndani ya ofisi.Regina aliishia kumwangalia Hamza namna alivyoshikiria barua hio akionekana katika mawazo na aliishia kuhema tu kwa masikitiko.
“Wanawake tunatofautiana sana . Wengine tupo tayari kumtegemnea mwanaume maisha yetu yote kwa kila kitu . Lakini kuna wengine wanataka kujitegemea kwa kujijengea nafasi katika jamii kupitia juhudi zao wenyewe . Yonesi ni aina ya wanawake wanaopenda kujitegemea , Hataki kuwa pambo kwa ajili ya mwanaume , hivyo unapaswa kumwelewa”Aliongea Regina.
Pengine kwa mtu wa nje angeona ni ajabu sana kwa Mke kumfariji mume kwasababu ya kuachwa na mchepuko . Lakini huyo ndio alikuwa Regina.
“Wife hata wewe ni kama Yonesi tu”
“Mh natamani kukutegemea katika kila kitu , lakini nyumba tunayoishi na hata gari unaloendesha vyote ni vyangu , hivyo nakutegemeaje sasa?”Aliongea na kumfanya Hamza kushikwa na haya.
“Unaonekana kuwa sahihi”
“Hebu ondoka kwanza. Nina kazi za kufanya”Aliongea Regina akirejea katika hali yake ya ubosi.
Hamza aliishia kusimama kivivu , alijua kwa kampuni nyingi ikifikia mwisho wa mwaka kuna mengi ya kufanya hivyo aliondoka kimyakimya lakini kabla hajasimama simu ya Regina iliita na alipokea mara moja.
“Hamza subiri kidogo”Aliita Regina mara baada ya kuona anakaribia kutoka nje.
“Kuna nini?”
“Lamla amepatikana”Aliongea Regina akionekana kufurahi.
Uwezo wa mtandao wa chatu kumtafuta mtu ulikuwa mkubwa mno na asubuhi hio waliweza kufanikisha kumpata na kumpigia simu Regina moja kwa moja.
Hamza mara baada ya kumuona Regina akijikusanya kwa ajili ya kuondoka alijikuta akishikwa na hisia zisizokuwa zikielezeka.
Ilionekana licha kwa muda mrefu Lamla na Regina kuwa maadui lakini bado alikuwa na hisia za undugu .
“Mbona umesimama sasa , fanya haraka ukaendeshe gari tumfuate”Aliongea Regina mara baada ya kuona Hamza amesimama tu kama sanamu.
Hamza hakutaka kuona Regina akienda peke yake kuonana na Lamla , hivyo hakuwa na jinsi kwenda kumsindikiza.
Baada ya lisaa kuendesha gari hatimae walifika Tegeta Sokoni na kuegesha gari upande wa pembeni na muda huo walisogelewa na bwana alievalia tisheni ya Arsenal na kofia ya chepeo.
“Wewe ndio Bro Hamza na Bosi Regina?”Aliuliza Yule bwana akiwa na tabasamu la uchangamfu.
“Ndio! Wewe ndio ulitupigia simu?”Aliuliza Hamza.
“Ndio, naitwa Marko , mimi ni meneja wa mtandao wa Chatu upande huu wa Tegeta . Nimesikia sana kuhusu wewe. Braza Hamza heshima yangu kwako ni kama mto usiokauka” “Sawa Marko , tuachane kwanza na mistari na tupeleke kuonana na Lamla”Aliongea Hamza akimzuia asije endelea kuwa chawa.
“Bro, Bosi Regina nifuateni niwapeleke .
Nimeaacha vijana kuendelea kumwangalia”
“Yupo wapi kwani?”Aliuliza Hamza maana kulikuwa na jua kali sana kwa Regina kutembea. “Kuna Bar moja upande wa chini kule”
“Yupo Bar! Amelewa au?”Aliuliza Regina kwa mshangao.
“Hapana. Nimesikia anaomba kazi ya kufanya”Aliongea Marko na kumfanya Regina kushangaa.
“Kwanini aombe kufanya kazi bar?”.
“Wife unadhani Lamla unaemjua ni yule yule mke
wa tajiri . Sifa hio imeshampotea na njia rahisi ya kuendesha maisha ni kwenda Bar sehemu anayoiweza kupata kazi kwa urahisi”Aliongea.
“Inaonekana ameteseka vya kutosha”Aliongea
Regina huku wakianza kutembea katikati ya soko na kuchepukia upande wa pili vichchoroni na kwenda kusimama katika Bar Moja ndogo ambayo ilionekana kuwa na mgahawa.
Kwa nje kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wakicheza Draft na mara baada ya kumuona Marko ametangulizana na mabosi walimsogelea haraka haraka.
“Marko bado yupo ndani . Nimesikia akipewa maagizo ya kwenda kuosha vyombo jikoni . ila mpaka sasa hajatoka”
“Kuosha vyombo?”Regina alonekana kushangaa , ilikuwa kawaida kwa mtoto wa kishua kama yeye kushangaa.
“Lamla hajawahi kuosha vyombo maisha yake yote tokea akiwa mdogo”Aliongea.
“Wife unadhani atafanya nini sasa , hana pakwenda , hata kama hajui hakuna namna atajifunza tu”Aliongea Hamza na Regina aliona ni sahihi.
“Bro tunafanyaje?”Aliuliza Marko.
“Wife si umekwisha amua? Kama ukiingia kuonana nae sina uhakika na kitakachotokea”
“Kama yupo hapa haina namna zaidi ya kuonana nae . Kama yupo tayari kubadilika na kuwa mtu mpya nitampa nafasi . Kama yupo kama mwanzo nitaachana nae”Aliongea Regina na Hamza alitoa tabasamu hafifu.
Kadri alivyokuwa akimjua Regina aligundua ukiachana na ukauzu wake na ukatili katika maswala ya kibiashara lakini alikuwa na moyo mzuri mno wa kusamehe.
Baada ya kuingia wakiongozwa na Marko uelekeo wa jikoni walisikia mwanaume akifoka kwa ndani huku Lamla akionekana kujitetea. Kwa haraka sana ilionekana amepasua sahani za udongo.
“Baba yangu naomba nifanye kazi hapa . Nitalipia sahani niliovunja na hela nitakayopata leo”
“Yaani kuosha vyombo hujui halafu unataka kuendelea kufanya kazi hapa uendelee kuvunja vyombo?”
“Samahani.. Nitakuwa makini. Mikono iliteleza bahati mbaya . Tafadhari naimba usinifukuze . Sina pakwenda”
“Haha … Sidhani kama utaweza kazi ya kuosha vyombo na kuhudumia wateja . Unaonaje ukinilipa kwa kuniacha nipige kimoja cha chapuchapu. Nitakuacha pia uendelee kufanya kazi hapa”Aliongea Yule mwanaume huku akimsogelea Lamla na kumshika kalio.
“Baba hapana.. “
Hamza na Regina walijikuta wakisita na kujishauri waingie ama wasiingie , lakini mara baada ya kusikia Lamla anataka kufanyishwa ngono , Regina hakujiuliza mara mbilimbili na kuingia ndani.
“Hey! Hebu muache”Aliongea Regina akimwangalia mwanaume ambae alikuwa amemsukumia Lamla kwenye kona ndani ya jiko hilo lililojaa uchafu wa majivu na mkaa.
“Wewe ni nani. Hebu jali mambo yako”Aliongea na yule mwanaume aligeuka na kumwangalia Regina.
Lamla alionekana kulia na nywele zake zilikuwa zimechanguka . Alionekana kama mwanamke kichaa. “Regina!1”
Aliongea Lamla huku akificha uso wake kwa aibu na kuanza kutoa kilio.
Regina macho yake yalijawa na unyevunyevu mara baada ya kumuona Lamla katika hali hio na chuki aliokuwa nayo zidi yake ilipotea palepale. Aliona kuna faida gani ya kumchukia mtu mwenye maisha magumu namna hio.
Hamza alimpa ishara Marko aliekuwa nyuma yake na palepale alielewa na aliwapa ishara wenzake.
“Mtoeni huyo mzee mkampe kichapo kwanza. Bro huyu mtu niachie tu mimi nitadili nae vizuri na kumfundisha tabia maana ndio zake”Aliongea Mark na Hamza alitingisha kichwa na baada ya yule mzee kuburuzwa nje Hamza alimsogelea Lamla.
“Sikuwa na mpango wa kukutafuta , ila mke wangu ni mtu mwenye roho nzuri na ndio alieniambia nikutafute. Hivyo acha kuendelea kulia na ongea nae”Aliongea Hamza na Lamla aliinua uso wake na kumwangalia.
“Regina… najutia mimi.. nisingefanya vile kwa baba yako . hiii.. hiiii”
Regina mara baada ya kukumbuka namna baba yake alivyyofariki kwa ajili ya kulinda mali za familia machozi yalimtoka.
“Baba alikupenda sana , lakini bado tu ukaamua kumsaliti . Kabla ya kuamua kujiua moyo wake ulishakufa . Unalijua hilo?”
“Najua .. ndio maana naona aibu hata kukuangalia
usoni. Hata kama uniue sidhani kama nitaweza lipia”
“Kama kukuua kungemrudisha baba yangu hai ningefanya hivyo . Lakini haiwezekani hivyo unapaswa kuendelea kuishi na kuungama dhami zako”Mara baada ya kuongea hivyo Regina alitoa ufunguo kwenye mkoba wake na kumrushia Lamla.
Lamla mara baada ya kuona ufunguo ule ulivyo macho yalimtoka .
“Regina…”
“Ijapokuwa sitaki kujihusisha chochote na wewe , lakini katika macho ya wengine wewe bado ni mama yangu wa kambo . Wakikuona unafanya kazi hapa na kukufahamu itaniharibia taswira yangu . Chukua huo ufunguo. Nyumba yetu ya zamani kule Msasani haina mtu wa kuifanyia usafi kila siku. Umeishi pale kwa zaidi ya miaka ishirini . Nataka uifanyie usafi kila siku na nitakuwa nakulipa mshahara”Ijapokuwa maneno ya Regina yalikuwa ya ukauzu lakini mara baada ya kumfikia Lamla aliliripukwa na furaha..
Regina aliamua kumrudisha katika nyumba ambayo aliishi kama mke wa baba yake mwanzo.
Kwa hali aliokuwa nayo Lamla , Pesa na hadhi havikuwa na umuhimu , alichohitaji ni kula na sehemu ya kulala.
“Regina umeninsamehe na unataka nirudi nyumbani kweli?”Aliuliza akiwa haamini.
“Sijasema nimekusamehe nafanya haya yote kwa ajili ya heshima ya baba”Aliongea Regina na kisha palepale aligeuka.Licha ya hivyo kwa Lamla alishukuru mno kiasi cha kuanza kutoa kilio
Regina mara baada ya kufika nje ya Bar hio .
Alijikuta akihema kwa nguvu akijitahidi kutulia.
“Wife nimekukubali. Kwenye dunia hii watu wa aina yako ni wachache mno”Aliongea Hamza.
“Wewe sema tu mimi ni mjinga . Mwenyewe hata sielewi kwanini nakuwa mjinga kiasi hichi”
“Haha upo sahihi , Maamuzi ya aina hii ni mjinga pekee anaeweza kufanya . Lakini muda mwingine hii ni sifa adimu sana kwa mtu . Ndio maana nimejikuta nikizidi kukupenda mke wangu”Hamza aliamua kuwa muwazi , kwa muda mrefu sana alivutiwa na urembo na umbo la Regina lakini muda huo alifurahishwa na ujinga aliokuwa nao Regina. Isitoshe alitamani sana kujua baadhi ya vitu vingi katika moyo wa Regina.
Kama kigezo cha kuoa ni mwanamke mrembo na anaevutia tu kuna haja gani ya kumfanya awe ni wa kufa na kuzikana ili hali kila uchao wanawake warembo wapo tu na wanaendelea kuzaliwa.
Regina mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Hamza alitoa tabasamu huku macho yake yakilegea utamu.
“Hatimae umeongea neno zuri leo”Aliongea Regina.
“Ah Wife . Nimeongea mambo mengi leo kwahio hio ndio sentesi pekee nzuri kutoka kwangu?”
“Wewe unaonaje. Muda mchache uliopita unajitilisha huruma kwa kuachwa. Halafu unategemea nifurahie kila unachoongea”Aliongea Regina akimkodolea macho.
“Haha.. Wife bwana. Tuachane na hayo kwanza. Maana sijui ni lini nitakuja kuonana na Yonesi tena”Aliongea Hamza.
Regina pia alikuwana wasiwasi kuhusu Yonesi. Isitoshe ndio moja ya marafiki wachache aliokuwa nao.
“Namuombea huko alipo awe salama tu”Aliongea Regina na Hamza hakuongea neno zaidi ya kuwa kimya. Uwezo wa kumtafuta alikuwa nao lakini hakutaka kufanya hivyo maana ingemfanya Yonesi kukidharau kwa maamuzi yake.Muda huo Marko na washikaji zake waliwarudia Hamza na Regina.
“Bro tushamshughulikia yule mshenzi tayari. Tupo tayari kwa maagizo mengine”
“Hakuna mengine. Asanteni”Aliongea Hamza.
Muda ule Regina aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa kibunda cha hela nyekundu. “Chukueni hiki kiasi kidogo cha hela mgawane”
“Hapana usijali kabisa madam. Hatuwezi kupokea hela ya Bro na wewe Mkurugenzi hata kama utupige mpaka tufe. Sisi tunaondoka sasa hivi”Aliongea Marko na baada ya pale aliwapa ishara wenzake na walipotelea vichochoroni. “Kuna haja ya kunikimbia, Nilitaka tu kuwashukuru”Aliongea Regina na kumfanya
Hamza aangalie bunda la hela aliloshikilia Regina na kumfanya kucheka.
“Wife namna yako ya kushukuru sio ya kawaida. Hela zote hizo?”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumkata jicho na alichukua lile burungutu la pesa na kulishindilia kwenye mfuko wa suruali ya Hamza.
“Kama wamezikataa zitakuwa zako za matumizi. Hata hivyo umejitahidi kufanya kazi nzuri wiki hii”Aliongea na kumfanya Hamza kukosa neno la kuongea na kujiambia mbona Regina anamfanya kama mdogo wake, Lakini alivyoangalia hela hizo zilivyosindiliwa alijikuta akicheka na Regina nae alicheka.
Mwanamke aliekuwa kwenye Gari na Saidi ni nani, mbona kama ni Lamla . Unadhani Lamla alistahili msamaha wa Regina au ndio kujipiga risasi mguuni?.
ITAENDELEA .
Amounjmosi
Finallyjmosi
UsikuSingano is typing.....
Huu ndio unaitwa uswahili uliokithiri.Umeahidi mwenyewe kuleta mzigo jana halafu unashindwa mwenyewe kusimamia maneno yako!!! Singano jrjmosi