Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

Kama unataka kuyapata maandiko yangu yote ya kipelelezi. Haya hapa[emoji116]

1. GEREZA LA HAZWA......5000 FULL

2. ULIMWENGU WA WATU WABAYA......3500 FULL

3. I WANT TO DIE JUDGE....... 3500 FULL

4. INNOCENT KILLER (THE REVENGE).....5000 FULL

5. NYARAKA NUMBER 72 (DOCUMENT NUMBER 72)......4000 FULL......KWA MLIPO ISHIA KUMALIZIA NI 1000 tu

6. ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD).....5000 FULL (4000 KWA ILIPO ISHIA)

7. JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)....5000 . KUNA SPECIAL OFA KWA LEO TU NI 3500 (LEO TAREHE 14, JANUARY 2024 TU)

Short stories (hizi utachagua unayo itaka wewe, ukinunua moja ya juu hapo short story unapewa free tu kupooza kichwa.

8. MIMI NAITWA GAMA

9. ABELA NDIYE MUUAJI

10. NILIUA KWA SABABU YA KUKULINDA "NITAKUUA DAVINA"

11. NAFSI YANGU-MAUTI YANGU)

12. MASAA 840 YA BINTI WA RAISI (35 DAY-Z)

13. HATIMA YA UJINGA WAKE

14. COLLEGE ROMANCE

Namba za malipo.

0745982347 (M-PESA)

0621567672 (HALO-PESA)......WhatsApp number

0714581046 (TIGO-PESA?

Zote jina moja FEBIANI BABUYA.View attachment 2871419View attachment 2871420View attachment 2871421View attachment 2871424View attachment 2871422View attachment 2871423View attachment 2871438View attachment 2871439View attachment 2871440View attachment 2871441View attachment 2871442
FB_IMG_1704861911572.jpg
View attachment 2871443

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 72

"Ile hali ya miguu yangu kupoteza nguvu nadhani ilisababishwa na kukaa muda mrefu kwenye kile kiti ambacho nilifungwa kwa mwaka mzima huku nikiwa nageuzwa geuzwa muda wa kubakwa tu pekee. Nicole aliiona hofu ambayo ni wazi ilikuwa inajionyesha mbele ya uso wangu huku nisijue nini ilikuwa hatima yangu ndani ya lile eneo, aliingiza mkono wake mfukoni na kunirushia kidonge kimoja cheupe kikubwa ambacho sikuwahi kukiona kabla. Baada ya kukimeza tu nilipata nguvu za ajabu mpaka nikashangaa, hali ile ilinifanya niamini kwamba kweli yule alikuwa mwanajeshi kwani mtu wa kawaida asingeweza kabisa kuwa na uwezo wa kuyajua mambo kama yale"

"Una kisu hapo?" Nilimuuliza maana tangu jana yake nilikuwa nimemkumbusha kuhusu hilo jambo, aliingiza tu mkono kinunoni kwake akanirushia kisu kikubwa sana mpaka nikajiuliza aliweza vipi kukificha hapo. Tulijibanza kwenye zile pembe mbili za mlango na nadhani Nicole alikuwa na wasiwasi kama nitaweza kujilinda"

"Kuna mwanaume aliingia akiwa anahema kwa nguvu sana mpaka nikawa nashangaa shida nini? Nilimpa ishara Nikole atulie, huyo alikuwa ni wangu. Jinsi nilivyo kizungusha kisu na kupita na shingo ya yule mwanaume hata Nikole alianza kuniogopa, nikatabasamu na kumpa ishara kwamba tutoke kwa pamoja kwa kasi kitu ambacho hakikuchukua hata sekunde tano, tuliwamiminia risasi wanaume wanne ambao walikiwa pale nje"

"Hawa wajinga nahisi walikuwa kucheza kamali ndiyo maana wamechelewa kula chakula hivyo sumu imeanza kuwaathiri mdogo mdogo wenzao walishakufa muda tu" kauli yake ilinipa jibu kwamba ndiyo maana yule mtu aliingia mle ndani akiwa anahewa kwa nguvu sana namna ile kumbe ni kwa sababu ya ile sumu.

"Baada ya kutoka pale nje ndipo nikaelewa kwamba kumbe muda wote ule nilikuwa chumba cha chini kabisa ya ardhi ambacho kilichimbwa ndiyo maana kulikuwa kiza sana huku mimi nikiwa nina imani kwamba nipo chumba cha juu. Baada ya kufika sebuleni hapakuwa na mtu hivyo Nikole akaufungua mlango wa kutokea nje, baada ya kuuona mwanga, ilinilazimu kuyafumba macho kwa dakika mbili maana ule mwanga ni kama uliniumiza macho yangu. Hapo ndipo rasmi baada ya mwaka mmoja kuisha nikawa nimefanikiwa kutoka nje na kuuona mwanga wa jua"

"Wakati tunafika pale nje, nilimuona mwanaume mmoja akiwa kwenye karo tena ndani ya kombati ya jeshi akiwa anajaribu kuitapika sumu ambayo bila shaka naye aliila kwenye kile chakula. Nilipiga makofi kwa nguvu na kumshtua yule mtu ambaye aliligeuka huku akiwa anacheka sana.

"Wewe malaya umetusaliti sisi? Unajua bosi atakacho kufanya akijua kwamba wewe ndiye umefanya hili tukio na umewaza kitakacho ikuta familia yako?" Aliongea kwa hasira akiwa anamtazama Nikole.

"Kuwa makini ni mtu hatari sana kwenye mapigano" Nikole aliongea akiwa anaitoa bastola yake lakini alikuwa amechelewa maana mwanaume yule alikuwa ameitoa kabla yake. Niliichukua bastola hiyo kwenye mikono ya Nikole na kumpa ishara ya kwamba alitakiwa kupigana naye na siyo kushindana kwa risasi ila Nikole alienda kwa kusita sita sana nikawa nimegundua kwamba alikuwa anamuogopa sana mtu huyo. Nikole alikuwa anasogea kwa hofu sana, nililitambua hilo lakini niliamua kufanya vile ili nipate hata dakika moja ya kuizoea hali ya pale nje maana kutoka tu na kuanza kupigana ingeniletea shida kubwa sana ambayo huenda ingenifanya nipoteze pambano ambalo lingenirudisha mle ndani.

Mwanaume yule alimtisha Nikole akiwa hajarusha ngumi hata moja alikwepa teke Kali lakini alikuwa amesimama kizembe sana maana alipigwa mtama makali huku akipigwa na mateke yote mfululizo kama sio mimi kumdaka huenda angeumia vibaya sana kwa kujipigiza ukutani. Baada ya kumsimamisha tena, mwanaume yule alikuwa anakuja kwa kasi ila niliona atatupotezea sana muda niliingilia na kumpiga teke la shingo ambalo lilimfanya ayumbe na kwenda kuegemea ukuta akiwa anatokwa na damu nyeusi mdomoni ambapo bila shaka ilikuwa ni ile sumu ambayo aliila kwenye chakula.

Wakati anaegemea ule ukuta alikuwa ameshajipotezea maisha yake tayari maana kwa hali ambayo alikuwa nayo asingeweza kabisa kukikwepa kisu ambacho nilikirusha kwa nguvu sana kilizama kwenye shingo yake mpaka kikaenda kukita kwenye ukuta baada ya kutoboa toboa shingo yake.

"Twende haraka hawa watu watakuwa hapa sasa hivi" Nikole aliongea akiwa anajifuta damu puani na kuonekana mwenye hofu sana.

"Umejuaje?" Nilimuuliz huku akiwa analifungua geti la kutokea nje.
"Ile alamu ambayo imepigwa, watu wale wanapata taarifa moja kwa moja kwenye simu zao hivyo watajua kwamba kuna tatizo watatuma watu kuja"
"Ok, familia yako ulikumbuka kuihamisha?"
"Ndiyo, nilijua wanaweza wakaanza nao hivyo nimewapeleka sehemu salama ambayo nitakaa nao huko mpaka nitakapo pata nafasi ya kutoka nje ya nchi hii"

"Unapenda kuishi Rwanda?" Nilimuuliza baada ya kuiona hofu yake
"Ndiyo, nimezaliwa Rwanda, napapenda sana na nilikuwa naipenda sana kazi yangu ila tulipo fikia sina namna tena"

"Nenda kaiweke familia yako eneo lililo salama zaidi, ila tu usiondoke kwani watakukamata mpakani. Ndani ya muda mfupi ujao hii serikali yenu itatolewa madarakani"
"Nani ataitoa?"

"Mimi ni jasusi kutoka ndani ya nchi ya Tanzania, huyu mtu ambaye aliniteka anahusika na ulipuaji wa bunge la nchi yetu hivyo nilikuwa hapa kwa ajili ya kuifanya kazi ya kuwajua watu ambao walikuwa wapo nyuma yake na kwa bahati mbaya akawa amewahi kunikamata hivyo mimi natakiwa kufika nyumbani kwa namna yoyote ile na baada ya hapo huyu mtu kuna watu watakuja kumchukua kimabavu na huo uovu wa raisi wenu utawekwa wazi nadhani nchi itakuwa yenye amani na mtaendelea na maisha ya kawaida, hata wewe nina uhakika utarudi kwenye kazi yako ambayo unaipenda sana" alikuwa amefurahi sana baada ya kulitambua hilo na ndipo nilipo furahi sana baada ya kumuona yule dereva wangu.

"Sister kumbe ushakuwa mwenyeji kabisa, hadi sehemu kama hii unaijua?" aliuliza kwa uchangamfu mkubwa sana

"Ndiyo kuna bishara ambayo imenileta mara moja, washa gari haraka twende Nyarutarama ila pia kuna mahali unatakiwa kunipeleka haraka" niliongea kwa sauti ambayo hata yeye alielewa kwamba sikuwa nahitaji mazoea kabisa, akawa ametulia vizuri. Baada ya kutembea mwendo wa kama dakika thelathini, kuna magari ambayo tulipishana nayo yakiwa kwenye mwendo mkali kuelekea kule ambako sisi tulitoka. Nikole alinikonyeza hapo nikaelewa kwamba ni watu wa Blaise Norbert.

"Usipite uwanja wa ndege wana watu kibao pale ambapo kama ukifika tu basi lazima wakukamate, una njia moja ya pekee ya kupita japo ni ngumu sana. Pitia ndani ya hifadhi ya Akagera, licha ya kuwa na baadhi ya wanyama hatari ila pia ni hifadhi ambayo inalindwa sasa na wanajeshi wa nchi ya Rwanda ikiwa chini ya kampuni la Akagera huku wakifanya kazi sambamba na shirika la hifadhi la nchi ya Rwanda liitwalo Rwanda Development Board. Hawa watu ni makatili sana wakikukamata kwani hawana huruma kabisa, wanafanya jambo lolote lile ili kuhakikisha wanyamapori wanakuwa salama hivyo wakikikukuta huko moja kwa moja watajua wewe ni muwindaji haramu hawawezi kukuacha"

"Licha ya kuwakwepa watu hao ila pia hakikisha wakati unaingia ndani ya hifadhi hiyo unavaa mabuti mazito sana, vaa gloves mikononi pamoja na nguo nzito nzito ila tu usivae nguo zenye rangi ya blue, zingatia sana hilo"

"Ukifika pale kama utatumia gari ya kawaida ni mwendo wa masaa mawili mpaka mtatu japo pia huwa kuna ndege ndogo ambazo huwa zinaenda kuko. Ukifanikiwa kufika pale kuhusu kuingia ni rahisi sana kwa sababu hata kama hauna vielelezo ukiwa na pesa tu unahonga na unaingia ndani ya hifadhi hiyo ila sasa ukikamatwa huko ndani ndo utakuwa hauna msaada maana utatakiwa kuweza kujitetea kwa namna unayohisi inakufaa wewe na kama ukishindwa watakufanyia ukatili ambao huenda hukuwahi kuuona"

"Ni mashariki mwa Kigali mahali ilipo hifadhi hiyo na hata ili kuweza kufika kwenu Tanzania bado utatakiwa kwenda upande wa mashariki ambapo utatokea ndani ya mkoa wa Kagera. Kitu pekee cha kufanya kama utabahatika kupita salama maeneo yote humo ndani ya hiyo hifadhi, utakutana na ziwa ambalo linaitwa Ihema, hilo ziwa haliruhusiwi kabisa kuendesha ishu za uvuvi wala mambo yoyote ambayo yatahatarisha usalama wa hifadhi. Ziwa hilo ndilo njia pekee ya wewe kufika kwenu Tanzania kwani ndilo linalo itenganisha Tanzania na Rwanda na hapo ili usafiri lazima utumie usafiri wa boti"

"Unalipa kwa dola, ili usafirishwe haraka wape pesa nyingi nadhani utakuwa umetokea upande wa Kagera ambako utakuwa salama na unaweza kufika ndani ya jiji la Dar es salaam kiwepesi sana" hayo yalikuwa maneno ya Nikole akiwa anaongea sauti ya chini sana ili dereva asiweze kusikia kile ambacho tulikuwa tunakizungumza.

Nilimshukuru sana, nikamhamishia kwenye akaunti yake milioni miatano kisha akashukia sehemu ambayo hata sikuwa naijua. Nilichukua vitu vyangu vya mhimu mwenye ile apartment kisha nikaianza safari ya kuelekea ndani ya hifadhi ya Akagera. Hifadhi ambayo ilinifanyia ukatili mkubwa wa nafsi nikatamani ni bora ningebaki kule kule kwenye lile jengo la Blaise Norbert kuwafurahisha wale wanaume, maana kuingia kwenye ile Hifadhi ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kuingia kwenye maisha magumu sana ya kunifanya nipoteze hata uwezo wangu kichwani nikaishia kuwa kama kichaa ambapo sikujua hata ndani ya Pwani niliwezaje kufika ambapo nimekuja kushtuka kaka yangu ukiwa mbele ya macho yangu, lakini wanasema ni bora kuthubutu maana ndiko kufanya nami nilithubutu" hiyo ni simulizi ya maisha ya dada yake ambayo Calvinjr alikuwa anaikumbuka vyema sana tena kwa uchungu ambayo alisimuliwa na dada yake kipenzi Tina.

Wakati huo Calvinjr alishtuliwa kwenye hiyo ndege ya abiria ambayo alikuwa amepanda yeye na mama yake, ni mama yake mzazi ambaye alimkurupua mwanae kutoka kwenye hiyo kumbu kumbu ambapo mama yeye alihisi mwanae alilala lakini haikuwa kweli. Walikuwa ndani ya Kigali International Airport ndani ya nchi ya Rwanda ili kuhakikisha wote walio mfanyia ukatili Tina wanapata kile wanacho stahili kwa mujibu wa sheria ikiwa ndiyo akili ya mama huyo lakini mwanaume alikuwa na kazi za ziada ya kuweza kuifanya ndani ya hilo jiji la Kigali.

Calvinjr tayari yupo ndani ya jiji la Kigali, una hamu ya kujua hili jiji linaenda kupitia yapi kupitia mkono wa huyu jasusi ambaye umejua wazi kwamba ni mtoto wa damu kabisa wa yule kiumbe hatari Calvin Jackson? Maandishi haya yatatupa majibu sahihi.

Episode ya 72 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Daah,tamu sana hii stori.Umetisha sana mwandishi
 
Itabidi utiambie Yule mhuni aliyemfanyia uhuni alijisikiaje baada ya mzee baba kuwa mkuu wa suti nyeusi😂😂
 
Ilishafika mwisho au mpaka jamaa ajisikie. Mtu chake bhana.
Mkuu let me be very clear to you: sijisikii na wala siileti kwa kujisikia.

Binafsi sijajua maandishi huwa unayachukuliaje ila maandishi ni biashara kama ambavyo wewe unawekeza nguvu zako kwenye kazi au biashara nyingine ila tupo kwenye taifa ambalo waandishi tunahesabika kama watu wa charity.

NB.
Sitaileta tena hapa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu let me be very clear to you: sijisikii na wala siileti kwa kujisikia.

Binafsi sijajua maandishi huwa unayachukuliaje ila maandishi ni biashara kama ambavyo wewe unawekeza nguvu zako kwenye kazi au biashara nyingine ila tupo kwenye taifa ambalo waandishi tunahesabika kama watu wa charity.

NB.
Sitaileta tena hapa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sawa mkuu tunashukuru hata kwa hapa tulipofikia ilipobakia tutatengeneza wenyewe mwisho wake
 
Mkuu let me be very clear to you: sijisikii na wala siileti kwa kujisikia.

Binafsi sijajua maandishi huwa unayachukuliaje ila maandishi ni biashara kama ambavyo wewe unawekeza nguvu zako kwenye kazi au biashara nyingine ila tupo kwenye taifa ambalo waandishi tunahesabika kama watu wa charity.

NB.
Sitaileta tena hapa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Tatizo mnaleta wenyewe kwa hiari yenu lakini mkiulizwa kama hivi mnaanza lawama.

Kama ulikuwa umefika mwisho basi ungesema.

Nb;Na hapa suala si nayachukuliaje maandishi, bali ni kazi km wengine walivyo na kazi zao. Kwa sababu hata mimi nikikupa kazi yangu uifanye hutaweza.

Naona ulikaa kimya kimtego kutafuta mtu aongee ili upate pa kuchomokea. Tutakuuliza tu hata ufanyeje! Hakuna haja ya kuleta story halafu unakaa mwezi ndiyo uje tena.

Kuna wengine waliacha kusoma story za humu.

But ulikuja kwa hiari na umeondoka kwa hiari , usitafute vimaneno maneno.

USHAURI

Unapoleta kazi yako ni bora ukasema nitaleta episodi kiasi fulani na baada ya hapo ni biashara.. Unatutafutaga ugomvi wewe.


HONGERA KWA KAZI NZURI NIMEZIPENDA KAZI ZAKO.
Ngoja nirudi Jijini nikacheze kamari. ASANTE na KARIBU!
 
Tatizo mnaleta wenyewe kwa hiari yenu lakini mkiulizwa kama hivi mnaanza lawama.

Kama ulikuwa umefika mwisho basi ungesema.

Nb;Na hapa suala si nayachukuliaje maandishi, bali ni kazi km wengine walivyo na kazi zao. Kwa sababu hata mimi nikikupa kazi yangu uifanye hutaweza.

Naona ulikaa kimya kimtego kutafuta mtu aongee ili upate pa kuchomokea. Tutakuuliza tu hata ufanyeje! Hakuna haja ya kuleta story halafu unakaa mwezi ndiyo uje tena.

Kuna wengine waliacha kusoma story za humu.

But ulikuja kwa hiari na umeondoka kwa hiari , usitafute vimaneno maneno.

USHAURI

Unapoleta kazi yako ni bora ukasema nitaleta episodi kiasi fulani na baada ya hapo ni biashara.. Unatutafutaga ugomvi wewe.


HONGERA KWA KAZI NZURI NIMEZIPENDA KAZI ZAKO.
Ngoja nirudi Jijini nikacheze kamari. ASANTE na KARIBU!
Umemaliza yote,huyu jamaa sjui ametuchukuliaje.?Unaleta hadithi kwa hiari afu unaanza maneno madogo madogo kwa wasomaji wako.
 
Back
Top Bottom