STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
FINAL EPISODE..............
TANZANIA
Mheshimiwa raisi Theobald Mnyika alikuwa ndani ya ofisi yake kwenye jumba lake kubwa hilo ambalo lilikuwa Mbezi beach. Tangu siku ya jana yake alikuwa akipiga simu nchini Rwanda kwa vijana wake hasa baada ya kuona mambo yameenda hovyo sana lakini simu hizo hazikuwa zikipokelewa kabisa, alichukia sana.
Alihisi kwamba vijana wale huenda walikuwa wanazidharau simu zake hivyo aliapa kwamba angawafanyia kitu kibaya sana pale ambapo angemaliza jambo hilo la Calvinjr kwanza ambalo lilionekana kuwa mbele yake. Pembeni yake alikuwepo kijana wake mtiifu Lestus Mzopari.
Akiwa anayawaza mambo hayo ambayo yalitokea tangu siku ya jana ndipo akaipokea taarifa ambayo ilikuwa mbaya sana kwa upande wake baada ya kuona kila kitu kilikuwa kmeharibiwa Rwanda, raisi Stophila Msanzu alipinduliwa madarakani huku kambi ambayo ilidaiwa kuwa ya M23 ikivamiwa na mtu asiye juliakana ambayo ilifichwa ndani ya hifadhi ya Nyungwe na mtu huyo akafanikiwa kuwaokoa watu wote na kuwaua magaidi wote. Wananchi wa Rwanda walikiwa wanatamani sana mtu huyo ajitokeze hadharani ili wampe asante yakd.
"Son of a b*****" alitukana akipigiza mkono wake kwenye meza kwa nguvu, licha ya kutotajwa kwenye jambo lile ila kila kilicho haribiwa kuanzia zile mali na fedha zilikuwa ni zake hivyo aliingizwa hasara moja ndefu sana. Msaidizi wake alikuwa anamjua sana bosi wake anapokuwa kwenye hiyo hali hakuthubutu hata kumuongelesha.
"Hii habari inaonekana kwamba tumechelewa kuipata, imetokea masaa mangapi yaliyopita?"
"Manne mkuu"
"Ina maana sasa ni saa kumi usiku uivyo imetokea saa sita usiku?"
"Ndiyo mkuu japo ilianza mapema kabla ya hapo maana kuna baadhi ya vyombo vya habari nchini Rwanda vimeripoti habari hiyo mapema japo vingi vimeripoti masaa manne yaliyo pita"
"Kutoka Rwanda mpaka Tanzania ni muda gani kwa ndege?"
"Masaa mawili tu kiongozi"
"Shiiit! Kwahiyo huyu mpuuzi lazima tayari amerudi nchini" aliongea akiwa na jaziba sana. Alihitaji watu wake waweze kuletwa pale sebuleni alihitaji kuwaua kwani aliona kama kijana wao alikuwa amemuingiza kwenye hasara moja kubwa sana na ilibakia kidogo naye atajwe kwenye lile tatizo ambapo hata hajui kama angewajibu nini watanzania.
Familia ya Calvinjr iletwa mbele yake huku akiwa na bastola mkononi, alimkwinda mkurugenzi Gulamu Leopard shingoni ambaye alikuwa amefungwa na kamba mikononi.
"Kwahiyo huyo kijana anajiona hodari sana sio, unajua kaniingiza hasara kiasi gani? Kaniulia watu wangu wote kisha amefanya wananchi wa Rwanda wampindue raisi wao unahisi naweza kuwaacha kwa hilo? Hahahaha lazima naye apitie maumivu makali sana kama ambayo napitia mimi kupoteza mali zangu, na sehemu ambayo nina imani kwamba ataumia sana ni kuwaua wale awapendao" alitamka kwa hasira sana.
"Nilikuonya mapema sana ila haukutaka kunielewa, sasa kinacho fuatia ni zamu yako wewe hapo maana yake anarudi na ushahidi wote kuhusu utumbo na ukatili ambao ulikuwa unaufanya huku ukijifanya kiongozi hodari sana mbele ya watu wasio kufaha....." Mr Gulamu Leopard hakuimalizia kauli yake kwani alipigwa risasi ya paja na kugugumia kwa maumivu makali sana.
"Mpuuzi wewe nakufuga mwenyewe leo unataka kunipandishia kibezi na kuanza kunitishia mimi? Leo naua familia nzima na huyo mjinga nampoteza na hakuna mtu atajua lolote kuhusu mimi hivyo siri zangu zinaendelea kuishi, nitaiba mali nyingi za wananchi na nitajijenga upya, hahahahahhaha" aliongea kwa majivuno huku akiwa anamsogelea mama yake Calvinjr ambapo alimuwekea bastola kichwani na kutaka kuachia risasi ila alisikia sauti.
"Ukimgusa huyo mama nakuua" ilikuwa ni sauti ya Imrani ambaye ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa familia hiyo, mheshimiwa raisi alisimamisha zoezi lake na kumsogelea huyo mwanaume.
"Ni nani wewe ambaye unaonekana kuwa na uchungu sana na familia hii? Nakuuliza wewe ni nani ambaye unaweza kuja na kumtishia kifo raisi wa nchi" aliongea kwa nguvu na hasira sana huku akiwa anampiga Imran risasi nyingi sana kichwani wote wakabaki wanatetemeka isipokuwa mkurugenzi. Kichwa cha mwanaume hiyo kiliharibiwa vibaya sana damu tu ikawa imetapakaa pale chini. Mama Calvinjr alikuwa analia kwa uchungu sana kwani mwanaume huyo aliitoa familia hiyo mbali sana licha ya kulipwa pesa nyingi ila aligeuka kuwa kama ndugu. Raisi aliichomoa bastola nyingine kiunoni kwake.
"Leo nataka niwaonyeshe huo upande wangu ambao mmekuwa mkisimuliwa tu ili mnijue vyema" aliongea akiwa anamsogelea mama huyo tena ili ampige risasi, Tina hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutoa machozi huku akiwa amebanwa na mbavu wawili. Sarafina tu pekee ndiye ambaye hakufungwa kabisa ila ndiye aliyekuwa anatetemeka zaidi maana kwenye maisha yake hakuwahi kabisa kuyazoea mambo ya kutisha kama hayo, akawa amejikunyata huku ameinama chini analia.
Akiwa anataka kuachia risasi hiyo kuna mlinzi alikuja akiwa anakimbia kwa kasi sana
"Mkuu kuna wageni wawili wamefika, mwanaume na mwanamke"
"Unawafahamu?"
"Hapana ila wamesema ni watu ambao unawatafuta sana"
"Walete mkiwa walinzi wengi sana, hakikisha hawana silaha yoyote ile"
"Sawa mkuu" mwanaume huyo alijibu akiwa anakimbilia nje kuwaleta watu hao. Kila mtu alibaki amechoka, mtu ambaye aliingia hapo alikuwa ni Calvinjr akiwa ameongozana na Mr Dark au waweza kumuita Eliza Boniphace. Mwanaume alikuwa ndani ya suti ya bei ghali mno hivyo hivyo hata mwanamke huyo Eliza alikuwa ndani ya suti kali mkononi mwake akiwa na laptop yake tena akitembea kwa mikogo.
Sarafina licha ya yote aliyokuwa ameyajua kwa mwanaume huyo hakuyajali, alimkimbilia na kumbusu kwa hisia kali sana, alijihisi amani sana mbele ya mwanaume wake. Calvinjr alimketisha chini mwanamke huyo na kwenda kupiga magoti mbele ya mama yake mzazi kama alivyokuwa anahisi yeye.
"Naomba unisamehe sana mama, nisamehe sana kwa kumuona mwanao kwenye hali kama ile nastahili adhabu yoyote kutoka kwako" aliongea akiwa na uchubgu sana, alikuwa akimpenda sana mama yake, huyo na dada yake alikuwa ndiye kila kitu kwake na wakati huo alikuwa anamfungua mama huyo kamba ambazo zilikuwa kwenye mkono wake kisha akalaza kichwa chake chini ya miguu ya mama huyo kama kumuomba msamaha.
Licha ya kwamba hakuwa mwanae wa kumzaa ila alikuwa akimpenda mno mtoto huyo, huyo kwake alikuwa ni kila kitu, alimuinua na kumkumbatia, Calvinjr aligeuka na kumkonyeza dada yake na kwenda kumfungua kisha akamfunga na bosi wake ambaye alimsikitikia kwa hali ambayo alikuwa nayo.
Mheshimiwa raisi alikuwa anawaangalia tu watu hao kwa hasira sana, aliacha wamalize kujishaua kisha angedili nao vizuri.
"Wewe mpumbavu u....."raisi alitaka kuongea ila alizuiwa na mwanaume huyo.
"Shiiiiii!" Mama yangu huwa hapendi kabisa makelele. Nimekuja hapa kistaarabu baada ya kugundua kwamba wewe ni baba mzazi wa Sarafina hivyo nikaamua kuja na kuyaacha maisha yako ili wananchi ndo waamue kama watakuacha hai au watakuua" kauli ya mwanaume ilimpa tabasamu, akajua hapa nina jambe ila iliyo fuatia baada ya hapo haikuwa nzuri kwa wote kwani walibaki wanaangaliana wasiamini kile kinacho endelea.
"Sara naomba unisamehe sana ila huyu ndiye baba yako mzazi na ndiye mtu ambaye amehusika kwenye kila udhalimu wa nchi hii. Najua huenda hautanisamehe ila ukiamua hivyo ni sawa, jambo ambalo linaenda kutokea hata mama yako atahusika maana bila kukusudia alihusika kutekeleza shambulio hilo ambapo anaweza kufungwa mpaka miaka mitano jela ila huyu hata nafasi ya kufungwa hiyo miaka mia moja hana huenda kifo ndiyo adhabu yake bora zaidi" mwanaume aliongea bila kupepesa mambo.
"Wewe mpuuzi unajua unaongea na raisi hapa, nimewaacha mfanye maigizo yenu kwa sabab Leo ndio mwisho wa maisha yenu wote ambao mpo humu ndani?" raisi alijigamba huku akiwa ananyoosha bastola yake kuielekeza kule alipokuwepo Calvinjr.
"Sawa mimi nitakuacha ufanye unacho kitaka wewe ila baada ya kuiona video hii kwanza" mwanaume aliongea bila wasiwasi akiwa anaichukua rimoti mezani na kuiwasha runinga hiyo humo ndani eneo hilo likiwa limezungukwa na wanaume wenye silaha nzito. Mheshimiwa raisi naye aligeuka kuona lilichokuwa kinafanyika ila cha ajabu ilikuwa ni chaneli ya vipindi vya kawaida.
Wakati hao wote wakiwa wanamshangaa Calvinjr maana hakukuwa na chochote, Mr Dark alikuwa ameinamia kwenye laptop yake, ghafla sana mambo yakabadilika ikawa inaonekana Video ya Madilu akiwa anaelezea uhusika wa raisi huyo kwenye kulipua bunge la nchi ambalo alililipua na watu wote ambao yeye alikuwa amewaua miamoja tisini na tisa.
Akiwa kwenye huo mshangao wa kuona hizo video zake zote ambazo zilikuwa zinamuelezea huo upande wake wa pili, ilionyeshwa mpaka video ya yule mke wa waziri wa ardhi akiwa anakiri kwamba alilazimishwa na watu wa Ikulu kusema uongo ili kuwaokoa wanae.
Hiyo haikutosha ndipo zilikuja taariza za hiyo DOCUMENT namba 72 ambayo kiongozi wao aliandikwa kwa code maalumu A.H, TOP official 255 ikiwa na maana ya Anorld Hazole, kiongozi mkuu wa Tanzania. Watu waliwekwa wazi mpaka namna mheshimiwa huyo alivyoweza kudanganya jina ili ayapate madaraka.
Hiyo kazi ilifanywa na Mr Dark ambaye alihaki vyombo vya habari vikubwa vyote nchini na ndipo akaisambaza habari hiyo. Calvinjr alizamisha mikono kifuani kwake na kuitoa DOCUMENT hiyo namba 72 ikiwa na idadi ya watu tisa.
"Kill them" raisi huyo alitamka akiwa anawapa amri walinzi wale lakini kitu cha kushangaza wale walinzi wote walimgeukia yeye na kumuweka chini ya ulinzi yeye na kijana wake Lestus Mzopari wakati huo mkurugenzi alitembea kwa kuchechemea na kwenda kuichukua bastola mikononi mwa raisi huyo na kumtandika risasi mbili za magotini kama kulipiza.
"Nilianza kukuhisi mapema sana mpuuzi wewe sema sikuwa na uhakika hivyo nikasambaza vijana wangu kila sehemu maana nilijua ipo siku kama ya leo itatokea. Hao wananisikiliza mimi tu maana ni majasusi wangu halafu wameshajua kwamba wewe ni mhalifu unahisi nani yupo tayari kwenda kunyongwa na wewe? Take him away" alimpa sababu iliyofanya vijana hao wamgeukie yeye huku akimtia kibao kikali sana shavuni akiwataka watu hao wampeleke anako stahili ila yule Lestus Mzopari alimpiga risasi ya kichwa pale pale.
Sasa Calvinjr alikalishwa chini na kusimuliwa historia nzima ya maisha yake maana alikuwa anastahili kuweza kuujua ukweli wote. Calvinjr aligoma na kuhisi kwamba labda watu hao walikiwa wakimtania tu ila wilimhakikishia kwamba huo ndo ukweli.
Aliumia na kutoa machozi akiamini kwamba familia yake ilimsaliti.
"Yuko wapi huyo mwanmke ambaye alinisaliti mimi?" Aliongea kwa hasira sana kumuulizia huyo mama yake mzazi ambaye alimfanya alelewe na mwanamke mwingine huku yeye akiwa upande mwingine wa dunia. Kazi nzito ambayo alikuwa ameifanya, aliamini kwamba huo ulikuwa ni wakati sahahi wa kufurahia na familia yake lakini mambo ya ajabu yalikuwa yanaendelea wakati huo kwa kukutana na taarifa mbaya kama hizo.
Wakati hayo yote yanaendelea akitaka kujibiwa na kujua mama yake huyo alikuwa wapi maana alihitaji kumuona ili akayajibu maswali ya mtoto huyo, alishangaa kumuona mama yake aliye mlea ambaye muda mfupi alitoka kumpa ukweli kwamba hakuwa mama yake mzazi pamoja na mkurugenzi wa shirika la kijasusi bwana Gulamu Leopard wakiinamisha vichwa chini kama kutoa heshima kwa mtu ambaye walikuwa wakimheshimu sana, hapo ndipo akageuka maana alihisi mlangoni kuna mtu.
Alishangaa sana na kushtuka mno, yule mtu ambaye alikuwa nyuma alikuwa ni master wake ambaye alimtengeneza kuwa binadamu hatari sana namna hiyo ila mtu ambaye alikuwa mbele ya master wake ndiye huyo ambaye alionekana kupewa heshima na mama yake pamoja na Mr Gulamu Leopard.
Kitu ambacho kilimshangaza sio tu watu hao kutoa heshima au master wake kufika hapo bali ni kile ambacho alikiona. Aliiona sura yake mbele yake, walichokuwa wamepishana ulikuwa ni umri tu ila sura hizo zilikuwa zinafanana kila kitu, akalazimika kujishika usoni maana alkuwa ni kama kwenye ndoto aisee.
Aliyekuwa mbele yake, alikuwa ni mtaamu wa zamani sana, Calvin Jackson Aron Mavunde, huyo ndiye alikuwa baba yake mzazi kabisa na ndiye ambaye alikuwa anaitwa Calvin mwenyewe mpaka yeye akapewa jina la Calvin Jr ikiwa ina maana ya Junior kwamba yeye ni mdogo na huyo ndiye baba mwenyewe ambaye ndo Calvin senior maana kila kitu walikuwa sawa.
Naam, ulikuwa nami tangu mwanzo mpaka nafika wa simulizi hii bora sana. Nisema tu asante kwako kwa kuweza kuigusa kalamu hii na kuwa moja ya watu ambo wamebahatika kulisoma andiko hili, natanguliza shukrani nyingi sana za dhati.
Kuisha kwa simulizi hii ni mwanzo mzuri zaidi wa chapter ya tatu ya simulizi hii ambayo itakwenda kwa jina la KALAMU ILIYO TUMWA KUNIUA,baada ya kufanikisha kuisoma sehemu ya kwanza kabisa ya andiko hili ambayo inakwenda kwa jila la ULIMWENGU WA WATU WABAYA.
Leo nakusanya kila kilicho changu najitoa kwenye chumba ambacho nilijifungia kwa muda mrefu sana kuiandaa simulizi hii panapo majaaliwa tutakutana tena wakati mwingine.
Wasalaam.
Wako,
FEBIANI BABUYA.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app