Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

SEHEMU YA 04:

Niliondoka kazini nikiwa ni kama nimechanganyikiwa, sikuwa namjua Shenaiza lakini sijui kwa nini nilihisi kama matatizo yake yalikuwa yakinihusu sana. Nikiwa kwenye kituo cha daladala nikiendelea kusubiri usafiri, ujumbe mfupi uliingia kwenye simu yangu, ulisomeka:
“Mwenye simu hii amelazwa Hospitali ya Amana, Ilala. Hali yake ni mbaya, hawezi kuzungumza.”
SASA ENDELEA…
“Mungu wangu,” nilisema baada ya kumaliza kuusoma ujumbe huo. Nilijaribu kuipiga tena namba hiyo, ikapokelewa lakini sauti haikuwa ya Shenaiza, akaniambia yeye ni Rozina, nesi katika hospitali ya Amana na kwamba yeye ndiye aliyekuwa akimhudumia msichana huyo.
Nilimuomba anitajie wodi aliyolazwa msichana huyo, akaniambia niende tu nikifika hospitalini hapo nipige kupitia namba hiyohiyo atakuja kunipokea. Niliita bodaboda na kumuelekeza kukimbia kadiri awezavyo kuelekea Amana. Abiria wengine waliokuwa pale kituoni wakisubiri daladala, walibaki kunishangaa lakini mwenyewe sikujali.
Nikaondoka na bodaboda huku nikimhimiza kuongeza mwendo ili tuwahi kufika. Baada ya kuhangaika sana kwenye foleni, kama ujuavyo Jiji la Dar es Salaam nyakati za jioni, hatimaye tuliwasili Amana. Nikapiga namba ya Shenaiza ambapo yule nesi alipokea tena, nikamweleza kwamba tayari nilikuwa nimefika, akaniambia nimsubiri mapokezi.
Sikuwa hata naijua sura ya huyo Shenaiza mwenyewe kwa sababu hatukuwahi kuonana zaidi ya kusikia sauti yake tu kwenye simu.
Muda mfupi baadaye, alitoka nesi mmoja, mwembamba, mrefu mwenye rangi ya weusi wa asili, akaniuliza kama mimi ndiye niliyekuwa nawasiliana naye kwenye simu. Nilipomjibu kwamba ni mimi, aliniuliza nilikuwa na uhusiano gani na mgonjwa?
Nikamjibu kwamba mimi ni kaka yake, nikamuona akiguna huku akinitazama kwa macho ya udadisi. Sikuelewa kwa nini ananitazama hivyo, nikajikaza kiume na kuonyesha kutobabaika.
“Nifuate!” alisema huku akianza kutembea kuelekea wodini, na mimi nikawa namfuata. Tulipita kwenye korido na kutokezea kwenye wodi za wanawake, nikawa naangaza macho huku na kule wakati tukipita pembeni ya vitanda walivyolazwa wanawake wengi, tukapita na kwenda kwenye wodi iliyokuwa imejitenga peke yake. Yule nesi akafungua mlango na kunipa ishara kwamba niingie.
Japokuwa kulikuwa na vitanda vinne ndani ya wodi hiyo, ni kimoja tu kilichokuwa kimelaliwa na mgonjwa aliyeonesha kutokuwa na fahamu. Yule nesi alinipa ishara kwamba yule ndiyo mgonjwa mwenyewe, nilimtazama kwa mshangao nikiwa kama siamini macho yangu.
Hakuwa Shenaiza yule ambaye nilimjengea picha kichwani mwangu, alikuwa mtu mwingine tofauti kabisa kiasi cha kunifanya nihisi huenda nesi amekosea kunipeleka au hatukuelewana katika mazungumzo yetu.
Hakuwa msichana wa Kitanzania kama nilivyokuwa nimemfikiria, alikuwa na mchanganyiko ambao siwezi kueleza moja kwa moja kama ni Mzungu au ni Mwarabu lakini alikuwa katikati ya jamii hizo mbili. Kiumri alionesha kuwa bado ni binti mdogo tofauti na nilivyomfikiria kwamba anaweza kuwa ni mwanamke mwenye kati ya miaka 25 hadi 30.
Alikuwa amelala tuli kitandani huku akiwa amefungwa bandeji kubwa kichwani, huku jicho lake moja likiwa limebadilika rangi na kuwa na weusi na wekundu kwenye ngozi inayolizunguka jicho kuonesha kwamba damu zilikuwa zimevilia kwa ndani. Pia mkono wake mmoja ulikuwa umezungushiwa bandeji kubwa kuanzia juu kidogo ya kiganja mpaka kwenye kiwiko cha mkono.
Dripu moja sambamba na chupa ya damu vilikuwa vikitiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake ya damu, nikajikuta nikipatwa na hali ambayo siwezi kuielezea kwa urahisi. Kwa kifupi, japokuwa bado sikuwa na uhakika kwamba yule ndiye Shenaiza tuliyekuwa tukiwasiliana naye, nilijikuta nikimuonea huruma sana kutokana na hali aliyokuwa nayo.
Nilitamani kujua nini kimemfika mpaka akawa kwenye hali hiyo. Nilitamani pia nimjue yeye ni nani na asili yake ni wapi hasa kwani hakuonesha kuwa Mtanzania japokuwa alikuwa akizungumza vizuri Kiswahili.
“Mbona unamshangaa sana? Kwani mlikuwa mnafahamiana kabla?” yule nesi aliniuliza baada ya kuniona hali niliyokuwa nayo, nilishusha pumzi ndefu na kuzugazuga, nikasogea pembeni ya kitanda cha Shenaiza na kumpa ishara kwamba tusogee pembeni ili tuzungumze zaidi.
“Samahani nesi, hebu nieleze nini kimetokea?”
“Nitakueleza lakini nataka na wewe unieleze ukweli, usije ukanisababishia matatizo kwenye kazi yangu, huyu ni nani kwako?”
“Nimeshakwambia kwamba ni dada yangu.”
“Hapana, siyo kweli! Hebu ngoja kwanza,” alisema huku akienda kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya kitanda cha Shenaiza, akanifuata na kuniuliza kama simu yangu nilikuwa nayo, nikamjibu kwamba ninayo, akaniambia nipige namba ya Shenaiza. Nikatoa simu yangu na kutafuta namba yake kisha nikampigia.
“Unaona amekusevu vipi?” aliniuliza yule nesi huku akinionesha jina lililotokea kwenye simu yake, nikabaki nimepigwa na butwaa kutokana na jinsi alivyokuwa amenisevu.
Sikutaka kuendelea kumbishia yule nesi kwa sababu angeweza kupata sababu ya kukataa kunipa ushirikiano baada ya kuamini kwamba nilikuwa nikimdanganya, nikaamua kukubali yaishe, nikamuacha aamini kile mwenyewe alichotaka kukiamini (nitafafanua zaidi baadaye jinsi alivyokuwa amenisevu).
Baada ya kuelewana na nesi huyo, alianza kunieleza kwamba walimpokea mgonjwa huyo majira ya saa tisa za jioni baada ya kuletwa na wasamaria wema ambao walidai wamemkuta amepigwa na kujeruhiwa vibaya nje ya nyumba yao.
“Alikuwa akitokwa na damu nyingi huku pia akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake, ikabidi tumpokee hivyohivyo na kuanza kumpatia matibabu lakini mpaka sasa hakuna anayejua jina lake, ametokea wapi na nini kilichomsibu, tunasubiri labda akirejewa na fahamu au ndugu zake wakija ndiyo watueleze kilichotokea,” alisema yule nesi, nikashusha pumzi ndefu na kugeuka kumtazama Shenaiza pale kitandani.
Baada ya kumaliza kuzungumza na nesi, nilimuomba niende kukaa pembeni ya Shenaiza mpaka atakaporejewa na fahamu zake lakini aliniambia kuwa ni kinyume na taratibu za hospitali hiyo, akanitaka nikakae nje ya wodi na kama kuna chochote, atanipa taarifa lakini akasisitiza kwamba mgonjwa alikuwa anahitaji damu zaidi kwa sababu amepoteza nyingi, akanitaka kama nipo tayari kumchangia anielekeze nini cha kufanya.
Sikuwa na kipingamizi, nilikubali kumchangia damu, yule nesi akanichukua mpaka kwenye wodi nyingine ambapo alinitambulisha kwa madaktari wenzake na kuwaeleza kwamba nilikuwa nataka kumtolea damu mgonjwa wangu Shenaiza. Nikachukuliwa vipimo vya awali na baada ya kuonekana nilikuwa fiti, niliingizwa kwenye chumba kingine na kuanza kutolewa damu.
Nikiwa naendelea kutoa damu, niliendelea kujiuliza maswali mengi kuhusu Shenaiza yaliyokosa majibu. Kuna wakati nilijilaumu sana kukataa kuonana naye mapema kwani niliamini pengine ningeweza kumsaidia asipatwe na kilichomtokea. Hata hivyo nilijipa moyo kwamba sikuwa nimechelewa, nikawa namuombea kwa Mungu apone na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Baada ya kumaliza kutolewa damu, nilirudi pale nje ya wodi na kukaa huku nikiendelea kutafakari mambo mengi. Tayari kigiza cha jioni kilishaanza kuingia lakini moyo wangu haukuwa radhi kuondoka hospitalini hapo, nilijiapiza kwamba hata ikibidi kukesha usiku kucha, nitafanya hivyo mpaka nifahamu kilichomsibu Shenaiza.
Ilipofika majira ya kama saa moja za jioni, yule nesi, Rozina alinifuata na kunipa habari ambazo zilinifanya mapigo ya moyo yanilipuke kuliko kawaida. Aliniambia Shenaiza amerejewa na fahamu na jambo la kwanza alilouliza ni kama nilikuwa nimempigia simu.
“Nimemwambia kwamba upo hapa nje, akaniomba sana akuone, lakini anazungumza kwa shida sana,” alisema nesi huyo, nikainuka na kuanza kumfuata harakaharaka kuelekea wodini.
Je, nini kitafuatia?
Endelea kuishi
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU) -7
ILIPOISHIA:
“Mungu wangu, akina nani tena hao usiku wote huu?” nilijiuliza huku nikirudi nyuma na kujibanza pale uchochoroni, nikawaona wale wanaume wakiendelea kugonga mlango kwa nguvu. Ugongaji wao ulionesha dhahiri kwamba hawakuwa wamekuja kwa heri, nikawa natetemeka nikiwa sijui nitafanya nini.
SASA ENDELEA…
Mlango uliendelea kugongwa kwa nguvu, nikiwa nimejibanza palepale, nikitetemeka mno kwa hofu kwani nilishaona hatari iliyokuwa mbele yangu. Niliwaona wale watu wakijadiliana na muda mfupi baadaye, mmoja kati yao aliondoka eneo hilo. Muda mfupi baadaye, alirudi akiwa amemkwida mtu ambaye nilipomtazama, nilimtambua haraka kuwa ni yule dereva teksi aliyetuleta.
Japokuwa sikuwa nasikia walichokuwa wakikizungumza lakini ilionesha wazi kwamba walikuwa wakimshinikiza awahakikishie kama pale ndipo tulipoingia.
Nikamuona akijitetea na kusisitiza kuwa ni penyewe, kufumba na kufumbua nilimuona mmoja kati ya wale watu akimpiga ngumi yule dereva iliyosababisha apepesuke na kutaka kuanguka, mwenzake akamdaka na kumsimamisha vizuri, wakawa wanaendelea kumhoji huku yule mwingine akiendelea kugonga mlango kwa nguvu.
Kwa ilivyoonesha, baada ya mimi na Shenaiza kuondoka hospitalini, watu wale walikuwa wakitufuatilia na ndipo walipofanikiwa kumpata dereva aliyetuleta pale nyumbani kwangu na kumteka. Nilijiuliza wale ni akina na nani na kwa nini walikuwa wakitufuatilia?
Niliendelea kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu, nilimlaumu pia Shenaiza kwa kutonieleza ukweli wa kilichokuwa kinaendelea kwani mpaka muda huo, nilikuwa nimenaswa kwenye mtego ambao sikuwa naujua. Sikuwa najua Shenaiza ni nani? Ilikuwaje mpaka akajeruhiwa kiasi kile na aliyemjeruhi ni nani na wale watu walikuwa na uhusiano gani naye! Nilikosa majibu.
Kingine kilichonitisha, kama yule dereva tu ambaye hakuwa na hatia yoyote alikuwa akipigwa kiasi kile, hali ingekuwaje endapo wangenikamata na mimi? Kwa kuwa nilikuwa nimefunga mlango kwa kufuli, tena geti lilikuwa la chuma, niliamini hawawezi kumpata Shenaiza, kwa lugha nyepesi, Shenaiza alikuwa salama mle ndani, tatizo lilikuwa ni kwangu mimi.
Nilichoamua kukifanya kabla hawajanishtukia, ilikuwa ni kuondoka haraka eneo hilo na kwenda kutafuta hifadhi sehemu nyingine salama. Harakaharaka niliondoka, mkononi nikiwa na mzigo wangu wa chipsi na kutembea mpaka mtaa wa pili.
Nilitokezea kwenye kituo cha Bajaj na bodaboda ambapo nilimuita dereva mmoja wa bodaboda ambaye mara kwa mara huwa ananibeba.
“Vipi bro mbona usiku? Siyo kawaida yako!”
“Aah! Chukulia poa, nataka unipeleke Kijitonyama,” nilisema huku nikipanda kwenye bodaboda, nikawa nageuka huku na kule kuhakikisha kama hakuna mtu anayenifuatilia. Kwa jinsi nilivyokuwa natetemeka, ungeweza kudhani nimetoka kumwagiwa maji ya baridi.
Tuliondoka eneo hilo huku nikiendelea kujiuliza maswali yaliyokosa majibu. Sikujua hatma ya Shenaiza pale nyumbani kwangu. Niliamua kwenda Kijitonyama kwa rafiki yangu na mfanyakazi mwenzangu, Justice ili akanipe hifadhi lakini pia anipe ushauri wa nini cha kufanya.
Dakika kadhaa baadaye, tayari nilikuwa nimeshafika Kijitonyama, nikamlipa yule dereva wa bodaboda na kushuka, nikakaza mwendo kuelekea kwenye uchochoro wa kuelekea kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Justice.
Kwa kuwa nilijua kwa muda ule watakuwa wameshafunga geti, nilienda kumgongea dirishani.
“Justice! Justice!”
“Mh! Nani tena usiku wote huu?”
“Ni mimi Jamal!”
“Jamal?” alihoji Justice kwa mshtuko, nikamuona akifungua pazia, akiwa ni kama haamini kwamba nimemfuata usiku huo. Alipohakikisha ni mimi, harakaharaka alienda kufungua mlango lakini nilipotaka kuingia ndani, alinizuia:
“Nipo na shemeji yako, vipi kwema utokako?”
“Dah!” nilijibu kwa kifupi, kauli yake kwamba alikuwa na mwanamke usiku huo ilinimaliza kabisa nguvu. Niweke wazi kwamba miongoni mwa matatizo ya rafiki yangu Justice, ilikuwa ni kupenda kubadilisha wanawake kama nguo. Mara kwa mara alikuwa na tabia ya kulala na wanawake tofautitofauti, jambo ambalo binafsi sikulifurahia.
Kibaya zaidi ni kwamba alikuwa akiishi kwenye chumba kimoja tu kwa hiyo akishakuwa na mgeni ndani, inakuwa vigumu kuingia, ikabidi nimwambie atoke ili tuzungumzie nje kwa sababu nilikuwa na matatizo makubwa.
Alirudi ndani kwani kwa muda huo alikuwa amejifunga taulo tu, alipotoka tena, alikuwa ameshavaa nguo.
“Samahani bwana sikujua kama utakuja, nisamehe kwa sababu tunazungumzia nje, si unajua tena,” alisema Justice huku akifunga vifungo vya shati lake, sikupoteza muda ikabidi nimueleza kwa kifupi kilichotokea.
“Mungu wangu, sasa itakuwaje?” alisema akionesha kupatwa na mshtuko mkubwa mno.
“Hata sielewi, ndiyo maana nimekuja kwako kupata ushauri.”
“Umeshaenda kuripoti polisi?”
“Sijaenda kwa sababu hata huyo msichana mwenyewe namna alivyofika nyumbani kwangu, ni kwamba nimefanya kumtorosha tu hospitalini,” nilimwambia lakini akasisitiza kwamba ni lazima twende tukatoe taarifa polisi ili chochote kitakachotokea, polisi wawe wanajua.
Kwa upande fulani nilikubaliana na alichoniambia, hatukuwa na muda wa kupoteza, alirudi ndani kumuaga msichana wake na alipotoka, tulielekea moja kwa moja kituo cha polisi. Kwa kuwa pale alipokuwa anaishi hapakuwa mbali na Kituo cha Polisi cha Kijitonyama au maarufu kama Mabatini, dakika kadhaa baadaye tulikuwa tumefika.
Tukaandikisha maelezo pale kaunta lakini kwa bahati mbaya zaidi, askari aliyekuwa zamu alisema askari wote wametoka kwenda kwenye doria kwa hiyo kama nahitaji msaada wa polisi, nisubiri mpaka warudi kutoka kwenye doria. Kutokana na hali ilivyokuwa, sikuwa na ujanja zaidi ya kubaki kusubiri hao askari warudi.
Kwa kuwa Justice alikuwa na mgeni wake, nilimruhusu aondoke kurudi kwake na kumshukuru kwa msaada aliokuwa amenipa. Akaondoka na kuniacha nimekaa kwenye benchi pale kituoni. Tayari saa ya kwenye simu yangu ilikuwa ikionesha kwamba ni saa sita za usiku.
Kutokana na pilikapilika nyingi, nilijikuta nimekaa muda mrefu bila kushika simu, nilipoishika nilikuta meseji kadhaa kutoka kwa rafiki zangu, moja ikiwa ni kutoka kwa Raya, msichana tuliyekuwa tukifanya naye kazi ambaye alitokea kunizoea sana.
Alikuwa ametuma ujumbe wa kunitakia usiku mwema kama ilivyo kawaida yake, nilishusha pumzi ndefu na kuendelea kutafakari hatma ya maisha yangu. Baada ya kukaa muda mrefu pale kituoni huku kukiwa hakuna dalili yoyote ya askari kuja, ilibidi niage na kuondoka kwa sababu kesho yake nilitakiwa kuwahi kazini kwani kuna kazi muhimu sana niliyokuwa natakiwa kuikamilisha.
Nikiwa naondoka, simu yangu ilianza kuita mfululizo, haikuwa kawaida mimi kupigiwa simu usiku huo, nikaitoa na kutazama namba ya mpigaji. Alikuwa ni Raya, nikashtuka kuona simu yake usiku huo, harakaharaka nikapokea.
“Vipi Jamal, umeshalala?”
“Hapana, bado sijalala Raya.”
“Mbona nakutumia meseji hupokei? Mpaka nimepatwa na wasiwasi.”
“Mh! Samahani kwa kuchelewa kujibu lakini usijali, niko poa na usiku mwema pia.”
“Haya ahsante, nilitaka nisikie tu sauti yako ndiyo nilale. Halafu mbona kama unatembea, unaenda wapi usiku wote huu?”
“Aah! Kuna mahali nimetoka ndiyo narudi nyumbani.”
“Jamal! Umetoka wapi usiku wote huu?” Raya alinibana kwa maswali. Jambo ambalo naomba niliweke wazi kuhusu Raya, japokuwa mimi nilikuwa namchukulia kama rafiki wa kawaida tu, alikuwa na hisia fulani juu yangu ambazo siwezi kuzielezea kwa urahisi.
Kwanza alikuwa anapenda sana kuwa karibu na mimi japokuwa mwenyewe nilikuwa nikimkwepa sana. Tukiwa kazini, alikuwa anapenda muda wa lanchi tutoke na kwenda kula pamoja na ikitokea nimeenda peke yangu, basi atanuna na kukosa raha siku nzima. Pia alikuwa anapenda hata wakati wa kutoka, tuongozane mpaka kituoni, ahakikishe nimepanda daladala kurudi kwangu ndiyo na yeye aende kwao kwani alikuwa akiishi Mwenge ya Mlalakua.
“Nipo Kijitonyama hapa jirani na Kituo cha Polisi cha Mabatini.”
“Please nakuomba tuonane usiku huuhuu, baba na mama wamesafiri tangu juzi, niko mwenyewe tu, nahisi haupo sawa na nahitaji kukusaidia, niambie nikukute wapi, nakuja na bodaboda sasa hivi,” alisema Raya, nikashusha pumzi ndefu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 8
ILIPOISHIA:
“Please nakuomba tuonane usiku huuhuu, baba na mama wamesafiri tangu juzi, niko mwenyewe tu, nahisi haupo sawa na nahitaji kukusaidia, niambie nikukute wapi, nakuja na bodaboda sasa hivi,” alisema Raya, nikashusha pumzi ndefu.
SASA ENDELEA…
Nilishindwa nimjibu nini Raya, ni kweli nilikuwa kwenye matatizo makubwa na nilihitaji mtu wa kunisaidia lakini nilipomfikiria Raya, nilijikuta nikikosa majibu. Nilikumbuka jinsi msichana huyo alivyokuwa anajitoa kwa ajili yangu, akihitaji ukaribu wangu tu.
Watu wengi walikuwa wakihisi kwamba huenda tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini haikuwa hivyo, nilimchukulia kama rafiki wa kawaida tu ingawa hata yeye alikuwa akiwaambia marafiki zake kwamba mimi ndiyo mumewe mtarajiwa.
Mara kwa mara alikuwa akinilazimisha sana aje nyumbani kwangu lakini nikawa nampiga chenga sana na hata akija, nahakikisha sipo peke yangu, namuita rafiki yangu Justice au Prosper kisha tunajumuika wote. Japokuwa alikuwa akionesha waziwazi anavyonipenda, nilikuwa namchukulia kama rafiki tu na sikutaka kabisa uhusiano wetu uvuke zaidi ya hapo.
Hata hivyo, hakuwahi kuchoka, naye akawa ananialika mara kwa mara niende nyumbani kwao lakini sikuwa tayari kwa hilo. Nilijiwekea mipaka kati yetu na kamwe sikutaka tuivuke zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida. Japokuwa nilikuwa najua kwamba namkera sana Raya kwa misimamo yangu lakini sikujali.
“Mbona hunijibu Jamal? Au hutaki nije?” swali hilo la Raya ndilo lililonizindua kutoka kwenye lindi zito la mawazo. Nilishasahau kwamba nazungumza na simu, nilizama kwenye mawazo ya kumfikiria Raya na kushindwa kuamua nini cha kufanya kwa wakati huo.
“Ok… ok… njoo hapa jirani na kituo cha polisi Mabatini, nakusubiri,” niliamua kukubali kwani sikuwa na ujanja mwingine, akakata simu. Mitaa yote ilikuwa kimya kabisa usiku ule, kelele pekee zilizokuwa zinasikika ni za vyura waliokuwa wakikoroma, wenyeji wa Kijitonyama watakuwa wananielewa vizuri kwani maeneo hayo hasa nyakati za mvua, huwa kunakuwa na vyura wengi wanaopiga sana kelele nyakati za usiku.
Nilisogea pembeni ya barabara na kusimama, nikawa namsubiri Raya ambaye hata dakika kumi hazikupita, akawasili akiwa kwenye bodaboda. Alishtuka sana kwa hali aliyonikuta nayo, mkononi nikiwa bado nimeshikilia mfuko wa chipsi nilizokuwa nimeenda kununua kwa ajili ya kula na Shenaiza.
“Jamal! What’s wrong with you?” (Jamal! Umepatwa na nini) alisema Raya huku akinisogelea, akionesha dhahiri alivyokuwa na shauku ya kutaka kujua kilichonitokea. Nilimjibu kwa kifupi kwamba ni stori ndefu na nipo kwenye matatizo makubwa.
“Twende tukaongelee nyumbani, it’s not safe out here in this dark hours (siyo salama hapa nje muda huu wa giza) alisema Raya huku akinipokea ule mfuko wa chipsi, akanitaka tupande ‘mshikaki’ kwenye bodaboda iliyomleta. Huo ulikuwa mtihani mwingine kwangu lakini sikujali sana.
Alitangulia yeye, akakaa kwa mtindo wa kujibinua, nilijua anafanya vile kwa lengo gani. Na Mimi nikapanda na kukaa nyuma yake, tukawa tumesogeleana sana kiasi cha miili yetu kugusana.
Hata hivyo, sikupatwa na hisia zozote kwani akili zangu hazikuwa hapo muda huo, nilikuwa nikiendelea kuwaza kuhusu hatima ya Shenaiza kule nyumbani kwangu. Dakika chache baadaye, tuliwasili nyumbani kwa akina Raya.
Kama alivyonieleza kwenye simu, kweli wazazi wake hawakuwepo, akanikaribisha mpaka sebuleni kwao, akafunga milango na mageti yote kisha akataka nimueleze kilichotokea. Tayari saa ya ukutani ilikuwa ikionesha kwamba ni saa saba za usiku.
Ilibidi nimueleze Raya ukweli wa kila kitu. Kwanza alinishangaa sana na kuniuliza nilipata wapi ujasiri wa kwenda kumtorosha hospitalini mtu ambaye ndiyo kwanza nimejuana naye siku hiyohiyo. Akazidi kunishangaa kwamba kwa nini sikumlazimisha msichana huyo anieleze ukweli wa kilichosababisha akajeruhiwa kiasi hicho na zaidi akaendelea kunilaumu kwa nini nimempeleka nyumbani kwangu, tena usiku ule.
“Mimi kila siku nikikwambia nije kukutembelea kwako unakuwa na visingizio lukuki, hata nikija hutaki tukae wawili tu lakini huyo umeweza kumuingiza kwako, tena usiku, kwa nini Jamal?” Raya alianza kulia kwa wivu.
“Naomba tuachane na hayo kwanza Raya, hebu tulimalize hili lililopo mbele yetu,” nilisema kwa upole kwani japokuwa alikuwa akisumbuliwa na wivu, kuna mambo ya msingi kabisa aliyoyaongea ambayo hata mimi nilipofikiria vizuri, niligundua kwamba nilikosa umakini katika kulishughulikia suala hilo.
Tukaanza kujadiliana nini cha kufanya ambapo aliniambia kwa sababu muda umeshaenda sana na nimeshatoa taarifa polisi, kwa usalama nilale hapohapo nyumbani kwao mpaka asubuhi ndiyo tutajua nini cha kufanya.
Sikuwa na cha kufanya, pamoja na ujanja wangu wote nikawa nimenasa kwenye tundu bovu, Raya akainuka na kuniandalia chakula kilichokuwa kimesalia, akaniambia zile chipsi nilizoenda kununua nizitupe kwani zinaweza hata kuwa zimewekwa sumu, nikakubaliana naye.
Ilibidi nijilazimishe tu kula kwani bado nilikuwa nikisumbuliwa sana na mawazo, nikala huku Raya akijitahidi kunichangamsha na kuniambia nichukulie kila kitu kilichotokea kuwa ni mipango ya Mungu.
“Huenda Mungu amesikia kilio changu cha siku nyingi cha kutaka uje kwetu,” alisema na kucheka mwenyewe, nikatabasamu kiaina kwani bado moyo wangu ulikuwa na hofu kubwa mno. Baada ya kumaliza kula, alinipeleka kuoga kisha kinarudi pale sebuleni.
“Si tunalala wote kitanda kimoja?” alisema Raya, kauli iliyonishtua sana kwa sababu niliona haiwezi kuwa tabia njema kwa mimi kulala naye kitanda kimoja wakati hakuwa mpenzi wangu, na pia tukiwa nyumbani kwao. Nikamkatalia katakata!
“Basi usijali, wewe utalala chumbani kwangu halafu mimi nitaenda kulala chumba cha wageni,” alisema akionesha kupoteza furaha. Nilimwambia yeye akalale chumbani kwake kama kawaida halafu mimi nikalale huko kwenye chumba cha wageni, akawa hataki, tukabishana kidogo lakini baadaye alikubali.
Akanipeleka mpaka kwenye chumba cha wageni huku mara kwa mara akinishika mwilini, niliamua kujikausha kwani nilijua endapo nitamchekea tu, usiku huo hautaisha salama, lazima tutaangukia dhambini.
Kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka kwa pilikapilika za siku nzima, nilipoingia tu chumbani na Raya kutoka, nilivua nguo na kubaki na bukta tu, nikajilaza kitandani ambapo muda mfupi baadaye, nilipitiwa na usingizi mzito.
Nilipokuja kuzinduka, nilishtuka mno baada ya kugundua kuwa sikuwa nimelala peke yangu bali kuna mtu mwingine, tena wa jinsia ya kike, na kibaya zaidi, hata ile bukta yangu niliyolala nayo, ilishavuliwa. Nilikurupuka kwa kasi lakini yule mtu aliyelala pembeni yangu akanituliza na kuniambia nisiogope.
“Mungu wangu,” nilisema baada ya kugundua kuwa kumbe alikuwa ni Raya, tena naye akiwa mtupu kabisa, akaniambia kwamba alikuwa anaogopa kulala peke yake na ndiyo maana amekuja kulala na mimi.
Sikupata hata muda wa kujibu chochote, Raya akanikumbatia kwa nguvu mwilini na kuanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, japokuwa sikuwa tayari kwa alichokuwa anakitaka, nilijikuta kwenye wakati mgumu mno, kwani ukichanganya joto la mwili wake na uzuri aliokuwa nao, ukizingatia kwamba tulikuwa wawili tu, nilijikuta nikishindwa cha kuamua, ‘Jamal’ wangu naye akaanza usumbufu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 09.


Sikupata hata muda wa kujibu chochote, Raya akanikumbatia kwa nguvu mwilini na kuanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, japokuwa sikuwa tayari kwa alichokuwa anakitaka, nilijikuta kwenye wakati mgumu mno, kwani ukichanganya joto la mwili wake na uzuri aliokuwa nao, ukizingatia kwamba tulikuwa wawili tu, nilijikuta nikishindwa cha kuamua, ‘Jamal’ wangu naye akaanza usumbufu.
SASA ENDELEA…
Nilishindwa kujizuia, na mimi nikamkumbatia Raya, kitendo ambacho kilimfurahisha mno, akausogeza mdomo wake kwangu, nami nikafanya hovyohivyo, ndimi zetu zikagusana, nikamsikia akitoa migumo ambayo ilizidi kuipagawisha akili yangu.
Japokuwa sikuwa mtaalamu sana kwenye mambo ya kikubwa, nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu kumuonesha Raya kwamba na mimi sikuwa mshamba, ‘amsha-amsha’ ziliendelea na hatimaye kipyenga kikalia kuashiria kuanza kwa mpambano wa kukata na shoka, usio na refa wala jezi, huku nikishindwa kuzidhibiti papara zangu.
Wakati nikijiandaa kusakata kabumbu, ghafla mawazo juu ya Shenaiza na kilichokuwa kinaendelea kule nyumbani kwangu yalipita kwa kasi kubwa ndani ya kichwa changu, nikashangaa ‘Jamal’ wangu ambaye muda mfupi uliopita alikuwa ngangari ile kinoma, akianza kunywea na kupoteza kabisa ukakamavu wake.
Raya ambaye tayari alishajiweka tayari kupokea ‘mashuti’ ya nguvu kutoka kwangu, alishtushwa na kilichotokea, akaacha kila alichokuwa anakifanya.
“Vipi tena jaman mpenzi wangu, na..ta…ka…,” alisema Raya kwa sauti iliyokuwa ikikatakata, ikitokea kwenye matundu ya pua zake.
“Subiri kidogo,” nilisema kwa aibu kubwa, sikuwahi kutokewa na hali kama hiyo hata mara moja, nikashangaa imekuwaje? Sikupata jibu. Ili kuzuga, ilibidi niamke na kujifanya nataka kwenda maliwatoni, nikamuacha Raya amelala palepale huku akiwa kimya kabisa, akionesha kuugulia maumivu ya ndani kwa ndani.
Harakaharaka nilitoka na kuelekea choo cha ndani, nikajifungia mlango na kuanza kutafakari kuhusu kilichotokea. Nilijisikia aibu sana kwani sikujua Raya atanichukuliaje kama amenitafunia kila kitu na kuniwekea kabisa mdomoni lakini nimeshindwa kumeza. Japokuwa ulikuwa ni usiku sana na kulikuwa na baridi, nilifungulia maji ya bomba la mvua na kuanza kujimwagia. Nilisimama huku maji yakiendelea kunimwagikia kwa zaidi ya dakika tatu mpaka nikaanza kutetemeka kwa baridi.
Nikafunga bomba na kurudi chumbani ambako nilimkuta Raya amelala vilevile kama nilivyomuacha. Nikawa najisemeshasemesha ili ‘kuua soo’, nikajifuta maji na kupanda kitandani, nikamvutia Raya kifuani kwangu ambapo alikuja mzimamzima, ni hapo ndipo nilipogundua kwamba kumbe alikuwa akilia.
Lawama zake kubwa kwangu ni kwamba sikuwa nikimpenda na ndiyo maana nilimfanyia hivyo lakini kiukweli, wala sikuwa nimepanga hayo yatokee bali nilijikuta tu nikiishiwa ukakamavu.
Nikawa nambembeleza kwa maneno matamu na kwa mara ya kwanza nikamtamkia kwamba nampenda sana japokuwa nilisema vile ili kumtuliza. Alifurahi sana aliposikia maneno hayo kutoka kwangu, nikamuona akitabasamu na kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, na mimi nikawa naonesha ushirikiano.
Niliamini safari hii nitaweza kukata kiu yake kwani ‘Jamal’ wangu naye alishaanza kuonesha ushirikiano, akawa anafura kwa hasira na kunipa matumaini makubwa kwamba nitaifuta aibu kubwa iliyokuwa inataka kunikabili.
Tuliendelea kufanya ‘warm-up’ kwa dakika kadhaa lakini safari hii Raya alionesha kutotaka kuchelewesha tena mambo, kabla hata kipyenga cha kuashiria kuanza kwa mpambano hakijalia, yeye alitaka kujianzishia mpira mwenyewe.
Katika hali ambayo sikuitegemea, mawazo juu ya Shenaiza yalijirudia tena akili mwangu, nikawa sijui nini kilichoendelea baada ya mimi kuondoka, kama ilivyokuwa mwanzo, ‘Jamal’ wangu akanywea, jambo lililomkasirisha sana Raya, safari hii akawa analia kwa sauti kama mtu aliyepokea taarifa za msiba.
“Kwa nini unanitesa hivi Jamal? Kwani mimi nina kasoro gani mpaka unifanyie hivi?” alisema huku akilia, nikaanza upya kazi ya kumbembeleza huku nikijisikia aibu kubwa ndani ya moyo wangu. Haikuwa kazi nyepesi kumtuliza Raya mpaka atulie, nikawa najaribu kujikakamua na kumfosi ‘Jamal’ wangu arudi tena mchezoni lakini ilikuwa sawa na kazi bure.
Mpaka kunapambazuka, hakuna kilichofanyika zaidi ya kubembelezana, saa kumi na moja alfajiri, wote tulipitiwa na usingizi mzito na tulipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni saa moja za asubuhi. Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuzinduka, nikajaribu kujikakamua tena kuona kama angalau naweza kufanya chochote lakini ilikuwa sawa na kazi bure, Jamal wangu alikuwa amelala doro, jambo lililonifadhaisha sana.
Muda mfupi baadaye Raya naye aliamka, macho yake yakiwa yamevimba na kuwa mekundu kutokana na kulia sana, akaenda chumbani kwake na kuniacha nikijiandaa. Baada ya kumaliza kujiandaa, nilitoka hadi sebuleni ambako nilimkuta Raya akiandaa kifungua kinywa.
Ule uchangamfu aliokuwa nao kwangu uliyeyuka kama theluji iyeyukavyo juani. Nilitamani sana ajue kwamba sikuwa nimemfanyia makusudi bali lilikuwa ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wangu lakini haikuwezekana, alichoamini Raya ni kwamba sikuwa nampenda na nilifanya vile kumkomoa.
Tulipata kifungua kinywa kimyakimya, kwa kuwa sikuwa najua kilichotokea nyumbani kwangu usiku ule, sikuwa na muda wa kuendelea kukaa pale, nilimuaga Raya na kumwambia tutakutana kazini baadaye lakini cha ajabu, alikataa katakata kuniacha niondoke peke yangu, akaniambia atanisindikiza na kama ni kuomba ruhusa kazini, niombe ya watu wawili, mimi na yeye.
Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwangu kwa sababu kwa kilichotokea kati yangu na yeye, nilihitaji kupata muda wa kukaa peke yangu na kutafakari kwa kina kilichosababisha hali ile iliyonitokea usiku.
Lakini kubwa zaidi, sikutaka kumuingiza kwenye matatizo yangu na Shenaiza, kwa kuwa nilikuwa nimeyaanza mwenyewe, nilitaka nikayamalize mwenyewe. Hata hivyo, sikutaka pia kuendelea kumuudhi, ikabidi nimkubalie ambapo tulitoka na safari ya kuelekea nyumbani kwangu ikaanza.
Tukiwa njiani nilimpigia simu bosi kazini na kumueleza kwamba nilikuwa nimepatwa na matatizo makubwa na kwamba nitachelewa kufika kazini. Sikutaka kumfafanulia kilichotokea, kwa bahati nzuri alinielewa. Nilimpigia pia simu Justice na kumtaka asizungumze chochote kazini kuhusu nilichomwambia jana yake.
“Sasa mbona umeomba ruhusa peke yako? Kwa nini usiniombee na mimi kama tulivyokubaliana?” Raya aliniuliza kwa sauti ya chini, iliyoonesha dhahiri kwamba hakuwa na furaha, Nilishindwa cha kumjibu zaidi ya kumtaka apige mwenyewe simu na kuomba ruhusa kivyake ili tusije kuonekana kwamba tumepanga kutega kazi kwa makusudi.
Kwa bahati nzuri naye alikubaliwa, tukaendelea na safari ya kuelekea kwangu kwa kutumia Bajaj ambayo Raya ndiye aliyelipa, kadiri tulivyokuwa tunazidi kukaribia kwangu ndivyo mapigo ya moyo wangu yalivyokuwa yanazidi kuongezeka, sikujua nitakutana na nini.
Nilimuelekeza dereva njia ya kupita kwani sikutaka kutokezea upande wa mbele wa mtaa niliokuwa naishi, nilitaka tutokezee uchochoroni kwa sababu za kiusalama, kweli dereva yule alinielewa na safari iliendelea. Hatimaye tukafika kwangu, tukashuka kwenye Bajaj na kumwambia yeye aondoke zake, tukaanza kupita kwenye uchochoro unaotokezea kwangu.
Tulipokaribia kufika, huku mapigo ya moyo wangu yakizidi kupiga kiasi cha kunifanya nitokwe na kijasho chembamba japokuwa bado ilikuwa ni asubuhi na kulikuwa na kibaridi, nilishtuka zaidi baada ya kuona umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika mbele ya nyumba niliyokuwa naishi.
“Mungu wangu,” nilisema huku nikifikicha macho na kutazama vizuri, kuna muda nilikuwa nahisi kwamba huenda nipo ndotoni lakini haikuwa hivyo, sikuelewa pale kwangu kuna kilichosababisha watu wajae kiasi kile.
Je, nini kitafuatia? Usikose next
 
SEHEMU YA 10.

Ilipoishia…
“Mungu wangu,” nilisema huku nikifikicha macho na kutazama vizuri, kuna muda nilikuwa nahisi kwamba huenda nipo ndotoni lakini haikuwa hivyo, sikuelewa pale kwangu nini kilisababisha watu wajae kiasi kile.
Songa nayo…
Niliendelea kujiuliza maswali mengi bila kupata majibu. Wasiwasi wangu zaidi ulikuwa ni kuhusu Shenaiza, nilijiuliza au wale watu niliowaona usiku uliyopita walivamia na kubomoa geti langu hata kuingia ndani kwenda kumfanyia unyama ndio ikawa sababu ya watu wale kujaa, lakini bado hata swali hilo sikuweza kulipatia majibu ya moja kwa moja.
Huku moyo ukidunda niligeuza shingo yangu na kumtazama Raya, uso wake ni kama ulikuwa unaniuliza nini kinaendelea nyumbani kwangu! Bila kuzungumza jambo lolote niliyatoa macho yangu kwa Raya nikayarudisha kule ulipokuwa umati wa watu waliyokuwa kwenye hamaki kubwa huku minong’ono ikiwa imetawala.
Nilizidi kuwatazama hatimaye ukafika wakati uzalendo ukanishinda nikaanza kusikia msukumo kutoka ndani ya mwili wangu ukinitaka kwenda kushuhudia nini kilikuwa kimetokea nyumbani kwangu ili kama lipo la kukabiliana nalo nifanye hivyo.
Huo ndiyo uamuzi nilioufikia baada ya kuwaza na kuwazua, kwa ujasiri mkubwa huku miguu yangu ikitetemeka kwa woga nilianza kupiga hatua kwenda mbele, Raya naye alianza kunifuata nyuma bila kuzungumza jambo lolote lile mpaka tulipoufikia kabisa ule umati wa watu.
“Mungu wangu!” Nilijikuta nikitamka kwa hamaki kiasi kwamba watu wengi wakageuza macho yao na kuanza kunitazama.
Wala sikuwa na muda wa kujali juu ya nini walikifikiria juu yangu, macho yangu niliyatoa pima nikishangaa kilichokuwa kimetokea nyumbani kwangu, geti langu la chuma lilikuwa limebomolewa na kutupwa pembeni jambo lililonifanya nizidi kuingiwa na woga juu ya usalama wa Shenaiza.
Ilikuwa ngumu kuamini kila kilichokuwa kinatokea kama kilinitokea nikiwa kwenye ulimwengu wa kawaida, muda mwingi nilikuwa nikifikiri huenda nilikuwa naota na kuna muda ningeweza kushituka, lakini hilo lilikuwa ni jambo lisilowezekana maana kila kilichokuwa kinatokea kilikuwa katika ulimwengu wa kawaida kabisa.
Huku kila mtu akionekana kunishangaa nilizipiga hatua zisizo za taratibu sana kuelekea ndani ya nyumba yangu, lakini baada ya kuvuka tu eneo la mlango na kupiga hatua chache nilianza kuona michirizi ya damu ikitokea ndani sebuleni.
Mapigo ya moyo yalizidi kudunda kwa kasi zaidi maana tayari kutokana na hali halisi nilifahamu Shenaiza yalikuwa yamekwisha mkuta yakumkuta. Nilizidi kupiga hatua za kasi kuifuata ile michirizi ya damu, wakati huo Raya naye alikuwa nyuma yangu lakini pia baadhi ya watu waliokuwa wamefika pale kulishuhudia tukio hilo nao walikuwa wakinifuata mpaka tukaingia ndani kabisa.
Aisee, ilikuwa ni vigumu kuamini nilichokuwa ninakiona mbele yangu. Mwili wa Shenaiza ulikuwa katikati ya dimbwi la damu iliyokauka huku akiwa kimya kabisa! Kwa ujasiri ambao sikuelewa ulitokea wapi nilianza kusogea ili kumgusa na kufahamu kama alikuwa amekufa au la, lakini nilipoendelea kumsogelea watu waliokuwa nyuma yangu walinikataza kufanya hivyo.
“Kaka sikia, usithubutu kumgusa huyo mtu, jambo la kufanya tutoe taarifa polisi,” ilisikika sauati ya mtu moja ikizungumza. Niligeuka na kumtazama.
“Kweli kabisa, yanapotokea mauaji kama hukuwepo eneo la tukio hata kama mtu anakuhusu hutakiwi kumgusa.” Mtu mwingine aliongeza.
Nilibaki nimesimama huku nikihisi miguu yangu ikiishiwa nguvu bila kufahamu nifanye nini, Raya naye alinisogelea na kunitaka niwe imara juu ya kile kilichotokea. Akanisihi kuwasikiliza watu hao nini walikuwa wanasema na zaidi kujikaza kwa sababu mimi ni mwanaume na nilikuwa na kila sababu ya kuwa imara.
Sikuwa mbishi na kama walivyoshauri wale watu ndivyo ilivyofanyika, wao wenyewe waliamua kusaidia kutoa taarifa polisi na baada ya robo saa gari la polisi lilifika nyumbani kwangu pale, bila kupoteza muda askari waliovalia mipira mikononi waliingia mle ndani tulimokuwa, wakauliza nani mwenyeji, nikajitambulisha, wakanitaka kutoa maelezo mafupi juu ya kilichotokea.
Ukweli ni kwamba sikufahamu niseme nini. Kuhusu Shenaiza sikuwa nikimfahamu kabisa tofauti na kuwasiliana naye ndani ya siku chache kwenye simu, jambo lililonifanya hata kubabaika kwenye maelezo, wale askari wakaniambia nilitakiwa kuambatana nao polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.
Hata hivyo jambo ambalo lilinishangaza mno baada ya wale askari kumgeuza Shenaiza waligundua kuwa hakuwa amekufa kama ambavyo sisi tulikuwa tukifikia. Moyo wake ulisikika ukidunda kwa mbali sana jambo ambalo kwa upande fulani nilinifanya kufurahi moyoni.
Walimbeba msichana huyo ambaye alikuwa amelowana chapachapa kwa damu, wakampeleka mpaka kwenye gari walilokuja nalo mahali pale, wakanitaka nami kupanda na kuambatana nao, Raya alipotaka naye kupanda ndani ya gari hilo walimkataza, ikabidi mimi nimwambia achukue usafiri mwingine na kulifuata gari lile la polisi ili aweze kufahamu ninapelekwa kwenye kitua gani jambo ambalo alitii.
Safari haikuwa ndefu sana na wala haikuchukua muda mrefu tayari tulikuwa tumekwishafika katika Kituo cha Polisi Osyterbay, bila kupoteza muda baada ya kuchukua kibali cha matibabu (PF3), gari lile la polisi liliondoka mahali pale na kuelekea hosipitali ambayo sikuifahamu kwa wakati huo, mimi ikabidi nibaki kwa ajili ya mahojiano.
Ukweli ni kwamba katika wakati wote huo nilikuwa kwenye hali mbaya sana. Nafsi yangu ilikuwa inajutia mno juu ya kumkubalia Shenaiza mawazo yake ya kumtorosha hospitali na kwenda naye nyumbani kwangu. Huo niliuona uamuzi wa kipuuzi usiyokuwa na mfano wake maana bila kufanya kwangu hivyo huenda nisingeingia kwenye matatizo hayo yote.
Hata hivyo sikuwa na namna zaidi ya kukubaliana na hali halisi iliyokuwa inaendelea, askari polisi wale waliniingiza katika chumba cha mahojiano na kuanza kunihoji juu ya kilichotokea mpaka Shenaiza akafikia katika hali kama ile aliyokuwa nayo, sikupenda kuficha juu ya ukweli niliokuwa ninaufahamu, zaidi niliwaeleza kuwa hata usiku uliyopita nilitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama maarufu kwa jina la Mabatini lakini sikuweza kupata msaada maana askari wote walikuwa kwenye doria.
Polisi wale walionyesha kushangazwa na jambo hilo, Mabatini kilikuwa kituo kikubwa ambacho ilikuwa si rahisi askari kukauka kabisa, kulionekana kuna uzembe fulani ulikuwa umefanyika, lakini hata hivyo maelezo yangu juu ya tukio na juu ya kumfahamu Shenaiza yalionekana kutowaridhisha wale askari polisi jambo lililofanya waniweke nyuma ya nondo.
Wakati hayo yote yanaendelea Raya alikuwa kituoni hapo na aliweza kupata taarifa za kila kitu kilichotokea, alijaribu kuwashawishi askari ili aweze kutoa dhamana lakini hawakumuelewa, walimwambia ilikuwa ni lazima nikae mahabusu pale wakati upelelezi wa tukio hilo ukiendelea.
Raya hakuwa na namna aliamua kuondoka kituoni kwenda kuwataarifu jamaa zangu wengine juu ya kilichokuwa kimetokea. Mimi nikiwa mahabusu hakuna kilichoendelea ndani ya akili yangu zaidi ya majuto, nilifahamu kabisa niliingia katika msala ambao sikuwa kabisa na hatia nao.
Saa zilikatika nikiwa bado nyuma ya nondo ambapo baadaye kama baada ya kupita saa tatu hivi au nne nilishangaa askari polisi akija kuniita, ambapo akanipeleka tena kwenye chumba cha mahojiano. Wakati huo nilikutana na sura mpya ambapo baada ya salamu askari huyo mwenye sura ya mkazo alianza kunihoji maswali.
Baada ya kumjibu jambo lililonishitua zaidi ni pale aliponiambia kuwa ilibainika Shenazia alikuwa ni mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Amana siku iliyopita na kutoroshwa, hoja ya msingi ilikuwa mimi nilimtoa wapi na utetezi wangu ni upi juu ya kuhusika kwenye tukio lililompata!
Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 12.


ILIPOISHIA:
Baada ya kumjibu jambo lililonishitua zaidi ni pale aliponiambia kuwa ilibainika Shenazia alikuwa ni mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Amana siku iliyopita na kutoroshwa, hoja ya msingi ilikuwa mimi nilimtoa wapi na utetezi wangu ni upi juu ya kuhusika kwenye tukio lililompata!
SONGA NAYO…
MACHO yalinitoka pima nikimtazama yule askari aliyekuwa amekaa mbele yangu akinihoji maswali mfululizo huku akiwa amenikazia macho. Nilijiuliza niseme nini hata askari huyo anielewe bila kupata majibu, ukweli ni kwamba japo moyoni nilifahamu sikuwa kabisa na hatia katika kila kilichokuwa kinaendelea juu ya Shenaiza lakini ilikuwa ni vigumu kuuelezea ulimwengu hata ukaniamini kuwa nilichosema ndicho kilikuwa kweli.
Moyoni nilizidi kugubikwa na majuto, nilifahamu fika hayo yote yaliyonitokea nilijitakia maana kama si ujinga wangu wa kumuamini msichana ambaye sikuwa ninafahamiana naye zaidi ya kuwa na mawasiliano naye kwenye simu nisingefika hapo nilipokuwa.
Huku hayo yote yakiendelea ndani ya akili yangu yule askari alizidi kunisisitiza kujibu maswali aliyokuwa ananiuliza, machozi yakinitiririka niliamua kufunguka kwa mara nyingine ukweli wote kuhusu mimi na Sheneiza. Kuanzia tulivyoanza kuwasiliana na hata nilivyopata taarifa kuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana na yote yaliyoendelea baada ya hapo.
Askari yule alikuwa ananisikiliza kwa makini huku akiandika kwenye kitabu chake kidogo (diary), nafkiri mambo muhimu kutoka katika maelezo yangu niliyompa. Hakuacha kunihoji maswali kwa ajili ya kupata uhakika kwa yale niliyokuwa ninamuelezea baada ya saa zima la mahojiana alimuita askari polisi aliyekuwa zamu akamtaka kunirudisha nyuma ya nondo.
Siyo siri kila kitu ndani ya maisha yangu niliona kuwa kilikuwa kimebadilika na kuwa kigeni mana hata siku moja sikuwahi kufikiri ningeingia mahabusu hasa kwa sababu kama hiyo iliyonipeleka wakati huo.
Nikiwa katika chumba hicho cha mahabusu machozi yalikuwa yanazidi kunibubujika mfururizo. Tofauti na mawazo niliyokuwa nayo hali halisi ilikuwa inatisha, hakukuwa na hewa ya kutosha maana kidirisha pekee kilichokuwepo katika chumba hicho kilikuwa kidogo na kilikuwa juu, kila mmoja alikuwa anagombania aweze kupata hewa kwa kuwa karibu na dirisha.
“Eee Mungu, naomba uniokoe katika mtihani huu, ni mkubwa sana kwangu, nashindwa kuhimili, onyesha miujiza yako ili maisha yangu yasiishie pabaya,” niliwaza huku machozi yakiendelea kunibubujika.
“Wewe vipi mbona unalialia, humu kiumeni unatakiwa kujikaza,” nilisikia sauti ikiniambia kutoka pembeni yangu.
“Mtoto wa mama huyu, humu ndiyo ubayani, hakuna baba wala mama, suipojikaza utaolewa,” alisema mtu mwingine.
Niligeuza uso wangu na kuwatazama kwa zamu hao waliokuwa wanazungumza, wote walionekana kuwa watu wa miraba minne tena wenye makovu mengi usoni, macho yangu yaliganda kwao kwa sekunde kadhaa kisha nikayatoa bila kujibu neno lolote lile.
Saa zikazidi kusonga mbele kwa tabu sana upande wangu nikiwa ndani ya chumba hicho cha mahabusu, majira ya mchana rafiki yangu Justice na Raya walifika katika kituo hicho cha polisi kufanya mipango ili niweze kuachiwa kwa dhamana.
Lakini suala hilo lilionekana kuwa bado gumu sana, polisi hawakuhitaji kabisa kuwasikiliza maana hata pale walipojaribu kuuzunguka mbuyu kwa kuhonga pesa kwa baadhi ya askari wenye nguvu ili angalau nitoke nje kwa dhamana huku upelelezi ukiendelea waliambiwa wasiwe na haraka kwanza maana ishu yenyewe haikuwa ndogo.
Waliambiwa wapelelezi walikuwa wameivalia njuga kesi hiyo na suala la muhimu kama kweli nilikuwa sihusiki katika mipango ya kumuua Sheneiza ilikuwa ni kusali kwa nguvu zote ili msichana huyo aweze kupata nafuu hata azungumze ukweli mzima wa nini kilimtokea mpaka akawa anaandamwa na watu waliokuwa wanataka kupoteza maisha yake.
Rafiki zangu hawakuwa na namna ya kulazimisha kama walivyokuwa wanataka wao, walichofanya ilikuwa ni kuomba ruhusa ya kuzungumza na mimi japo kwa dakika chache tu. Kwa kuwa kuna chochote walikuwa wamekwishapenyeza kwa askari hao hilo halikuwa suala gumu sana, waliruhusiwa, nikatolewa mahabusu na kwenda kuzungumza nao.
“Haya yote yatakwisha, hutakiwi kujali kabisa baba, jipe moyo kila kitu kitakuwa sawa,” Raya aliniambia huku machozi yanambubujika kwa wingi.
“Asante Raya, ninaamini hivyo pia, Mungu atanisimamia na kila kitu kitakwenda sawa.” Nilimjibu.
“Hapa kaka ni muhimu kuomba kwa nguvu zote huyo mgonjwa maendeleo yake yawe mazuri ili aeleze ukweli mzima wa nini kimetokea, hicho pekee ndicho kinachoweza kukutoa kwenye hii hatia,” Justice aliniambia.
“Ndivyo askari walivyosema?”
“Ndiyo, mimi pia ninaunga mkono suala hilo maana hakuna njia nyingine ya kukunusuru.”
“Dah! Kwani Sheneiza amelazwa wapi?” Nilimuuliza Justice swali lingine.
“Yuko Mwananyamala hospitali lakini sijafahamu amelazwa katika wodi namba ngapi.”
“Fuatilia kaka ufahamu pia na maendeleo yake maana huyo ndiyo kila kitu kwenye hili suala kama unavyosema. Lakini kuna kitu pia nilikuwa ninakifikiria ambacho tunaweza kuzungumza na askari polisi wazidishe ulinzi katika hospitali hiyo kutokana na hali halisi, hao watu wanaotaka kumuua wakigundua kuwa bado ni mzima lazima wataendelea kumuandama.”
“Hilo ni kweli kaka, niachie mimi, nitazungumza na mkuu wa kituo maana ni mtu mzuri, ametupokea vyema mimi na Raya.”
Baada ya kuzungumza mawili matatu na rafiki zangu hao ambao walionekana kuniunga mkono kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kunifariji katika matatizo yangu hayo yaliyokuwa yananisonga, nilirudishwa mahabusu na wao walikwenda kama tulivyozungumza kwa mkuu wa kituo na kumwambia juu ya kuongeza ulinzi kwenye Hospitali ya Mwananyamala.
Hatimaye siku hiyo ilimalizika nikiwa ndani ya kituo hicho cha polisi, siku iliyofuata majira ya asubuhi Raya alikuwa kituoni hapo kwa ajili ya kuniletea kifungua kinywa. Ukweli ni kwamba hakuna wakati niliyomuona Raya kuwa ni mtu wa muhimu kwangu kama wakati huo nilipopata matatizo.
Huko nyuma nilikuwa mtu wa kumchukulia poa sana kwa vitendo vyake vya kuonyesha kuwa ananipenda lakini wakati huo thamani yake niliiona na niliamini kweli mwanamke huyo alikuwa ananipenda kwa dhati.
Baadaye Raya aliondoka na mimi niliendelea kukaa kwenye chumba kile cha mahabusu ambapo mchana nikiwa sina hili wala lile nilishituka baada ya kumuona askari polisi akija kwenye nondo na kuita jina langu, nilipoitika alinichukua mpaka mapokezi nikapewa nguo zangu na kuambiwa nivae, baada ya kuvaa akanitaka nimfuate kuelekea nje, nilifanya hivyo na tulipoanza tu kutoka nje askari wengine watatu walioshika mtutu wa bunduki mkononi walitufuata nyuma tukaenda kuingia pamoja kwenye difenda.
Difenda hilo liliwashwa na kuanza kuelekea mahali ambapo sikuweza kupafahamu kwa mara moja, nilikaa kimya katikati ya askari hao bila kuzungumza neno lolote lile na safari ikazidi kupamba moto. Nilikuja kugundua kuwa huenda tunaelekea Mwananyamala Hospitali baada ya kuumaliza Mtaa wa Makumbusho na kushika barabara ya Mwananyamala, moyoni nilianza kugubikwa na maswali mengi, nilijiuliza kama ni kweli ninapelekwa katika hospitali hiyo ilikuwa ni kufanya nini?
Je, nini kitaendelea kwenye simulizi hii?
 
SEHEMU YA 12.


ILIPOISHIA:
Nilikuja kugundua kuwa huenda tunaelekea Mwananyamala Hospitali baada ya kuumaliza Mtaa wa Makumbusho na kushika Barabara ya Mwananyamala, moyoni nilianza kugubikwa na maswali mengi, nilijiuliza kama ni kweli nilipelekwa katika Hospitali hiyo ilikuwa ni kufanya nini?
SASA ENDELEA…
“Tumekuleta huku hospitalini kwa sababu kwanza maelezo uliyoyatoa kituoni, kwa kiasi fulani yanapishana na maelezo aliyoyatoa huyu mgonjwa kwa sababu wewe ulisema humfahamu kwa undani zaidi ya kuanza kuwasiliana naye kwenye simu siku chache zilizopita.
“Lakini yeye amesema wewe ni mpenzi wake wa siku nyingi, mna mipango ya kufunga ndoa na tayari ana ujauzito wako,” alisema askari mmoja wa kike, miongoni mwa wale waliokuja kunichukua mahabusu, wakati huo tukiwa tayari tumeshawasili Hospitali ya Mwananyamala.
Akaendelea: “Lakini kingine ni kwamba amekataa kutoa ushirikiano wa kueleza nini kilichotokea mpaka wewe uwepo ndiyo maana tumekufuata, hutakiwi kuzungumza chochote, umenielewa?”
Nilitingisha kichwa kuonesha kukubali kile alichokisema. Mfululizo wa matukio ya kushangaza ulikuwa unaendelea, nilijiuliza iweje tena Shenaiza awaeleze polisi kwamba mimi nilikuwa mpenzi wake na kwamba tulikuwa na mipango ya kufunga ndoa?
Yote tisa, kumi nilijiuliza iweje awaambie kwamba alikuwa na ujauzito wangu wakati hatukuwahi kukutana kimwili hata mara moja? Kama kweli alikuwa mjamzito, mimi nilikuwa nahusikaje? Nilikosa majibu.
“Jamal! Ooh my God! Thanks for coming my dear,” (Jamal! Ooh Mungu wangu, ahsante kwa kuja mpendwa wangu) alisema Shenaiza kwa sauti ya chini akionesha kwamba yupo kwenye maumivu makali, alizungumza kwa Kiingereza kizuri huku akitanua mikono yake kama ishara ya kunitaka nimkumbatie.
Sikuwahi kumsikia akizungumza Kiingereza, nikabaki na swali jingine lakini sikutaka kumuonesha chochote, nikalilazimisha tabasamu usoni kwangu, nikamuinamia pale kitandani alipokuwa amelala, dripu ikiendelea kutiririka kwa kasi kuingia mishipani mwake, nikamkumbatia, akanibusu shavuni na kuning’ang’ania kifuani kwake, tukiwa kwenye hali hiyo alinibusu mdomoni na kunifanya nijisikie aibu ndani ya moyo wangu.
Kwa jinsi alivyokuwa akinidekea, mtu yeyote angeweza kuamini kwamba kweli sisi ni wapenzi wa muda mrefu, nikageuka na kumtazama yule askari ambaye moyoni ni kama alikuwa anasema ‘unabisha nini sasa? Kama siyo mpenzi wako angekubusu mdomoni?’.
“Please help me Jamal, they want to kill me! You are my only savior,” (Tafadhali nisaidie Jamal, wanataka kuniua! Wewe ndiyo mkombozi wangu wa pekee) alisema Shenaiza kwa sauti ya chini akiwa bado amenikumbatia. Japokuwa yule askari alikuwa mita chache tu kutoka pale kitandani, hakuweza kusikia chochote.
Kwa kuwa nilishaambiwa sitakiwi kuzungumza chochote, sikumjibu chochote zaidi ya kumtazama usoni huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua hao anaosema wanataka kumuua ni akina nani na ilikuwaje mpaka watake kumuua?
“Inatosha sasa, hebu kaa pembeni. Binti, naamini sasa utatoa ushirikiano maana uliyekuwa unamtaka tumeshamleta,” alisema yule askari huku akinielekeza kukaa pembeni ya kitanda cha mgonjwa, akarudi kinyumenyume na kufungua mlango, askari wengine watatu, akiwemo yule aliyenihoji mimi wakaingia na kusimama kwa kutuzunguka.
Yule askari wa kike akawaeleza jambo kwa sauti ya chini ambayo mimi na Shenaiza hatukusikia kisha tukawaona wote wakitoka, akabaki yule mmoja aliyenihoji mimi siku iliyopita, mkononi akiwa na ‘diary’, akavuta kiti na kukisogeza karibu na pale Shenaiza alipokuwa amelala.
“Si umeshaambiwa maelezo yote kwamba hutakiwi kuzungumza chochote?” yule askari ambaye nilishamtambua kwamba ni mpelelezi, aliniambia.
“Ndiyo.”
“Oke vizuri, binti unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri,” alijibu Shenaiza, akamwambia anataka kuanza upya kumhoji na anaamini atatoa ushirikiano kwa sababu mimi nilikuwepo.
“Jina lako kamili unaitwa nani?”
Shenaiza alinitazama kabla ya kuanza kujibu, akanionesha ishara ambayo sikuielewa, nikabaki kumtazama tu huku na mimi nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia maelezo yake maana kiukweli hata mimi sikuwa namfahamu kwa undani.
“Shenaiza Petras Loris,” alijibu Shenaiza. Nilishangazwa na jina lake, sikuwahi kusikia Mtanzania yeyote akiwa na jina hilo, akilini nikaanza kupata majibu kwamba kile nilichokuwa nakihisi awali kwamba msichana huyo hakuwa Mtanzania kutokana na mwonekano wake kilikuwa kweli.
Yule askari aliendelea kumhoji maswali kama polisi wote wanavyofanya, akafikia swali la kabila na utaifa wake, Shenaiza akanitazama tena na kushusha pumzi ndefu kisha akamjibu:
“Kabila langu ni Aethikes,” alijibu, yule askari akapigwa na butwaa na kuacha kuandika, akamtazama Shenaiza kwa muda kisha akanigeukia na mimi, mshangao aliokuwa nao ulikuwa sawa na niliokuwa nao mimi.
‘Bini, hebu kuwa ‘serious’, hilo ndiyo kabila gani? Tangu nianze kufanya kazi huu mwaka wa kumi sasa sijawahi kusikia kabila kama hilo hapa Tanzania, hebu taja kabila lako,” alisema yule askari kwa sauti iliyoonesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
“Mimi siyo Mtanzania, natokea Greece (Ugiriki), asili yetu ni Attica, baba yangu amezaliwa na kukulia kwenye Jiji la Athens lakini mama yangu ni mpare wa Mtae, Lushoto mkoani Tanga ndiyo maana unaona naweza kuzungumza Kiswahili vizuri,” alisema msichana huyo huku akionesha kujiamini mno.
Nilimuona yule askari akiandika maelezo hayo kwenye ‘diary’ yake, akaendelea kumhoji maswali mengine ambapo niligundua kwamba msichana huyo, alikuwepo nchini kisheria na kubwa zaidi, kumbe alikuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mahojiano yaliendelea, kikafikia kipengele cha muhimu ambacho ndiyo hasa nilichokuwa nakisubiri kwa shauku kubwa, cha kutaka kujua nini kilitokea mpaka msichana huyo mrembo akajeruhiwa vibaya na kwenda kulazwa Hospitali ya Amana kabla ya mimi kumsaidia kutoroka mpaka nyumbani kwangu, na kile kilichokuwa kimetokea nyumbani kwangu usiku.
Shenaiza alivuta pumzi ndefu baada ya kuulizwa swali hilo, akazishusha kisha akatulia, ukimya mkubwa ukapita kati yetu mle wodini. Ilibidi yule askari avunje ukimya na kurudia tena kumuuliza swali lile lakini badala ya kutoa majibu kama alivyokuwa akifanya kwa maswali yote, alikaa kimya huku machozi mengi yakimtoka na kulowanisha uso wake.
‘Kijana hebu naomba utupishe mara moja, toka nje nitakuita,” alisema yule askari, ikabidi nitii, nikawaacha wenyewe wawili mle wodini.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU 13.


ILIPOISHIA:
Ilibidi yule askari avunje ukimya na kurudia tena kumuuliza swali lile lakini badala ya kutoa majibu kama alivyokuwa akifanya kwa maswali yote, alikaa kimya huku machozi mengi yakimtoka na kulowanisha uso wake.
“Kijana hebu naomba utupishe mara moja, toka nje nitakuita,” alisema yule askari, ikabidi nitii, nikawaacha wenyewe wawili mle wodini.
SASA ENDELEA…
Nilihisi kichwa changu kikipata moto, nilikuwa na shauku kubwa mno ya kutaka kuufahamu ukweli wa kilichokuwa kimemtokea Shenaiza. Lile swali la awali kwamba yeye ni nani, tayari nilishapata majibu kwa kiasi fulani lakini bado nilitaka kujua nini hasa kilichomtokea.
Mazungumzo kati ya Shenaiza na yule mpelelezi kule ndani yaliendelea kwa muda na baada ya kama dakika kumi na tano kupita, mlango ulifunguliwa na yule mpelelezi akatoka, akanionesha ishara kwamba niingie ndani.
Nikaenda ambapo nilimkuta Shenaiza akiwa anajifuta machozi, macho yake yakiwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu sana.
“Come to me Jamal, you are my comfort,” (Njoo Jamal, wewe ndiyo faraja yangu) alisema Shenaiza kwa sauti ya chini, nikamsogelea pale kitandani na kumkumbatia, akanibusu shavuni na kuniomba radhi kwa kilichotokea.
“Unaniomba radhi kwa nini Shenaiza?”
“Najua hujajisikia vizuri kwa mimi kuzungumza kilichonitokea wakati wewe ukiwa nje, nilitamani na wewe usikie lakini naona kwa sasa siyo muda muafaka lakini nakuahidi kwamba muda mfupi ujao nitakueleza wala usijali,” alisema Shenaiza huku akiendelea kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu.
Nilimtoa wasiwasi na kumtaka awe huru na mimi, akaniachia kisha nikakaa pembeni ya kitanda chake.
“Walitaka kuniua jana, yaani ni Mungu tu na naamini hata wao wanajua kwamba nimekufa, wamenipiga sana,” alisema Shenaiza na kuniambia anajisikia vibaya sana kuniingiza kwenye matatizo ambayo wala hayakuwa yakinihusu.
“Nakuomba sana nikishapata nafuu kidogo tu tuondoke, hata ikibidi kwenda kuishi hotelini mimi nitagharamia kila kitu maana wanaweza kurudi tena kule nyumbani kwako kwa sababu wanaamini kwamba nimeshakwambia kila kitu kinachoendelea.”
“Kwa hiyo unataka kusema wanaweza tena kurudi nyumbani kwangu?”
“Ndiyo! Wanaweza kurudi na kukudhuru bure wakati hauna hatia yoyote,” alisema Shenaiza, kauli ambayo ilinishangaza na kunijaza hofu kubwa moyoni. Kuna wakati nilikuwa najuta sana kwa kujiingiza kwenye mdomo wa mamba bila kujua.
Shenaiza aliendelea kuniongelesha mambo mbalimbali lakini wala akili yangu haikuwa pale, nilikuwa nikiwaza mambo tofauti kabisa. Baadaye nesi aliingia na kunieleza kwamba mgonjwa alikuwa anahitaji kupumzika kwa hiyo nitoke na kumuacha peke yake.
Shenaiza alikuwa mbishi kidogo lakini baadaye alikubali, akaomba kabla sijatoka nimbusu, nikamuinamia pale kitandani kwa lengo la kumbusu kwenye shavu lake lakini alinishika shingoni na kunivutia kwake, ndimi zetu zikagusana na kunifanya nipigwe na ganzi kwa sekunde kadhaa, aliponiachia, nilibaki nimeganda vilevile mpaka nesi aliponishtua.
“Inabidi uende nje kaka ili tumhudumie mkeo kisha apate muda wa kupumzika,” alisema yule nesi, nikashtuka kama mtu aliyekuwa usingizini, nikageuka na kumtazama Shenaiza pale kitandani, akanifinyia jicho lake moja na kunibusu kwa mbali, nikatoka mpaka nje huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wangu.
“Jamal! Uko salama mpenzi wangu? Nakupigia simu lakini sikupati mpaka imebidi nije huku,” alisema Raya ambaye aliponiona tu nikitoka wodini, alikuja na kunikumbatia kwa nguvu, akionesha kuwa na hofu kubwa na ukimya wangu.
Hata hivyo sikumtilia sana maanani, japokuwa nilitoka nikiwa natabasamu, nilipomuona nilikunja sura, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa simu, nikagundua kuwa kumbe kweli ilikuwa imejizima bila mimi kufahamu, nikaiwasha na kusogea mpaka pembeni kulikokuwa na mabenchi, nikakaa. Raya naye akaja na kukaa pembeni yangu, akawa na shauku kubwa ya kutaka kusikia chochote kutoka kwangu.
“Niache kidogo Raya, akili yangu haijatulia kabisa, tutazungumza baadaye,” nilimjibu msichana huyo kwa kifupi, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kutulia kimya. Maskini Raya! Alionesha kuwa na hisia nzito juu yangu lakini kwa bahati mbaya mwenzake nilikuwa namchukulia kawaida sana.
Sote tukiwa kimya kabisa, nilikumbuka kilichotokea kati yangu na Raya usiku na kujikuta nikishindwa kumeza chakula nilichotafuniwa, nikageuka na kumtazama usoni, naye akanitazama, nikagundua kwamba alikuwa akilengwalengwa na machozi.
“Najua hunipendi Jamal lakini hiyo isiwe sababu ya kuninyanyasa, nakupenda sana mwenzio kuliko mtu yeyote chini ya jua, naamini ipo siku utaujua ukweli,” alisema msichana huyo, nikarudia kumsisitiza kwamba aniache kidogo hayo mambo tutayajadili baadaye, safari hii nilizungumza kwa sauti ya chini nikiwa kama nambembeleza f’lani, nikamuona ametulia.
Nikiwa nimekaa pale, nilimuona yule askari mpelelezi akiwa na wenzake, nikamuomba Raya anisubiri hapohapo, nikainuka na kumfuata huku bado nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua alizungumza nini na Shenaiza.
Hata hivyo, licha ya kumfuata askari huyo na kumuomba anidokeze alichoelezwa na Samantha, alikataa katakata kwa maelezo kwamba atavuruga upelelezi, nikakosa cha kufanya. Nilirudi hadi pale nilipokuwa nimemuacha Raya, nikakaa pembeni yake huku nikiwa kimya kabisa.
“Nakushuru kwa jinsi ulivyojitoa kunisaidia katika haya matatizo yanayonikabili,” nilivunja ukimya na kumsemesha Raya, nikamuona akiinua uso wake ambao muda wote alikuwa ameuinamisha chini, akanitazama huku tabasamu hafifu likichanua kwenye uso wake.
“Usijali Jamal, nipo kwa ajili yako na kamwe sitakuacha peke yako hata iweje.”
“Yaani japokuwa ulikuwa unalia lakini macho yako yamezidi kuwa mazuri,” nilimtania Raya, akashindwa kujizua na kucheka kwa nguvu. Hakuna kitu alichokuwa anakipenda Raya kama kusikia kauli yoyote ya kumsifia kutoka kwangu. Ile huzuni aliyokuwa nayo, iliyeyuka kama theluji juani, akachangamka kabisa.
“Na leo si tutaenda kulala pamoja nyumbani kwetu?”
“Kwani wazazi wako bado hawajarudi?”
“Bado!”
“Ok, tutaangalia itakavyokuwa,” niliamua kumjibu hivyo Raya ili kumridhisha ingawa ukweli ni kwamba kauli hiyo haikuwa imetoka ndani ya moyo wangu. Wakati tukiendelea kuzungumza, niligundua jambo lisilo la kawaida.
Mita chache kutoka pale tulipokuwa tumekaa, kulikuwa na maegesho ya magari. Magari mengi yalikuwa yameegeshwa lakini miongoni mwa magari hayo, ndani ya gari moja kulionekana kuwa na watu zaidi ya mmoja ambao baadaye nilikuja kushtukia kwamba walikuwa wakitutazama sana mimi na Raya pale tulipokuwa tumekaa na zaidi walikuwa wakiniangalia mimi.
Nilipogeuka haraka na kuwatazama, macho yangu na yao yaligongana lakini wakazuga kwamba hawakuwa wakinitazama, wakawa wanaendelea na mazungumzo yao.
“Kwani nini wananitazama mimi?” nilijikuta nikizungumza kwa sauti, Raya akashtuka na kuniuliza nilikuwa namaanisha nini? Nikataka kumzuga lakini haikuwa rahisi, akafanikiwa kugundua kuwa nilikuwa nawatazama watu gani.
“Hata mimi nimewaona muda mrefu tu, tangu unatoka wodini walikuwa wakikutazama lakini sikuwatilia maanani.”
“Tuondoke!” nilisema huku nikiinuka pale nilipokuwa nimekaa kwani tayari kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa changu, Raya naye akainuka, tukaanza kuelekea kwenye lango la kutokea nje ya hospitali hiyo lakini cha ajabu zaidi, tukiwa getini tunataka kutoka, nililiona lile gari nalo likija kule tulipokuwepo.
Je, nini kitafuatia? Usikose
 
SEHEMU YA 14.


ILIPOISHIA:
“Tuondoke!” nilisema huku nikiinuka pale nilipokuwa nimekaa kwani tayari kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa changu, Raya naye akainuka, tukaanza kuelekea kwenye lango la kutokea nje ya hospitali hiyo lakini cha ajabu zaidi, tukiwa getini tunataka kutoka, nililiona lile gari nalo likija kule tulipokuwepo.
SASA ENDELEA…
“Bodaboda! Bodaboda!” niliita kwa sauti huku tukitembea kwa haraka kuelekea nje ya hospitali, lile gari nalo likizidi kuja kwa kasi kule tulipokuwepo. Ilibidi nimshike mkono Raya kwani kwa jinsi alivyokuwa ‘mayai’ ningeweza kumuacha pale na kumsababishia matatizo.
Kwa bahati nzuri, dereva mmoja wa bodaboda alituona na harakaharaka akawasha pikipiki yake na kutufuata, mwenyewe akijiona amewazidi wenzake ujanja kwa kuwahi abiria.
“Tupeleke Kijitonyama,” nilisema huku nikimsaidia Raya kupanda, na mimi nikapanda lakini dereva wa bodaboda hakutaka kuondoka mpaka tukubaliane kwanza.
“Twende bwana nitakupa kiwango chochote unachotaka.”
“Lakini siku hizi haturuhusiwi kupakiza mishikaki nitakamatwa.”
“Twendeee,” nilisema kwa sauti ya juu, yule dereva akaondoa pikipiki, kabla hajafika popote wote tulishtukia bodaboda ikikoswakoswa kugongwa kwa nyuma na lile gari lililokuwa linatufuata kwa kasi. Dereva wa bodaboda alitaka kusimama pembeni kulipisha gari hilo lakini nilimsisitiza kuongeza mwendo na kuhakikisha analipoteza kabisa lile gari.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Akiwa haelewi kinachoendelea, hofu kubwa ikiwa imemkumba moyoni, yule dereva bodaboda alikata kona ya ghafla na kuingia kwenye uchochoro mita chache mbele, hali iliyosababisha lile gari ambalo lilikuwa likijiandaa kutugonga kwa nyuma lipitilize kwa kasi, likaenda kusimama mita chache mbele.
Raya alikuwa akipiga kelele kwa nguvu huku akilitaja jina la Mungu wake, hakuelewa kilichotokea kiasi cha kujikuta katikati ya mtego wa kifo kama ule, nikawa nambembeleza na kumtaka atulie.
Lile gari lilirudi kinyumenyume na kujaribu kupita kwenye ule uchochoro kuifuata ile bodaboda lakini sehemu ilikuwa ndogo, likashindwa. Nikawa namsisitiza dereva kuzidi kuongeza kasi, tukatokeza mtaa wa pili na kuingia kwenye barabara ya lami, safari ikazidi kupamba moto.
“Usipite barabara kubwa, wanaweza kuwa wanatufuatilia, ingia kushoto hapo mbele,” nilimwambia, wazo ambalo dereva huyo alilifuata, tukawa tunazidi kukata mitaa tukitumia njia za uchochoroni.
“Nataka twende nyumbani kwetu Jamal,” alisema Raya huku akiwa bado na hofu kubwa moyoni.
“Ok sawa,” nilimjibu kwa kifupi kwa sababu kiukweli sikuwa nataka kupata muda wa kukaa peke yangu na Raya kama ilivyotokea usiku uliopita lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa sikuwa na ujanja.
Dakika kadhaa baadaye, tayari tulikuwa tumefika Kijitonyama lakini kwa kukwepa kuonekana tumeelekea wapi, tuliamua kushuka kwenye bodaboda, tukakubaliana bei na dereva huyo ambaye licha ya kulipwa fedha zake, alionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea.
Hata hivyo, sikuwa tayari kumueleza chochote, akaondoka kwa shingo upande huku akigeukageuka nyuma, kuna wakati alihisi huenda alikuwa ametubeba majambazi lakini alikosa ushahidi wa hilo.
Yule dereva bodaboda alipoondoka tu, mimi na Raya tulipanda kwenye Bajaj ambayo ilitupeleka mpaka nyumbani kwa akina Raya, tukawa na uhakika mkubwa kwamba hata kama wale watu wataamua kutufuatilia, haitakuwa rahisi kutupata.
“Naomba ukaoge kwanza wakati mimi nafanya utaratibu wa chakula,” alisema Raya baada ya kuhakikisha milango yote ya nyumba hiyo imefungwa kwa ndani, kuanzia geti kubwa la nje mpaka milango ya ndani.
Kwa kuwa wazazi wa Raya hawakuwa wamerejea safarini kama mwenyewe alivyonieleza, kwa mara nyingine tulijikuta tukiwa peke yetu ndani ya nyumba.
Wakati nikiendelea kujiuliza kuhusu mfululizo wa matukio yaliyokuwa yakiendelea kuniandama kiasi cha kunifanya nikose uhakika juu ya maisha yangu, Raya alikuwa akifikiria jambo jingine tofauti kabisa.
Niliingia kwenye chumba cha wageni ambacho ndicho nilicholala usiku uliopita na kubadilisha nguo, nikajifunga taulo na kuelekea bafuni, mawazo mengi yakiendelea kukisumbua kichwa changu.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Bado nilishindwa kupata majibu kuhusu Shenaiza, sikuwa nikielewa kama Shenaiza alikuwa ni mtu wa namna gani, akina nani walikuwa wakiyawinda maisha yake na alikuwa na uhusiano gani nao. Kila swali nililojiuliza halikuwa na majibu.
“Shenaiza Petras Loris,” nililikumbuka jina kamili la msichana huyo alilolitaja wakati akihojiwa na yule mpelelezi.
“Kabila langu ni Aethikes… mimi siyo Mtanzania, natokea Greece (Ugiriki), asili yetu ni Attica, baba yangu amezaliwa na kukulia kwenye Jiji la Athens lakini mama yangu ni mpare wa Mtae, Lushoto mkoani Tanga,” maneno ya Shenaiza wakati akijieleza yalikuwa yakijirudiarudia ndani ya kichwa change kama mkanda wa video.
“Lazima niujue ukweli! Lazima!” nilisema wakati nikifungulia bomba la maji ya mvua, maji ya baridi yakawa yananimwagikia na kuufanya mwili wangu uliokuwa umechoka sana upate nguvu mpya.
Japokuwa msichana huyo hakuwa tayari kunieleza ukweli zaidi ya kuishia kuniambia nisubiri ataniambia, niliamua kuutafuta ukweli kwa njia nyingine ingawa bado sikuwa naijua ni njia gani na nitafanyaje kumfahamu Shenaiza.
Nilikaa muda mrefu bafuni, nikiwa naendelea kujimwagia maji huku akili yangu ikienda mbio kuliko kawaida. Nilikuja kushtuka baada ya kusikia Raya akiniita na kuugonga mlango wa bafuni.
“Mbona hutoki bafuni mpenzi wangu,” alihoji Raya kwa sauti ya kubembeleza, harakaharaka nikafunga bomba na kuchukua taulo, nikajifuta na kufungua mlango, macho yangu yakagongana na Raya ambaye naye alikuwa amejifunga khanga moja tu.
“Na mimi nataka kuoga, nisubiri tuondoke wote,” alisema msichana huyo huku akinitazama kwa macho yaliyojaa ujumbe mzito, taratibu akanirudisha bafuni, nilishindwa kumzuia, naye akaingia na kufunga mlango kwa ndani.
“Nataka leo na mimi nideke, naomba uniogeshe,” alisema Raya na kunifanya nijikute kwenye wakati mgumu kwa mara nyingine, nikiwa bado sijui nijibu nini, msichana huyo alifungua khanga na kuitundika nyuma ya mlango, akabaki kama alivyoletwa duniani, vifuu viwili vikiwa vimechomoza kwenye kifua chake na kunifanya nisisimke mwili mzima.
Akalishika taulo nililokuwa nimejifunga na kulivuta kisha akalitundika pale alipoweka khanga yake, tukabaki saresare maua! Akanisogelea jirani kabisa kiasi cha kila mmoja kuanza kuzisikia pumzi za mwenzake, tukawa tunatazamana machoni huku ‘Jamal’ wangu naye akianza kufura kwa hasira.
***
Baada ya kumaliza kumhoji Shenaiza, yule askari mpelelezi, alitoka hadi nje alikowaacha wenzake, akawavuta pembeni na kuanza kuwaeleza alichoelezwa na msichana huyo, kila mmoja akawa ametulia akimsikiliza. Maelezo aliyoendelea kuyatoa, yalimshangaza kila mmoja, wakawa wanatazamana wakiwa ni kama hawaamini walichokuwa wakiendelea kukisikia kutoka kwa mwenzao.
“Kwani amesema asili yake ni wapi?”
“Ni Athens, Greece! Na kubwa zaidi, amesema jina lake kamili ni Shenaiza Petras Loris.”
“Unataka kusema kwamba ni mtoto wa Petras Loris huyu tunayemjua?”
“Sijamuuliza lakini kwa maelezo yake, upo uwezekano mkubwa akawa ni mwanaye au wana undugu fulani.”
“Aisee! Mbona hii inaonekana kuwa ngoma nzito?”
“Ni ngoma nzito kwelikweli, halafu kuna huyu kijana ameingizwa kwenye mtego bila mwenyewe kujua chochote, mpaka namuonea huruma.”
Je, nini kitafuatia? Usikose
 
SEHEMU YA 15.


ILIPOISHIA:
“Aisee! Mbona hii inaonekana kuwa ngoma nzito?”
“Ni ngoma nzito kwelikweli, halafu kuna huyu kijana ameingizwa kwenye mtego bila mwenyewe kujua chochote, mpaka namuonea huruma.”
SASA ENDELEA…
“Kwa akili zako unafikiri huyu kijana atakuwa ameingia kwenye mtego mwenyewe akiwa hajui chochote?”
“Hajui chochote, hata maelezo aliyokuwa anayatoa, yanaonesha kabisa hakuna anachokijua.”
“Unafikiri inawezekana mtu akaingizwa kwenye kumi na nane za Loris kama hana umuhimu? Hata kama mwenyewe hajui naamini lazima kuna jambo ambalo limefanya aingizwe kwenye huu mtego.”
“Lakini hajaingizwa na Loris mwenyewe isipokuwa binti yake.”
“Nani ambaye hajui kwamba Loris amekuwa akimtumia mwanaye kwenye kazi zake, hasa pale anapoona mambo yameanza kuwa magumu kwake?”
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Yote yanawezekana lakini taarifa za ndani zinaonesha kwamba huyu binti mwenyewe ameshachoka kumtumikia baba yake na ndiyo maana unaona anaandamwa na matatizo makubwa!”
“Unataka kusema ndiyo maana anatishiwa kuuawa?”
“Inawezekana kabisa, nahisi kuna jambo kubwa analolifahamu lakini hataki kueleza ukweli kwa sababu hata ukifuatilia maelezo aliyokuwa anayatoa, anazungumza vitu nusunusu sana.”
“Mh! Kweli hii ngoma nzito! Kwa hiyo tunafanyaje?”
“Inabidi tuwasiliane kwanza na mkuu, si unajua mtandao wa Loris unahusisha mpaka viongozi wetu?”
***
Raya alishika taulo nililokuwa nimejifunga na kulivuta kisha akalitundika pale alipoweka khanga yake, tukabaki saresare maua! Akanisogelea jirani kabisa kiasi cha kila mmoja kuanza kuzisikia pumzi za mwenzake, tukawa tunatazamana machoni huku ‘Jamal’ wangu naye akianza kufura kwa hasira.
“Quench my thirst dear Jamal! I’m in deep love with you, take me and let me feel like a real woman!” (Nikate kiu yangu mpenzi wangu Jamal! Nipo kwenye penzi lenye kina kirefu na wewe, nichukue na unifanye nijihisi kuwa mwanamke niliyekamilika!) alisema Raya kwa sauti iliyokuwa ikisikika kama ya mtoto mchanga.
Bado sikuwa najua nifanye nini kwa sababu sitaki kusema uongo, ukiachilia mbali ukweli kwamba sikuwa na hisia za kimapenzi dhidi yake, Raya alikuwa ni msichana mzuri sana ambaye mwanaume yeyote aliyekamilika, asingeweza kumuacha, hasa katika mazingira kama yale tuliyokuwepo.
Akionesha kuwa na shauku kubwa, alinikumbatia kwa nguvu na tukagusanisha ndimi zetu, nikahisi kama mwili wangu umepigwa na shoti kali ya umeme.
Kwa kutumia mkono mmoja, alifungua bomba la maji, yakawa yanatumwagikia mithili ya watu waliokumbatiana kwenye mvua kali, hali iliyonizidishia msisimko mkali kwani japo maji yalikuwa ya baridi, joto la mwili wake lilinifanya nijihisi kama nipo kwenye ulimwengu wa tofauti kabisa.
Alifunga bomba na kuchukua sabuni, ingawa tayari nilishakuwa nimeoga, alianza upya kunipaka sabuni mwili mzima, nikazidi kusisimka pale mikono yake laini ilipokuwa ikinipaka sabuni, alipomaliza alitaka na mimi nifanye kama vile. Nikaanza kumpaka sabuni mwili mzima, kusema ukweli hakuna siku ambayo nilisisimka kama siku hiyo.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Baada ya kumaliza, alifungua tena maji, tukaoga huku mara kwa mara tukigusanisha ndimi zetu, tulipomaliza alichukua taulo na kunifuta kwa mahaba mazito kisha akanifunga kiunoni, na yeye akachukua khanga yake moja na kujifunga bila hata kujifuta.
Kwa kuwa mwili wake ulikuwa na maji, khanga ile ilishikana na ngozi ya mwili wake na kulifanya umbo lake lionekane vizuri, hasa maeneo ya kiunoni kwa nyuma ambayo yalikuwa si haba! Kwa makusudi kabisa, akatangulia mbele na kuanza kutembea kwa maringo kuelekea chumbani kwake.
Nilijikuta nikiwa kama kondoo anayepelekwa machinjioni, nikawa namfuata nyumanyuma huku macho yangu yakiwa hayabanduki kwenye mwili wake, nikimeza mate kama fisi aliyeona mfupa. Sikuelewa kilichofuatia zaidi ya kujishtukia tukiwa juu ya kitanda chake kikubwa.
Hata sikukumbuka taulo langu nililivua muda gani, achilia mbali khanga yake, zaidi ya kujikuta wote wawili tukiwa kama tulivyoletwa duniani, hakukuwa na mazungumzo tena, kilichosikika kilikuwa ni miguno ya hapa na pale wakati joto la huba likizidi kupanda kwenye mtima wa kila mmoja.
Dakika kadhaa baadaye, kila mmoja alikuwa tayari kwa pambano la kirafiki lisilo na jezi wala refa, Raya akionesha kuukamia mchezo kuliko kawaida. Kabla hata kipyenga cha kuashiria mpambano kuanza hakijalia, tayari Raya alishamkamata ‘Jamal’ wangu na kumuelekeza kwenye lango la kuingilia ngome kuu, nami nikawa mtiifu kwa kila alichokuwa anakifanya Raya.
Tofauti kabisa na nilichokuwa nimekitegemea, ‘Jamal’ wangu alikutana na ukuta mgumu wa ngome hiyo, ikabidi nimuongezee nguvu ya kusonga mbele, nikamuona Raya akiuma meno na kufumba macho yake, zoezi lililosindikizwa na miguno ambayo sikuelewa kama ilikuwa ya raha au maumivu.
Miguno ile iliniongezea hamasa, huruma zikaniishia kabisa, nikaongeza nguvu na muda mfupi baadaye, tayari tulikuwa tukielea kwenye ulimwengu mwingine tofauti kabisa, ambao kwa Raya ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuufikia. Nikiri kwamba kwa mara ya kwanza, nilijikuta nikiijutia nafsi yangu kwa kushindwa kumuelewa Raya mapema na kumpa nafasi ndani ya moyo wangu.
Haikuwa rahisi kwa msichana mrembo kama yeye, kwa umri wake, elimu yake na uwezo wa familia yao, kuwa bado hajaguswa mpaka siku hiyo. Kwangu niliiona ni zaidi ya bahati na nikaendelea kujilaumu kwa kuchelewa kusoma alama za nyakati. Tuliendelea kusakata kabumbu kwa zaidi ya dakika ishirini, Raya akijitutumua kadiri ya uwezo wake ili asionekane mgeni kabisa kwenye sanaa hiyo ya kikubwa.
Mpaka kipyenga kinalia kuashiria kumalizika kwa mpambano huo, dimba lote lilikuwa halitamaniki, ungeweza kufananisha na machinjio ya Vingunguti au ya Pugu.
“Ahsante, ahsante sana Jamal, hatimaye ndoto zangu za muda mrefu zimetimia, umenifanya nijione mwanamke niliyekamilika!” alisema Raya kwa sauti iliyokuwa inasikika kama ya mtoto mchanga, machozi yakiulowanisha uso wake. Akawa ananibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu.
Kwa kuwa dimba lilishachafuka, ilibidi turudi tena bafuni, tukarudia tena kuogeshana, safari hii kwa hisia kali kuliko mwanzo kisha tukarudi kwenye chumba cha wageni ambacho kimsingi ndiyo nilichotakiwa kulala. Raya akaniganda kama ruba na hatimaye, tukajikuta tukiingia tena dimbani kwa ngwe ya lala salama. Kipyenga kilipolia kuashria kumalizika kwa dakika tisini, tulipitiwa na usingizi wa pono.
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kuzinduka, alfajiri ya siku ya pili ambapo kilichonizindua, ilikuwa ni mlio wa simu yangu iliyokuwa inaita mfululizo. Kwa taabu niliichukua simu na kutazama namba ya mpigaji. Moyo ukanilipuka baada ya kugundua kuwa alikuwa ni Shenaiza.
Nilimtazama Raya aliyekuwa bado amelala juu ya kifua changu, nikajiuliza mara mbilimbili kama nipokee au la. Mpaka simu inakata, sikuwa nimeamua nini cha kufanya, ikaanza tena kuita mfululizo ambapo nililazimika kuipokea, sauti ya Samantha ikasikika upande wa pili, ikinipa taarifa ambazo zilinishtua mno.
“Unasemaaa?” nilijikuta nikiuliza kwa sauti ya juu, iliyomzindua Raya usingizini.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 16.


ILIPOISHIA:
Simulizi za Majonzi: Nilimtazama Raya aliyekuwa bado amelala juu ya kifua changu, nikajiuliza mara mbilimbili kama nipokee au la. Mpaka simu inakata, sikuwa nimeamua nini cha kufanya, ikaanza tena kuita mfululizo ambapo nililazimika kuipokea, sauti ya Shenaiza ikasikika upande wa pili, ikinipa taarifa ambazo zilinishtua mno.
“Unasemaaa?” nilijikuta nikiuliza kwa sauti ya juu, iliyomzindua Raya usingizini.
SASA ENDELEA…
Wamekuja tena hapa hospitalini wanataka kuniua na wametishia kwamba wanahisi na wewe unahusika kwenye hiki kinachoendelea kwa hiyo wameapa kufanya kila kinachowezekana kuhakikisha wanatupoteza wote wawili.
“Lakini Shenaiza, hivi ingekuwa wewe ndiyo upo kwenye nafasi yangu ungejisikiaje? Yaani unajikuta tu upo katikati ya mambo ya hatari, maisha yako yanawindwa usiku kucha lakini hata huelewi chanzo ni nini, ungejisikiaje?”
“Ningejisikia vibaya Jamal lakini si nilishakwambia nitakueleza kila kitu? Wala huna haja ya kuwa na haraka wala kukasirika.”
“Utaniambia lini? Unajua kilichonitokea nilipoondoka hapo hospitalini? Bado kidogo ningekufa leo, kibaya ni kwamba sijui hasa kinachoendelea, sijui chochote kuhusu wewe wala matatizo yako ambayo sasa yameshakuwa yangu pia.”
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Huu sio muda wa kulaumiana Jamal, nakuomba kama ulivyofanya mara ya kwanza, njoo unitoroshe tena hospitali na nakuahidi safari hii tukitoka tu, nitakueleza ukweli wa kila kitu.”
“Hapana! Siwezi Shenaiza, tafuta mtu mwingine wa kuifanya kazi hiyo, sipo tayari.”
“Jamani Jamal, kwa hiyo upo tayari kuona nakufa wakati uwezo wa kunisaidia unao? Tena asubuhi hii ndiyo muda mzuri, watu wakija kuwaletea wagonjwa chai na sisi tunatumia muda huohuo kutoroka, nipo chini ya miguu yako,” alisema Shenaiza kwa sauti iliyoonesha alikuwa akilengwalengwa na machozi.
Nilishindwa cha kumjibu, nikamuona Raya naye ambaye bado alionesha kuwa na usingizi, akijigeuza pale kitandani na kunikumbatia tena ikiwa ni ishara kwamba hakufurahishwa na kitendo cha mimi kuzungumza na Shenaiza alfajiri ile.
“Ok, basi sawa nitajua cha kufanya,” nilijibu harakaharaka kisha nikakata simu. Nililazimika kumkatisha kwa sababu sikutaka kuendelea kumkasirisha Raya.
“Good morning baby!” (Habari za asubuhi mpenzi) alisema Raya huku akijinyoosha mwili kwa uchovu, akanibusu mdomoni na kunikumbatia tena.
“Ulikuwa unaongea na nani kwenye simu?” aliniuliza swali ambalo nilijua kwamba majibu yake anayo ila anataka kunitega.
“Si huyu Shenaiza, asubuhi yote hii anaanza kuleta matatizo mengine!”
“Mh! Anasemaje tena?”
“Ananiambia kuwa wale watu wanaotaka kumuua, wameanza kunitafuta na mimi na wamemuapia kuwa ni lazima watufanye kitu kibaya, mimi na yeye.”
“Ooh! Mungu wangu, nakuomba Jamal uachane na huyo msichana, achana kabisa na mambo yake, kama ni matatizo ni yake wala wewe hayakuhusu, isitoshe mtu mwenyewe ndiyo kwanza mmejuana, achana naye nakuomba,” alisema Raya kwa hisia za hali ya juu.
Japokuwa alikuwa na hoja kwa alichokuwa anakizungumza, akili zangu zilikuwa ni kama zimezingirwa na ukungu, nikawa sielewi nataka nini maishani mwangu. Niliona kama matatizo yaliyokuwa yanamkabili Shenaiza, yalikuwa yananihusu sana na ni mimi pekee ndiye niliyekuwa na uwezo wa kumsaidia.
Japokuwa kuna wakati mwingine nilikuwa nikiona kama nabebeshwa mzigo nisioustahili, bado niliona ninayo nafasi ya kumsaidia. Ilibidi niamke na kuelekea bafuni, Raya naye akaamka na kunifuata, tukaoga pamoja huku Raya akionesha kufurahishwa mno na ukaribu wangu.
Tulirudi chumbani ambapo wakati mimi nikijiandaa, Raya alienda jikoni kuandaa kifungua kinywa. Nilipomaliza kujiandaa, tayari kifungua kinywa kilikuwa tayari, Raya akiwa ndani ya khanga moja tu, akanikaribisha mezani.
Mwenyewe alitamani asubuhi hiyo tuendelee kukaa kimahaba kama ilivyokuwa usiku lakini akili zangu zilikuwa zikienda mbio sana, nikapata kifungua kinywa harakaharaka kisha nikamuaga.
Haikuwa rahisi kwake kuniruhusu, ikabidi nimdanganye kwamba nitarudi muda mfupi baadaye na sitatoka tena siku hiyo mpaka usiku. Ilibidi aniruhusu kwa shingo upande lakini akanitaka kuwa makini sana kwa kila kitu nitakachokuwa nakifanya.
Tulikumbatiana, nikambusu kwenye paji la uso wake kisha nikatoka, hatua kadhaa mbele niligeuka na kumtazama, nikamuona machozi yakimlengalenga, sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea na safari yangu.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilitoka na kwenda moja kwa moja mpaka hospitalini alikokuwa amelazwa Shenaiza, bado ilikuwa ni mapema sana na ndugu, jamaa na marafiki wa wagonjwa wengi walikuwa wakiwapelekea vifungua kinywa.
Ilibidi na mimi niingie kwenye mgahawa mmoja ulikuwa nje ya hospitali na kuchukua kifungua kinywa kwa ajili ya Shenaiza. Nilifanya hivyo ili isiwe rahisi kwa walinzi na madaktari kunihisi vibaya. Saa kumi na mbili kamili nilikuwa nikiingia kwenye mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa Shenaiza.
Niliingia kimyakimya bila kuonekana na mtu yeyote mpaka pembeni ya kitanda cha Shenaiza, nikamuinamia na kumsemesha kwa sauti ya chini.
“Shenaiza! Shenaiza!”
“Ooh! Jamal, ahsante kwa kuja mpenzi wangu,” alisema Shenaiza ambaye kwa ilivyoonesha, hakuwa amelala bali aligeukia ukutani tu, akanikumbatia na kunibusu kwa hisia nzito huku akionesha mwili wake kuwa kwenye maumivu makali.
“Ni wewe pekee ndiye unayeweza kunisaidia kwa sababu hata polisi nao naona wanasuasua tu, najua nakubebesha mzigo mzito lakini nakuhakikishia wema wako hautapita bure, usichoke kunisaidia,” alisema Shenaiza kwa sauti ya chini akijaribu kujikakamua na kuinuka pale kitandani.
Nilimsaidia kufanya hivyo, akakaa juu ya kitanda na kuanza kuangaza macho huku na kule.
“Huu ndiyo muda mzuri, inabidi tuondoke kabla hawa mashetani hawajafika,” alisema Shenaiza, nikawa naitika kila kitu alichokuwa ananiambia. Japokuwa nilikuwa najua kwamba ninachokifanya ni kosa jingine kubwa, nilijikuta nikiwa sina cha kufanya zaidi ya kutii kile Shenaiza alichokuwa anakitaka.
Tukatoka mpaka nje ya hospitali hiyo bila kugunduliwa na mtu yeyote, sikutaka kufanya makosa kama yale niliyoyafanya siku ile nilipomtorosha Shenaiza kule Amana, tukaenda mpaka kwenye kituo cha daladala na kupanda iliyokuwa inaelekea Makumbusho.
Ili kuzidi kupoteza ushahidi, nilimwambia Shenaiza ajifunike khanga yake, na mimi nikavaa kofia kubwa ya pama, tukatulia kwenye siti ya watu wawili. Abiria wengine waliendelea kuingia na baada ya gari kujaa, safari ilianza huku moyoni nikisali kusitokee jambo lolote baya.
“Sidhani kama tutafika salama huko tunakokwenda, moyo wangu unasita sana,” alisema Shenaiza kwa sauti ya kutetemeka. Sijui alikumbwa na nini mpaka aanze kuzungumza maneno yake, nikawa nampa moyo kwamba asiogope chochote.
Safari iliendelea mpaka tuklipofika Magomeni ambako kulikuwa na foleni kubwa sana asubuhi hiyo, jambo ambalo halikuwa la kawaida.
“Nimekwambia kwamba sijui kama tutafika salama, umewahi kuona asubuhi namna hii kunakuwa na foleni kama hii?” alisema Shenaiza huku akizidi kuonesha hofu kubwa ndani ya moyo wake, nikawa nazidi kumtuliza.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 17.


ILIPOISHIA:
Safari iliendelea mpaka tulipofika Magomeni ambako kulikuwa na foleni kubwa sana asubuhi hiyo, jambo ambalo halikuwa la kawaida.
“Nimekwambia kwamba sijui kama tutafika salama, umewahi kuona asubuhi namna hii kunakuwa na foleni kama hii?” alisema Shenaiza huku akizidi kuonesha hofu kubwa ndani ya moyo wake, nikawa nazidi kumtuliza.
SASA ENDELEA…
Tulikaa kwenye foleni kwa zaidi ya dakika ishirini, magari yakiwa hayaendi mbele wala hayarudi nyuma. Nilitegemea kwamba muda mfupi baadaye askari wa usalama barabarani (trafiki) watafika na kusaidia kuondoa foleni hiyo lakini haikuwa hivyo.
Madereva wengine walipochoka, walianza kupiga honi kwa nguvu, huku wengine wakiteremka kwenye magari yao na kusogea upande wa mbele kujaribu kuangalia kilichokuwa kinasababisha foleni hiyo.
“Nasikia kuna ajali huko mbele, hapa hatuwezi kuondoka sasa hivi mpaka trafiki waje, wapime ajali yenyewe, wayatoe magari yaliyopata ajali unafikiri itakuwa sasa hivi?” kondakta wa daladala tuliyopanda, alisema na kutufanya abiria wote tuishiwe nguvu.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Sasa tutafanyaje?”
“Inabidi tushuke tutembee kwa miguu, kule hospitali wakishtukia kwamba nimetoroka wanaweza kuanza kutufuatilia na huenda wakatukamata hapahapa, tuondoke,” alisema Shenaiza huku akisimama kwenye siti aliyokuwa amekaa, na mimi nikasimama, tukamlipa kondakta nauli yake kisha tukashuka.
“Inabidi tutembee mpaka upande wa pili tukachukue Bajaj au bodaboda,” alisema Shenaiza huku akizidi kujitanda ushungi wake ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kumtambua, na mimi nilishusha kofia yangu ya pama, tukawa tunatembea kuelekea kule kwenye Bajaj.
Tukiwa tunatembea katikati ya tuta la barabara lililokuwa linatenganisha barabara mbili za lami, ghafla tulishtushwa na muungurumo mkali wa pikipiki kubwa mbili zilizokuwa zinakuja upande wetu, tukiwa hata hatujui zimetokea wapi.
“Tulijua lazima tutakupata tu, wewe ndiyo unajifanya kimbelembele kuingilia ishu za watu si ndiyo?” alisema mwanaume mmoja kwa sauti ya kukwaruza, wote wakiwa wamesimamisha pikipiki zao kubwa huku na kule na kutufanya mimi na Shenaiza tubaki katikati, hofu kubwa ikanitanda ndani ya moyo wangu.
Cha ajabu zaidi, wakati wakiwa wametuzunguka pale barabarani, foleni ilianza kutembea, magari yakaanza kuondoka huku abiria waliokuwa wameshuka, nao wakiingia kwenye magari na kuendelea na safari.
“Leave him alone, what wrong has he done? (Mwacheni, kwani kuna jambo gani baya amefanya?) Kama mnanitaka mimi nichukueni lakini siyo huyu kijana wa watu,” alisema Shenaiza lakini hakuna aliyemsikiliza, ukichanganya na kelele za magari na vyombo vingine vya usafiri vilivyokuwa vikiondoka baada ya foleni kuanza kutembea, hakuna mtu aliyejua kilichokuwa kinaendelea.
“Siku nyingine hutakiwi kuingilia mambo yasiyokuhusu,” alisema mwanaume mmoja huku akinisogelea, nikawa nazidi kutetemeka kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, wangeweza kunifanya chochote wanachokitaka bila mtu yeyote kujua kilichokuwa kinaendelea.
“Nimesema muacheni?” alisema Shenaiza lakini kabla hata hajamalizia, mmoja kati ya wale wanaume wanne, alimtwanga ngumi nzito ya usoni, akapepesuka na kutaka kudondoka lakini mwingine alimdaka na kumsimamisha.
Hofu niliyoipata ilikuwa haielezeki, kama Shenaiza, mwanamke mrembo kiasi kile alipigwa ngumi nzito kiasi kile, mimi je? Nilijiuliza huku nikizidi kutetemeka, tayari nilishaanza kusikia harufu ya mauti.
Ghafla iliibuka pikipiki nyingine ambayo tofauti na zile nyingine, yenyewe ilikuwa na mtu mmoja tu, tena mwanaume aliyeonesha kuwa na umri mkubwa kuliko wale wengine, akafunua kioo cha kofia ngumu (helmet) aliyokuwa ameivaa, akanitazama kwa ukali, macho yangu yakagongana na yake.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilichokigundua, hakuwa Mtanzania na kwa kiasi kikubwa, alikuwa na sura inayofanana na Shenaiza kwa mbali, jambo lililonifanya niamini kwamba lazima atakuwa na uhusiano wa kindugu na msichana huyo, aliendelea kunitazama bila kuzungumza kitu chochote.
Nikiwa bado naendelea kutetemeka, magari yaliyokuwa kwenye foleni yakiwa yamepungua kabisa na eneo lote kurejewa na hali yake ya utulivu, nilimuona yule mwanaume akiwapa ishara fulani wale watu waliooonesha kuwa ni wafuasi wake, Shenaiza ambaye sasa alikuwa akivuja damu nyingi puani, akabebwa juujuu na kupakizwa kwenye pikipki ya yule mwanaume kisha akaondoka kwa kasi kubwa na kutokomea.
“Hili litakuwa funzo kwako na kwa watu wengine wenye tabia kama yako, usipende kuwasogelea wanawake usiowajua,” alisema mmoja kati ya wale wanaume, nikashtukia nikipigwa na kitu kizito kichwani, nikadondoka mzimamzima kama gunia. Sikuweza hata kupiga kelele za kuomba msaada.
Nikiwa pale chini, kwa taabu nilimuona mwanaume mmoja akichomoa kisu kikubwa na kunikalia, akakinyanyua na kukishindilia upande wa kushoto wa kifua changu bila huruma. Siwezi kuyaelezea maumivu ambayo niliyasikia, nikafumbua mdomo ili kupiga kelele za kuomba msaada lakini sauti haikutoka, nikasikia wale watu wakipongezana kisha wakapanda kwenye pikipiki zao na kuondoka kwa kasi.
Damu nyingi zilikuwa zinanitoka upande wa kushoto wa kifua changu kiasi cha kunifanya nilowe chapachapa. Nilijitahidi kuinuka pale nilipokuwa nimelala huku damu nyingi zikiendelea kunitoka lakini maumivu makali yalinirudisha chini.
Kwa kutumia mikono yangu miwili, nilijaribu kuminya pale kwenye jeraha kubwa ili kuzuia damu isiendelee kunimwagika lakini nilijikuta mikono ikikosa nguvu, kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo nilivyokuwa nazidi kuishiwa nguvu.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Watu wengi walianza kukimbilia pale nilipokuwa nimeanguka na kunizunguka, niliwasikia wengine wakishindwa kuficha hisia zao na kuanza kuangua vilio. Nadhani hali waliyoniona nayo iliwafanya waamini kwamba siwezi kabisa kupona kutokana na damu zilivyokuwa zinaendelea kunimwagika mithili ya bomba lililopasuka.
Nikiwa kwenye maumivu makali, nilijigeuza na kuanza kutazama angani, upeo wa macho yangu ukagota kwenye mawingu meupe na ya bluu yaliyokuwa yakilipendezesha anga, nikabaki nimetulia nikiwa kwenye hali hiyo.
Kelele za watu wengi waliokuwa wanazidi kuongezeka eneo la tukio kunishangaa, zilianza kupungua taratibu masikioni mwangu, zikazidi kupungua na baadaye nikawa nasikia kama watu wananong’ona. Kwa mbali nilisikia mlio wa ving’ora ambavyo hata hivyo sikujua ni vya nini.
Nikiwa naendelea kutazama angani, taswira ndani ya mboni za macho yangu ilianza kufifia taratibu na kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndivyo nayo ilivyozidi kufifia, japokuwa ilikuwa ni asubuhi, kigiza kikaanza kutanda kwenye macho yangu.
Nakumbuka neno la mwisho nililofanikiwa kulisema, ingawa ilikuwa ni kwa taabu kubwa kutokana na midomo yangu kuwa mizito, ilikuwa ni: Mungu nisaidie! Nikafumba macho na giza totoro likatawala kila sehemu, sikuelewa tena kilichoendelea baada ya hapo!
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 18.

ILIPOISHIA:
Nakumbuka neno la mwisho nililofanikiwa kulisema, ingawa ilikuwa ni kwa taabu kubwa kutokana na midomo yangu kuwa mizito, ilikuwa ni: Mungu nisaidie! Nikafumba macho na giza totoro likatawala kila sehemu, sikuelewa tena kilichoendelea baada ya hapo!
SASA ENDELEA…
Katika hali ambayo sikuitegemea na ambayo mpaka leo huwa siwezi kuifafanua, muda mfupi baadaye nilijikuta nikizinduka lakini nikiwa kwenye hali ya tofauti kabisa. Nilizinduka nikiwa palepale nilipokuwa nimelala awali lakini katika hali ya ajabu, nilikuwa mwepesi sana.
Nikajikuta nikianza kupaa taratibu kuelekea juu. Nikiwa juu kidogo, niligeuka na kutazama pale nilipokuwa nimeangukia, nikashangaa kuona bado mwili wangu ulikuwa umelala palepale, damu nyingi zikiendelea kutoka kwenye jeraha la kifuani, tena safari hii zikitoka kwa mabongemabonge.
“Mungu wangu! Hiki ni kitu gani tena?” nilijikuta nikisema kwa sauti ya chini, ungeweza kudhani nilikuwa kwenye ndoto lakini haikuwa hivyo. Nilijiuliza kama mwili wangu bado ulikuwa pale chini, mimi niliyekuwa napaa nilikuwa ni nani? Sikupata majibu.
Niliendelea kupaa kuelekea juu mpaka nikafikia umbali wa mita kadhaa, ulioniwezesha kuona vizuri kila kitu kilichokuwa kinaendelea eneo la tukio. Niliwaona watu wakizidi kumiminika kwa wingi eneo la tukio, wengine wakishika vichwa vyao baada ya kuuona mwili wangu ukiwa kwenye hali ile.
Hali hiyo ya ajabu iliendelea kunitokea, nakumbuka niliendelea kushuhudia kila kitu kilichoendelea, jinsi mwili wangu ulivyochukuliwa kutoka eneo la tukio na kukimbizwa mpaka hospitali ambako nako niliona madaktari walivyokuwa wakichakarika kuokoa maisha yangu.
Niendelee kusisitiza kwamba wakati haya yote yakitokea, katika ulimwengu wa kawaida sikuwa na fahamu hata kidogo, nilikuwa nimefumba macho na kulala pale kitandani kama maiti, nikiwa nimeunganishwa na mashine ya kunisaidia kupumua lakini katika ulimwengu mwingine ambao hata sijui niuiteje, nilikuwa nimesimama kwenye pembe moja ya ile wodi, nikishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Kazi ya kuokoa maisha yangu iliendelea, madaktari na manesi wakawa wanapishana huku na kule, huyu kabeba dawa, huyu kabeba chupa ya damu, huyu mikasi na sindano, ilimradi kila mmoja alikuwa bize.
Nilijisikia ahueni kubwa ndani ya moyo wangu kuona watu ambao pengine hata hawakuwa wakinijua, wakipigana kuokoa maisha yangu. Niliendelea kuwatazama wanavyohangaika, kuna wakati machozi ya uchungu yalikuwa yakinitoka kwa sababu ya kilichotokea, nikawa naendelea kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
Narudia tena, mpaka leo huwa napata sana ugumu kuelezea hasa kile kilichotokea ni nini, yaani mimi niliyekuwa nashuhudia hayo yote nilikuwa nani na ule mwili ambao watu wote walikuwa wakiamini kwamba ni mimi, ulikuwa kitu gani?
Jambo pekee ninaloweza kusema, ni kwamba kila jambo linatokea maishani linatokea kwa sababu maalum na kuna mambo mengi sana yanayoendelea kutokea hapa duniani ambayo mimi na wewe hatuyajui. Huenda mimi nilitokewa na haya ili leo nije kutoa ushuhuda kwa watu ambao huwa ni wagumu kuamini kwamba kuna maisha mengine zaidi ya haya tunayoyajua.
Maisha haya ya kawaida ya binadamu tulio wengi, yamejawa na mambo mengi sana ambayo kwa akili za kawaida huwezi kuyaelewa na nilichojifunza ni kwamba mambo mengi humu duniani, hayapo kama ambavyo tumezoea kufikiria yapo. Kwamba hakuna jambo ambalo linatokea kwa bahati mbaya! Hata hizi ajali ambazo wengi huwa tunaona kwamba zimetokea kwa bahati mbaya, huwa hazitokei tu!
Waingereza wana msemo mmoja maarufu kwamba ‘everything is predestined’ wakimaanisha kila kinachotokea maishani tayari kilishapangwa! Nasisitiza hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya.
Yawezekana hata wewe usinielewe kwa sasa lakini napenda kukuhakikishia kwamba mambo mengi sana ambayo tunayajua na kuyaamini, hayapo vile ambavyo kwa miaka mingi tumekuwa tukiyaamini. Nikisema dunia nzima imejaa vitu vingi ambavyo havipo kama tulivyozoea kuviona, huenda ukawa hunielewi kwa urahisi lakini mimi nasimulia mambo ambayo yamenitokea mwenyewe.
Ukitaka kuamini, kuanzia sasa, anza kutazama kila kitu kwa jicho la tatu! Hata lile jambo ambalo ulikuwa unaamini kwamba unalijua au ulikuwa unaamini kwamba ni ukweli, hebu anza kulitazama kwa namna nyingine na jiulize maswali katika kila jambo, kuanzia kuhusu wewe mwenyewe, kwamba wewe ni nani, kwa nini upo duniani, umetoka wapi na unaelekea wapi na mambo yote yanayokuzunguka, utaanza kuelewa ninachokimaanisha.
Basi nikiwa nimesimama palepale kwenye pembe moja ya ile wodi, nikishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea kwenye mwili wangu uliokuwa umelazwa pale kitandani ukiwa hauna fahamu hata kidogo, nilishtuka baada ya kuhisi upepo mkali ukianza kuvuma mle ndani ya wodi.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Sikuelewa ule upepo umetokea wapi kwa sababu milango na madirisha yote yalikuwa yamefungwa, baadhi ya vifaa vilivyokuwa mezani, vilianza kudodondoka, vikiwemo vichupa vya dawa na vifaa vingine vya kidaktari, manesi wakawa na kazi ya kuviokota na kuviweka sawa.
Ghafla nilihisi kama nashikwa na mtu mwenye nguvu sana, nikanyanyuliwa kutoka pale nilipokuwepo, kufumba na kufumbua, nikajikuta nipo kwenye mazingira mengine tofauti kabisa, mahali ambapo hata sijui nipaelezeeje. Kulikuwa na giza totoro kila upande, kiasi kwamba hata ukisogeza kidole jirani kabisa na jicho lako, usingeweza kuona kitu chochote.
Yule mtu ambaye alikuwa amenishika na kunitoa kule wodini, ambaye nasema ni mtu kwa sababu mikono yake ilikuwa ya kibinadamu kwa sababu na mimi nilimshika nikitaka kumjua ni nani lakini nikashindwa hata kumuona kwa sababu ya giza, aliniachia, nikajikuta nimesimama sehemu ambayo sikujua mbele ni wapi wala nyuma ni wapi, giza lilikuwa nene kikwelikweli.
“Jamal!” nilisikia sauti nzito, iliyokuwa ikisikika kama mwangwi, ikiliita jina langu. Umewahi kuingia kwenye sehemu ambayo ina uwazi mkubwa halafu ukatamka neno lolote na kusikia likijirudiarudia? Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu, ile sauti nzito ilijirudiarudia mara kadhaa.
“Mungu wangu, hiki ni nini tena?” nilijisemea moyoni kwa hofu kubwa lakini tofauti na nilivyotegemea, wakati mimi nikiamini kwamba najisemea moyoni, niliisikia sauti yangu ikisikika utafikiri niliyatamka maneno yale mdomoni wakati ukweli ni kwamba niliyasemea moyoni.
Nikajikuta nikitetemeka kuliko kawaida, hofu kubwa ikiwa imeukumba moyo wangu ambao sasa ulikuwa ukidunda kwa nguvu kiasi cha mapigo yake kusikika vizuri kabisa hata kwa mtu aliyekuwa pembeni yangu.
“Jamal!” ile sauti ilisikika tena lakini tofauti na mwanzo, safari hii ilisikika ikionesha aliyeitoa alikuwa amesogea mbali kabisa na mimi, nikawa natamani kuitikia lakini nilishindwa kutokana na hofu kubwa iliyokuwa imenizingira.
“Jamal!” ile sauti ilisikika tena kwa mara ya tatu, safari hii ikionesha kwamba aliyekuwa akiniita alikuwa mbali zaidi. Katika hali ambayo siwezi kuielezea, nilijikuta nikianza kutembea kuelekea kule sauti ile ilikokuwa inazamia. Kwa mbali nikaanza kusikia sauti kama za watu wanaougulia maumivu makali, sauti za watoto wachanga waliokuwa wakilia na sauti za kutisha za wanyama ambazo nyingine hata sijawahi kuzisikia tangu nizaliwe.
Kuna wakati hofu ilinizidi na kutaka nigeuze nilikotoka lakini kitu ndani ya moyo wangu kikaniambia nizidi kusonga mbele. Kadiri nilivyokuwa nazidi kusonga mbele ndivyo zile sauti zilivyokuwa zinazidi kuongezeka, nikazidi kutetemeka kwa hofu huku nikiwa sijui nini itakuwa hatma yangu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next
 
SEHEMU YA 19.

ILIPOISHIA:
Kuna wakati hofu ilinizidi na kutaka nigeuze nilikotoka lakini kitu ndani ya moyo wangu kikaniambia nizidi kusonga mbele. Kadiri nilivyokuwa nazidi kusonga mbele ndivyo zile sauti zilivyokuwa zinazidi kuongezeka, nikazidi kutetemeka kwa hofu huku nikiwa sijui nini itakuwa hatma yangu.
SASA ENDELEA…
Sauti zilizidi kuongezeka, nikawa nasikia sauti nyingine zikiugulia maumivu makali mno, nilitamani nione nini kilichokuwa kinaendelea lakini sikuweza kutokana na lile giza. Ilifika mahali ikabidi niwe natembea kwa uangalifu sana kwani nilihisi nilikuwa nikipita jirani kabisa na wale watu waliokuwa wakilia kwa maumivu makali.
Kiasili mimi ni mwoga sana kiasi kwamba nikiwa nyumbani kwangu, hata panya akipita darini kwa kasi, lazima nitashtuka sana lakini nashangaa siku hiyo kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo hofu ilivyokuwa inazidi kupungua.
Haikuwa rahisi kupita sehemu ambayo unasikia kabisa wenzako wanalia kwa kusaga meno kwa maumivu makali kama ile. Ukiachilia mbali sauti hizo za watu, kulikuwa pia na sauti za watoto wachanga waliokuwa wamepamba moto kulia, ungeweza kudhani wamelazwa kwenye siafu.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilizidi kutembea kusonga mbele kufuata ile sauti iliyokuwa ikiliita jina langu, zile sauti za watu zikaanza kupungua kidogo kuonesha kwamba tayari nilishapita eneo walilokuwepo, zikawa zinasikika za wale watoto wachanga huku pia sauti za wanyama wakali nazo zikianza kuongezeka.
Nikiwa naendelea kutembea, nilishtukia sauti ya kutisha ya ndege mkubwa ikija kwa kasi pale nilipokuwepo, kufumba na kufumbua nilijikuta nikipigwa kikumbo na ndege yule mkubwa ambaye hata sikuweza kujua ni ndege gani kutokana na jinsi alivyokuwa mkubwa.
Kucha zake kali zikaniparua upande wa shavu langu la kushoto na kunifanya nijihisi maumivu makali sana. Hata hivyo, nilijikaza na kuendelea kusonga mbele. Lile dege ambalo baada ya kunipiga kikumbo lilipotelea mbali, nililisikia likianza kurudi tena, safari hii likipiga kelele kwa sauti kubwa kuliko mwanzo.
Sikumbuki kama katika maisha yangu ya kawaida nimewahi kusikia mlio wa namna hiyo wa ndege. Ilibidi niwe makini lisije kuniumiza tena, nikainua mikono na kujiziba upande wa usoni, likaja kwa kasi na kunipita, nikasikia upepo ukinipuliza kisha likatokomea kule ile sauti iliyokuwa ikiniita ilikokuwa inatokea.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilipojigeuza pale lilipokuwa limeniparua, niligundua kwamba vitu vya majimaji vilikuwa vikinitoka. Niliamini kwamba ni damu kwa sababu binadamu anapoumia, kinachotoka ni damu ingawa kutokana na giza lile, sikuweza kuthibitisha hilo zaidi ya kuendelea kujiaminisha mwenyewe.
Nikiwa nazidi kuelekea kule ile sauti ilikotokea, kwa mbali nilianza kuona kama mwanga hafifu ukionekana mita nyingi kutoka pale nilipokuwa nimefika. Nilishusha pumzi ndefu kwa sababu niliamini mwanga ni dalili ya uhai, nikajua lazima naweza kupata msaada nikifika pale kwani mpaka muda huo, sikuwa naelewa nini itakuwa hatima yangu.
Milio ya wanyama wa kutisha ilizidi kusikika kutoka kila upande lakini sikukata tamaa, nilizidi kusonga mbele huku giza bado likiwa nene vilevile, akili zangu zote zikiwa ni kwenye ule mwanga niliokuwa nauona. Cha ajabu, licha ya kutembea sana, bado ule mwanga uliendelea kuonekana ukiwa umbali uleule, jambo ambalo lilinishangaza sana.
Nilijaribu kuongeza urefu wa hatua lakini ilikuwa sawa na kazi bure, miungurumo ya wanyama wakali ikawa inazidi kuongezeka huku kwa mbali nikisikia sauti kama za yule ndege mkubwa aliyenijeruhi zikija tena lakini tofauti na awali, safari hii ilionesha kwamba walikuwa zaidi ya mmoja kutokana na ukubwa wa sauti zao.
“Mungu wangu, nimekwisha,” nilijikuta nikijisemea moyoni lakini jambo la ajabu tena, wakati mimi nikiamini maneno hayo niliyasemea moyoni, yalisikika kwa sauti kubwa utafikiri nimezungumza kwa kufumbua mdomo.
“Jamal mbona hufiki? Fanya haraka,” ile sauti iliyoniita ilisikika tena kutokea umbali ambao siwezi kuukadiria, nikataka nifumbue mdomo na kumuuliza yule mtu aliyekuwa ananiita ni nani, pale ni wapi na nilipelekwa pale kufanya nini lakini nilipofumbua mdomo, nilishangaa sauti ikiwa haitoki.
“Leo ndiyo mwisho wa maisha yangu,” nilijisemea moyoni baada ya kuona nimeshindwa kuwasiliana na yule mtu lakini cha ajabu tena, sauti ilisikika kwa nguvu. Nilishangaa sana, yaani nikifumbua mdomo na kuzungumza, sauti haisikiki lakini nikizungumza kimoyomoyo ndiyo sauti inasikika, nilibaki nimepigwa na butwaa.
Niliamua kujaribu kitu, kuzungumza kimoyomoyo kumuuliza yule mtu yale niliyotaka kumuuliza. Cha ajabu sasa, sauti yangu ndiyo ilisikika kwa nguvu na naamini yule mtu aliyekuwa ananipa maelekezo alinisikia.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Wewe ni nani? Hapa ni wapi na kwa nini nimeletwa huku?”
“Mh! Hutakiwi kuuliza swali lolote,” ilisikika sauti ile kwa mwangwi mkubwa kama ilivyokuwa mwanzo.
“Mbona natembea lakini sifiki?” nilijisemea tena moyoni lakini sauti ikasikika vizuri kabisa.
“Geuka ulikotoka,” ilisikika ile sauti, safari hii milio ya wale ndege wakubwa ilikuwa imekaribia kabisa na kwa jinsi walivyokuwa wanakuja kwa kasi, nilijua lazima watanijeruhi tena.
Nilijaribu kugeuka kwa kutumia upande wa kulia lakini nikashangaa mwili wangu ukiwa mzito mno, nikajaribu upande wa kushoto, nikageuka bila tatizo lolote, nikawa natazama kule nilikotokea ambako nako kulikuwa na giza totoro kama kule nilikokuwa naelekea, tofauti yake ni kwamba huku nilikogeukia hakukuwa na mwanga unaoonekana kwa mbali.
“Haya tembea kinyumenyume,” ilisikika ile sauti, kweli nilipojaribu kupiga hatua moja tu, nilijikuta mwili ukiwa mwepesi sana, nikawa naenda bila kikwazo chochote, huku nyuma sauti za wale ndege zikawa zinazidi kufifia. Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa nimefika pale ule mwanga ulipokuwa unatokea, niliisikia ile sauti ikiniamuru kugeuka, nikafanya hivyo, macho yangu yakatua kwenye jiwe la ukubwa wa wastani lililokuwa likiwaka bila kuteketea.
Nilishangaa sana kuona jiwe likiwaka, tena moto mkali unaoweza hata kuchemsha maji ndani ya muda mfupi. Hata hivyo, licha ya kwamba jiwe hilo lilikuwa likiwaka, mwanga wake haukuweza kunisaidia kuona chochote, nikawa naangaza macho huku na kule nikitarajia naweza kumuona yule mtu aliyekuwa ananipa maelekezo lakini haikuwa hivyo.
Kufumba na kufumbua, lile jiwe lilianza kutetemeka kama kuna tetemeko la ardhi kisha likaanza kubingirika kuelekea upande wa kushoto kutoka pale lilipokuwepo. Nilishtuka mno, nikawa natetemeka kwa hofu kubwa. Likaendelea kubingirika kwa kasi huku ikionesha kwamba kule lilikokuwa likiendelea kulikuwa na mteremko.
Sijui akili gani ilinituma kuanza kulifuata lile jiwe kwani hakika huo haukuwa uamuzi sahihi. Nilipopiga tu hatua moja, nilijikuta nikianza kuserereka kuelekea kule lile jiwe lilikokuwa linaelekea.
Nilijaribu kufunga breki lakini ilikuwa sawa na kazi bure, niliendelea kuserereka na kila nilipojaribu kujishikiza sehemu, sikuona chochote cha kunisapoti, ikafika mahali na mimi nikawa nabingirika kulifuata lile jiwe huku mteremko ukizidi kuwa mkali kadiri nilivyokuwa nasonga mbele.
Kwa mbali nilianza kuhisi joto kali huku lile giza nene likianza kupungua na kumezwa na mwanga mwekundu ambao hata bila kuuliza, nilijua kuwa ni wa moto mkubwa uliokuwa unawaka. Zile sauti za watu waliokuwa wakilia kwa maumivu makali, nilianza kuzisikia tena lakini tofauti na awali, safari hii zilikuwa kubwa zaidi huku ikionesha kwamba zilikuwa zikitoka kwa kundi kubwa la watu.
Nilizidi kuserereka kwa kasi kubwa kuelekea kule chini huku joto nalo likizidi kuongezeka. Nikiwa mdogo nimewahi kusikia kwamba Jehanum kuna moto mkali unaowaka muda wote, ambao ni maalum kwa ajili ya kuwateketeza watu wanaofanya dhambi duniani.
*Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilianza kuhisi kwamba huenda kule nilikokuwa nikisererekea ni kwenye moto wa Jehanum na zile sauti za watu waliokuwa wakilia kwa kusaga meno walikuwa ni watu wenye dhambi, nikajikuta nikitetemeka kuliko kawaida.
Mpaka muda huo nilikuwa nimeshindwa kabisa kujizuia nisiendelee kuporomokea kule chini, kwa mbali nikaanza kuliona shimo kubwa ambalo ukubwa wake hata sijui nifananishe na nini lakini kwa kifupi lilikuwa kubwa mno, lisilo na mwisho, moto mkali ukiwa unawaka ndani yake. Kibaya zaidi, na mimi nilikuwa nikiendelea kuporomoka kuelekea ndani ya shimo hilo, nikajua huo ndiyo mwisho wangu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next
 
SEHEMU YA 20.


ILIPOSHIA:
Mpaka muda huo nilikuwa nimeshindwa kabisa kujizuia nisiendelee kuporomokea kule chini, kwa mbali nikaanza kuliona shimo kubwa ambalo ukubwa wake hata sijui nifananishe na nini lakini kwa kifupi lilikuwa kubwa mno, lisilo na mwisho, moto mkali ukiwa unawaka ndani yake. Kibaya zaidi, na mimi nilikuwa nikiendelea kuporomoka kuelekea ndani ya shimo hilo, nikajua huo ndiyo mwisho wangu.
SASA ENDELEA...
“Jamal! Jamal! Don’t go my love, come back to me! Come back Jamal,” (Jamal! Jamal! Usiende mpenzi wangu, rudi kwangu! Rudi kwangu Jamal) wakati nikiendelea kuporomokea kule kwenye lile shimo kubwa lililokuwa na moto mkali ambao siwezi kuuelezea, nilisikia sauti ikiniita.
Tofauti na sauti za kutishatisha nilizokuwa nikizisikia, hii ilionesha dhahiri kwamba siyo ngeni masikioni mwangu. Ilikuwa ni sauti ambayo niliitambua kuwa ni ya Raya, msichana aliyetokea kunipenda kwa moyo wake wote.
Raya alikuwa akipaza sauti huku akilia, maneno aliyokuwa akiniambia yalinichoma sana moyoni mwangu.
Katika hali ambayo sijui niielezeeje, nilijikuta nikipata nguvu kubwa kutoka ndani, nikajipindua kwa nguvu na kujikuta ile kasi ya kuporomokea kule chini inapungua, nikazidi kufurukuta kupambana na ile nguvu kubwa iliyokuwa inanivuta na hatimaye nikajikuta nikiangukia sehemu nyingine tofauti kabisa na kule nilikokuwa nikielekea.
Pale nilipoangukia, palikuwa na unyevunyevu mkubwa chini utafikiri nimekanyaga matope lakini giza lilikuwa nene pengine hata kule nilikotoka, nikawa naangaza macho huku na kule lakini sikuweza kuona chochote. Ukimya wa ajabu ukatanda kiasi cha kunifanya nianze kuyasikia mapigo ya moyo wangu yalivyokuwa yakinidunda.
Kufumba na kufumbua, nilijikuta nimerudi pale nilipokuwepo mwanzoni kabisa, kwenye kona ya ile wodi niliyolazwa. Kama ilivyokuwa mwanzo, nilikuwa nauona mwili wangu ukiwa umelazwa pale kitandani lakini tofauti na awali, safari hii nilikuta ubize mle ndani ya wodi ukiwa umeongezeka sana.
Madaktari walikuwa wakipigana vikumbo, kila nesi alikuwa bize kuhakikisha anaokoa maisha yangu. Sikuelewa nini kimetokea mpaka ubize uongezeke kiasi kile lakini niliwasikia baadhi ya madaktari wakijadiliana kwamba kilichonitokea kilikuwa kitu adimu sana.
“His heartbeats almost stopped but now they are stabilizing, ooh my God he was dead!” (Mapigo ya moyo wake yalisimama kabisa lakini sasa naona yameanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida, ooh Mungu wangu, alikuwa tayari amekufa).
“It’s my eleventh year in this career and I have never witnessed something like this,” (Huu ni mwaka wangu wa kumi na moja nafanya kazi hii, sijawahi kushuhudia tukio kama hili) alisema daktari mmoja, kila mtu akawa anaendelea kuzungumza lake.
Bado niliendelea kujiuliza maswali mengi bila majibu lakini kwa jinsi mazungumzo hayo yalivyokuwa yakiendelea, inaonesha nilikuwa nimetokewa na jambo baya sana. Nikiwa bado palepale kwenye kona ya ile wodi, nikiangalia kila kilichokuwa kinaendelea mle ndani, niliisikia tena ile sauti niliyoisikia muda mfupi uliopita, tena ikizungumza maneno yaleyale.
“Jamal! Jamal! Don’t go my love, come back to me! Come back Jamal,” (Jamal! Jamal! Usiende mpenzi wangu, rudi kwangu! Rudi kwangu Jamal).
Ilikuwa ni sauti ya Raya na ilionesha ikitokea nje ya ile wodi. Nilijikuta nikiwa na shauku ya kutaka kumuona Raya, ile kuwaza tu kwamba nataka kumuona, nilijikuta tayari namtazama lakini katika mazingira ambayo yalionesha kwamba yeye pamoja na watu wengine wote waliokuwa wamemzunguka, hawakuwa na taarifa juu ya uwepo wangu mahali pale.
“Jamal is dead! (Jamal amekufa) Nitakuwa mgeni wa nani mimii? Eeeh Mungu, kwa nini mimi? Why?”
“Raya ukilia sana unakufuru. Wewe unajua jinsi Jamal alivyo rafiki yangu kipenzi lakini mwenzio bado sitaki kuamini kama ni kweli ametangulia mbele za haki. Hebu jikaze, tunaweza kuwa tunamchulia akafa kweli.”
“Usinipe moyo Justice, wote tumeshuhudia mashine ya kusoma mapigo yake ya moyo ikishuka mpaka mwisho kuonesha kwamba mapigo yake ya moyo yamesimama, madaktari wamefanya kila kitu na kujiridhisha kwamba amekufa, ina maana huamini tu?”
“Angekuwa ameshakufa angezungushiwa shuka la kijani pale kitandani kwake na madaktari wote ungeona wameshatoka chumba cha wagonjwa mahututi, mimi naamini bado yupo hai,” Justice na Raya walikuwa wakizungumza pale nje, Raya akilia kwa uchungu huku wafanyakazi wenzao kadhaa pamoja na watu wengine, wakisaidiana kumtuliza msichana huyo.
Pembeni kulikuwa na kundi lingine la watu ambao siwafahamu vizuri, lakini nao walionesha kufika pale kwa sababu yangu, muda mwingi wakawa wanajadiliana huku wakiwatazama akina Raya.
Niliwaona pia waandishi wawili wa habari, mmoja nadhani alikuwa anatoka kwenye kituo cha runinga na mwingine wa magazeti. Niliwatambua hivyo kutokana na jinsi walivyokuwa wamevaa na zana za kazi ambazo kila mmoja alikuwa amebeba. Nilijaribu kuangaza huku na kule kuangalia kama nitamuona Shenaiza lakini hakuwepo eneo hilo.
Nilitamani sana kujua ukweli wa mambo yote ambayo Shenaiza alikuwa akinificha lakini sikujua nitaanzia wapi. Yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha matatizo yote yaliyonitokea lakini cha ajabu ni kwamba hata mimi, muathirika namba moja wa mambo yote yale yaliyokuwa yakiendelea kutokea, nilikuwa sielewi hasa nini kilichojificha nyuma ya pazia.
Kwa tafsiri nyepesi nyepesi, kama Mungu angeamua kunichukua moja kwa moja, ningeacha maswali mengi sana ambayo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuyajibu, zaidi ya Shenaiza mwenyewe. Hali ilikuwa ya simanzi kubwa pale nje ya hospitali, niliwaona watu wengine wakizungumza na simu, kila mmoja akilitaja jina langu.
Maneno mengi yalikuwa yakiendelea kumtoka Raya, akiendelea kulia kwa uchungu kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru. Kwa juujuu tu, kupitia maelezo yake pamoja na yale niliyoyasikia kule ndani kwa madaktari, nilielewa kilichokuwa kimetokea.
Ilionesha kwamba, kuna muda mapigo ya moyo wangu yalisimama, kwa tafsiri nyepesi, kuna muda nilikufa! Lilikuwa ni jambo la ajabu ambalo lilinitisha sana. Sikuelewa ni muda gani nilikuwa nimekufa kwa sababu muda wote nilikuwa timamu na nilikuwa naelewa kila kilichokuwa kinaendelea.
Sikukumbuka muda ambao pengine nilipoteza fahamu au sikuwa naelewa kinachoendelea! Nasisitiza tena, muda wote nilikuwa na akili zangu timamu. Nilijisikia uchungu sana kwa jinsi Raya alivyokuwa akilia, ukichanganya na hofu kubwa niliyokuwa nayo, nilijikuta nikianza kutokwa na machozi. Ajabu ni kwamba, wakati mimi nikiendelea kulia, wale madaktari pale kitandani walishtuka baada ya kuona mwili wangu nao ukitokwa na machozi, wakawa wanatazamana. Nikiwa naendelea kulia, nilipaliwa na mate, hali iliyofanya nikohoe mfululizo, ajabu zaidi, na ule mwili wangu pale kitandani ukakohoa, madaktari wakazidi kupigwa na butwaa, wakawa wanatazamana wakiwa ni kama hawaamini kilichokuwa kinatokea.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Back
Top Bottom