STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 72
"Ile hali ya miguu yangu kupoteza nguvu nadhani ilisababishwa na kukaa muda mrefu kwenye kile kiti ambacho nilifungwa kwa mwaka mzima huku nikiwa nageuzwa geuzwa muda wa kubakwa tu pekee. Nicole aliiona hofu ambayo ni wazi ilikuwa inajionyesha mbele ya uso wangu huku nisijue nini ilikuwa hatima yangu ndani ya lile eneo, aliingiza mkono wake mfukoni na kunirushia kidonge kimoja cheupe kikubwa ambacho sikuwahi kukiona kabla. Baada ya kukimeza tu nilipata nguvu za ajabu mpaka nikashangaa, hali ile ilinifanya niamini kwamba kweli yule alikuwa mwanajeshi kwani mtu wa kawaida asingeweza kabisa kuwa na uwezo wa kuyajua mambo kama yale"
"Una kisu hapo?" Nilimuuliza maana tangu jana yake nilikuwa nimemkumbusha kuhusu hilo jambo, aliingiza tu mkono kinunoni kwake akanirushia kisu kikubwa sana mpaka nikajiuliza aliweza vipi kukificha hapo. Tulijibanza kwenye zile pembe mbili za mlango na nadhani Nicole alikuwa na wasiwasi kama nitaweza kujilinda"
"Kuna mwanaume aliingia akiwa anahema kwa nguvu sana mpaka nikawa nashangaa shida nini? Nilimpa ishara Nikole atulie, huyo alikuwa ni wangu. Jinsi nilivyo kizungusha kisu na kupita na shingo ya yule mwanaume hata Nikole alianza kuniogopa, nikatabasamu na kumpa ishara kwamba tutoke kwa pamoja kwa kasi kitu ambacho hakikuchukua hata sekunde tano, tuliwamiminia risasi wanaume wanne ambao walikiwa pale nje"
"Hawa wajinga nahisi walikuwa kucheza kamali ndiyo maana wamechelewa kula chakula hivyo sumu imeanza kuwaathiri mdogo mdogo wenzao walishakufa muda tu" kauli yake ilinipa jibu kwamba ndiyo maana yule mtu aliingia mle ndani akiwa anahewa kwa nguvu sana namna ile kumbe ni kwa sababu ya ile sumu.
"Baada ya kutoka pale nje ndipo nikaelewa kwamba kumbe muda wote ule nilikuwa chumba cha chini kabisa ya ardhi ambacho kilichimbwa ndiyo maana kulikuwa kiza sana huku mimi nikiwa nina imani kwamba nipo chumba cha juu. Baada ya kufika sebuleni hapakuwa na mtu hivyo Nikole akaufungua mlango wa kutokea nje, baada ya kuuona mwanga, ilinilazimu kuyafumba macho kwa dakika mbili maana ule mwanga ni kama uliniumiza macho yangu. Hapo ndipo rasmi baada ya mwaka mmoja kuisha nikawa nimefanikiwa kutoka nje na kuuona mwanga wa jua"
"Wakati tunafika pale nje, nilimuona mwanaume mmoja akiwa kwenye karo tena ndani ya kombati ya jeshi akiwa anajaribu kuitapika sumu ambayo bila shaka naye aliila kwenye kile chakula. Nilipiga makofi kwa nguvu na kumshtua yule mtu ambaye aliligeuka huku akiwa anacheka sana.
"Wewe malaya umetusaliti sisi? Unajua bosi atakacho kufanya akijua kwamba wewe ndiye umefanya hili tukio na umewaza kitakacho ikuta familia yako?" Aliongea kwa hasira akiwa anamtazama Nikole.
"Kuwa makini ni mtu hatari sana kwenye mapigano" Nikole aliongea akiwa anaitoa bastola yake lakini alikuwa amechelewa maana mwanaume yule alikuwa ameitoa kabla yake. Niliichukua bastola hiyo kwenye mikono ya Nikole na kumpa ishara ya kwamba alitakiwa kupigana naye na siyo kushindana kwa risasi ila Nikole alienda kwa kusita sita sana nikawa nimegundua kwamba alikuwa anamuogopa sana mtu huyo. Nikole alikuwa anasogea kwa hofu sana, nililitambua hilo lakini niliamua kufanya vile ili nipate hata dakika moja ya kuizoea hali ya pale nje maana kutoka tu na kuanza kupigana ingeniletea shida kubwa sana ambayo huenda ingenifanya nipoteze pambano ambalo lingenirudisha mle ndani.
Mwanaume yule alimtisha Nikole akiwa hajarusha ngumi hata moja alikwepa teke Kali lakini alikuwa amesimama kizembe sana maana alipigwa mtama makali huku akipigwa na mateke yote mfululizo kama sio mimi kumdaka huenda angeumia vibaya sana kwa kujipigiza ukutani. Baada ya kumsimamisha tena, mwanaume yule alikuwa anakuja kwa kasi ila niliona atatupotezea sana muda niliingilia na kumpiga teke la shingo ambalo lilimfanya ayumbe na kwenda kuegemea ukuta akiwa anatokwa na damu nyeusi mdomoni ambapo bila shaka ilikuwa ni ile sumu ambayo aliila kwenye chakula.
Wakati anaegemea ule ukuta alikuwa ameshajipotezea maisha yake tayari maana kwa hali ambayo alikuwa nayo asingeweza kabisa kukikwepa kisu ambacho nilikirusha kwa nguvu sana kilizama kwenye shingo yake mpaka kikaenda kukita kwenye ukuta baada ya kutoboa toboa shingo yake.
"Twende haraka hawa watu watakuwa hapa sasa hivi" Nikole aliongea akiwa anajifuta damu puani na kuonekana mwenye hofu sana.
"Umejuaje?" Nilimuuliz huku akiwa analifungua geti la kutokea nje.
"Ile alamu ambayo imepigwa, watu wale wanapata taarifa moja kwa moja kwenye simu zao hivyo watajua kwamba kuna tatizo watatuma watu kuja"
"Ok, familia yako ulikumbuka kuihamisha?"
"Ndiyo, nilijua wanaweza wakaanza nao hivyo nimewapeleka sehemu salama ambayo nitakaa nao huko mpaka nitakapo pata nafasi ya kutoka nje ya nchi hii"
"Unapenda kuishi Rwanda?" Nilimuuliza baada ya kuiona hofu yake
"Ndiyo, nimezaliwa Rwanda, napapenda sana na nilikuwa naipenda sana kazi yangu ila tulipo fikia sina namna tena"
"Nenda kaiweke familia yako eneo lililo salama zaidi, ila tu usiondoke kwani watakukamata mpakani. Ndani ya muda mfupi ujao hii serikali yenu itatolewa madarakani"
"Nani ataitoa?"
"Mimi ni jasusi kutoka ndani ya nchi ya Tanzania, huyu mtu ambaye aliniteka anahusika na ulipuaji wa bunge la nchi yetu hivyo nilikuwa hapa kwa ajili ya kuifanya kazi ya kuwajua watu ambao walikuwa wapo nyuma yake na kwa bahati mbaya akawa amewahi kunikamata hivyo mimi natakiwa kufika nyumbani kwa namna yoyote ile na baada ya hapo huyu mtu kuna watu watakuja kumchukua kimabavu na huo uovu wa raisi wenu utawekwa wazi nadhani nchi itakuwa yenye amani na mtaendelea na maisha ya kawaida, hata wewe nina uhakika utarudi kwenye kazi yako ambayo unaipenda sana" alikuwa amefurahi sana baada ya kulitambua hilo na ndipo nilipo furahi sana baada ya kumuona yule dereva wangu.
"Sister kumbe ushakuwa mwenyeji kabisa, hadi sehemu kama hii unaijua?" aliuliza kwa uchangamfu mkubwa sana
"Ndiyo kuna bishara ambayo imenileta mara moja, washa gari haraka twende Nyarutarama ila pia kuna mahali unatakiwa kunipeleka haraka" niliongea kwa sauti ambayo hata yeye alielewa kwamba sikuwa nahitaji mazoea kabisa, akawa ametulia vizuri. Baada ya kutembea mwendo wa kama dakika thelathini, kuna magari ambayo tulipishana nayo yakiwa kwenye mwendo mkali kuelekea kule ambako sisi tulitoka. Nikole alinikonyeza hapo nikaelewa kwamba ni watu wa Blaise Norbert.
"Usipite uwanja wa ndege wana watu kibao pale ambapo kama ukifika tu basi lazima wakukamate, una njia moja ya pekee ya kupita japo ni ngumu sana. Pitia ndani ya hifadhi ya Akagera, licha ya kuwa na baadhi ya wanyama hatari ila pia ni hifadhi ambayo inalindwa sasa na wanajeshi wa nchi ya Rwanda ikiwa chini ya kampuni la Akagera huku wakifanya kazi sambamba na shirika la hifadhi la nchi ya Rwanda liitwalo Rwanda Development Board. Hawa watu ni makatili sana wakikukamata kwani hawana huruma kabisa, wanafanya jambo lolote lile ili kuhakikisha wanyamapori wanakuwa salama hivyo wakikikukuta huko moja kwa moja watajua wewe ni muwindaji haramu hawawezi kukuacha"
"Licha ya kuwakwepa watu hao ila pia hakikisha wakati unaingia ndani ya hifadhi hiyo unavaa mabuti mazito sana, vaa gloves mikononi pamoja na nguo nzito nzito ila tu usivae nguo zenye rangi ya blue, zingatia sana hilo"
"Ukifika pale kama utatumia gari ya kawaida ni mwendo wa masaa mawili mpaka mtatu japo pia huwa kuna ndege ndogo ambazo huwa zinaenda kuko. Ukifanikiwa kufika pale kuhusu kuingia ni rahisi sana kwa sababu hata kama hauna vielelezo ukiwa na pesa tu unahonga na unaingia ndani ya hifadhi hiyo ila sasa ukikamatwa huko ndani ndo utakuwa hauna msaada maana utatakiwa kuweza kujitetea kwa namna unayohisi inakufaa wewe na kama ukishindwa watakufanyia ukatili ambao huenda hukuwahi kuuona"
"Ni mashariki mwa Kigali mahali ilipo hifadhi hiyo na hata ili kuweza kufika kwenu Tanzania bado utatakiwa kwenda upande wa mashariki ambapo utatokea ndani ya mkoa wa Kagera. Kitu pekee cha kufanya kama utabahatika kupita salama maeneo yote humo ndani ya hiyo hifadhi, utakutana na ziwa ambalo linaitwa Ihema, hilo ziwa haliruhusiwi kabisa kuendesha ishu za uvuvi wala mambo yoyote ambayo yatahatarisha usalama wa hifadhi. Ziwa hilo ndilo njia pekee ya wewe kufika kwenu Tanzania kwani ndilo linalo itenganisha Tanzania na Rwanda na hapo ili usafiri lazima utumie usafiri wa boti"
"Unalipa kwa dola, ili usafirishwe haraka wape pesa nyingi nadhani utakuwa umetokea upande wa Kagera ambako utakuwa salama na unaweza kufika ndani ya jiji la Dar es salaam kiwepesi sana" hayo yalikuwa maneno ya Nikole akiwa anaongea sauti ya chini sana ili dereva asiweze kusikia kile ambacho tulikuwa tunakizungumza.
Nilimshukuru sana, nikamhamishia kwenye akaunti yake milioni miatano kisha akashukia sehemu ambayo hata sikuwa naijua. Nilichukua vitu vyangu vya mhimu mwenye ile apartment kisha nikaianza safari ya kuelekea ndani ya hifadhi ya Akagera. Hifadhi ambayo ilinifanyia ukatili mkubwa wa nafsi nikatamani ni bora ningebaki kule kule kwenye lile jengo la Blaise Norbert kuwafurahisha wale wanaume, maana kuingia kwenye ile Hifadhi ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuingia kwenye maisha magumu sana ya kunifanya nipoteze hata uwezo wangu kichwani nikaishia kuwa kama kichaa ambapo sikujua hata ndani ya Pwani niliwezaje kufika ambapo nimekuja kushtuka kaka yangu ukiwa mbele ya macho yangu, lakini wanasema ni bora kuthubutu maana ndiko kufanya nami nilithubutu" hiyo ni simulizi ya maisha ya dada yake ambayo Calvinjr alikuwa anaikumbuka vyema sana tena kwa uchungu ambayo alisimuliwa na dada yake kipenzi Tina.
Wakati huo Calvinjr alishtuliwa kwenye hiyo ndege ya abiria ambayo alikuwa amepanda yeye na mama yake, ni mama yake mzazi ambaye alimkurupua mwanae kutoka kwenye hiyo kumbu kumbu ambapo mama yeye alihisi mwanae alilala lakini haikuwa kweli. Walikuwa ndani ya Kigali International Airport ndani ya nchi ya Rwanda ili kuhakikisha wote walio mfanyia ukatili Tina wanapata kile wanacho stahili kwa mujibu wa sheria ikiwa ndiyo akili ya mama huyo lakini mwanaume alikuwa na kazi za ziada ya kuweza kuifanya ndani ya hilo jiji la Kigali.
Calvinjr tayari yupo ndani ya jiji la Kigali, una hamu ya kujua hili jiji linaenda kupitia yapi kupitia mkono wa huyu jasusi ambaye umejua wazi kwamba ni mtoto wa damu kabisa wa yule kiumbe hatari Calvin Jackson? Maandishi haya yatatupa majibu sahihi.
Episode ya 72 inafika mwisho.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app