Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Singano upo vizr sana ila huyu hamza mbona anafanana character na roma??? Vitu vingi naona vinaringana na kile kitabu tulicho maliza..
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR.

SEHEMU YA 168.
Tone la Ukombozi.
Hamza mara baada ya kusikia sifa hizo kutoka kwa Himidu alijikuta akishindwa kujua acheke ama alie maana ni kama alikuwa amezidisha.
“Halafu bosi kabla sijasahau , nimekubaliana na wazee kwa niaba yako kwa ajili ya kupewa cheo cha heshima cha uchifu wa kambi ya nyoka”Aliongea Afande Himidu.
Kundi hilo la wazee wa kambi ya Nyoka wote walimwangalia Hamnza na matarajio makubwa.
“Kwanini ukubali kwa niaba yangu ikiwa hata hatujaliongelea?”Aliuliza Hamza na palepale Himidu alimsogelea Hamza karibu na kuanza kuongea kwa sauti ya chini.
“Bosi si umesema unataka kujiingiza katika familia ya Wanyika na kuazima nguvu yao hapa nchini? Licha ya kwamba familia ya Wanyika wana ushawishi mkubwa ndani ya kitengo cha Malibu lakini bado upande wa kambi za mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi hawako vizuri ndio maana wanatenga fungu kubwa sana kutoa msaada jeshini kwa ajili ya kupeleka wanajeshi nje ya nchi kwa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi. Kambi ya Nyoka ikijengwa upya na wewe ukiwa kama Chifu wa heshima moja kwa moja utakuwa na faida ya kuweza kupokelewa kwa kupewa Yulia”Aliongea Himidu kwa kirefu.
Hamza mara baada ya kusikia hivyo , aliona ilikuwa kweli kabisa . Ingawa atakuwa Chifu wa heshima kwa kambi hio maana yake wakuu wa kambi hio watamtegemea kwa ajili ya ulinzi na moja kwa moja itakuwa ni kama kuimiliki hio kambi.
“Sawa nimekubali , lakini naomba nieleweke kwenye kitu kimoja , mnitafute wakati wa kambi ikiwa shakani zidi ya usalama wake , vinginevyo sitotaka usumbufu”Aliongea Hamza. Hakutaka kuhusika na maswala ya kila siku ya kambi hio.
Baada ya mazungumzo baadhi ya wafuasi wanafunzi wa kambi hio waliokuwepo walipewa majengo ya jeshi mkoani hapo hapo Morogoro huku kambi yao ikipangwa kuanza kujengwa upya baada ya Mkuu wa jeshi kupeleka bajeti kuidhinishwa serikalini.
Baada ya mazungumzo kuisha Hamza alipanga kurudi Dar es salaam siku hio hio . Alipanga kwanza kushuka chini mjini kwa ajili ya kupata simu maana aliokuwa amefika nayo ilikuwa imeunguzwa na Nyakasura hivyo ilikuwa ngumu kuwasiliana na familia yake.
Wakati wakiangalia Hamza akitembea bila wasiwasi kushuka mlima,Afande Simba macho yake yalikuwa katika hali ya kumtafakari.
“Himidu unataka kusema miaka mitatu iliopita , alikuwa na nguvu kubwa kama hii pia?”Aliuliza mkuu wa majeshi .
“Afande nadhani itakuwa sahihi zaidi kumuuliza hilo swali Nyakasura. Kwa uwezo wangu mdogo ni ngumu kujua uwezo wote wa bosi wangu”Aliongea Himidu akionekana kujitetea
“Unajua kujitetea sana”Aliongea Afande Simba huku akimchunguza Himidu kama alikuwa akiongea ukweli, “Kama ni hivyo niambie kwa mtazamo wako unahisi wakati anapigana na Nyakasura alitumia uwezo wake wote?”
“Afande Simba haijalishi utauliza mara ngapi , sitokuwa na uwezo wa kujibu maswali yako . Ni ngumu sana kuongea..”
Jibu hilo la Himidu lilimfanya Afande Simba kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa nje.
“Nashindwa kuamini kama uwezo wake unatokana na mafunzo yake aliotunga pekee. Kuna hisia zinaniambia kuna kitu cha ajabu katika mwili wake”Aliongea
“Sina uhakika kama ni kweli mwili wa bosi una kitu cha ajabu lakini uwezo wa kuvuna nishati aliokuwa nao hapo mwanzo , ulikuwa ni wa juu mno kwa watu wa kawaida kufikia . Sina mashaka kabisa na uwezo wake wa sasa, Vinginevyo Black Emperor angekwisha kujua kama mashaka yako yana ukweli”Aliongea Himidu na kumfanya Afande Simba kutingisha kichwa akionyesha kwamba maneno ya Himidu yalikuwa na maana.
*****
Ni ndani ya jengo la Apartment ambalo linamilikuwa na baba yake Prisila , ndani ya jengo hilo ndio sehemu aliokuwa akiishi Serena na Prisila pia. Mwanzoni Serena alipaswa kwenda kuishi kwenye nyumba ya peke yake ambayo Prisila alipanga kuipangisha kwake , lakini hakupenda nyumba hio na badala yake alichagua kuishi katika Apartment.
Prisila licha ya kuwa na jumba kubwa la kifahari lakini vilevile alikuwa na Apartment yake katika jengo lao ambapo mara nyingi akichoka kuishi nyumbani hupumzika hapo.
Hivyo kuishi kwa Serena ndani ya Apartment hio iliwafanya kuwa kama majirani na katika kipindi chote cha Serena kuanza kuishi hapo , Prisila alijikuta akitumia muda mwingi kukaa katika jengo hilo la Apartment ili kuwa karibu na Serena na kuendelea kujifunza vitu vingi kutoka kwa profesa huyo.
Sasa ikiwa ni jioni ilionekana gari moja ya kifahari aina ya BMW ikiingia ndani ya maegesho ya jengo hilo na baada ya kuzimwa alishuka mwanamke mzungu na kuzipiga hatua kuzisogelea lift., Ile anafika katika lift hizo aliweza kukutana na mwanamke mwingine mrembo ambae pia alionekana kusubiria lift kufunguka.
“Prisila na wewe ndio unarudi?”Aliuliza na Prisila alitngisha kichwa.
“Umetokea Supermarket?”Aliuliza Prisila huku akiangalia mfuko ambao alikuwa ameshikilia Serena.
“Ndio, unaonaje leo tukipika chakula cha usiku na kula pamoja. Mvinyo na Nyama ya kukaanga unaonaje?”Aliuliza Serena kwa Kingereza na kumfanya Prisila kuanza kusita kidogo na kisha akakubali.
“Sawa. Asante”
“Karibu. Napenda kila ukija kulala huku tuwe tunakula pamoja , chakula cha kula mwenyewe kinachosha”Aliongea Serena na Prisila alimuunga mkono. Hata yeye pia alikuwa akichoka kupika na kula mwenywe na ndio maana tokea baba yake asafiri nje ya nchi alikuwa akila mgahawani.
Wawili hao baada ya lift kufunguka waliingia na ile mlango unataka kujifunga wafanyakazi kadhaa wa mapambo waliingia ndani ya lift hio wakiwa wamebeba vifaa.
Moja ya wafanyakazi wale baada ya lift kuanza kupanda alijikuta akivutwa nyuma na ile anajizuia asidondoke kifaa kama msumeno ndani ya mfuko ulimpitia Prisila kwenye mkono na kumkata.
“Arghhh!
Prisila alijikuta akilalama kwa maumivu. Alijikuta akiinua mkono wake na kuangalia na aliweza kuona damu ikimtoka na ndio muda huo yule fundi alishituka na kugeuka nyuma na ndio alipoweza kuona msumemo uliokuwa kwenye mfuko ulikuwa umetoboa na kuishia kumkata Prisila.
“Samahani sana Dada. Haikuwa makusudi”Aliongea yule bwana akijitetea na Prisila aliishia kutingisha kichwa.
“Usijali ..”Aliongea kwa sauti hafifu lakini yule bwana bado alionekana kuwa na wasiwasi.
“Nisamehe sana..”Aliongea na Prisila alitingisha kichwa akimwambia asiwe na wasiwasi kwani ni bahati mbaya.
“Prisila una roho nzuri mno”Aliongea Serena wakati wakitoka kwenye lift na Prisila aliishia kutabasamu na kisha kuingia kwenye apartment yake na Serena hivyo hivyo.
Prisila mara baada ya kuingia ndani aliangalia kidonda kilichokuwa kwenye mkono wake na alihisi maumivu makali na kumfanya kushikwa na wasiwasi wa kuona sehemu hio inaweza kuacha kovu.
Ilikuwa ni kawaida kwa mwanamke mrembo kama Prisila kujali sana kuhusu ngozi yake , isitoshe nguo zake nyingi hazikuwa za mikono mirefu kuziba eneo hilo.
Dakika ileile wakati akiwaza namna ya kutibu kidonda hicho , kuna wazo lilimjia , hakujua wazo hilo lilitoka wapi lakini ni kama sauti ilikuwa ikimwambia nenda kaweke kidonda hicho mbele ya moto, na baada ya kusita kidogo alijikuta akielekea jikoni na palepale aliwasha jiko la gesi na akanyoosha ule mkono ulioumia kulekea kwenye moto.
Kitendo kile kiliifanya ile miale ya moto wa gesi kuanza kupinda kama vile ilikuwa ikivutwa na sumaku na Prisila alisogeza mkono karibu na ile miale ilikivaa kile kidonda kama vile ni kuni zimemwagiwa mafuta ya taa.
Sekunde chache tu baada ya moto ule kuvamia mkono wake kile kidonda na damu vilipotea palepale bila ya kuacha hata kovu na kurudi katika hali yake ya mwanzo.
Prisila aliishia kuangalia mkono wake na mwonekano ambao haukuwa wa mshangao.
Prisila moja ya siri yake kubwa tokea akiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuchezea moto hasa akiwa jikoni , tokea kipindi hiko hakujua sababu ni nini lakini alikuwa na uwezo wa kuweka mkono wake karibu ya miale ya moto na hakuweza kuungua kabisa na badala yake ngozi ya mikono yake ilikuwa ikilainika.
Mtu pekee ambae alikuwa akijua kuhusu hilo ni Profesa Singano na Mjomba wake Hizza mkuu wa kituo cha kulelea Yatima na walimuonya asicheze na moto hata kama hakuwa akiungua na ndio aliacha kabisa na kusahau lakini baada ya ile siku kutekwa na Saidi na mwili wake kushika moto ndio siku alipojua alikuwa tofauti na vile ambavyo alifikiria na siku nyingine hisia zilikuwa zikimwambia pengine hata mama yake alimtelekeza kutokana na kutokuwa wa kawaida. Baba yake pia alikuwa akimfokea asichezee na moto kwasababu ya kutotaka aonekane sio wa kawaida.
Sasa hisia zake juu ya uwezo huo zilirudi upya na kutaka kujua maswali baada ya kukutana na Nyakasura.
“Ding Dong !”
Prisila alishitushwa na sauti ya kengere na kumfanya haraka haraka kuzima jiko na kutembea moja kwa moja kufungua mlango akidhania atakuwa ni Serena anaegonga.
“Sister Serena what ‘s wrong?”Aliuliza baada ya kufungua na kumuona Serena.
“Nimeleta vifaa vya huduma ya kwanza kwa ajili ya kukusaidia kufunga kido..”Kabla hata hajamaliza kuongea alijikuta macho yakimtoka wakati akiangalia sehemu ambayo Prisila alikuwa na jeraha.
Prisila mara baada ya kuona mshangao wa Serena alijikuta akipatwa na wasiwasi na kujiambia hakuwa makini.
“Sihitaji tena .., ukweli sikupata jeraha pale . ila asante sana Dada Serena kwa kunijali”Aliongea Prisila kwa kubabaika.
Serena alikuwa katika hali ya bumbuwazi kwa sekunde kadhaa na alijikuta akijitahidi kuondoa mshangao wake kwa kupepesa macho kwa sekunde chache na kwa namna alivyomuona Prisila aliona haina haja ya kumuuliza zaidi .
“Oh, so it's like that. I'll go back first. You can come over later. We can talk while cooking.”Aliongea akimwambia aje baadae ili waanze kupika pamoja huku wakiongea.
Prisila mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akipatwa na hali ya ahueni mno.
“Sawa ngoja nikabadili nguo kwanza”Alijibu Prisila
“Usichelewe sana”Aliongea Serena huku akigeuka huku akiwa katika mwonekano kama vile hakuona kitu cha kumshangaza kabisa.
Pengine ingekuwa ni mtu mwingine angekuwa katika hali ya maswali mengi , maana sio Serena tu alieona damu hata yule fundi alikuwa ameona damu pia ndio maana aliomba msamaha sana kwa kumkat lakini ghafla tu Prisila amepona jeraha lile.
Prisila mara baada ya kufunga mlango alijikuta akihema kwa nguvu kutokana na mapigo ya moyo kwenda spidi. Alikuwa akiogopa sana watu kujua hakuwa wa kawaida.
Muda huo huo simu yake ilianza kuita na alisogea na kuitoa kwenye mkoba wake na mara baada ya kuangalia anaepiga , aligundua ilikuwa namba mpya.
“Hello! Naongea na nani ?”Alipokea na kuuliza.
“Wewe ni Prisila Singano , Kuna mzigo wako kutoka DHL. Vipi upo nyumbani?”
“Mzigo wangu kutoka DHL! Mbona sijawahi kuagiza mzigo wa kutaka kuletewa , nadhani utakuwa umekosea ?”Aliongea Prisila akiwa katika hali ya mshangao.
“Haiwezi ikawa nimekosea. Hii ni namba yako na pia jina lako linaonekana katika hii nyaraka”Sauti ya kiume iliendela kuongea.
“Huo mzigo kabidhi kwa Mlinzi hapo getini nitashuka kuuchukua baadae”Aliongea Prisila akiamini alikuwa na marafiki wengi ndani na nje ya nchi pengine ni kweli, isitoshe ilikuwa ngumu kukosea jina na namba kwa wakati mmoja , aliona pengine ni baba yake alitaka kumpa surprise maana jana aliwasiliana ila hakumwelezea chochote kuhusu swala la mzigo.
“Samahani Dada napaswa kupata saini yako kuthibitisha umepokea mzigo”Aliongea mleta mzigo na Prisila ajifikiria na alihisi uvivu kweli wa kushuka chini.
“Basi unaweza kuja nao juu ghorofa ya nne nyumba namba kumi na tano . Mwambie mlinzi nimekuruhusu”Aliongea Prisila na kisha aliweka simu chini kusubiria kuona ni mzigo gani huo.
Dakika chache tu mleta mzigo aliwasili na Prisila alifungua mlango na aliweza kumuona mwanaume mrefu alievalia kofia kichwani na kufanya uso wake usionekane vizuri lakini alikuwa mweusi . Mkononi alikuwa na nyaraka na sakafuni bwana yule alikuwa ameweka kiboksi kilichofungwa.
Prisila hakutaka hata kuuliza jina lake ama kuona sura yake na alinyoosha mkono kuchukua karatasi ili asaini lakini sasa kitendo cha kunyoosha mkono yule bwana aliudaka na palepale aliitoa kitambaa kutoka mfuko wake wa nyuma na kwa spidi ya hali ya juu kitambaa kile kilimfikia Prisila puani.
Ijapokuwa Prisila alishituka kuhusu tukio lile , lakini alikuwa slow kwenye kufanya maamuzi na kumfanya bwana yule kumshambulia haraka. Alifurukuta kidogo tu na kisha akapoteza fahamu na yule mwanaume alimdaka na kisha alianza kuangalia kulia na kushoto na hakuchelewa alimbeba Prisila na kuingia nae ndani na kufunga mlango.
Baada ya pale alitoa simu yake na alibonyeza namba kadhaa na kisha akaweka simu ile sikioni.
“Bosi Shabaha namba moja ipo mikononi mwangu , Nahitaji maelekzo mengine”Aliongea.
“Mchukue na shuka nae mpaka kwenye maegesho ya chini na angalia utaona gari aina ya Min-van rangi nyeusi mercedenz na mwingize kisha toka nae”
“Vipi kuhusu mlinzi?”
“Atakufungulia upite bila shida yoyote. Hakikisha tu mlengwa haonekani”Aliongea.
“Sawa bosi”
“Jiamini , ukishamtoa endesha gari kupitia ramani inavyonekana kwenye hilo gari mpaka mwisho”.
“Sawa bosi”
Mwanaume yule mara baada ya kupokea yale maelekezo alimbeba Prisila na kumuweka begani na kisha alitembea nae kutoka ndani ya chumba hiko na kuzisogelea lift.
Muda huo huo kabla lift haijafunguka Serena alitoka kwenye Apartment yake akiwa amejifunga Apron.
Ile anaangalia mbele alijikuta amcho yakimtoka mara baada ya kumuona Prisila ambae hakuwa na fahamu akiwa amebebwa na mwanaume.
“Wewe ni nani?”Aliuliza Serena kwa kingereza akimsogelea upande wa lift kwa haraka.
Yule mwanaume mara baada ya kusikia sauti ya Serena aligeuka na mara baada ya kuona ni Mzungu macho yake yalionyesha hali ya ukatili na palepale alianza kutembea kumsogelea Serena.
Serena mara baada ya kuona vile haraka haraka alirudi nyuma na kukimbia kwenye Apartment yake na ile anafunga, mlango ulipigwa teke zito na lock zake zilifyatuka.
Kitendo cha lock za mlango kufyatuka ilimfanya Serena kushangaa mno. Hakutegemea mtu wa kawaida anao uwezo wa kufyatua lock hizo kwa teke moja tu.
Muda ule alipotaka kujiokoa kwa kukimbilia nje yule mwanaume alikuwa ashamuweka Prisila Chini na kumsogelea na kisha kumziba na kitambaa mdomoni kwa ustadi wa hali ya juu na kumfanya Serena kufurukuta kwa sekunde kadhaa na kupoteza fahamu palepale.
Mwanaume yule mwenye mwili wa kikakamavu alitoa simu yake na kupiga ile namba kwa mara nyingine.
“Nini tatizo?”
“Bosi kuna usumbufu umejitokeza . Kuna mwanamke wa kizungu ameniona naondoka na sasa yupo kwenye himaya yangu , nimuue?”
“Hapana namjua huyo mwanamke ni Profesa wa kigeni na anafahamiana na Hamza pia , kwasababu ushamuweka chini ya himaya yako chukua wote kisha njoo nao.”
“Sawa bosi”
Mwanaume yule hakuzubaa tena na aliwabeba wote kwa pamoja Serena na Prisila na kisha alitembea na kuingia ndani ya lift.
*****
Muda wa jioni alionekana Eliza akiingia na gari yake ndani ya jengo la Apartment za Lotusi. Mara baada ya kuingia na kutoka kwenye lift alishangaa kumuona mwanaume aliempa mgongo akiwa amesimama kando ya mlango wa kuingilia ndani kwake , mara baada ya kumwangalia mwanaume yule alishangaa.
“Hamza unafanya nini hapa , hujanipigia hata simu umejuaje leo nitakuja kulala huku?”Aliuliza kwa mshangao.
“Niliamua kukufanyia surprise , unajua akili yangu inawaza kama wewe ndio maana nilijia lazima leo utakuja kulala huku. Vipi kwani siruhusiwi kumfanyia kipenzi changu surprise?”Aliuliza huku akicheka.
“Hamna ni kwasababu nilisikia kutoka kwa Mkurugenzi kuna mahali umeenda kushughulikia tatizo , vipi umefanikiwa?”Aliuliza Eliza na Hamza alitingisha kichwa.
“Kama ningekuwa sijayamaliza ningepata muda wa kuja kukutafuta?”
“Kumbe! Vizuri sana maana makao makuu hali sio tulivu kabisa , kila mtu anapaniki kwa kile kilichotokea na imetuchukua kazi kutuliza watu wanahofia uvamizi mwingine usije tokea”Aliongea Eliza huku akitembea na kusogelea mlango na kuingiza nywira na kuufungua.
“Ingia ndani , mimi nitabadilisha haraka haraka , sijanunua mahitaji ya kupikia itakuwa vizuri tukienda kula mgahawani leo”
“Elizabeth! Kwanini usiache tu kubadilisha , nitakuchukua na kukupeleka sehemu ambayo hujawahi fika na nina uhakika utapapenda. Unaonaje?”
Eliza mara baada ya kusikia hivyo alionekana kushangaa .Muda huo akisitisha zoezi la kuvua koti la suti kwani alihisi kuna kitu hakipo sawa na palepale aligeuka na kumwangalia mwanaume huyo machoni.
“Kwanini leo ghafla tu ukaamua kuniita kwa jina langu lote ?”Aliuliza Eliza na swali lile lilimfanya Hamza kucheka.
“Si kuna muda mwingine nakuita kwa jina lako lote , kwani kuna shida nikikuita hivyo?”Aliongea.
Eliza alijikuta akiwa katika hali ya kutafakari na kisha palepale akacheka.
“Hamna tu , nimefurahi kukuona.. subiri kidogo nitabadilisha na tutaondoka haraka”Aliongea Eliza na kisha palepale alikimbilia kwenda chumbani kwake na kufunga mlango. Dakika ambayo aliingia ndani alijikuta akijiziba mdomo huku mapigo ya moyo yakienda spidi mno. Haraka sana alichukua simu yake na kupiga na palepale ilipokelewa.
“Lizzy babe tulikuwa na wazo sawa , ndio sasa hivi nimeshuka kwenye treni na ndio nataka nikupigie hapa ila naona umeniwahi .. umenimisi sana nini?”
Eliza mara baada ya kusikia sauti hio palepale maswali yake yalijibiwa moja kwa moja.
“Hamza….kuna…”
Muda huo huo mlango wa kuingia ndani kwake ulipigwa teke na ukafunguka kwa nguvu na mbele yake aliweza kuonekana Hamza akimwangalia Eliza kwa macho yaliojaa ukali wa hali ya juu.
“Leta hapa hio simu ..”Aliongea yule mwanaume huku akinyoosha mkono apatiwe simu.
Eliza licha ya kwamba alikuwa akitetemeka lakini hakutaka kumpatia ile simu na alikimbia kuzunguka kitanda huku akipiga kelele.
“Hamza kuna mtu kafanana na wewe , njoo hara.”
Kabla ya kusikia jibu la Hamza , Hamza mwingine alikuwa ashafika mbele yake na kunyakua ile simu na kisha akaipigisha kwenye ukuta.
Eliza alijikuta akikaa chini kwa hofu . akimwangalia mwanaume ambae alikuwa akifanana kwa kila kitu na mpenzi wake Hamza. Swala hilo lilimfanya kuwa katika hali ya woga usiokuwa na kifani.
“Wewe ni nani ? Kwanini unaigiza kuwa Hamza?”
“Inashangaza! Umejuaje nilikuwa feki, mwonekano wangu na sauti yangu inafanana kwa asilimia kubwa na ya Hamza , au umenifahamu kwasababu ya namna nilivyokuita jina lako ?”Aliongea yule mwanaume akirudi katika sauti yake akiacha kuigizia kuwa Hamza tena.
Hata mara moja Hamza hakuwahi kumuita kwa jina lake lote yaani Elizabeth na ndio maana aliona kuna kitu hakipo sawa na kukimbilia chumbani kumpigia simu Hamza.
Kwasababu alikuwa amempigia simu Hamza , ijapokuwa hakumwelezea kinachoendelea lakini alijua lazima ataona kuna tatizo na kuwahi kumsaidia . Kitu pekee alichopaswa kufanya muda huo ni kuvuta muda.
“Unataka kweli kujua?”Aliuliza Eliza akijitahidi kuwa katika hali ya kawaida?”
“Ndio nataka kujua ili siku nyingine niwe bora zaidi”Aliongea.
“Kwa msingi upi unataka nikuambie ilihali ulikuwa ukiigiza kuwa Hamza?”Aliuliza Eliza akijitahidi kupoteza muda na wakati huo alikuwa akiangaza macho y ake pande zote kuona kama ataweza kupata kitu cha kumsaidia kujiokoa lakini mwanaume yule alionekana kuwa na akili.
“Huna haja ya kupoteza muda . Usiponiambia haraka nitakuua hapa hapa..”Aliongea na Eliza mara baada ya kufikiria nguvu aliokuwa nayo mwanaume huyo mpaka kufyatua lock za mlango wa kuingilia chumbani kwake hofu ilimvaa palepale.
“Ni.. ni Hisia..”Aliongea
“Hisia!?”Aliuliza yule mwanaume akiwa katika hali ya mshangao.
“Unamaanisha nini kuhusu hisia?”.
“Sikuona hisia zozote za mapenzi kwenye macho yako . Kama angekuwa Hamza macho yake tu yanatosha kuniambia unanipenda lakini wewe macho yako ni makavu na yenye hali ya ukatili “Aliongea Eliza na yule mwanaume alionekana kushangaa.
“Kumbee .. Nyie wanawake ni viumbe wa ajabu sana lakini kwa bahati mbaya siamini kwenye huo ushenzi unaoitwa hisia za mapenzi”
“Umeniuliza mwenyewe na nimekujibu , siwezi kukusaidia kama huamini”
“Kama sikwamini basi usifikirie naweza kuamini kwasababu tu umejibu . Umetoa sababu ya kijinga sana”Aliongea yule mwanaume kwa kejeli.
“Najua lazima utakuwa na kinyongo na Hamza na unataka kunitumia kwa ajili ya kulipa kisasi. Lakini unadhani ukifanya hivyo utakuwa na furaha? Kama huamini katika upendo hakuna atakaekupenda . Hata kama ukifanikiwa kulipa kisasi kwa kila aliekukosea mwishoni utafaidika na nini?”Aliongea Eliza na kumfanya yule Hamza feki midomo yake kupinda vibaya.
“Kaa kimya! Usubiri saa nitakayomkata unaemwita mpenzi wako ulimi na kuutafuna ndio utajua nini maana ya furaha ya kulipa kisasi”
Mara baada ya kuongea vile yule mwanaume alitoa kitambaa na kisha alimsogelea Eliza kwa ajili ya kumzimisha.
Lakini sasa muda huo huo kivuli cha mtu kiliingia ndani ya chumba hicho kwa kasi kupitia dirishani.
“Clang!!”
Licha ya kuingia kwa kupasua kioo lakini mtu yule alifanikiwa pia kumshambulia yule mwigizaji kwa teke mpaka akadondoka chini.
Eliza dakika ile ndio fahamu zilimrejea maana tukio lilikuwa la haraka sana na alitaka kujua ni nani kaingia lakin ile anaangalia kwa umakini alijikuta akishangaa baada ya kuona ni mwanaume mwenye nywele nyeupe kabisa akiwa amevalia koti jeusi na jeans.
Kilichomshangaza zaidi Eliza ni kwamba mwanaume yule ngozi yake ilikuwa nyeupe kiasi kwamba alishindwa kujua ni mzungu au ana ulemavu wa ngozi kutokana na kwamba ngozi yake haikuashiria kuwa na damu kabisa kutokana na namna ilivyopauka , alikuwa kama vile ni ile midoli ya kizungu ya fasheni kwani hata ile mboni ya macho yake ilikuwa sio ya kawaida.
“Miss Elizabeth , uko salama?” Yule mtu kama mdoli wa kizungu aliuliza kwa lugha ya kiswahili lakini lafudhi yake ilionesha hakuwa mtanzania.
Eliza mara baada ya kusikia jina lake likitajwa alishangaa na kuona huyo ni mtu anaemfahamu na mtu yule alionekana kuuliza kwa upole sana.
“Niko salama wewe ni…”
Kabla hata hajajibiwa yule Hamza feki aliekuwa amedondoka chini alisimama na kuchomoa kisu kikali na kutaka kumshambulia nacho yule mwanaume kwa nyuma.
Yule mtu hakuhitaji kuambiwa kuhusi hatari nyuma yake kwani palepale kwa ustadi wa hali ya juu alizunguka na teke la shingo na kumpiga yule mvamizi na kumfanya apepesuke na kwenda kujingonga kwenye ukuta.
Bam!!
Kilikuwa ni kishindo kizito kilichofanya mpaka taa na mapambo ya ukutani kudondoka chini , huku yeye mwenyewe akionekana kuumia kiasi kwamba kile kisu alishindwa kukishikilia mkononi vizuri na kikadondoka chini huku akitetemeka kama vile ana kifafa.
Yule mtu mweupe hakumuacha palepale na alisogea mbele na kuokota kile kisu na kisha akamchinja yule mtu shingo , lakini palepale kuna kitu kilionekana hakikuwa sawa , yule mtu licha ya kukatwa shingo hakuna damu iliotoka na badala yake eneo lile liliachia na kuonyesha kwa ndani chuma na mfumo sakiti ‘circuit’ wa ramani wa kieletroniksi.
Yule mtu mweupe alijikuta akishangazwa na jambo lile , Eliza nae ilikuwa hivyo hivyo.
“Ni kama roboti!!!?”Aliongea Eliza huku akifikicha macho kuangalia kama macho hayamdanganyi.
Muda ule yule roboti alianza kuzungusha shingo yake na ilianza kusikika mlio wa kubip na yule mtu mweupe mara baada ya kusikia mlio huo haraka sana aligeuka na kumbeba Eliza juu juu na kuruka nae kupitia dirishani.
“Boom!!!” Ni Mlipuko.


SEHEMU YA 169.
Kulitokea mlipuko mkubwa wa bomu ikiashiria yule mtu kama roboti alikuwa na mfumo wa kujimaliza.
Wakati huo yule bwana mweupe aliweza kutua na Eliza mikononi chini ardhini bila madhara yoyote.
"I'm sorry, Miss Elizabeth . It was no offense. The situation just now was very urgent.”Aliongea kwa kingereza yule mzungu akijitetea kutokana na namna alivyokuwa amenshikilia Eliza bila ridhaa yake.
Eliza alikuwa akihema kwa nguvu kiasi cha kushika magoti na aliinua macho yake akiwa haamini ameshuka kutoka kule juu na kutua chini kabla ya kulipuka.
“No.. no problem . Asante kwa kuniokoa , lakini wewe ni nani hasa?”Aliuliza
“Jina langu naitwa GreyWolf. Nipo hapa chini ya maagizo ya Prince kukupa ulinzi kwa siri”Aliongea.
“Prince? Ni nani huyo Prince?”Aliuliza Eliza akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa.
“Jina lake Prince la kitanzania anaitwa Hamza Mzee”
“Hamza!?” Ingawa Eliza alikuwa na hisia ni Hamza tokea mwanzo lakini bado alikuwa katika hali ya mshangao mkubwa.
“Hamza ndio aliekutuma uje kunilinda? Tangu lini alitoa hayo maagizo?”
“Ni siku kadhaa zilizopita . My-Prince alionekana kuwa na hisia za mtu kutaka kulipiza kisasi kupitia watu wake wa karibu na alitupa taarifa ya kuingia Tanzania na kuwalinda kwa siri”Aliongea na kisha akaendelea.
“Lakini usiwe na wasiwasi , tunaijua mipaka yetu , ukiwa haupo kwenye hatari hutotuona kabisa kama tunakulinda na kuingilia maisha yako , tuna mbinu zetu za kutoa ulinzi pasipo ya kuonekana kwa macho ya kawaida”Aliongea lakini muda huo sauti ilisikika.
“Lizzy hujaumia?”
Eliza mara baada ya kusikia sauti hio aligeuka haraka na aliweza kumuona Hamza akisogea na GreyWolff mwonekano wake ulikakamaa na palepale alipiga goti kwa mguu moja na kuweka mkono mmoja kifauni.
“MY-PRINCE.”Aliongea kwa heshima na Hamza alimpa ishara ya kusimama
“No need for formalities. Graywolf, you did well. You can leave now.”Aliongea akimaanisha kwamba haina haya ya heshima mbele yake na amefanya vizuri hivyo anaweza kuondoka.
“Ni bahati kwangu sijakuangusha”Aliongea Graywolf na palepale muda huo watu upande mwingine walianza kutoka kwa kukimbia na yule bwana anaefahamika kwa jina la Mbwamwitu wa kijivu alikimbia mpaka kwenye bustani ya maua karibu na bwawa na kisha alitoweka.
“Hamza nini kimetokea..?”Aliongea Eliza huku akijirusha kwenye kumbatiao la Hamza “Kulikuwa na mtu aliekuwa akifanana kwa kila kitu na wewe , alionekana kama roboti..”Aliongea Eliza na kumfanya Hamza kuishia kupumua kwa nguvu akimwonea huruma mrembo wake.
“Sio roboti ila ni muunganiko endelevu wa kisayansi kati ya biolojia na roboti..kuna mtu aliniponyoka mara ya mwisho ndio aliemtuma”Aliongea Hamza.
“Ni nani huyo alikuponyoka?”Aliuliza Eliza kwa shauku.
“Eliza unaonaje ukienda kwenye nyumba yako kubwa kule au hotelini, usiwe na wasiwasi kuhusu usalama maana Graywolf yupo karibu yako kukulinda. Mimi kuna sehemu nataka kwenda kushughulika na hili swala”Aliongea Hamza akipotezea swali la Eliza.
Ijapokuwa Eliza alikuwa na wasiwasi , lakini hakuuliza aliona lazima kuna tatizo kubwa ambalo Hamza anakwenda kushughulika nalo na kwasababu aliingia kwenye hatari aliamini lazima na Regina atakuwa hatarini zaidi.
“Sawa, wewe nenda tu , mimi nitatafuta hoteli yoyote iliokaribu”Aliongea Eliza na Hamza alimuaga na kisha kuondoka huku akipishana na watu wengi waliokuwa wakitoka kwenye jengo hilo pamoja na gari la Zimamoto.
Hamza mara baada ya kuachana na Eliza palepale alitoa simu yake na kupiga namba flani na haikuchukua muda ilipokelewa na sauti ya mwanamke upande wa pili.
“My Prince! ni kama ulivyotarajia , Saidi hajakufa bado”Sauti iliongea kwa lugha ya kingereza.
“Sally ukiachana na Eliza nini kingine kimetokea wakati nikiwa sipo?”Aliuliza Hamza katika sauti iliojaa usiriasi.
Ukweli ni kwamba tokea siku ambayo Hamza alikutana na Leviathan waliongea uwezekano wa Saidi kutokufa na ni siku ile ile alipowasiliana na Sally kufanya utaratibu wa baadhi ya watu wake kuzamia Tanzania na kutoa ulinzi kwa siri sana. Hakutaka kumfanya yoyote anaelindwa kuwa na wasiwasi ndio maana alichukua hatua ya namna hio.
Hamza hakuwa Mungu hivyo asingeweza kulinda kila mtu kwa wakati mmoja na alijua kwa tabia aliokuwa nayo Saidi kama kweli bado yupo hai basi kisasi chake angekifanya katika njia ya kikatili mno kwa kuanza na watu wake wa karibu.
Ilikuwa ni kama alivyotarajia , kile alichokuwa akihisia kuwa kweli hatimae kimetokea , lakini Saidi kwa bahati mbaya licha ya kuja na mbinu nyingine lakini uwezo wake wa mapambano ulikuwa wa chini.
“Crow kasema Regina alitembelewa na mwingine ambae alijifanyisha kuwa mfanyabiashara na alipanga akikutana nae achukue hatua lakini aligundulika mapema na kuchukuliwa . Pia kuna mwingine mwenye mwonekano wako alionekana katika makazi ya Dina na Viper alimmaliza kabla hata hajachukua hatua, Dina hakupata usumbufu kabisa. Kuhusu Prisila kwasababu ulisema tumpe jaribio Serena, Lnyx hajachukua hatua yoyote. Prisila pia yupo salama”Aliongea Sally.
“Saidi amepanua sana uwezo wangu wa kufikiri. Sally hebu mwambie kijana wako anielekeze ni wapi Prisila kashikiliwa”
“Yes My prince! Nitamwambia Pakamwitu(liksi) akutafute sasa hivi”Aliongea na simu palepale ilikatwa.
Muda uleule baada ya kukata simu , iliita tena na alikuwa ni Regina aliekuwa akipiga.
“Hamza kuna nini jamani! Kuna mwanamke wa kigeni hapa kajitambulisha kwa jina la Crow amesema umemtuma kuja kunilinda? Ni lini ukaweka mtu anaejiita Kunguru kama mlinzi wangu?”Aliongea Regina huku sauti yake ikionekana kuwa katika mshangao.
“Wife ni stori ndefu . Ni kwasababu yule Saidi hajafa bado”
“Mh Saidi! Kwanini hajafa tu?”
“Sikuwa makini , nilidharau uwezo wake ndio maana , lakini usiwe na wasiwasi , nitalishughulikia hili mapema ili nisikutie shaka”
“Wewe…”Regina alionekana kutaka kusema kitu lakini Hamza alikuwa ashakata simu kwasababu Liksi alikwisha kutuma coordinates(uelekeo).
Hamza aliangalia ramani na palepale aliona shabaha haiko mbali sana na hakujali tena kwani palepale safari ya kuelekea huko ilianza mara moja.
******
Upande mwingine nje kidogo na mjini ndani ya Dar es salaam ilionekana gari aina ya Mercedenz umbo la Noah ikiingia ndani ya uzio wa mabati katika nyumba ya ghorofa nne kwenda juu ambayo ujenzi wake ulikuwa umesitishwa muda mrefu.
Mara baada ya gari ile kusimama kando ya kifusi cha mchanga na mawe, alishuka mwanaume na kisha alizunguka nyuma na kutoa viroba vizito na kuviingiza ndani ya jengo hilo.
“Bosi mateka hawa hapa”Aliongea yule mwanaume huku akivua ile kofia aliovaa kichwani wakati akitoa taarifa kwa mwanaume alievalia koti la kimaabara. Mwanaume huyo hakuwa mwingine bali ni Saidi au Adamson jina la utotoni.
Mwonekno wa Saidi ulikuwa ni ule mzito na aliangalia kishikwambi kilichokuwa katika mikono yake na alionekana kung’ata meno kwa hasira.
“Damn you Hamza.. Kumbe ulikuwa ukijilinda zidi yangu , umejuaje juaje sikufariki?”Aliongea akiwa na shauku kubwa.
“Mende tofauti na wewe , wenzako wote wamefeli misheni zao, hawakuwa watu wa kutegemea kabisa”Aliongea.
“Nini! Bosi unasema maroboti mawili ya kibailojia uliotengeneza pia yamefeli?”Aliongea yule bwana aliefahamika kwa jina la Mende kwa mshangao.
“Misheni yao imefeli kabisa. Kifaa cha kujimaliza kilishajiwasha ikiashiria wamelipuka”Aliongea Saidi huku akiwa na hali ya kutokuwa na furaha katika uso wake.
“Hayo maroboti yote mawili yana mfanano kabisa wa Hamza .Wamejuaje ni feki?”Aliongea Mende.
“Sio mbaya , Kwanza ni toleo la kwanza na bado ninayo nafasi ya kuboresha zaidi , ni kwamba tu muda niliokuwa nao ni mchache na bajeti haikuwa rafiki , vinginevyo yangekuwa bora zaidi”Aliongea Saidi.
“Bosi wewe ni jiniasi . Hebu niangalie mimi nilivyo sasa baada ya kuninywesha Tone la Ukombozi. Sasa hivi nimekuwa ngangari kama Maksai. Nina uhakika utaweza kulipa kisasi chako vizuri tu na kung’ara tena”Aliongea na kumfanya Saidi kumshika Mende bega lake.
“Nilivyorudi nilidhania wote mliokuwa chini yangu mmenikimbia lakini bado tupo pamoja , usiwe na wasiwasi mkiwa chini yangu siku njema zinakuja”Aliongea Saidi.
“Asante sana bosi”
Kama wafanyakazi waliokuwa chini ya kampuni ya utafiti ya Saidi kutokana na skendo ile ya mauaji ya Saidi, walivyoomba kuajiriwa katika kampuni nyingine walikataliwa hivyo wakajikuta wakiwa majobless. Baada ya Saidi kurudi na kuwatafuta wote walikubali na kurudi kufanya nae kazi upya.
Kama watu wa kawaida wanaojitafuta, Mende na wenzake walijawa na furaha hasa pale walipolishwa Tone la Ukombozi na kuwa na nguvu kubwa.
“Nenda kawaamshe Serena na Prisila”Aliongea Saidi na haraka sana Mende alifanya kama alivyoagizwa . Baada ya kuwafungua kwa kuwatoa kwenye viroba aliwamwagia maji na wote walishituka.
“Tuko wapi?” Serena ndio aliekuwa wa kwanza kuropoka huku akizungusha shingo kulia na kushoto , alifurukuta kujaribu kujifungua mikono yake iliokwisha kufungwa.
“Saidi!!!”
Prisila alijikuta akiwa katika hali ya mshangao baada ya kumuona mwanaume aliekuwa mbele yake na palepale mwili wake ulifubaa kwa hofu.
“Prisila babe , tunakutana tena , vipi ulinimiss?”
“Wewe,, Inamaana hukufariki?”Aliuliza Prisila huku akijihisi ni kama anaota.
“Kufa? Mbona unanidharau hivyo mrembo. Mimi Saidi nakufaje ilihali mpango wangu wa kukufanya kuwa mke wangu haujatimia?”Aliongea Saidi huku akicheka akiwa ameinama na kushika shavu la Prisila.
“Kwasasa shauku yangu kubwa ni kuifahamu siri yako. Ule moto ulikuwa ni kitu gani uliotoa siku ile! Nataka nikupatie mtu wa kumuunguza ili nione?”Aliongea.
Selina licha ya Saidi kuongea kiswahili lakini alielewa vyema na macho yake yalichanua kwa mshangao.
"Prisila !" Who is he?! Why did you want to capture us!?”Aliongea akiuliza ni nani na kwanini amewakamata.
Prisila alikuwa katika hali ya wasiwasi mno . Alitamani kumuunguza Saidi kama ile siku lakini hakujua namna ya kufanya hivyo.
Lakini aliona hata kama angekuwa na uwezo wa kuwasha moto asingefanya hivyo kwasababu alikuwa amefungwa karibu na Serena,isitoshe hakuwa akijua namna ya kudhbiti uwezo wake .
“Sister Serena usiwe na wasiwasi naamini Hamza atafika na kutusaidia”Aliongea Prisila.
“Eti Hamza atakuja! Huyo mshenzi wala hakufikirii, kama angekuwa anakufikiria angekuwekea ulinzi kama alivyofanya kwa wengine, ni wewe tu pekee ambae hakujisumbua kukulinda . Unadhani imekuwaje rahisi kukuleta hapa?”Aliongea Saidi.
Prisila mara baada ya kusikia hivyo uso wake ulikosa hisia kabisa , alionekana kuwa katika hali ya kukata tamaa.
“Hata kama Hamza hajatuma mtu wa kunilinda ni suala la kawaida , haina haja ya kumuongelea vibaya hapa kwa kuyakuza”Aliongea Prisila lakini wakati huo Serena yeye muonekano wake ulionekana kuwa na mashaka flani hivi.
“Usiwaze , isitoshe sipo hapa kwaajili ya kuchafua mahusiano yako.. maana hutokuja kumuona tena”Aliongea Saidi ki uovu.
“Wewe… unamaanisha nini ?”Aliuliza Prisila huku akiwa na wasiwasi kwenye sura yake.
Saidi alitembea hadi pembeni bila ya kuongea neno na kisha alibeba helmeti flani hivi la ajabu kwenye meza , Helmeti hilo lilionekana kuwa na muunganiko na mamia ya taarifa yaliokuwa yakisambazwa kutoka kwenye tarakishi.
Saidi alisogea na kutaka kumvalisha Prisila lile helmeti lakini mwanamke huyo alitingisha kichwa kukataa.
“Hicho ni kitu gani , usije kunivalisha mimi”Aliongea Prisila kwa kuamrisha akikataa kutoa ushirikiano na jambo lile lilimfanya Mende kusonya na palepale alichukua sindano ya ganzi na kumchoma Prisila na sekunde chache tu Prisila alilegea na palepale Saidi alimvalisha lile helmeti.
“Usiwe na wasiwasi Prisila hutosikia maumivu kabisa , utakachoweza kuona ni kama ndoto za kujirudia rudia tokea kipindi ukiwa mdogo mpaka sasa hivi .."Aliongea na Selena ambae alikuwa akielewa kiswahili kwa shida aliweza kufahamu Saidi alichokuwa akidhamiria kufanya.
“Are you trying to copy her brain memories?”Aliuliza Serena akimaanisha je anataka kukopi kumbukumbu zake.
“Kama nilivyotarajia kutoka kwa mwanasayansi . Sikudhania utakuwa na uwezo wa kugundua nia yangu mapema”Aliongea Saidi akiwa katika hali ya mshangao lakini jibu lake lilimshangaza zaidi Serena.
“Umejifunzia wapi hio teknolojia ? Kwa ninayofahamu mpaka sasa hakuna maabara yote duniani ilioweza kufanikisha kivitendo nadharia ya kuclone kumbukumbu za binadamu”Aliongea Serena akiwa na shauku kubwa.
“Mnajiona sana nyie wazungu mnajua kila kitu , lakini hamna mnachokifahamu? Watu wenye karama ya akili siku zote ndio wenye kudharaulika na ni jamii ya wachache na ni sisi weusi. Nyie wazungu baada ya kuona watu weusi tunapiga hatua mkaanza kucheza na akili zetu ili tujidharau. Lakini nikwambie mimi Saidi ni zaidi ya makundi ya wanasayansi mliojichimbia kwenye chumba kufanyia kazi tafiti moja bila majibu”Aliongea Saidi kwa majigambo.
“Ongea yako inanikumbusha mtu mmoja..”Aliongea Serena akiacha kumzingatia kuhusu maneno yake.
“Niwie radhi . Sina haja ya kumjua huyo mtu ni nani”Aliongea Saidi kwa kejeli na kisha palepale aligeuka na kuanza kufanya kazi na tarakishi.
“Umemdharau sana Hamza , hivi unadhani hakutuma mtu kwa ajili ya kumlinda Prisila?”Aliuliza Serena.
“Unamaanisha nini?”Aliuliza Saidi huku akiacha kile anachokifanya na kumwangalia lakini Serena hakujibu na badala yake alianza kupiga makelele ya kuomba msaada.
Na kitendo cha kupiga makelele tu mlango wa kuingilia eneo hilo ulifunguliwa na mtu ambae hakuwa akionekana zaidi ya kivuli tu.
“Clank!”
Muda uleule aliweza kuonekana mwanaume wa makamo , Mzungu ambae alikuwa na nywele zilizojikunja kunja za rangi ya kahawia, Uso wake likuwa ni ule wa usiriasi mno wenye vidoadoa vya joto.
Mende mara baada ya kuona mtu ameingia palepale aliruka akijiandaa kushambulia.
“Wewe ni nani?”
“Unauliza nini wewe mjinga , ni watu wa Hamza hao walikuwa wakikufuatilia”Aliongea Saidi na Prisila mara baada ya kusikia hivyo furaha ilimvaa.
“Nilijua tu Hamza hawezi kunitelekeza”Aliongea.
Muda huo sasa ni kama Mende akili yake ilianza kufanya kazi na kwa kutumia nguvu zake zote alimsogelea yule mzungu na kumrushia ngumi.
Lakini yule mzungu ni kama hakujisumbua kwani ngumi ile ilivyomkaribia alichokifanya ni kuudaka mkono wake na kisha aliuvuta na kumtupia mbali.
Mende alijikuta akihisi kizunguzungu wakati wa kudondoka huku akishindwa kuamini licha ya mwili wake kukombolewa na Tone la Ukombozi na kumfanya kuwa na nguvu lakini bado mtu huyo ameweza kumsukuma kwa urahisi kabisa kama vile alikuwa mtoto wa miaka mitatu.
Haraka sana yule mzungu alimvua Prisila lile helmeti na kisha alionyesha ishara ya kuomba radhi mbele yake.
“Samahani sana Miss Prisila , The lynx came late”Aliongea akimaanisha kwamba Yeye Pakamwitu amekuja kwa kuchelewa.
Saidi kawekewa mtego kaingia mzima mzima . Unadhani atapona kwa mara ya pili mbele ya Hamza.
NB: Ukitaka tone la ukombozi nicheki
ITAENDELEA.
 
Back
Top Bottom