STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 53
"Kwenye nchi hii miaka mingi sana iliyopata kupita huko nyuma kuna bwana mmoja ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana tena ambaye alikiwa ni kijana mdogo tu, kuna wema aliufanya ila wema wake ndilo likaja kuwa kosa kubwa la yeye kuwahi kulifanya kwenye maisha yake baada ya kumsaidia mwanaume mmoja ambaye alikutana naye barabarani na kumgonga na gari wakati akiwa ametoka kwenye biashara zake na huo ndio ukawa mwanzo wao wa kujuana"
"Mwanaume huyo alimsaidia bwana huyo ambaye alikuwa na maisha magumu sana na kumfanya kuwa tajiri mkubwa mno ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania, usaliti ukaanzia hapo. Kama ilivyo kawaida ya wanadamu, akiwa ana shida atatia kila namna ya huruma, atakuheshimu sana ila akishazimaliza shida zake na pesa zikamtembelea basi atasahau kila kitu ana kuhisi kwamba ni jitihada zake ndizo zimefanya afike pale alipo ndicho kilicho tokea kwa bwana yule Juma ambaye alisaidiwa"
"Ilifika sehemu akawa anazitaka mali zote za mtu ambaye alikuwa amemsaidia azimiliki yeye, hapo ndipo unakuja kuwapima wanadamu jinsi walivyo na akili fupi. Hakuona namna ya kuweza kuzipata mali za mtu huyo hivyo akaamua kumuua huku akiamini kwamba atazipata kupitia mtoto wa mtu huyo kwani alikuwa anabaki pekeyake bila msaada wowote baada ya wazazi wake kufa na bwana huyo alihitaji kuitumia nafasi ya kujifanya anatoa msaada ili apate nafasi ya kuzichukua mali za mtoto huyo kirahisi kwani aliamini kwamba kwa wakati huo mtoto huyo hakuwa na nafasi ya kuweza kumuamini mtu mwingine zaidi yake"
"Bila kujua, kumuua mzee yule ambaye alimsaidia kipindi cha miaka kadhaa ya huko nyuma, akawa amefanya moja ya makosa makubwa sana kwenye maisha yake. Na mzee huyo ambaye aliuawa na huyo rafiki yake aliye msaidia ndiye Jackson Aron Mavunde mwenyewe aliyekuwa na ukwasi wa kutosha sana. Lengo la bwana yule kuweza kuzipata mali za mtoto yule kwa kuamini atamuweka karibu alikosea sana kwenye kuzipiga hesabu zake kwani inadaiwa kwamba kabla ya kufa baba yake aliweza kumuachia usia wa mwisho na kumuonya kwamba asije akamwamini binadamu yeyote yule huku akiuacha utajiri wote kwenye mikono ya mtoto huyo na kumtaka aelekee ndani ya nchi ya Japan ambako kuna mtu alitakiwa kumtafuta ambaye alikuwa rafiki wa baba yake na mtu huyo angemfundisha namna sahihi ya kuweza kuishi na wanadamu" Victor alitulia kidogo na kumuangalia mheshimiwa raisi huyo huku akimeza mate na kuendelea kumpasha ni ipi ilikuwa sababu haswa ya kutokea kwa mambo yote ambayo yalidaiwa kuwa na historia ya kutisha sana ndani yake.
"Huyo bwana mdogo ambaye namzungumzia hapa aliyekuwa anapewa haya maagizo na baba yake ndiye huyo Calvin Jackson Aron Mavunde mwenyewe na ndicho kiumbe ambacho wewe unataka kuijua historia yake leo hii. Baada ya kufika huko Osaka Japan, alitua kwenye mikono ya mwanaume mmoja jasusi aliyekuwa anatafutwa na ulimwengu mzima. Kila nchi ilikuwa inamhitaji mwanaume huyo ambaye alidaiwa kuwa ni hazina kubwa sana hivyo kama kuna nchi ingempata basi ingefanya makubwa sana ulimwenguni hapa, ila mwanaume huyo alikuja kufia ndani ya nchi ya Tanzania"
"Whaaat? Alifia ndani ya nchi ya Tanzania? Kivipi?" Mheshimiwa hakuelewa hivyo akaamua kuuliza kwa pupa maswali mfululizo.
"Mheshimiwa umesema unahitaji kuijua historia, nadhani ni vyema ukawa mpole ili niweze kukusimulia kila ambacho kilitokea kwa wakati huo au kama hautaki kuijua basi unaweza ukaondoka na kwenda ulipo toka" ilikuwa ni lazima aweze kuipata historia hiyo hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuwa mpole na mstaarabu ili apate kila nutka ya hadithi hiyo.
"Huyo jasusi inadaiwa kwamba aliwahi kukutana na Jackson kwenye biashara ambapo Jackson alifanikiwa kumsaidia na urafiki wao mkubwa ukawa umeanzia hapo. Sasa Calvin kutua kwenye mikono ya mtu huyo akaanza kupewa mafunzo ya hatari sana ili aweze kuja kujilinda mwenyewe duniani na hapo akawa amepatiwa jasusi mmoja wa kimarekani ili amfunze. Jasusi huyo nchi ya Marekani walijua alishakufa miaka mingi sana ila jasusi wa kijapani aliye itwa Hinata Haruto Haru alifanikiwa kumuokota kwenye mto Yamato na kumsaidia"
"Baada ya kumsaidia alimgeuza na kuwa kijana wake ambaye alikuaa muaminifu sana hivyo baada ya Calvin kufika huko huyo mwanaume ndiye ambaye alianza kumpa mafunzo makali. Calvin anadaiwa kwamba kwa kizazi hiki ndiye mtu ambaye alibahatika kufundishwa na walimu wa hatari sio chini ya wanne, alikutana na master wa kichina, India, akafundishwa udaktari na udhaifu wa mwili wa binadamu na mengine mengi"
"Lakini baada ya kumaliza hayo mafunzo yake kwa hao watu ndipo alipo fanikiwa kukutana na huyo mwalimu mwenyewe Hinata Haruto Haru. Mtu huyo alikuwa ana uwezo wa kutisha sana kiasi kwamba kuna watu walikuwa wanaamini kwamba anatumia uchawi"
"Kitu kikubwa zaidi ambacho yeye alimfundisha Calvin na inadaiwa ndicho kilimfanya kuwa binadamu hatari sana kuwahi kuishi duniani ni HISIA, alifundishwa kuyafanya mambo kwa hisia kiasi kwamba anakuwa anaenda na spidi ya hisia zake hivyo anakuwa anaweza kuyafanya mambo ya kutisha bila hata wewe kushtuka kwamba ameyafanya, anaweza kuyafumba macho yake na akapigana na watu hata mia moja kwa wakati mmoja"
"Na zoezi kubwa alilokuwa amepewa na mzee huyo na kama angefanikiwa kumpiga ngumi hata moja mzee huyo basi angempa ruhusa ya kuweza kurudi Tanzania kuja kulipa kisasi ila kama angeshindwa basi angetakiwa kuendelea kuishi huko kwa miaka mingine miwili ambayo ingefuatia, alipewa dakika tatu kuweza kutekeleza jambo hilo ambalo alifanikiwa sekunde ya mwisho baada ya mwalimu wake huyo kumkumbusha kwamba kwenye hisia inatakiwa kutumia zaidi akili kuliko nguvu hivyo utulivu unahitajika sana"
"Kufanikiwa kwa jambo hilo ndiyo ikawa sababu kubwa ya yeye kupewa upanga wa hazina wa nchi ya Japan ambao ulikuwa kwenye mkono wa mzee huyo. Huo upanga alimpatia Calvin na kumpa ruhusa ya kwenda kulipa kisasi huku akimtaka asiutumie vibaya uwezo wake kwani angeweza kuwa binadamu hatari zaidi kuwahi kuishi chini ya jua, na huo ndio ukawa mwanzo wa yale mauaji ya kutisha sana ambayo yaliifanya nchi hii ije kuwa sehemu ambayo ilianza kuwatisha watu kuishi"
"Ebu ngoja kwanza umesema alikuwa anatumia upanga?"
"Ndiyo"
"Hata haya mauaji yamefanyika kwa upanga"
"Una wasiwasi kwamba ni yeye?"
"Unahisi atakuwa nani?"
"Mheshimiwa sijajua, naomba nikumalizie kwanza stori yako kisha uende, wanangu wanavyorudi sitaki kabisa wawakute walinzi wako hapa. Sipendi kabisa wahusike kwa lolote na haya mambo ya siasa"
"Sawa Nakusikiliza"
"Baada ya kurudi alianza msako wa kuwatafuta wahusika wote ambao walikuwa wameishambulia familia yake na kwa wakati huo mimi nilikuwa jasusi ndani ya nchi hii, hivyo kesi ya kwanza ya mauaji ambayo aliifanya ilidondokea kwenye mkono wangu mimi nikaamua kuivalia njuga haswa ili kuifuatilia na kwa mara ya kwanza nilikuwa na hasira naye sana na kama ningempata niliapa ningemfanya kitu cha kutisha sana ila ni jambo ambalo hata mimi sikulijua kwani ulikuwa mlima ambao ulikuwa juu ya uwezo wangu kuupanda"
"Nilifanikiwa kuja kukutana naye kwa mara ya kwanza, sina kumbukumbu sana ila nahisi siku ili nilipigwa mpaka nikazimia, niliwahi kuamini kwamba kwenye nchi hii hakuna mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kusimama na mimi kwenye mapigano ila siku ile sikuamini kitu ambacho nilifanywa kwani ilikuwa ni zaidi ya ukatili ule ndipo nikajua kwamba yule hakuwa binadamu wa kawaida kama tulivyo sisi"
"Baadae baada ya yeye kunipa nafasi nyingine ya kuweza kuishi ndipo nilikuja kugundua kwamba nilifanya makosa makubwa sana kumlaumu mwanzo kwa aliyokuwa anayafanya kwani hata ningekuwa mimi ningefanya yale yale na kitu ambacho kiliniuma sana ni pale mwanaume ambaye nililikuwa namheshimu kama baba yangu, nilikuja kujua kwamba ndiye alikuwa mhusika mkuu wa mambo yote yale, hakuwa mwingine bali Kasisi Chacha ambaye alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa"
"Yule ndiye mwanaume ambaye alinilea mimi lakini alifanya mambo makubwa na mabaya sana kwenye maisha yangu na maisha ya watu wengine hivyo hata kifo chake sikuwahi kabisa kukijutia. Hiyo ndiyo sababu ambayo ilipelekea Calvin kuanza kuwaua watu vibaya sana mpaka pale alipo hakikisha kwamba amewamaliza wote. Lakini wakati anaendelea na watu hao ambao walikuwa wamehusika kuiua familia yake, yule mwalimu wake alikuja kumuangalia kijana wake ambapo alifia kwenye mikono yake baada ya kijana wake huyo kuweza kuimaliza kazi yake"
"Wakati mwalimu wake anakufa alimuachia wosia kwamba ile ngome ya Japan yeye ndiye ambaye alipaswa kwenda kuiongoza hivyo hakutakiwa kukaa tena Tanzania bali alipaswa kuweza kwenda huko Japan ambapo aliahidi kwamba hatakuja kuishi tena ndani ya nchi ya Tanzania kwa maisha yake yote labda tu kama atarudi kuja kuangalia makaburi ya wazazi wake" stori ambayo Victor alimsimulia mheshimiwa raisi ilikuwa ya kusisimua mno.
"Sasa kwanini mliamua kuifuta hadithi yake?"
"Kulikuwa na mambo mawili, kwanza hatukutaka jina lake lije kutumika vibaya na wanasiasa lakini pia tuliamua kuitoa historia hiyo kama sehemu ya kuwafanya wananchi wayasahau yale mambo ambayo yalitokea kwa wakati ule"
"Sasa kama hayo mambo yaliisha wakati huo kwanini arudi tena?" Mheshimiwa raisi aliuliza huku akiwa na hofu sana
"Yule hawezi kurudi tena ndani ya nchi hii"
"Sasa unahisi atakuwa ni nani mtu ambaye anafanya kama yeye? Unaweza ukanionyeesha picha yake?" Mheshimiwa raisi alihitaji kuijua sura ya mtu huyo.
"Bila shaka" Victor aliitoa simu yake na kumuonyesha mzee huyo mtu ambaye alitaka kumuona, baada ya kuiona picha hiyo alishtuka sana mpaka akataka kudondoka kwenye kiti alichokuwa amekalia.
"Nooo, nooo. Haiwezi kuwa kweli" aliongea huku jasho jingi sana likiwa linamtoka kwenye mwili wake.
"Vipi unamfahamu?" Hilo ndilo lilikuwa swali la Victor.
"Ndiyo namjua sana tena sana tu" mheshimiwa raisi aliongea akiwa anaitoa simu yake na kuitafuta picha moja ambayo alipiga yeye na mtu mwenye sura kama hiyo japo zilikuwa na utofauti mdogo sana, Victor mwenyewe alishangaa mpaka akawa amejishika mdomo.
"Huyu ni nani?" Aliuliza kwa mshangao
"Anaitwa Calvinjr"
Hahahahaha walichoka wote kwa pamoja.
Wanasema hivi kiendacho kwa mganga huwa hakirudi na usiku wa kiza huwa unafanya mambo mengi yasijulikane lakini ukitokeza mwanga kila kitu huwa kinakuwa hadharani, sina cha kuwasaidia labda tusaidiane kushangaa kwa pamoja.
Episode 53 inafika mwisho.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app