Wikitatu
New Member
- Jan 6, 2025
- 2
- 1
Hahaha.... Hivi Ile ya nilimdhania kahaba kumbe bikra iliisha? Story ndefu inasomwa miaka 3!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha.... Hivi Ile ya nilimdhania kahaba kumbe bikra iliisha? Story ndefu inasomwa miaka 3!!!
Hii na ile ya kahaba bikira ni pipa na mfunikoHahaha.... Hivi Ile ya kahaba bikra iliisha? Story fupi inasomws miaka 3!!!
HahahaaaHii itakuwa Pipa
Lushoto,MBaramo ipi mkuu
mhm!! kwa walichomfanyia wale waarabu, sizani kama atapata nguvu za kuleta mwendelezo....Tukumbuke na Leo bwana singano
Tumalize weekend yetu vizuri
Asante mkuu .Tuendelee kuishi humuWakuu hatimae nimepata video clip inayoonesha mapigano ya jamii za china (youcu) zinazotumia nishati za mbingu na Ardhi, kweli singano ni mtunzi anaesakanya data vyema, nimemuelewa sana sasa akisema aura naelewa
Jioni ya leoUsiku wa leo mwendelezo[emoji1787]
Singanooooooooooo mida ndo hiiUsiku wa leo mwendelezo[emoji1787]
Ni Usiku sasa acha tukagonge mlango kwa Regina tulaleSHETANI RUDISHA AKILI ZETU.
MTUNZI:SINGANOJR.
SEHEMU YA 170.
Unataka kuigusa?.
Mende alijikuta akihisi kizunguzungu wakati wa kudondoka huku akishindwa kuamini licha ya mwili wake kukombolewa na Tone la Ukombozi na kumfanya kuwa na nguvu lakini bado mtu huyo ameweza kumsukuma kwa urahisi kabisa kama vile alikuwa mtoto wa miaka mitatu.
Haraka sana yule mzungu alimvua Prisila lile helmeti na kisha alionyesha ishara ya kuomba radhi mbele yake.
“Samahani sana Miss Prisila , The lynx came late”Aliongea akimaanisha kwamba Yeye Pakamwitu amekuja kwa kuchelewa.
Mara baada ya Linksi kuongea vile, palepale alipitisha kucha zake katika zile kamba zilizokuwa zimewafunga na kuachia mara moja. Kutokana na lafudhi yake ya kuongea Selena alionekana kumfahamu palepale .
“Lazima utakuwa ni moja ya walinzi wa siri chini ya Sally? Kama ni hivyo basi ulikuwepo hapa muda mrefu ila kwanini umesubiri muda mrefu mpaka kuchukua hatua ?”Aliuliza Serena.
“Prince alihitaji kujua mtu anaemtafuta alipo , hivyo sikuchukua hatua mapema kutokana na kumsubiria”Aliongea
Saidi uso wake ulivimba na bila ya kuchelewa palepale alichukua kishikwambi mezani na kisha helmeti na kukimbia . Lakini ile alivyokuwa akitaka kutoke nje kabisa palepale aliweza kuona mtu akiingia kutoka nje ya geti na alikuwa na spidi kubwa kama vile ni pepo.
“Saidi ni wapi unaenda?”Aliuliza Hamza aliekuwa amefika hapo akiwa katika mwonekno usioelezeka.
Liksi mara baada ya kusikia sauti ya Hamza palepale alikimbilia nje na kuonyesha heshima yake kwa kuliita jina la MY-Prince.
“Umefanya kazi nzuri Pakamwitu, unaweza kuondoka sasa”Aliongea Hamza akimruhusu Liksi na palepale alisimama na kupotelea gizani.
“Hamza .. wewe umejuaje sikufariki?”Aliuliza Saidi.
“Nilifikiria na kujiuliza ni kichaa gani anaeweza kuuwa familia nzima ya wavuvi. Namna ambavyo maharamia wa kunti la The Shark walivyokufa nilihisi tu lazima itakuwa ni kazi yako . Ili kujihakikishia, nilitega macho ya watu wengi kukufuatilia. Kama usingerudi Tanzania nisingeweza kukufuatilia zaidi . Ila angalia kiburi chako kilipokufikisha”Aliongea Hamza ila upande wa Saidi hakuonekana kuwa na hofu na palepale alipiga hatua kumsogelea Hamza.
“Nilidharau uwezo wako ndio maana nimefeli . Sikudhania utakuwa na watu wengi wa kukufanyia kazi . Ila nitakubali kushindwa awamu hii lakini kaa ukijua nikirudi tena siwezi feli.”Aliongea.
Hamza mara baada ya kuona Saidi alikuwa akimsogelea bila hali ya hofu yoyote , alihisi kuna kitu hakikuwa sawa na mara baada ya kumsikia akiongea hivyo ni kama alipata ufumbuzi.
“Naona ushang’amua tayari?”Aliongea Saidi huku akionyesha tabasamu la kejeli na kuanza kucheka kama kichaa huku akimsogelea Hamza kwa kasi.
“Pumbavu..”Hamza alijikuta haraka sana akirudi nyuma kumkwepa na palepale Saidi mwili wake ulishika moto na kulipuka , ikionyesha alikuwa na mfumo wa kujimaliza.
Hata Helmeti na Kishikwambi alichokuwa ameshikilia mkononi kila kitu kiligeukwa na kuwa skrepa.
Mende ambae hakuwa mbali mara baada ya kuona tukio lile la bosi wake kulipuka alishituka mno.
“Bosii!!”
Prisila na Serena ambao ndio kwanza wakitoka nje walishangaa baada ya kushuhudia Saidi akilipuka.
Hamza alijikuta akisugua paji la uso wake akionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa katika hali ya mkanganyiko na aliishia kumwangalia Saidi ambae aligeuka na kuwa skeleton la chuma na alijikuta akiongea kwa chini chini.
“Ndio maana akachagua eneo lililotelekezwa kama hii, kumbe alikuwa ni feki”
Hamza hapo ndio alijua Saidi halisi hakuwa huyo . Ijapokuwa akili inaweza kuwa yake lakini mwili ulikuwa tofauti.
Ukweli huo ulimfanya Hamza sasa aone Saidi pengine alikuwa na hisia na yeye alikuwa amejipanga na mpaka hapo ilikuwa ngumu kujua nani alikuwa ameshinda au amepoteza au nani ambae kanufaika.
Hamza alitembea na kumsogelea Mende na kisha alimshika tai kwa nguvu akiwa siriasi.
“Bosi wako yupo wapi?”Aliuliza Hamza.
Ingawa alipanga kutokujibu lakini Hamza alidhamiria kupata taarifa kutoka kwake.
“Mimi sijui,Meneja wetu ndio aliekuwa akifika hapa kila siku kuongea na bosi. Mimi ninachojua huyu ndio bosi”Aliongea kwa kujitetea.
“Kama ni hivyo nitajie jina la Meneja wako na wenzako wote ambao mnawasiliana na Saidi”Aliongea Hamza.
Swali hilo lilimfanya Mende macho yake kuonyesha hali ya hofu kwa kuona Hamza angemuua. Sekunde tu ile anataka kuongea sauti ya ajabu ilisikika kutoka kwenye mwili wake na kabla hata haijajulikana ni nini kilichosikika.Eneo la kifua chake lilionekana kupasuka.
Mende licha ya kujiona akifa lakini bado alikuwa katika uchungu mwingi sana , hakuwahi kudhania kifaa ambacho alikuwa akivaa akijua ni cha mawasiliano kilikuwa pia ni bomu.
Ilionekana mara baada ya Saidi kuona Mende anataka kuvujisha siri alichukua hatua na kisha kumlipua.
Hamza aliishia kurusha maiti ya Mende pembeni huku akijifuta damu zilizosambaa katika uso wake . Aina hio ya bomu la mfukoni halikuwa hatari kwake lakini lilitosha kumuua binadamu wa kawaida.
“Hamza uko sawa?”Aliuliza Prisila kwa wasiwasi . Msichana huyo alikuwa katika hali ya hofu hasa alipoona namna Hamza alivyokuwa amechafuka na damu usoni.
“Niko sawa usiwaze , Prisila mchukue Serena na mtangulie kuondoka . Nataka nimtafute Saidi mpaka nimpate”Aliongea Hamza.
“Hamza huyu mtu ni nani hasa? Anaonekana kumiliki teknolojia ya hali ya juu ?”Aliuliza Serena kwa shauku.
“Kuhusu kuwa nani hilo halina umuhimu kwasasa .Ninachojua kuhusu mtu huyu hapaswi kuendelea kuishi”
“Hamza hakuna njia nyingine ya kutatua hili suala ? Mpaka sasa sijui ni kwanini Saidi anafanya haya yote”Aliongea Prisila kwa sauti ya unyonge.
“Prisila ukianza kufikiria sababu kwanini anafanya haya yote utajiumiza kichwa tu. Usiwe na waswasi nitadili na hili swala kikamilifu”Aliongea Hamza na hakutaka kuendelea kubakia hapo na aliwaambia waondoke pamoja haraka iwezekanavyo.
Baada ya wanawake hao kuondoka . Hamza aliita na Liksi ambae alikuwa amejificha alitokeza kutoka gizani.
“Sire! Any orders?”
“Kuna kitu cha tofauti umekiona kutoka kwa Serena?”Aliuliza Hamza akiwa na mwonekano usiosomeka.
“Anaonekana kukufahamu vizuri . Alijua uwepo wangu tokea muda mrefu ndio maana hakuonekana kupaniki”Aliongea
“Kwa akili yake ni sahihi kujua hilo . Hili bado siwezi kulichukulia kama ushahidi”Aliongea Hamza akitingisha kichwa.
“Sire , Kwasababu una shuku kuna kitu hakipo sawa kuhusu Serena, kwanini hukumuua au kumkamata na kumhoji?”Aliuliza Linksi.
“Unadhani hapa ni Toharani! Kama ushahidi sina siwezi kumfanya chochote. Kuna uwezekano pia alimkumbuka hayati mume wake ndio maana akaamua kuja na kuishi Tanzania na kukutana kwetu ni kwa bahati mbaya , unadhani naweza tu kumkamata mjane wa rafiki yangu na kuanza kumhoji?”
“Lakini kama ana nia mbaya si maana yake Prisila atakuwa hatarini?”Aliuliza Linksi.
“Ndio maana nahitaji uongeze umakini katika kumlinda, nitawaruhusu na Crow , Viper na Grewwofl kukusaidia. Kwasasa Saidi anaamini watu wangu wote wakaribu nimewawekea ulinzi hivyo hatowagusa tena”Aliongea Hamza na mara baada ya Linksi kusikia hivyo palepale aliitikia na kisha akaondoka.
Hamza mara baada ya kutembea mpaka kwenye kituo cha daladala alikaa chini huku akiwasha sigara na muda huo huo alitumia kumpigia simu Sally.
“Sally si umeweza kuzidukua kamera zote za CCCTV ndani ya Dar , Vipi bado hujapata uelekeo wa kiota cha Saidi?”Aliuliza Hamza.
“Nimeangalia karibia Kamera zote , ila huyu Saidi anaonekana kuwa mjanja mno hajaacha viashiria vyvoyote nyuma . Inaonekana alikwepa maeneo yote yenye Kamera.”
“Kama ni hivyo unadhani ni njia gani rahisi ya kumpata Saidi ?”Aliuliza Hamza bila kuonekana kushangaa. Saidi kama IQ yake ingekuwa ndogo angekuwa ashakamatwa muda mrefu , ila kutokana jambo hilo aliona itakuwa usumbufu mkubwa sana mpaka kuja kumpata.
“Kuna njia tatu za haraka za kuweza kumpata . Ya kwanza ni kuwashirikisha Binamu kupitia teknolojia yao ya Jicho la Anga na kutusaidia kupata taarifa zake”Aliongea Sally mara baada ya kusita kidogo.
Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akitabasamu kwa uchungu. Binamu kitengo ambacho kilikuwa kipo chini ya watu wa Bonde la Giza au watu wa Bondeni ambao walikuwa na uhusiano na Regina.
Kama angetaka kweli kuomba taarifa isingekuwa ngumu sana kutokana na kwamba bado alikuwa chini ya umiliki wa pete yao lakini alisita kufanya hivyo.
“Lazima utakuwa umefanya mawasiliano na watu wa Binamu.]Wamesema nini kumhusu Saidi?”Aliuliza Hamza.
“Sir tabia za watu wa binamu zinashangaza sana. Nilipowauliza kuhusu Saidi waliishia kunionyeshea ‘dole la kati’ na kukata mawasiliano”Aliongea Sally na kumfanya Hamza kukunja sura.
“Hawawezi kutoa taarifa hao bila kuwa na bargaining chip. Tutafute tu njia nyingine. Si umesema kuna njia tatu wewe? Niambie njia ya pili”
“Njia ya pili ni kuomba msaada kitengo cha Malibu kuagiza watu wao kufanya upelelezi . Kwa hadhi yako na uwepo wa Himidu, nina uhakika watakubali ombi lako”
“Nakataa! Teknolojia ambayo Saidi ameifanikisha ni hatari mno. Kama Malibu wakijua kuhusu hilo sio tu kwamba hawatomuua lakini pia watampa ulinzi. Mbele ya nchi ndogo kama hii ambayo inajitafuta katika nyanja ya teknolojia hakuna zuri wala baya mbele ya mteknolojia wao wanachoangalia ni namna ya kufaidika”Aliongea Hamza.
Hamza alikuwa ashaamua tokea mwanzo kutowahusisha Malibu katika swala hilo maana kama wakijua wataanza kumlinda kama hazina ya taifa na ingekuwa ngumu kudili nae.
“Basi tutumie njia ya tatu ila itachukuwa muda kidogo . Niruhusu majasusi wetu kuzamia Tanzania kupitia baharini na Manowari yetu ya teknolojia ya Baffold chini ya Asimuntis, nina uhakika wataweza kupata viashiria vya mahali alipojificha ndani ya masaa ishirini na nne”Aliongea Sally.
“Kuhusu hilo nakataa pia . Umeona tu namna ilivyokuwa hatari kuingiza walinzi wanne ndanii ya Tanzania. Nina uhakika ikitokea Malibu wakajua nimeingiza watu kutoka Kisiwa Toharani hawatoacha kunishika mkia na kutaka kunikausha damu”Aliongea Hamza.
“Sir kwa hazi yako kuna ulazima wa kuogopa kitengo kidogo namna hicho cha daraja A?”Aliongea Sally na kumfanya Hamza kukunja sura kwa uchungu.
Mara nyingi Sally akikasirika sauti yake inatoka kuwa yenye usiriasi na kuwa ya kitoto.Lakini hata hivyo ilieleweka kwa mazingira ambayo Sally amekulia na damu yake ya urithi ni ngumu sana kuheshimu kitengo cha taifa dogo kama la Tanzania.
“Sally usipaniki. Ninachohofia sio Malibu lakini watu waliopo nyuma yake, kwanza ndio nimegundua sasa hivi wana ushirikiano na viumbe wa damu ya Phoenix. Nchi ndogo lakini maji yake ni ya kina kirefu ndio maana nakuwa makini nisije kuzama. Si hata wewe pia ulisikia ule uvumi unaondelea kwenye ulimwengu wa giza?”.
“Unamaanisha kuhusu mshindi wa Vita ya Miungu?”Aliuliza Sally na Hamza kuitikia.
“Ndio kwanza nimetoka kupambana na Nyakasura , ingawa nimefanikiwa kumshinda lakini sitaki kuhatarisha maisha yangu tena na mbaya bado sijajua nani ana nguvu zaidi licha ya kushinda kati yangu na wenzake. Nimesikia Nyakasura baba yakae ni mtu ambae anajua kumdhibiti kama mtu huyo yupo si maana yake ana nguvu kumzidi Nyakasura?, Swali lingine nimeishi katika mataifa mengi lakini kwa mara ya kwanza ni hapa Tanzania kitengo cha Malibu bila wasiwasi kilianza kuniwekea masharti ya ajabu ajabu bila hofu. Kuna kitu kinaniambia kuna nguvu ambayo haionekani ila inalipa nguvu jeshi la Tanzania na pengine ni nguvu ambayo pia ina uhusiano wa karibu na Mzee”Aliongea Hamza.
Inawezekana Hamza hakuonekana kama mtu ambae alikuwa akichukua hatua juu ya misheni iliomfikisha nchni , lakini ukweli alijua uwepo wake nchini tu inatosha kumpa majibu kama ambavyo ilitokea tu akapigana na Nyakasura.
Licha ya kwamba hakujitangaza juu ya uwezo wake , lakini sifa zake pekee zilitosha kujitangaza na watu aina ya Nyakasura ndio watu pekee ambao wanajua mambo mengi kutokana na kushi muda mrefu, hivyo alijua lazima watataka kujitokeza tu kumpima na majibu yake yataanza kujibika taratibu taratibu , lakini hata hivyo hakutaka kulipa gharama kubwa katika kuyajua majibu.
Kulikuwa na kila uzushi katika ulimwengu wa siri uliokuwa ukizungumzia mambo mengi , ikiwemo uwepo wa watu wenye umri mrefu sana , uwepo wa viumbe wasionekana kama vile Night walkers au Night Shadows na mengineyo mengi.
Mfano tu alianza kusikia kuhusu jiina la Nyakasura miaka sita iliopita na wakati habari hizo anazisikia ilikuwa ni kama uzushi lakini mara baada ya kuja Tanzania na kumuona ana kwa ana , aliamini pengine simulizi nyingi alizosikia kuhusu ulimwengu wa siri zipo kweli, pengine watu walioishi karne ndani ya dunia hii licha ya kujalisha ni binadamu au viumbe wa jamii nyingine yote hayo yanaweza kuwa kweli.
Hamza ashawahi kusikia hata uwepo wa wenye damu ya Ki-Malaika wanaishi duniani lakini hakuwahi kuamini kama ni kweli. Kwa habari alizosikia likija swala la mapigano ilisemekana ni aina ya viumbe ambao uwezo wao ni kukaribiana na ule wa aliewaumba. Sio malaika tu bali alisikia uwepo wa viumbe jamii ya majini na jamii nyingine nyingi.
“Sir kama kweli yanayovumuishwa katika ulimwengu wa siri yapo , unapaswa kuwa makini sana , lakini utkija kuhusu hili swala la Saidi njia zote tatu zimeonekana kutokuwa sahihi , tunampataje sasa?”Aliuliza.
“Nimekumbuka kuna mwanasayansi nguli hapa nchini?”
“Unamlenga Sajenti Yulia?”
“Umejuaje?”Aliuliza Sally kwa mshangao.
Hamza muda huo ndio aliamini mtu ambae anaweza kumsaidia kumpata Saidi ni Yulia. Alijiambia kama mwanamke huyo alikuwa na uwezo wa kutafuta mpaka Manowari ya jeshi la Marekani anashindwaje kumpata Saidi.
“Nafuatilia kwa umakini wanawake wote wanaokuzunguka . Ukweli tokea nimjue Yulia nimeona anafaa zaidi kuwa mke wako kuliko Regina , ana busara na akili nyingi”Aliongea Sally na kumfanya Hamza kukunja sura asijue acheke ama alie.
“Sally kuhusu maswala ya hisia zangu binafsi sitaki ushauri , maswala ya mapenzi unafananisha vipi na akili ya mtu”
“Mh! Kwa upembuzi wangu bila kuweka hisia ukiachana na Regina kujua biashara lakini hakuna kitu kingine anachojua , ni mtu wa kubadilika badilika , hashikiki na hajui kuangalia mambo kwa ukubwa wa picha yake. Hakufai kabisa”
“Kimya wewe ! Sipo tayari kuona unamwongelea mke wangu vibaya , ndio najua ana madhaifu yake lakini hakuna aliekamilika . Nimetokea kumpenda, hivyo nipo tayari pia kuyapokea madhaifu yake . Sally hujawahi kupenda ndio maana, hivyo kabla ya kupata uzoefu usije ongelea hii mada tena , Nitakasirika”
“Kwahio unasema simfikii Regina kwa chochote . Sidhani kama kuna mwanamke mrembo duniani kunizidi mimi na ninachoweza kukufanyia mimi hawezi milele”Aliongea na kumfanya Hamza kukuna kichwa.
“Sally , wewe ni kweli ni mrembo sana kwenye ulimwengu huu na ni watu wachache sana wa kuweza kupinga hilo lakini kwenye macho yangu utaishia kubakia kama Prisila . nyie ni wadogo zangu wa kike. Hivyo usiongee upuuzi tena”.
“Wewe ndio mfalme, Mimi ni nani hata nipinge”Aliongea Sally katika sauti ya uchungu.
Hamza alimjua vizuri Sally , hivyo hakuwa na muda wa kuendelea kubishana nae na kukata simu palepale na kisha aliitafuta namba ya Yulia na kumpigia.
Upande wa pili kwa Yulia alionekana kama vile alikuwa kwenye sherehe na alichelewa kuongea baada ya kupokea simu ikioneakna alisogea katika eneo lenye utulivu.
“Wewe unataka nini? Nipo kwenye sherehe sina muda”
“Babe Yulia acha hizo kuna kitu nataka unisaidie, Kuna mtu ni mjanja sana na watu wengi wamejaribu kumtafuta lakini wameshindwa. Kwa akili zako naamini utafanikisha”Aliongea Hamza akimpamba.
“Acha porojo, Nani unamtafuta”Aliongea Yulia akionekana yupo kwenye mudi mbaya.
“Saidi”
“Nini! Si amekufa?”
“Hajafa , yupo hai tena hapa nchni , ametengeneza hadi roboti la kibailojia linalofanana na mimi kwa ajili ya kuwadhuru watu wangu . Sasa wewe ndio uniambie mtu wa aina hii unadhani ni hatari kiasi gani akiruhusiwa kuendelea kubakia uraiani. Unaonaje ukinisaidia ?”
“Mh! Siku ile nilikuomba ukae na mimi usiku lakini ukaniacha kwasababu ya Regina . Kwasababu unamthamini sana mwambia akusaidie na usinisumbue”
“Hayo yanatokea wapi , Regina anajuaje kumtafuta mtu?”Aliuliza Hamza akiwa katika hali ya uchungu wa maneno ya wivu kutoka kwa Yulia.
“Kwahio ukiwa na shida ndio unanitafuta ila ukiwa huna shida mkeo ndio muhimu. Nenda kaendelee kumdanganya Regina ila sio mimi , unadhani mimi Yulia ni mwepesi mwepesi eh? Huyo Saidi wako kama anao uwezo kweli anisogelee , nitamuua mwenyewe. Kwaheri Sitaki usumbufu niko bize”Baada ya hapo alikata simu.
Hamza alijikuta akikuna kichwa huku akichezesha ulimi , alijiambia laiti angekuwa anajua Yulia ni mwanamke mwenye wivu namna hio asingemgusa tokea mwanzo.
Muda ule wakati akijiuliza ni hatua gani nyingine ya kuchukuwa, simu yake ilitoa ishara ya ujumbe kuingia na baada ya kuusoma aliona ulitoka kwa Yulia.
“Ndani ya nusu saa tukutane Kunduchi , nijie na kahawa yenye maziwa takeaway kubwa ”
Hamza mara baada ya kusoma ujumbe huo a alijikuta akicheka kwa uchungu .Alijua mwanamke huyo hata awe na wivu kiasi gani hawezi kumkatili . Lakini swala gumu, muda huo ulikuwa tayari ni usiku na kuanza kutafuta Kahawa ya Maziwa ilikuwa kasheshe.
Hamza hakutaka kupoteza muda baada ya kuingia katika mgahawa maarufu aliweza kufanikisha kupata alichoagizwa na haraka sana alianza safari ya kuelekea Kunduchi kwenye hoteli inayomilikiwa na Yulia.
Haikuwa mara yake ya kwanza kufika katika hoteli hio , mara ya mwisho alifika hapo akiwa na Prisila na ndio siku ya kwanza alioweza kukutana na Saidi.
Mara baada ya kufika tu gari nyingine aina ya Bentley iliingia na kwenda kusimama karibu na mlango. Yulia aliekuwa amevalia koti la Channel ambalo halijafungwa vifungo na kufanya kijisweta cha rangi nyeupe kuoekana kwa ndani alishuka.
Alikuwa amevalia pia cheni ya Polaroid yenye kishaufu cha madini ya Almasi.
“Bosi Yulia!!”Kitendo cha kushuka kutoka kwenye gari kundi la wafanyakazi walikimbilia nje kumpokea.
Yulia aliishia kuitikia kwa kichwa bila kuzingatia sana , alikuwa ashazoea na alitembea mpaka aliposimama Hamza na kumpokea kahawa yake bila hata ya kumwangalia usoni na kisha akampita.
Hamza aliishia kufuata nyuma nyuma huku akiwa na mwonekano wa kumshangaa.
“Tajiri Yulia tunafanya nini kwenye hili eneo , si nilisema unisaidie kumtafuta mtu?”Aliongea Hamza.
“Nifuate acha kelele”Aliongea huku akiingia kwenye lift na Hamza aliishia kufuata kimya kimya na kuja kuingia katika chumba ambacho kilionekana kuwa kama ofisi kutokana na wingi wa vitabu.
Yulia alisogea mpaka kwenye meza ndani mule na kisha alianza kuzungusha tufe la ramani ya dunia kwa staili ya aina yake kwa sekunde kadhaa, palepale moja ya shelfu ya vitabu ilionekana kuachia na kutengeneza mlango uliokuwa na Password.
Yulia alisogelea mlango ule na kisha aliingiza pasword na baada ya kufanikiwa aliambiwa aweke kiganja cha mkono akafanya hivyo na kisha palepale kitaa kiliwaka na kuambiwa aweke sura yake vizuri na hatimae mlango ukafunguka.
Hamza alishindwa kujizuia na kuishia kushangaa . Hakuamini kwenye jengo hilo la club Yulia alikuwa na maabara yake.
“Hebu ingia acha kuonekana kama mjinga , unashangaa nini sasa?”Aliongea kwa kufoka na Hamza hakukasirika zaidi ya kujichekesha na kuingia ndani ya maabara hio.
Kitendo cha kuingia tu taa za eneo hilo ziliwaka. Ilikuwa ni maabara kubwa ya saizi ya kati iliosheheni skrini nyingi za monitor na baadhi ya vifaa ambavyo Hamza hakuvifahamu . Ilikuwa ikipendezesha macho sana.
Yulia aliweka kile kikombe cha takeway cha kawaha chini na kisha alisogelea Control panel.
“Ni lini Saidi alirudi Tanzania?”Aliuliza Yulia na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.
“Kama miezi miwili iliopita hivi”
“Amekutumia maroboti mangapi?”Aliuliza na swali lile lilimsahngaza Hamza.
“Yulia unapanga kweli kumtafuta , mbona kama maswali yako hayahusiani na kumtafuta?”
“Nitakuelezera mara moja tu na sitorudia hivyo sikiliza kwa umakini. Kama Saidi ametengeneza haya maroboti hapa Tanzania au kama anaendelea atakuwa na matumizi makubwa ya umeme . Siku zote maabara za kisayansi zinatumia umeme mwingi , najua kuna maabara kadhaa ndani ya Dar lakini nitaangalia eneo ambalo kuna mambadiliko makubwa ya matumizi ya umeme kwanzia miezi miwili iliopita. Pili anahitaji madini adimu kwa ajili ya kuundia haya maroboti na najua lazima atakuwa amenunua kwa njia zisizo rasmi . This wasn't a Barbie doll, it was a bionic robot.
Kama tukigeuza vyanzo vya nishati na malighafi kuwa data na kutengeneza Parameter za kitaarifa , tutaweza kukadilia eneo alipo ..”Aliongea Yulia na kumfanya Hamza kupagawa.
“Kwahio unasema una mfumo wa kuweza kujua hizo taarifa hapa ndani?”
“Mbona una maswali mengi sana . Nina njia zangu”Aliongea Yulia na kumfanya Hamza kujionea aibu na kumjibu maswali yake yote.
Yulia alionekana kuandika programu kulingana na maelezo ya Hamza na ndani ya dakika chache tu skriini zilianza kuonyesha michoro mbalimbali ya Data Analysis na kidukuzi maalumu kilianza kufanya kazi yake.
Yulia alikaa kwenye kiti cha mzunguko huku akinywa kahawa yake taratibu , huku miguu akiwa ameipandisha juu ya meza na kufanya kigauni chake kuacha mapaja wazi.
“Kaa na usubiri tutaweza kupata majibu ndani ya nusu saa . Kama tusipompata basi pengine kutakuwa na tatizo na majibu ulionipatia au Saidi ana IQ kubwa kuliko ninavyompimia”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa tu lakini muda wote alikuwa akiangalia miguu ya Yulia iliononona juu ya meza.
Yulia aligundua Hamza alikuwa akikodolea miguu yake na palepale macho yake yalibadilika na kuwa ya dhihaka.
“Vipi unataka kuigusa?”Aliuliza na Hamza hakujivunga kwani alitingisha kichwa kukubali . Ijapokuwa walikuwa bize muda huo lakini aliona hata kama mtu yupo bize vipi anapaswa kujipa breki fupi.
“Unadhani ni rahisi hivyo?”
“Nitakununulia kahawa nyingine”
“Unaniona mtoto wa miaka mitatu? Ninachotaka ni kunipatia tafiti zote za Saidi baada ya kumpata”
Hamza aliishia kutabasamu kwa uchnngu , ni kama alivyotarajia kwa mwanasayansi kujali zaidi kuhusu tafiti.
“Kwanza uliniambia utanifanya niwe kiongozi wa familia ya Wanyika , lakini sioni maendeleo yoyote. Ila sasa hivi nakuambia unisaidie kupata tafiti zake unaona nimeomba kitu kikubwa, au unataka tu mimi niwe na manufaa kwako lakini mimi sipati manufaa yoyote . Umekaa muongo muongo tu . Kama huwezi kunioa basi nionyeshe hata manufaa ya kuendelea na wewe na sio kucheza na hisia za mwanamke mpole kama mimi”
“Sawa nitakupatia , ila uniahidi tu hutokabidhi tafiti hizo serikalini”Aliongea Hamza akiamini atajua maana yake kwanini hataki zitue kwenye mikono ya serikali.
Yulia alionekana kuridhishwa na jibu hilo na alichia tabasamu na kujiegamiza zaidi kwa Hamza huku akizidi kukaa kihasara.
“Kwahio umesema unataka kuigusa tu au na kuinyonya kabisa?”Aliongea huku akifanya hila za kumpagawisha Hamza.
SEHEMU YA 171.
Hamza karika mambo kama hayo ya kutegwa hajawahi kuwa mzembe kabisa , kwani palepale bila ya kuongea neno alisogea na kumbeba juu juu na kumuweka kwenye meza.
“Ah! Wewe niache..”
“Tratata..”
Sauti ya kuchanika kwa nguo ya ndani ilisikika kwa nyuma na kumfanya mrembo huyo kuanza kutetema.
“Hehe.. unanitega namna hio unadhani ningefanya nini, umenileta hapa ukiwa na malengo ya hili kukutokea , sina namna kukamilisha mipango yako”Aliongea Hamza akimnong’oneza kwa kumpulizia pumzi ya masikio.
“Wewe niache ..”Yulia alikuwa nataka sitaki huku sura yake ikiwa imeiva ., ukweli hakujua hata kwanini anasema aachiwe ilihali kwenye moyo wake licha ya kuona Hamza anatumia nguvu lakini alikuwa akitegemea pigo za kuridhisha.
Wakati data zikicheza kwenye skrini kumtafuta Saidi upande wa Yulia na Hamza walikuwa wakiyatafuta magoli kwa kubadilisha mikao.
Baada ya kidukuzi kusimama Hamza aliona na palepale alimwachia Yulia na kwenda kusimama upande uliokuwa ukionyesha kidoti cha rangi nyekundu.
Yulia miguu ilikuwa imekufa gazi wakati akiwa amchanuliwa kwenye kiti na alihisi kizunguzungu.
Hamza upande wake aliishia kuvaa suruali yake vizuri huku macho akiwa ameyakazia kwenye skrini na palepale picha za satilaiti zilionyesha mazingira kuzunguka eneo lililowekewa alama.
“Hilo eneo mbona ni la makazi ya watu , kuna uwezekano wa kuwepo kwa maabara hapo?”Aliuliza Hamza.
“Sehemu ambayo huwezi kufikiria ndio mahali salama kwake, unapaswa kuharakisha . Nina uhakika Saidi anajiandaa kuhama , ukichelewa kidogo tu na akamaliza kukusanya kila kitu chake utakuta peupe”Aliongea Yulia kivivu.
Hamza palepale aligeuka na kisha alimshika Yulia kidevu na kumpa french kiss kwa sekunde kadhaa na kumwachia huku akiwa na tabasamu.
“Babe Yuli ,Asanate sana … mimi naondoka”
Mara baada ya kuongea hivyo hakuangalia nyuma kabisa na kupotelea nje ya maabra hio.
Yulia aliishia kushika lipsi zake zilizopigwa busu na mwonekano wake ilikuwa ngumu kuelezea.
Nje kidogo ya jiji la Dar es salaam , Mtaa maarufu wa Kwa Mzee Mkulima ndani ya kambi ya muda mfupi ya Saidi alionekana Lamla.
“Master kwani kuna haja ya kuondoka , si tumefuta viashiria vyote?”Aliuliza Lamla akimwangalia Saidi ambaye alikuwa akihangaika kulia na kushoto akikusanya baadhi ya vifaa vyake muhimu.
Ijapokuwa aliona ni hasara kuacha baadhi ya vifaa vikubwa vya glasi , lakini hata hivyo aliona sio muda wa kujali , angenunua popote pale atakapo anzisha maskani mpya.
Vitu pekee ambavyo hakutaka kupoteza ni vile ambavyo vingemsaidia kuendeleza kutengeneza maboroboti ya kibailojia.
Baadhi ya watu ambao walikuwa ni waajiriwa wake , muda huo alikuwa amewageuza misukule yenye nguvu kubwa kwa kuwalisha Tone la Ukombozi na ndio waliokuwa wakihangaika kutoa msaada wa kubeba vitu vizito.
Muda huo alikuwa bize kutoa maelekezo kwa watu hao wakati akisikia swali la Laml;a na alikasirishwa na swali lile na bila kujiuliza mara mbili mbili aligeuka na kumchapa kibao kwa hasira.
Kibao kile kilikuwa kikubwa kiasi cha kumdondocha chini Lamla huku akishika sura yake kwa kutetemeka.
“Master samahani nimekosea , sikupaswa kuuliza maswali mengi”
“Unajua nini wewe mjinga! Kama Hamza ameweza kujilinda yeye na watu wake unajuaje kama hana uwezo wa kunitafuta na kunifikia kwa urahisi. Unataka niendelee kukaa hapa kubetia usalama wanagu, kama umepapenda sana baki ila mimi naondoka”
Lamla uso wake ulikuwa katika hali ya uchungu mkubwa wakati akiangalia kipande cha lopi ya binadamu ambayo haijakamilika na alihisi uchungu kuiacha kazi hio hapo ikaja haribiwa.
“Lakini Master vipi kuhusu Frank…”
Alikuwa akiulizia kuhusu roboti la kibailojia ambalo ujenzi wake ulishia kwenye kichwa na kifua tu ambalo kila kitu sura yake ilikuwa ni kama ya Frank marehemu mwanae.
Mpango wa Saidi kutaka kumuunda Frank feki ni kwa ajili ya kutimiza hatua ya pili ya mpango wake. Lakini kutokana na mpango wa awali kufeli Saidi hakuwa na muda wa kummalizia kumtengeneza.
“Huyo sio mwanao ni feki , siku ile kule Australia nilishindwa kukopi kumbukumbu zake vizuri , hivyo hata kama nikimaliza kumtengeneza hatoweza kukumbuka kama mama yake”Aliongea Saidi kwa hali ya kumkejeli na kumfanya Lamla machozi kumtoka.
“Lakini hata kama awe feki , vinasaba vyake vitakuwa sawa na vya kwangu na baba yake hivyo atakuwa bado ni Frank kwanini nisijali?. Ndoto yangu ni Frank kurudi tena na kuwa hai , hata kama hatonifahamu angalau ata bakia kuwa ndugu yangu wa damu..”
“Wewe mpuuzi , kwanini kila siku zinavyoenda unazidi kuwa mjinga . Ukiendelea kunililia nitakuacha hapa hapa Hamza akukutea akuue. Unadhani nakujali sana . Mimi Master wako nitaenda nje tu huko na kukuokota mwanamke mwingine wa kunituliza hamu zangu”
Mara baada ya kuongea alimchapa tena kibao na kumfanya atoe kilio cha maumivu huku damu zikimtoka puani.
Lamla alikuwa akitia huruma , kulikuwa na hali ya kukata tamaa kwenye macho yake na aliishia kunyamaza huku akipaliwa na mate yake mwenyewe na kuanza kumsaidia Saidi kukusanya vitu ili waondoke pamoja.
Lakini sasa sekunde hio hio waliweza kusikia kishindo kizito kutoka nje ya maabara kama vile kuna mlipuko umetokea
“Tii! Tiiii Bang !”
Kishindo hicho kilimshitua mno Saidi na haraka sana alikimbia kutoka nje na ndipo alipoweza kuona msukule wake akikimbilia kuingia ndani.
“Arghhhhh! Bosi kuwa makini tumevamiwa….”Aliongea yule mfanyakazi wake na kumfanya Saidi kumwanglia kwa shauku.
“Kuna nini kinachoendelea huko nje?”Aliuliza akimwangalia mfanyakazi wake huyo ambae alionekana nguvu kumuishia kutokana na kupigwa. Lakini kabla hajajibiwa aliweza kusikia sauti aliokuwa akiifahamu.
“Saidi unaonekana kuwa mjanja mno kwenye kujificha”Aliongea Hamza akiingia katika eneo hilo na sigara mdomoni alimwangalia Saidi kwa macho ya ukauzu.
Hamza mara baada ya macho yake kutua katika sura ya Lamla alijikuta akishangaa kidogo lakini sio kwa sana . Alijua lazima aliokolewa na Saidi baada ya kushambulia maharamia wa The Shark.
Muda huo Lamla alimwangalia Hamza kwa macho ya kujikatia tamaa , hakuwa na woga wala hofu aliishia tu kukaa chini kama sanamu.
“Hamza umepajuaje hapa?”Aliuliza Saidi lakini Hamza hakwa na muda wa kuelezea.
“Gari lako ulilopanga kuondoka nalo nishaliharibu. Kama unataka kuhama naomba nikwambie itakuwa ngumu”
Saidi mara baada ya kuona hakukuwa na namna ya kukimbia tena alichokfianya ni kurudi haraka ndani ya maabara na kisha alichukua chupa ya kemikali ya Sulphuric acid na kumrushia Hamza, lakini Hamza aliweza kukwepa tindikali ile na badala yake ilivaa moja ya watu wake na kumfanya aanze kuungua palepale huku akitoa ukulele.
Hamza hakutaka kumsubiria Saidi kufanya shambulizi la pili na palepale alimsogelea na kumkaba shingo yake.
Licha ya Saidi kuutengeneza mwili wake kuwa na nguvu lakini ilikuwa ngumu kushindana na Hamza.
“Nilishakupa nafasi ya kuanza maisha mapya upya . lakini kwa bahati mbaya naona husameheki. Hivyo usinilaumu kwa mimi mtu mwenye uwezo finyu kufikiria kukudhuru”
“Sio kosa langu , Wenye makosa ni walenzi wangu waliokuwa na roho mbaya na kunitesa mpaka nafsi yangu ikabadilika na kuwa ya mnyama. Hivi unajua ni kwa kiasi gani niliteseka?” Alijitetea
“Tokea mwanzo mpaka sasa macho yako yanaona watu waliokufanyia ubaya . Kwenye ulimwengu wako hakuna mtu mzuti kabisa ni ulimwengu usio na jua .Naelewa kuhusu maumivu yako kwasababu nimekwisha yapitia lakini kwa bahati nzuri niliokolewa ndani ya muda na ndio maana niliamua kufumbia macho kile unachokifanya lakini bado hukunielewa , Hivyo sina jinsi zaidi ya kukuua ili nilinde watu ninao wapenda”Aliongea Hamza na hakutaka kuongea tena kwani palepale alikaza mkono wake akitaka kumvunja Saidi shingo . Lakini sasa ile anataka kuivunja Hamza aligundua kuna kitu hakipo sawa.
“Nakuchukia nakuchukia.. nakuchukia”Saidi aliongea kwa sauti huku shingo yake ikijizungusha.
Hamza palepale alijikuta akili yake ikifanya kazi , Saidi aliekuwa mbele yake sio halisi bali ni roboti pia. Hamza aliishia kukaza mkono wake na palepale aliweza kuona vyuma ndani ya shingo yake.
Lamla mara baada ya kuona jambo hilo alijikuta akishangaa mno kiasi cha kuziba mdomo wake.
“Ime.. imekuwaje ..”
Hamza aliishia kuangalia mazingira yote ya maabara hio lakini bado hakuona kitu.
“Damn it!”
Hamza alijikuta akishikwa na Hasira na kuipiga ngumi meza na kuiharibu palepale . Alimchukulia Saidi poa ila kumbe alionekana kuwa na akili nyingi sana na kumfanya asimpate kwa mara ya pili pale ambapo aliona amemkamata.
Hamza aliishia kutembea kivivu akimsogelea Lamla.
“Niambie ni wapi amehamia au niambie tu ni wapi mwili wake halisi kauhifadhi?”
Lamla aliishia kurudi kutoka katika mshituko na aliishia kutingisha kichwa chake haraka sana akikataa.
“Sijui chochote… siku zote niliamini Saidi niliekuwa nae ni halisi ..”Aliongea kwa kutetemeka.
Kwa namna tu Lamla alivyokuwa akiongea ilionekana ni dhahiri hakuwa akidanganya.
“Mpango wake ulikuwa ni upi?”
“Mpango wake ni huu uliofeli , kuna haja ya kukuelezea tena?”
“Nikiuliza swali jibu swali”Aliongea Hamza akiwa siriasi.
“Siongei chochote , kama unaniua wewe nimalize tu…”Hamza aliishia tu kumwangalia mwanamke huyo.
“Siwezi kuuwa mtu ambae amekwisha kufa tayari”
Mara baada ya kuongea hivyo aligeuka na kuzisogelea tarakishi , mpango wake ukiwa ni kutaka kukopi kila kitu ili akampatie Yulia. Bahati nzuri ni kwamba mfumo wake haukuwa mgumu kuelewa kama ilivyokuwa mfumo wa Yulia.
Kwasababu alikuwa amemwahidi, hata kama alikuwa akijilazimisha aliona afanye hivyo.
Lamla alikuwa katika mshangao , hakuamini Hamza amemuacha hai.
“Hamza acha kuigiza , mimi ndio niliemuua Wilsoni .Ni mimi pia niliepanga kuwadhuru wewe na Regina . Inamaana hunichukii?”Aliongea na kumfanya Hamza kugeuka.
“Kukuchukia ni kujichosha na ni matumizi mabaya ya hisia”Mara baada ya kuongea hivyo aliendelea na kile alichokuwa akifanya .
Baada ya kumaliza alichomoa hard drive na kujiandaa kuondoka . Lamla mara baada ya kuona Hamza anaondoka alimsimamisha.
“Hebu subiri!!”
“Kuna nini kingine unachotaka , kama unataka kufa jimalize mwenyewe sitaki nuksi”
“Saidi bado yupo hai na mpango wake ni kuwatengenezea kopi wapenzi wako wote na kisha kukuua baada ya kuonyesha udhaifu. Baada ya hapo anapanga kulipiza kisasi kwa kuwageuza misukule. Kasema pia anapanga kumfufua Frank ili afanye vitendo vya kumchafua Regina . Anapanga kukufanya wewe na Regina kufanya mapenzi na maroboti yake ..”
Hamza mara baada ya kusikia hivyo jasho la baridi lilimtoka . Aliona Saidi alikuwa amedhamiria kweli kumfanya asiwe na amani.
“Najua hivyo tu . Nenda kamwambie Regina awe makini . Kama Saidi akijitokeza asije kuingia mtegoni ..”Aliongea Lamla na kumfanya Hamza kukunja sura.
“Kwanini unaniambia hayo yote?”
“Ijapokuwa nawachukia lakini namchukia Saidi zaidi kwa kumuua mtoto wangu”
Hamza alitingisha kichwa na kuonekana kusita kidogo na kisha alisogea na kumbeba Lamla.
“Unafanya nini?”
Hamza alimwaga kemikali chini na kisha alitupia sigara kwenye ile kemikali na moto ulianza kuwaka.
“Huwezi kuendelea kukaa hapa nitakutoa nje”Aliongea Hamza na muda ule ndio Lamla alijua Hamza alipanga kuunguza kila tafiti ya Saidi na miili iliokuwepo humo ndani ili asimpe nafasi ya kutengeneza maroboti.
Baada ya kuangalia sura ya Frank feki ikiungua alijikuta akianza kulia tena.
Hamza alimtoa Lamla mpaka nje ya nyumba na kumuweka pembeni.
“Mimi naondoka kama unataka kuendelea kuishi ni wewe kama unataka kufa ni wewe ila isije tokea ukamsumbua Regina”
“Nitaanzaje kumsumbua. Nina uhakika sekunde atakayoniona atataka kuniua”Aliongea kinyonge.
Hamza wala hakutaka kuendelea kumsikiliza na palepale alipotea katika eneo hilo.
Kwasababu hakuweza kumkamata Saidi katika mwili wake halisi alijiambia anapaswa kuwa makini sana na ulinzi. Hivyo mpango wake ilikuwa ni kurudi alikomuacha Yulia ili kufikiria namna ya kudili na suala hilo.
Hamza mara baada ya kurudi hotelini aliambiwa Yulia alikuwa akioga na aliruhisiwa kuingia bila ya kuzuiwa na wafanyhakazi kutokana na ukaribu wake na Yulia
“Unafanya nini . Hujui kugonga mlango!?”Yulia alishituka mara baada ya mtu kuingia ndani kwake kwenye jakuzi ila alitulia baada ya kugundua ni Hamza.
Kwa jinsi mrembo huyo ngozi yake ilivyokuwa laini alijiambia ingekuwa siku ya kawaida asingempa hata nafasi ya kukauka na kumvamia juu juu.
“Taarifa ulizotaka hizi hapa”Aliongea Hamza akiweka Hard drive mezani “Saidi kaacha roboti la sura yake ndani ya maabara na yeye kakimbia”Aliongea Hamza.
“Nini! Najikuta naanza kumkubali huyu Saidi . Anatumia akili sana na namna ya kuendelea kujiweka hai ina ufanisi mzuri”Aliongea Yulia huku akicheka.
“Unacheka nini sasa . Siku moja utashangaa bodigadi wako ni roboti la Saidi. Utaweza kuzuia asikuue?”
“Wasiwasi wa nini sana. Saidi hawezi kutoroka nina njia nyingi za kumpata”
“Kumbe! Njia ngani hizo au unazungumzia bado ule mfumo wako wa kusearch?”
“Hapana , nina njia ya moja kwa moja”Aliongea Yulia akisimama kutoka kwenye jakuzi na kuchukua taulo jeupe na kujisitiri na kisha alitembea kwa maringo kabisa mpaka kwenye meza na kuchukua ile Harddrive.
“Ukweli ni kwamba mwaka jana nilifanikiwa kutengeneza mfumo wa akili bandia kupitia Nanotechnology. Mfumo huu unao uwezo wa kumtafuta mtu kupitia vinasaba ya damu yake pekee na kuonyesha eneo alipo. Nimeunyumbulisha katika vidukuzi vidogo vidogo ili kurahisisha utafutaji na kwa DNA zake ninaweza kumpata ndani ya saa ishirini na nne .Hata kama Saidi amefanikiwa kutoka nje ya Dar es salaam . Nina uhakika bado hatosafiri kwenda nje ya nchi na atajichimbia mikoani huko.
Uzuri ni kwamba DNA zake ziliingizwa kwenye mfumo na wafanyakazi wake hivyo haitokuwa ngumu.
Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo ya Yulia alijikuta akiwa katika hali ya bumbuwazi.
“Kwahio una mfumo wa aina hio pia? Ni teknolojia ulioitoa kwenye Earth Axis nini?”
“Ndio. Unadhani kama sio uwezo wangu wa kuifanyia utafiti , ningewezaje kutengeneza teknolojia ya ajabu kama hii?”
“Kama ni hivyo kwanini usitumie hivyo viroboti vyako na kuanza kumtafuta?”
“Hio ndio kete yangu ya siri . Kwanza sina uhakika kama unaweza kunipatia kitu ninachotaka”Aliongea Yulia huku akitingisha Hardisk iliokuwa kwenye mikono yake kwa kejeli.
Hamza hakuwa na ujanja tena mpaka hatua hio na aliishia kuwa mpole huku akiona anapaswa kupiga hatua moja baada ya nyingine maana kama ni kumchezea hila imeshindikana.
Ila alijiambia saa atakayofanikisha kumkamata Saidi atamkomesha.
ITAENDELEA.