Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Stori nzuri hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi nimependa uandishi wako hakika naburudika . Baada ya hii nakucheki whatsapp ninunue kazi zako zingine. Bravo
Shukrani sana mkuu.Kiongozi nimependa uandishi wako hakika naburudika . Baada ya hii nakucheki whatsapp ninunue kazi zako zingine. Bravo
Habari njemaTukutane baadae kuhitimisha andiko hili [emoji996].
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu mbona statement niliyo itoa inajitosheleza kabisa.Tunasubiri Mwendelezo.
Au ndio imeisha?
ShukranSTORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
FINAL EPISODE..............
TANZANIA
Mheshimiwa raisi Theobald Mnyika alikuwa ndani ya ofisi yake kwenye jumba lake kubwa hilo ambalo lilikuwa Mbezi beach. Tangu siku ya jana yake alikuwa akipiga simu nchini Rwanda kwa vijana wake hasa baada ya kuona mambo yameenda hovyo sana lakini simu hizo hazikuwa zikipokelewa kabisa, alichukia sana.
Alihisi kwamba vijana wale huenda walikuwa wanazidharau simu zake hivyo aliapa kwamba angawafanyia kitu kibaya sana pale ambapo angemaliza jambo hilo la Calvinjr kwanza ambalo lilionekana kuwa mbele yake. Pembeni yake alikuwepo kijana wake mtiifu Lestus Mzopari.
Akiwa anayawaza mambo hayo ambayo yalitokea tangu siku ya jana ndipo akaipokea taarifa ambayo ilikuwa mbaya sana kwa upande wake baada ya kuona kila kitu kilikuwa kmeharibiwa Rwanda, raisi Stophila Msanzu alipinduliwa madarakani huku kambi ambayo ilidaiwa kuwa ya M23 ikivamiwa na mtu asiye juliakana ambayo ilifichwa ndani ya hifadhi ya Nyungwe na mtu huyo akafanikiwa kuwaokoa watu wote na kuwaua magaidi wote. Wananchi wa Rwanda walikiwa wanatamani sana mtu huyo ajitokeze hadharani ili wampe asante yakd.
"Son of a b*****" alitukana akipigiza mkono wake kwenye meza kwa nguvu, licha ya kutotajwa kwenye jambo lile ila kila kilicho haribiwa kuanzia zile mali na fedha zilikuwa ni zake hivyo aliingizwa hasara moja ndefu sana. Msaidizi wake alikuwa anamjua sana bosi wake anapokuwa kwenye hiyo hali hakuthubutu hata kumuongelesha.
"Hii habari inaonekana kwamba tumechelewa kuipata, imetokea masaa mangapi yaliyopita?"
"Manne mkuu"
"Ina maana sasa ni saa kumi usiku uivyo imetokea saa sita usiku?"
"Ndiyo mkuu japo ilianza mapema kabla ya hapo maana kuna baadhi ya vyombo vya habari nchini Rwanda vimeripoti habari hiyo mapema japo vingi vimeripoti masaa manne yaliyo pita"
"Kutoka Rwanda mpaka Tanzania ni muda gani kwa ndege?"
"Masaa mawili tu kiongozi"
"Shiiit! Kwahiyo huyu mpuuzi lazima tayari amerudi nchini" aliongea akiwa na jaziba sana. Alihitaji watu wake waweze kuletwa pale sebuleni alihitaji kuwaua kwani aliona kama kijana wao alikuwa amemuingiza kwenye hasara moja kubwa sana na ilibakia kidogo naye atajwe kwenye lile tatizo ambapo hata hajui kama angewajibu nini watanzania.
Familia ya Calvinjr iletwa mbele yake huku akiwa na bastola mkononi, alimkwinda mkurugenzi Gulamu Leopard shingoni ambaye alikuwa amefungwa na kamba mikononi.
"Kwahiyo huyo kijana anajiona hodari sana sio, unajua kaniingiza hasara kiasi gani? Kaniulia watu wangu wote kisha amefanya wananchi wa Rwanda wampindue raisi wao unahisi naweza kuwaacha kwa hilo? Hahahaha lazima naye apitie maumivu makali sana kama ambayo napitia mimi kupoteza mali zangu, na sehemu ambayo nina imani kwamba ataumia sana ni kuwaua wale awapendao" alitamka kwa hasira sana.
"Nilikuonya mapema sana ila haukutaka kunielewa, sasa kinacho fuatia ni zamu yako wewe hapo maana yake anarudi na ushahidi wote kuhusu utumbo na ukatili ambao ulikuwa unaufanya huku ukijifanya kiongozi hodari sana mbele ya watu wasio kufaha....." Mr Gulamu Leopard hakuimalizia kauli yake kwani alipigwa risasi ya paja na kugugumia kwa maumivu makali sana.
"Mpuuzi wewe nakufuga mwenyewe leo unataka kunipandishia kibezi na kuanza kunitishia mimi? Leo naua familia nzima na huyo mjinga nampoteza na hakuna mtu atajua lolote kuhusu mimi hivyo siri zangu zinaendelea kuishi, nitaiba mali nyingi za wananchi na nitajijenga upya, hahahahahhaha" aliongea kwa majivuno huku akiwa anamsogelea mama yake Calvinjr ambapo alimuwekea bastola kichwani na kutaka kuachia risasi ila alisikia sauti.
"Ukimgusa huyo mama nakuua" ilikuwa ni sauti ya Imrani ambaye ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa familia hiyo, mheshimiwa raisi alisimamisha zoezi lake na kumsogelea huyo mwanaume.
"Ni nani wewe ambaye unaonekana kuwa na uchungu sana na familia hii? Nakuuliza wewe ni nani ambaye unaweza kuja na kumtishia kifo raisi wa nchi" aliongea kwa nguvu na hasira sana huku akiwa anampiga Imran risasi nyingi sana kichwani wote wakabaki wanatetemeka isipokuwa mkurugenzi. Kichwa cha mwanaume hiyo kiliharibiwa vibaya sana damu tu ikawa imetapakaa pale chini. Mama Calvinjr alikuwa analia kwa uchungu sana kwani mwanaume huyo aliitoa familia hiyo mbali sana licha ya kulipwa pesa nyingi ila aligeuka kuwa kama ndugu. Raisi aliichomoa bastola nyingine kiunoni kwake.
"Leo nataka niwaonyeshe huo upande wangu ambao mmekuwa mkisimuliwa tu ili mnijue vyema" aliongea akiwa anamsogelea mama huyo tena ili ampige risasi, Tina hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutoa machozi huku akiwa amebanwa na mbavu wawili. Sarafina tu pekee ndiye ambaye hakufungwa kabisa ila ndiye aliyekuwa anatetemeka zaidi maana kwenye maisha yake hakuwahi kabisa kuyazoea mambo ya kutisha kama hayo, akawa amejikunyata huku ameinama chini analia.
Akiwa anataka kuachia risasi hiyo kuna mlinzi alikuja akiwa anakimbia kwa kasi sana
"Mkuu kuna wageni wawili wamefika, mwanaume na mwanamke"
"Unawafahamu?"
"Hapana ila wamesema ni watu ambao unawatafuta sana"
"Walete mkiwa walinzi wengi sana, hakikisha hawana silaha yoyote ile"
"Sawa mkuu" mwanaume huyo alijibu akiwa anakimbilia nje kuwaleta watu hao. Kila mtu alibaki amechoka, mtu ambaye aliingia hapo alikuwa ni Calvinjr akiwa ameongozana na Mr Dark au waweza kumuita Eliza Boniphace. Mwanaume alikuwa ndani ya suti ya bei ghali mno hivyo hivyo hata mwanamke huyo Eliza alikuwa ndani ya suti kali mkononi mwake akiwa na laptop yake tena akitembea kwa mikogo.
Sarafina licha ya yote aliyokuwa ameyajua kwa mwanaume huyo hakuyajali, alimkimbilia na kumbusu kwa hisia kali sana, alijihisi amani sana mbele ya mwanaume wake. Calvinjr alimketisha chini mwanamke huyo na kwenda kupiga magoti mbele ya mama yake mzazi kama alivyokuwa anahisi yeye.
"Naomba unisamehe sana mama, nisamehe sana kwa kumuona mwanao kwenye hali kama ile nastahili adhabu yoyote kutoka kwako" aliongea akiwa na uchubgu sana, alikuwa akimpenda sana mama yake, huyo na dada yake alikuwa ndiye kila kitu kwake na wakati huo alikuwa anamfungua mama huyo kamba ambazo zilikuwa kwenye mkono wake kisha akalaza kichwa chake chini ya miguu ya mama huyo kama kumuomba msamaha.
Licha ya kwamba hakuwa mwanae wa kumzaa ila alikuwa akimpenda mno mtoto huyo, huyo kwake alikuwa ni kila kitu, alimuinua na kumkumbatia, Calvinjr aligeuka na kumkonyeza dada yake na kwenda kumfungua kisha akamfunga na bosi wake ambaye alimsikitikia kwa hali ambayo alikuwa nayo.
Mheshimiwa raisi alikuwa anawaangalia tu watu hao kwa hasira sana, aliacha wamalize kujishaua kisha angedili nao vizuri.
"Wewe mpumbavu u....."raisi alitaka kuongea ila alizuiwa na mwanaume huyo.
"Shiiiiii!" Mama yangu huwa hapendi kabisa makelele. Nimekuja hapa kistaarabu baada ya kugundua kwamba wewe ni baba mzazi wa Sarafina hivyo nikaamua kuja na kuyaacha maisha yako ili wananchi ndo waamue kama watakuacha hai au watakuua" kauli ya mwanaume ilimpa tabasamu, akajua hapa nina jambe ila iliyo fuatia baada ya hapo haikuwa nzuri kwa wote kwani walibaki wanaangaliana wasiamini kile kinacho endelea.
"Sara naomba unisamehe sana ila huyu ndiye baba yako mzazi na ndiye mtu ambaye amehusika kwenye kila udhalimu wa nchi hii. Najua huenda hautanisamehe ila ukiamua hivyo ni sawa, jambo ambalo linaenda kutokea hata mama yako atahusika maana bila kukusudia alihusika kutekeleza shambulio hilo ambapo anaweza kufungwa mpaka miaka mitano jela ila huyu hata nafasi ya kufungwa hiyo miaka mia moja hana huenda kifo ndiyo adhabu yake bora zaidi" mwanaume aliongea bila kupepesa mambo.
"Wewe mpuuzi unajua unaongea na raisi hapa, nimewaacha mfanye maigizo yenu kwa sabab Leo ndio mwisho wa maisha yenu wote ambao mpo humu ndani?" raisi alijigamba huku akiwa ananyoosha bastola yake kuielekeza kule alipokuwepo Calvinjr.
"Sawa mimi nitakuacha ufanye unacho kitaka wewe ila baada ya kuiona video hii kwanza" mwanaume aliongea bila wasiwasi akiwa anaichukua rimoti mezani na kuiwasha runinga hiyo humo ndani eneo hilo likiwa limezungukwa na wanaume wenye silaha nzito. Mheshimiwa raisi naye aligeuka kuona lilichokuwa kinafanyika ila cha ajabu ilikuwa ni chaneli ya vipindi vya kawaida.
Wakati hao wote wakiwa wanamshangaa Calvinjr maana hakukuwa na chochote, Mr Dark alikuwa ameinamia kwenye laptop yake, ghafla sana mambo yakabadilika ikawa inaonekana Video ya Madilu akiwa anaelezea uhusika wa raisi huyo kwenye kulipua bunge la nchi ambalo alililipua na watu wote ambao yeye alikuwa amewaua miamoja tisini na tisa.
Akiwa kwenye huo mshangao wa kuona hizo video zake zote ambazo zilikuwa zinamuelezea huo upande wake wa pili, ilionyeshwa mpaka video ya yule mke wa waziri wa ardhi akiwa anakiri kwamba alilazimishwa na watu wa Ikulu kusema uongo ili kuwaokoa wanae.
Hiyo haikutosha ndipo zilikuja taariza za hiyo DOCUMENT namba 72 ambayo kiongozi wao aliandikwa kwa code maalumu A.H, TOP official 255 ikiwa na maana ya Anorld Hazole, kiongozi mkuu wa Tanzania. Watu waliwekwa wazi mpaka namna mheshimiwa huyo alivyoweza kudanganya jina ili ayapate madaraka.
Hiyo kazi ilifanywa na Mr Dark ambaye alihaki vyombo vya habari vikubwa vyote nchini na ndipo akaisambaza habari hiyo. Calvinjr alizamisha mikono kifuani kwake na kuitoa DOCUMENT hiyo namba 72 ikiwa na idadi ya watu tisa.
"Kill them" raisi huyo alitamka akiwa anawapa amri walinzi wale lakini kitu cha kushangaza wale walinzi wote walimgeukia yeye na kumuweka chini ya ulinzi yeye na kijana wake Lestus Mzopari wakati huo mkurugenzi alitembea kwa kuchechemea na kwenda kuichukua bastola mikononi mwa raisi huyo na kumtandika risasi mbili za magotini kama kulipiza.
"Nilianza kukuhisi mapema sana mpuuzi wewe sema sikuwa na uhakika hivyo nikasambaza vijana wangu kila sehemu maana nilijua ipo siku kama ya leo itatokea. Hao wananisikiliza mimi tu maana ni majasusi wangu halafu wameshajua kwamba wewe ni mhalifu unahisi nani yupo tayari kwenda kunyongwa na wewe? Take him away" alimpa sababu iliyofanya vijana hao wamgeukie yeye huku akimtia kibao kikali sana shavuni akiwataka watu hao wampeleke anako stahili ila yule Lestus Mzopari alimpiga risasi ya kichwa pale pale.
Sasa Calvinjr alikalishwa chini na kusimuliwa historia nzima ya maisha yake maana alikuwa anastahili kuweza kuujua ukweli wote. Calvinjr aligoma na kuhisi kwamba labda watu hao walikiwa wakimtania tu ila wilimhakikishia kwamba huo ndo ukweli.
Aliumia na kutoa machozi akiamini kwamba familia yake ilimsaliti.
"Yuko wapi huyo mwanmke ambaye alinisaliti mimi?" Aliongea kwa hasira sana kumuulizia huyo mama yake mzazi ambaye alimfanya alelewe na mwanamke mwingine huku yeye akiwa upande mwingine wa dunia. Kazi nzito ambayo alikuwa ameifanya, aliamini kwamba huo ulikuwa ni wakati sahahi wa kufurahia na familia yake lakini mambo ya ajabu yalikuwa yanaendelea wakati huo kwa kukutana na taarifa mbaya kama hizo.
Wakati hayo yote yanaendelea akitaka kujibiwa na kujua mama yake huyo alikuwa wapi maana alihitaji kumuona ili akayajibu maswali ya mtoto huyo, alishangaa kumuona mama yake aliye mlea ambaye muda mfupi alitoka kumpa ukweli kwamba hakuwa mama yake mzazi pamoja na mkurugenzi wa shirika la kijasusi bwana Gulamu Leopard wakiinamisha vichwa chini kama kutoa heshima kwa mtu ambaye walikuwa wakimheshimu sana, hapo ndipo akageuka maana alihisi mlangoni kuna mtu.
Alishangaa sana na kushtuka mno, yule mtu ambaye alikuwa nyuma alikuwa ni master wake ambaye alimtengeneza kuwa binadamu hatari sana namna hiyo ila mtu ambaye alikuwa mbele ya master wake ndiye huyo ambaye alionekana kupewa heshima na mama yake pamoja na Mr Gulamu Leopard.
Kitu ambacho kilimshangaza sio tu watu hao kutoa heshima au master wake kufika hapo bali ni kile ambacho alikiona. Aliiona sura yake mbele yake, walichokuwa wamepishana ulikuwa ni umri tu ila sura hizo zilikuwa zinafanana kila kitu, akalazimika kujishika usoni maana alkuwa ni kama kwenye ndoto aisee.
Aliyekuwa mbele yake, alikuwa ni mtaamu wa zamani sana, Calvin Jackson Aron Mavunde, huyo ndiye alikuwa baba yake mzazi kabisa na ndiye ambaye alikuwa anaitwa Calvin mwenyewe mpaka yeye akapewa jina la Calvin Jr ikiwa ina maana ya Junior kwamba yeye ni mdogo na huyo ndiye baba mwenyewe ambaye ndo Calvin senior maana kila kitu walikuwa sawa.
Naam, ulikuwa nami tangu mwanzo mpaka nafika wa simulizi hii bora sana. Nisema tu asante kwako kwa kuweza kuigusa kalamu hii na kuwa moja ya watu ambo wamebahatika kulisoma andiko hili, natanguliza shukrani nyingi sana za dhati.
Kuisha kwa simulizi hii ni mwanzo mzuri zaidi wa chapter ya tatu ya simulizi hii ambayo itakwenda kwa jina la KALAMU ILIYO TUMWA KUNIUA,baada ya kufanikisha kuisoma sehemu ya kwanza kabisa ya andiko hili ambayo inakwenda kwa jila la ULIMWENGU WA WATU WABAYA.
Leo nakusanya kila kilicho changu najitoa kwenye chumba ambacho nilijifungia kwa muda mrefu sana kuiandaa simulizi hii panapo majaaliwa tutakutana tena wakati mwingine.
Wasalaam.
Wako,
FEBIANI BABUYA.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
KaribuKali sana hongera sana ndugu muandishi,mi nitakuwa nasupport story zote kali kuanzia apa
Shukrani kiongozi, unakaribishwa sana [emoji120]Hii kitu ni safi sana, nilichelwa kuanza kuisoma, nimeisoma kwa siku tatu , kiukwel imenifanya nisifuatilie jambo lingine kwa ufasaha ndan ya siku hizi tatu
Kongole kwa mwandishi
InapendezaHADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: +18
UTANGULIZI................
SURA YA 1.
MIMI NI NANI?
MZIZIMA,
Mvua zilizokuwa zimeambatana na upepo mkali zilikuwa zikiendelea kulisumbua jiji la bandari ya Salama, jiji la kale ambalo watu wa zamani walilijua kama mzizima. Mvua hizo ziliwafanya Tanesco wapate kisingizio kizuri kabisa cha kuweza kuukata umeme ambao ulikuwa unaimulika mitaa mbali mbali na kuonyesha umaridadi wake.
Kwenye chumba kimoja maeneo ya Kigogo Mwisho alionekana ndani mwanaume mmoja, kuonekana kwake kulidhihirisha wasiwasi na hofu ambayo ilikuwa imeugubika uso wake na simanzi ikauzidisha upole wa ile sura yake ambayo haikuwa ikionekana vyema huenda kwa sababu ya kukosekana kwa mwanga. Uso wake ulitoa taarifa ya kwamba maisha yake hayakuwa salama ndiyo maana alikuwa hana amani wala kuwa na utulivu wa kutosha, alikuwa ameketi kwenye mkeka ambao ulikuwa umetandikwa chini kwenye chumba kidogo cha hovyo ambacho kiligubikwa na joto kali kwa kukosa nyenzo mhimu za kupambana na joto. Sanjari na hilo udogo wa chumba nao ulichangia kwa kiasi kikubwa.
Mwanaume yule alijizoa kutoka kwenye ule mkeka na kusimama, alijisogeza kwenye dirisha dogo ambalo lilifunikwa kwa tambala kuu kuu lilolokuwa chafu, alifunua kidogo pazia hilo ili kujua kama nje kulikuwa na chochote lakini hakufanikiwa kuona jambo lolote lile zaidi ya radi ambazo zilikuwa inamulika kila wakati kwenye kiza totoro kilicho lifanya jiji hilo kuwa na utulivu ambao sio kawaida yake. Alirudi tena kwenye mkeka wake akiwa anatweta kwa jasho kutokana na joto kali huku akiwa anajifuta jasho hilo kwa kutumia shati lake ambalo lilikuwa mwilini.
Akiwa anaendelea kuhema kwa hesabu maalumu ambazo alizijua yeye na nafsi yake, alihisi kama kuna kitu kinamtekenya kwenye mfuko wake wa suruali, hapo ndipo akakumbuka kwamba kwenye mfuko huo alikuwa amehifadhi kisimu kidogo ambacho alikuwa amekifunga funga kutokana na uchakavu ambao kilikuwa nao. Aliipokea haraka simu hiyo ambayo namba yake haikuwa na jina na kuiweka kwenye sikio lake.
"Ondoka haraka kwenye hilo eneo, una dakika kumi na tano tu za kuyaokoa maisha yako, vinginevyo unakufa" sauti ya upande wa pili iliongea kwa msisitizo kisha simu ikakatwa. Alibaki kwenye mshangao mithili ya mtoto ambaye alikuwa ametelekezwa na mama yake mzazi huku akiamini kwamba alikuwa na usalama wa kutosha kwa sababu mama yake alikuwa karibu.
Alijizoa kivivu huku moyo wake ukiwa unamuenda mbio, alisogea kwenye ule mkeka na kuukunja upande wa juu ambapo eneo hilo kulikuwa na udongo ambao ulijazwa, aliufukua haraka haraka na kukitoa kimfuko cha plastiki. Alikifungua na ndani yake kulikuwa na pesa za kigeni maarufu kama dola huku pembeni yake kukiwa na bastola moja pamoja na kisu kimoja. Alizoa pesa haraka haraka na kuzitupia kwenye mfuko wake, bastola akaipachika kwenye kiuno chake huku kisu akikishika mkononi.
Alipafukia kama alivyokuwa amepakuta mwanzo na kuurudishia ule mkeka kwa mara nyingine tena kisha akanyanyuka na kuanza kutoka nje. Baada ya kufika mlangoni alikuwa amepoteza dakika tatu tayari, aliufungua mlango taratibu kisha akaangaza kila upande ili kuona kama angefanikiwa kuona kile ambacho alikuwa ameambiwa kinaenda kutokea lakini hali ilikuwa shwari kabisa hivyo akajitosa kwenye maji ya mvua na kuanza kutembea haraka haraka ili kuelekea kilipokuwepo kituo cha magari.
Alikunja kona ya kwanza akiwa anapishana na sauti ya kudondoka kwa maji, akakutana na uwazi ambao ulikuwa na mita kama kumi na tano, sehemu ambayo ilimshtua kidogo kwa sababu moyo wake ulimuenda mbio isivyokuwa kawaida. Alitembea haraka haraka ili aweze kulivuka eneo hilo salama huku kwenye mkono wake kisu akiwa amekishikilia vyema, ila hakupiga hatua hata kumi akahisi kabisa kulikuwa na harufu ya mtu ndani ya eneo hilo hali ambayo ilimfanya kupunguza mwendo na kumfanya aanze kutembea taratibu.
Aligeuka kuangalia nyuma yake, hakuona kitu zaidi ya anga ambalo lilikuwa linamcheka hivyo akahitaji kuendelea na safari yake tena lakini nafsi iligoma kabisa, moyo wake ulikuwa mzito na hakuwa mtu wa kuupuuzia huo mlango wake wa sita ambao ulikuwa wa hisia. Alishuka chini kama anajilaza kifudi fudi lakini hakufika chini kwa sababu ule mkono wenye kisu ndio ambao ulitangulizwa kisu ndicho kikafika chini na hata baada ya kufika pale chini kwa mkono wake hakuzubaa, alijigeuza kwa sarakasi kwa kuuviringisha mwili wake hali ambayo ilimfanya atue pembeni.
Mahesabu yake yalikuwa sahihi kwa sababu wakati anashuka pale chini, juu yake kilipitishwa kisu kutoka kwenye mikono ambayo ilionekana kuwa na nguvu kubwa na lengo la mtu huyo halikuonekana kuwa kumzimisha tu bali alikuwa anahitaji kuondoka na nafsi yake moja kwa moja. Hata baada ya kutua pale chini hakuzubaa kwa sababu alijua huenda akampa adui nafasi nzuri ya kuweza kufanikisha jambo lake kitu ambacho hakutaka kiweze kutokea kwake yeye ndiyo maana alijiviringisha kwa sarakasi na kutua pembeni. Kujiviringisha kwake kulimfanya kulikwepa buti zito la ngozi ambalo lilikuwa limeshushwa na mwanaume ambaye alionyesha kuwa na uhasama naye mkubwa mithili ya mtu ambaye alimuibia mkewe, buti hilo kama lingefanikiwa kutua kwenye mgongo wake basi asingefanikiwa kutembea tena kwenye maisha yake yote.
Kiza kinene kilimfanya mwanaume huyo ashindwe kumtambua mwanaume ambaye alikuwa amekuja mbele yake ila mwanga wa radi ulimumulika mtu huyo ambaye bila shaka alikuwa ni mweusi usoni akiwa kwenye ghadhabu isiyo pimika. Aliukunjua mkono wake ambao ulikuwa na kisu kwa sababu alijua kwamba anatakiwa kufa wakati huo asipo yatetea maisha yake, hakupata muda wa kutosha wa kupiga tathmini juu ya uwezekano kama alikuwa anamfahamu mwanaume huyo kwa sababu alikuwa anamjia kwa kasi pale alipokuwepo huku mabuti yake yakiwa yanapiga piga kwa nguvu kwenye maji ambayo yalikuwa yametuama chini.
Miguu yenye nguvu miwili ilikuwa inakuja kwenye uso wake, kama bahati tu, tope lililokuwa chini lilimsaidia kuteleza kidogo na kurudi nyuma hali ambayo iliifanya miguu hiyo kumkosa na badala yake akarushiwa maji machafu usoni ambayo yalimuingia kwenye macho. Mtetemo wa ardhi aliusikia vyema baada ya ile miguu ambayo ilimkosa kutua chini na kukita kwa nguvu. Aliyafumbua macho yake haraka ili kujilinda, alichelewa kwenye mahesabu, ngumi ilizama kifuani na kumfanya ahisi kama kuna mtu alimpasua na shoka.
Ndiyo kwanza kabisa tunaufungua utangulizi wa simulizi hii mpya ya NAFSI ZILIZO TELEKEZWA. Hii ni simulizi bora zaidi kati ya simulizi zangu tisa za kijasusi ambazo nimeziandika.
Ndani yake utakutana na stori kali zilizo simama, utakutana na watu kutoka mataifa makubwa na mashirika makubwa ja kijasusi duniani hususani IRINA ESPANOVICH, mwanamama kutoka ndani ya KGB ambayo alikuja akaiweka Tanzania kwa mkono wake baada ya kutoroka nchini mwake akiwa anatafutwa kwa nguvu na Moja ya mashirika makubwa duniani, shirika la kijasusi la Uruai KGB kwa kuwasaliti wenzake na kufanya Umoja wa nchi za kisovieti kudondoka mwaka 1991.
Kutoroka kwake ukawa mwanzo wa kuanzisha jamii ya hatari ndani ya TANZANIA ambayo ilifahamika kama LUNATIC SOCIETY. IRINA alifanikiwa vipi kuwakimbia watu wa kutisha hao wa KGB kwa kuwasaliti mbele ya CIA halafu akafanikiwa kufika Tanzania?
Hiyo jamii ambayo aliianzisha ilikuwa inajishughulisha na nini hasa na mwisho wake ulikuwaje?
IRINA ni nani hasa na alifanya usaliti wa namna gani mpaka KGB wamsakame kila kona ya ulimwengu huku yeye akipotelea Tanzania?
Hizo NAFSI ZILIZO TELEKEZWA Zina maana ipi na ni NAFSI za nani na nani?
Maswali ni mengi lakini ungana NAMI wakati huu uweze kusoma simulizi yangu bora kuliko zote ambazo nimeziandika. Ipo tayari kuanzia muda huu.
Bei yake ni shilingi 6000 tu za kitanzania unajipatia nakala yako kwa mfumo wa softcopy (pdf) kwa kulipia kwa namba hizi hapa.
0621567672 (HALOPESA)..... WHATSAPP
0745982347 (M-PESA)
0714581046 (TIGO-PESA)
0689440143 (AIRTEL MONEY)
Zote jina ni FEBIANI BABUYAView attachment 3000144