Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

Malizia jmn mpka naogopa, hivi ni ya kweli au??
Angalia sehemu ya 23 kuna maandishi yameandikwa Simulizi za Majonzi kwa maandishi ya blue. Click hapo itakupeleka kwenye page ya hiyo story.
Kazi kwako
 
SEHEMU YA 01:

Damu nyingi zilikuwa zinanitoka upande wa kushoto wa kifua changu kiasi cha kunifanya nilowe chapachapa. Nilijitahidi kuinuka pale nilipokuwa nimelala huku damu nyingi zikiendelea kunitoka lakini maumivu makali yalinirudisha chini.
Kwa kutumia mikono yangu miwili, nilijaribu kuminya pale kwenye jeraha kubwa ili kuzuia damu isiendelee kunimwagika lakini nilijikuta mikono ikikosa nguvu, kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo nilivyokuwa nazidi kuishiwa nguvu.
Watu wengi walianza kukimbilia pale nilipokuwa nimeanguka na kunizunguka, niliwasikia wengine wakishindwa kuficha hisia zao na kuanza kuangua vilio wakilitaja jina langu. Nadhani hali waliyoniona nayo iliwafanya waamini kwamba siwezi kabisa kupona kutokana na damu zilivyokuwa zinaendelea kunimwagika mithili ya bomba lililopasuka.
Nikiwa kwenye maumivu makali, nilijigeuza na kuanza kutazama angani, upeo wa macho yangu ukagota kwenye mawingu meupe na ya bluu yaliyokuwa yakilipendezesha anga, nikabaki nimetulia nikiwa kwenye hali hiyo.
Kelele za watu wengi waliokuwa wanazidi kuongezeka eneo la tukio kunishangaa, zilianza kupungua taratibu masikioni mwangu, zikazidi kupungua na baadaye nikawa nasikia kama watu wananong’ona. Kwa mbali nilisikia mlio wa ving’ora ambavyo hata hivyo sikujua ni vya nini.
Nikiwa naendelea kutazama angani, taswira ndani ya mboni za macho yangu ilianza kufifia taratibu na kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndivyo nayo ilivyozidi kufifia, japokuwa ilikuwa ni mchana, kigiza kikaanza kutanda kwenye macho yangu.
Nakumbuka neno la mwisho nililofanikiwa kulisema, ingawa ilikuwa ni kwa taabu kubwa kutokanana midomo yangu kuwa mizito, ilikuwa ni: Mungu nisaidie! Nikafumba macho na giza totoro likatawala kila sehemu, sikuelewa tena kilichoendelea baada ya hapo!
Katika hali ambayo sikuitegemea na ambayo mpaka leo huwa siwezi kuifafanua, muda mfupi baadaye nilijikuta nikizinduka lakini nikiwa kwenye hali ya tofauti kabisa. Nilizinduka nikiwa palepale nilipokuwa nimelala awali lakini katika hali ya ajabu, nilikuwa mwepesi sana.
Nikajikuta nikianza kupaa taratibu kuelekea juu. Nikiwa juu kidogo, niligeuka na kutazama pale nilipokuwa nimeangukia, nikashangaa kuona bado mwili wangu ulikuwa umelala palepale, damu nyingi zikiendelea kutoka kwenye jeraha la kifuani, tena safari hii zikitoka kwa mabongemabonge.
“Mungu wangu! Hiki ni kitu gani tena?” nilijikuta nikisema kwa sauti ya chini, ungeweza kudhani nilikuwa kwenye ndoto lakini haikuwa hivyo. Nilijiuliza kama mwili wangu bado ulikuwa pale chini, mimi niliyekuwa napaa nilikuwa ni nani?Sikupata majibu.
Niliendelea kupaa kuelekea juu mpaka nikafikia umbali wa mita kadhaa, ulioniwezesha kuona vizuri kila kitu kilichokuwa kinaendelea eneo la tukio. Niliwaona watuwakizidi kumiminika kwa wingi eneo la tukio, wengine wakishika vichwa vyao baada ya kuuona mwili wangu ukiwa kwenye hali ile.
Niliwaona watu kadhaa ambao nilikuwa nikiwafahamu wakiwa na nyuso za huzuni kali, wengine wakiangua vilio kwa nguvu. Nilimuona rafiki yangu na mfanyakazi mwenzangu ambaye muda mfupi kabla ya tukio nilikuwa naye, Justice akiwa analia kwa uchungu mno huku akilitaja jina langu.
Nilimuona pia Raya, msichana ambaye naye tulikuwa tukifanya naye kazi na ambaye alikuwa anapenda sana kuwa karibu na mimi ingawa mara kwa mara nilikuwa nikimkwepa (nitaeleza zaidi kuhusu msichana huyu baadaye), naweza kusema yeye ndiye aliyekuwa na hali mbaya kuliko watu wengine wote kwani alikuwa akilia kwa sauti ya juu huku akilitaja jina langu kiasi cha kusababisha muda mfupi baadaye aanguke na kupoteza fahamu.
Niliwaona pia baadhi ya watu wakiupiga picha mwili wangu kwa kutumia simu zao za mikononi, niliwaona pia waandishi kadhaa wa habari ambao nao walikuwa wakipiga picha nyingi eneo la tukio, za mnato na za video.
Muda mfupi baadaye, walifika askari wanne waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki mbili, maarufu kama tigo ambao niliwaona wakianza kuwarudisha watu nyuma kutoka pale mwili wangu ulipokuwa umelala.
Mmoja wao alisogea jirani kabisa, nikamuona akiuchunguza mwili wangu kisha akaugusa shingoni kama anayesikiliza mapigo ya moyo, nikamuona akiinuka na kuwasogelea wenzake, wakawa wanazungumza jambo ambalo sikuelewa ni nini. Mmoja akatoa simu ya upepo (radio call) na akawa anazungumza na upande wa pili.
Nikiwa bado naendelea kushangaa kwani kila kitu kilikuwa kigeni kwangu, nilianza kusikia ving’ora kwa mbali, nikakumbuka kwamba kabla sijapoteza fahamu kutokana na kutokwa na damu nyingi, nilivisikia tena ving’ora hivyo lakini tofauti yake ni kwamba sasa nilikuwa na uwezo wa kuona kila kilichokuwa kinaendelea.
Lilikuwa ni gari la kubebea wagonjwa (ambulance) ambalo lilikuwa likija kwa kasi eneo lile mwili wangu ulipokuwepo. Nyuma yake lilikuwa limeongozana na difenda ya polisi ambayo niliitambua kwa urahisi kutokana na namba zake za usajili na maandishi yaliyokuwa ubavuni yaliyosomeka ‘Police’.
Wale askari waliokuwepo eneo la tukio waliwatawanya watu upande ule ile ambulance ilikokuwa inatokea, gari likasogea mpaka jirani kabisa na pale mwili wangu ulipokuwepo.
Likasimama ambapo manesi wanne waliovalia nguo nyeupe waliteremka wakiwa na machela, sambamba na askari kadhaa waliokuwa kwenye ile difenda, wote wakasogea na kuuzunguka mwili wangu.
Wakasaidiana kuuinua mwili wangu pale chini na kuulaza kwenye machela kisha wakauingiza kwenye ambulance. Nilimuona Justice naye akipanda. Raya yeye alipakizwa kwenye lile gari la polisi akiwa hajitambui.
Gari likaondoka kwa kasi kubwa likifuatiwa na difenda kwa nyuma, wale askari wa pikipiki waliendelea kuwepo pale eneo la tukio kwa dakika kadhaa wakiwa makini kuwasikiliza watu walichokuwa wanakisema huku wakiwahoji wengine kadhaa.
Kwa muda wote huo, bado nilikuwa najiuliza kilichotokea bila kupata majibu, sikuelewa nipo kwenye hali gani kwa sababu kama ni mwili wangu, tayari ulishapakizwa kwenye ambulance na kukimbizwa hospitali lakini nilishangaa mimi bado nipo eneo lile nikielea angani.
Nilijiuliza ule mwili wangu unapelekwa wapi lakini pia sikupata majibu. Ghafla nilipata wazo la kuifukuzia ile ambulance ili nijue wanaupeleka wapi mwili wangu. Wazo nililoona linafaa, ilikuwa ni kushuka chini na kuchukua bodaboda kwani niliamini kutokana na foleni iliyokuwepo na kasi ya ambulance, ni usafiri huo pekee ndiyo unaoweza kuniwahisha.
Nilishuka jirani kabisa na pale mwili wangu ulipokuwepo muda mfupi uliopita, watu wakawa wameshaanza kutawanyika huku wengine wakijikusanya vikundivikundi pembeni na kujadiliana kuhusu kilichotokea. Nilimsikia mzee mmoja akiwaambia wenzake: “Kwa hali aliyonayo, hawezi kupona, lazima afe.”
Nikashtuka sana kusikia kauli hiyo kwa sababu sikujua wanamzungumzia nani kwamba lazima afe wakati mimi bado nilikuwa hai na nilikuwa nawasikia wanachokisema.
Sikutaka kupoteza muda, harakaharaka nilisogea pembeni ya barabara na kupunga mkono kusimamisha bodaboda, japokuwa dereva alikuwa akija upande wangu, nilishangaa akinipita kama hajaniona. Akaja wa pili naye licha ya kumpungia mkono kwa nguvu hakusimama, akanipita kwa kasi.
Nilijitazama vizuri mwilini kwani nilihisi huenda wanaogopa kusimama kutokana na mwili wangu kulowa damu lakini kituambacho pia nilishindwa kukielewa, shati nililokuwa nimevaa halikuwa na hata tone la damu. Lilikuwa ni shati lilelile ambalo mwili wangu wakati unatolewa eneo lile lilikuwa halitamaniki kwa damu.
Nilishindwa kuelewa ni nini hasa kimetokea, nikajitazama vizuri mwili wangu na kugundua kwamba ulikuwa na hali fulani kama ya kung’aa kusiko kwa kawaida, nilijishika pale kifuani lakini hapakuwa na alama kwamba nilikuwa nimejeruhiwa vibaya, nikazidi kuchanganyikiwa.
Ilibidi nisogee mpaka kwenye maegesho ya bodaboda nikiamini pale itakuwa rahisi kuzungumza na dereva yoyote ili aniwahishe kabla ile ambulance haijapotea kabisa. Nilipopiga hatua moja nilijiona kuwa mwepesi sana halafu tambo lilikuwa refu sana tofauti na kawaida. Sehemu ambayo ningetembea hata hatua ishirini, nilipiga hatua mbili tu, nikawa nimeshafika pale kwenye bodaboda.
Je, nini kitafuatia?
Duh! lete m,wendelezo wake.
 
SEHEMU YA 24:

ILIPOISHIA:
Treni ilizidi kushika kasi, ikafika kipindi nikawa nahisi kwamba haikanyagi kwenye reli bali inapaa angani kwa jinsi ilivyokuwa ikienda kasi. Ghafla, nilipogeuka huku na kule, nilishtuka kugundua kwamba nilikuwa nimebaki peke yangu kwenye treni hilo, sikukumbuka kama kuna sehemu lilisimama, nikawa najiuliza wale abiria wengine wameenda wapi?
SASA ENDELEA…
Kuna wakati nilihisi pengine huenda nilikuwa kwenye ndoto lakini bado sikuwa na uwezo wa kuthibitisha kwamba ile ilikuwa ni ndoto, maisha halisi au kitu gani, kila kitu kilikuwa gizani. Treni lilizidi kushika kasi, moshi mwingi ukiwa unazidi kuingia ndani na kufanya hata ule mwanga hafifu niliokuwa nauona awali nao umezwe na moshi huo mweusi.
Ghafla, nilihisi kama naguswa na mtu pembeni yangu, nikajikuta nikiruka kwa hofu kubwa, nilipogeuka na kumtazama aliyenigusa, alionesha ni mwanamke kwa jinsi alivyokuwa amevaa lakini uso wake alikuwa ameuinamisha chini.
“Jamal! Jamal, ni wewe?” alisema yule mtu kwa sauti ya chini lakini ambayo ilisikika vizuri licha ya kelele ya vyuma vya treni lile, muungurumo mkubwa na upepo uliokuwa unavuma.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Badala ya kuitikia, niligeuka na kumtazama kwa hofu kubwa mno, yeye wala hakugeuka kunitazama zaidi ya kuendelea kujiinamia vilevile, akisubiri majibu kutoka kwangu. Licha ya zile kelele na yeye mwenyewe kuzungumza kwa sauti ya chini, bado niliweza kuitambua vyema sauti hiyo, haikuwa ngeni kabisa masikioni mwangu.
“Mbona hunijibu!” aliuliza tena lakini tofauti na mwanzo, sauti yake ilisikika kwa nguvu ikiambatana na mwangwi ambao uliyaumiza masikio yangu.
“Wewe ni nani?” nilimuuliza lakini nikashangaa sauti haitoki, nikakumbuka sheria za huko ambapo haraka nilifumba mdomo na kuzungumzia moyoni, sauti kubwa ikasikika lakini badala ya kunijibu, nikamuona akiinua uso wake taratibu na kunigeukia.
“Mungu wangu!” nilijisemea kwa hofu kubwa. Kwa msaada wa mwanga hafifu uliokuwepo ndani ya treni hiyo, niliweza kumtambua kwamba yule mtu alikuwa ni Shenaiza lakini tofauti na yule ninayemfahamu, maeneo yake ya kwenye macho yalionesha kutokuwa na macho ya kawaida kama binadamu wengine, yalikuwa meusi tii ambayo hata sijui niyafananishe na nini.
“Ni mimi Shenaiza, au umenisahau? Nataka kukufuata huko uliko, nimechoka maisha ya duniani, nichukue Jamal!” alisema na kuanza kugugumia kwa kilio kilichoonesha kwamba yupo kwenye maumivu makali mno.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea, muda mfupi uliopita nilikuwa nikizungumza naye katika kile mwenyewe alichoeleza kwamba yupo ndotoni na ameniona mimi kama mzimu, lakini muda huo tulikuwa tukizungumza kwa kawaida, akiniambia kwamba anahitaji nimchukue!
Kwanza nilishangaa, nimchukue kumpeleka wapi? Na hapo tulipokuwepo ni wapi? Na yeye alitokea wapi kwa sababu wakati mimi napanda kwenye treni hilo la ajabu, hakuwepo, aliingiaje? Nilijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
“Mbona unanishangaa hivyo Jamal?” aliniuliza huku mkono wake mmoja akinishika shingoni, nikashangazwa na jambo jingine kwamba mwili wake ulikuwa wa baridi kuliko kawaida. Nilitamani kupiga kelele kwa hofu niliyokuwa nayo, nilihisi kama nimekutana na kiumbe wa ajabu mwenye sura ya kibinadamu na sasa alikuwa anataka kuyakatisha maisha yangu.
“Usiniogope Jamal! Hata mimi mwanzo nilikuwa nakuogopa lakini hushangai sikuogopi tena?”
“Kwani hapa ni wapi Shenaiza na wewe umefikaje huku?”
“Mh! Hata mimi sielewi hapa ni wapi lakini nafikiri tunaelekea sehemu nzuuuri ambayo ndiyo itakuwa makazi yetu ya milele, si unajua duniani tunapita tu?”
“Sijakuelewa, kwa hiyo hapa siyo duniani?”
“Siyo duniani Jamal, duniani si kule tulikokuwa tunaishi siku zote? Kwani unaona hapa kunafanana na kule?”
“Sasa kama siyo duniani ni wapi na wewe imekuwaje uje huku?”
“Sijui hapa ni wapi, mimi nimekuja huku kwa sababu nimechoka kuishi, yaani kila siku wananichoma dawa za usingizi, nikiamka tu wananichoma tena, leo nimeamua kujiovadozi kwa makusudi ili nife?”
“Niniii? Shenaiza, unazungumzia nini mbona sikuelewi?”
“Nimeamua kukufuata Jamal, kwa kuwa wewe ulikufa na mimi nikiwa ndiyo chanzo, nimeamua na mimi nife tu.”
“Lakini mimi sijafa Shenaiza, mimi niko hai.”
“Ungekuwa hai ndiyo ungekuwa huku? Acha kujidanganya Jamal!”
“Hapana sijafa! Mimi sijafa! Niko haiii,” nilisema kwa sauti kubwa iliyofuatiwa na kilio.
***
Hali ilikuwa ya patashika nguo kuchanika ndani ya makazi ya siri ndani ya jumba la kifahari la baba yake Shenaiza, lililokuwa Kurasini. Hakuna ambaye alielewa nini kimetokea kwa sababu kama ilivyo kawaida, Shenaiza alizinduka kutoka usingizini baada ya dawa alizokuwa amedungwa awali kuisha nguvu.
Tofauti na awamu zote, safari hii alipozinduka usingizini, alijikokota na kuinuka kutoka kitandani kwake, akasogelea mpaka kwenye kabati lililokuwa ndani ya chumba hicho. Mfanyakazi maalum aliyepewa jukumu la kuhakikisha anapata huduma zote muhimu, alishtuka kumuona akiwa amefungua kabati, ikabidi amuwahi na kumlaza kitandani.
“Nasikia njaa sana, kaniletee chakula,” alisema Shenaiza, harakahara yule mhudumu akatoka kwenda kumletea chakula kwani tayari kilishaandaliwa kwa ajili yake. Alipotoka tu, Shenaiza alisimama na kurudi tena pale kabatini.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Muda mfupi baadaye, alichukua kichupa kidogo pamoja na bomba la sindano, harakaharaka akarudi pale kitandani kwake na kujilaza, akavificha vile vitu chini ya mto. Mhudumu alipoingia akiwa na sinia lililokuwa limejaa vyakula vya kila aina, Shenaiza alitulia kimya kama hajui kinachoendelea.
Yule mhudumu alimuandalia chakula ambapo tofauti na alivyotegemea kwamba atakula kwa sababu alikuwa na njaa kama mwenyewe alivyodai, Shenaiza alishikashika tu kisha akamwambia atoe.
“Mbona sasa hujala?”
“Hamu ya kula imeniisha ghafla, weka nitakula baadaye.”
“Lakini dada, mimi nilikuwa na ushauri mmoja juu yako. Unajua baba anakupenda sana ila anase…”
“Shiii! Ishia hapohapo, we toa vyakula vyako kisha uondoke, sitaki kusikia kitu chochote kwa sasa, niache,” alisema Shenaiza kwa sauti iliyoonesha kutokuwa na masihara hata kidogo.
Yule mhudumu alikusanya vyombo vyake na kutoka nje, akawaacha walinzi wakiwa mlangoni hapo kumlinda Shenaiza kama walivyoelekezwa na baba yake.
Baada ya mhudumu huyo kutoka, harakaharaka Shenaiza alichukua kile kichupa kilichokuwa na maandishi yaliyosomeka Diazepam, akakitingisha na kuchukua bomba la sindano, akavuta dawa nyingi kiasi cha kulifanya bomba lote lijae, akachukua mtandio wake na kujifunga mkononi kwa nguvu, akatafuta mshipa mkubwa wa damu.
Akajichoma na kuanza kuisikumia ile dawa ndani ya mshipa wake wa damu. Hakuweza kuimaliza yote, aliposukuma kiasi cha nusu ya bomba kuingia mwilini mwake, usingizi mzito ulimpitia, akalala huku bomba hilo likiwa bado linaning’inia mkononi.
Yule mhudumu aliporudi kwa mara ya pili kuja kumalizia vyombo vichache vilivyosalia, alishtuka kupita kiasi baada ya kuona damu nyingi ikiwa inatoka kwenye mkono wa Shenaiza na kulowanisha shuka lake huku mwenyewe akitapatapa kama anayetaka kukata roho, mapovu yakimtoka kwa wingi mdomoni na puani.
Harakaharaka, huku akilia, aliwaita walinzi ambao nao walimuita daktari wa familia hiyo, muda mfupi baadaye wote wakawa wamejaa ndani ya chumba hicho wakijaribu kuokoa maisha ya msichana huyo lakini ilionesha kwamba tayari walikuwa wamechelewa.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 25:

Harakaharaka, huku akilia, aliwaita walinzi ambao nao walimuita daktari wa familia hiyo, muda mfupi baadaye wote wakawa wamejaa ndani ya chumba hicho wakijaribu kuokoa maisha ya msichana huyo lakini ilionesha kwamba tayari walikuwa wamechelewa.
SASA ENDELEA…
Shenaiza alikuwa akitapatapa, akirusharusha mikono na miguu, mapovu mengi yaliyochanganyikana na damu yakimtoka mdomoni na puani, harakaharaka Shenaiza alitolewa kwenye chumba alichokuwa amefungiwa na kulazwa juu ya kitanda cha magurudumu, akakimbizwa kwa kasi mpaka nje na kupakizwa kwenye gari.
Muda mfupi baadaye, gari lililombeba lilikuwa tayari lipo barabarani, likikimbia kwa kasi kubwa, taa zote za mbele zikiwa zimewashwa huku yule daktari akiwa bize kuhakikisha anaokoa maisha ya Shenaiza.
Japokuwa baba wa msichana huyo mrembo hakuwepo nchini kwa muda huo, tayari taarifa zilimfikia huko alikokuwa juu ya kilichomtokea binti yake.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Naye akajikuta akichanganyikiwa mno kwani Shenaiza alikuwa mtu muhimu sana kwake. Bila yeye, mambo yake mengi yangekwama, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea. Muda hohuo aliwapigia simu wasaidizi wake na kuwaambia ni lazima wafanye kila kinachowezekana kuhakikisha anapona.
Baada ya kufikishwa hospitalini, harakaharaka Shenaiza alilazwa juu ya kitanda chenye magurudumu, akakimbizwa kupelekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi, madaktari kadhaa, wakisaidiana na yule daktari wa familia, walianza kuhaha kuhakikisha wanaokoa maisha ya msichana huyo.
***
“Lakini mimi sijafa Shenaiza, mimi niko hai.”
“Ungekuwa hai ndiyo ungekuwa huku? Acha kujidanganya Jamal!”
“Hapana sijafa! Mimi sijafa! Niko haiii,” nilisema kwa sauti kubwa iliyofuatiwa na kilio.
“Sasa unalia nini Jamal? Kwani kufa ni jambo la ajabu? Mbona mimi mwenyewe nimeamua kuyakatisha maisha yangu?”
“Hapana, mimi bado nina ndoto zangu nyingi sana sijazitimiza maishani. Isitoshe umri wangu bado mdogo, familia yangu haijafaidi matunda yangu hata kidogo, bado sijaoa wala sina mtoto hata mmoja, itakuwaje nife?”
“Kwani wote wanaokufa wanapenda wenyewe kufa? Usikufuru Jamal, inabidi umshukuru Mungu kwa kila kitu, naamini hakuna kilichoharibika, si utakuwa hapa na mimi?”
“Hapana Shenaiza, hapanaaa!” nilizidi kupingana naye, akazidi kuning’ang’aniza kwamba eti nilikuwa tayari nimekufa na hilo halikuwa tatizo kubwa kwa sababu hata yeye aliamua mwenyewe kufa.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Bado akili yangu ilikuwa na maswali mengi yaliyokosa majibu. Unajua mtihani ambao Mungu ametupa sisi wanadamu, ni kushindwa kuelewa kinachotokea baada ya mtu kufa. Kama angekuwepo mtu hata mmoja, ambaye angekuwa na uwezo wa kuelezea kwa ufasaha kinachotokea baada ya mtu kufa, pengine angewasaidia sana binadamu kupunguza hofu ya kifo inayowatesa.
Kwangu mimi hali ni tofauti, hata sielewi nitumie maneno gani kuelezea kilichotokea lakini naamini kwamba ukiendelea kunifuatilia msomaji wangu, utaelewa ni nini hasa kilichotokea na pengine kitakusaidia na wewe kuweza kuyaelewa maisha na kifo katika upeo mpana zaidi, pengine kuliko ulivyokuwa unafikiria mwanzo.
Bado mjadala mkubwa kati yangu na Shenaiza, ulikuwa ni juu ya suala la kifo. Msichana huyo alikuwa akisisitiza kwamba mimi na yeye tumekufa na ndiyo maana tulikuwa kule lakini mimi nikawa naendelea kumbishia kwamba sijafa kwa sababu bado nilikuwa na akili zangu timamu.
Nilikuwa naelewa vizuri kila kilichokuwa kinaendelea, jambo ambalo bado hakuna ushahidi wa kutosha kwamba wafu huwa wanaelewa kinachoendelea. Nitakuja kulifafanua hili zaidi hapo baadaye.
Basi ile safari ambayo hata sijui mwisho wake ulikuwa ni wapi, iliendelea, treni lilizidi kuchanja mbuga, moshi ukazidi kuongezeka mle ndani sambamba na kelele za vyuma kugongana. Hata hivyo, bado niliweza kumsikia vizuri Shenaiza kwa kila alichokuwa anakizungumza.
Bado nilikuwa na hamu ya kutaka kujua ni nini kilichotokea mpaka na yeye aseme amekufa kwa sababu mpaka muda huo, bado nilikuwa gizani. Nilifumba macho na kujaribu kuvuta picha kwa nguvu, nikashtuka kuliko kawaida kujikuta nimetokezea kwenye wodi nyingine tofauti na ile ambayo mwili wangu ulikuwepo.
Nilipotazama vizuri ndani ya wodi hiyo, kama ilivyokuwa mwanzo kule kwenye ile wodi niliyokuwa nimelazwa, madaktari wengi walikuwa wakihangaika kuokoa maisha ya mtu aliyekuwa amelala juu ya kitanda, akionesha kabisa kwamba alikuwa kwenye hatua za mwisho za uhai wake.
Nilipomtazama vizuri mtu huyo, hakuwa mwingine bali Shenaiza ambaye sekunde chache zilizopita nilikuwa nimekaa naye kwenye siti moja ya treni la ajabu. Ni hapo ndipo nilipoelewa kile alichokuwa anakisema Shenaiza kwamba ameamua kuyakatisha maisha yake.
Madaktari walikuwa wakihangaika mno, Shenaiza akaunganishwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua huku dripu nyingi zikitiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake ya damu.
Kibaya zaidi, kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndivyo mashine maalum ya kusoma mapigo ya moyo aliyokuwa ameunganishiwa msichana huyo na kuunganishwa kwenye kompyuta, ilivyokuwa ikionesha kwamba mapigo yake ya moyo yalikuwa yakishuka kwa kasi kubwa, jambo ambalo lilimaanisha kwamba muda mfupi baadaye, mapigo ya moyo yatasimama kabisa na kukata roho.
“Hapana! Hapana… Shenaiza noooo!” nilipiga kelele kwa sauti kubwa, nikajikuta muda huohuo nimehama kutoka kule hospitalini mpaka ndani ya treni, nikageuka kumtazama Shenaiza, nikamuona akiwa amejikunyata na kujiinamia, kama anayesubiri jambo fulani litokee.
Sijui nilipata wapi nguvu lakini nilijikuta nikimshika Shenaiza na kuanza kumtingisha kwa nguvu, akashtuka kwa nguvu na kunitolea macho akionesha kukasirishwa na kitendo changu cha kumshtua.
Wakati ananitazama, alianza kupiga chafya mfululizo, akili yangu ilihama tena na kurudi wodini, nikapigwa na butwaa baada ya kumuona mgonjwa akipiga chafya mfululizo huku damu ikimtoka puani na mdomoni kwa mabongemabonge!
“She is back into her consciousness! Ooh thanks God! She was almost dead!” (Amerejewa na fahamu zake! Ooh ahsante Mungu, alishafikia hatua ya kufa) nilimsikia daktari mmoja akipaza sauti mle wodini, nikaona nyuso za wote waliokuwemo ndani ya wodi hiyo ya wagonjwa mahututi zikianza kuonesha matumaini makubwa, tofauti kabisa na mwanzo.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Harakaharaka Shenaiza alizungukwa pale kitandani, kazi ya kunusuru maisha yake ikazidi kupamba moto. Nikiwa naendelea kushangaashangaa, nilishtuka nikiguswa begani, akili zangu zikarudi tena kule kwenye treni.
“Kwa nini umeniokoa? Ungeniacha nife,” alisema Shenaiza huku akilia, nikatanua mikono yangu kama ishara ya kumkumbatia, akajilaza kifuani kwangu na kunikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia.
Nikiwa katika hali ileile, nilishtuka muda mfupi baadaye na kujikuta nikiwa nimejikumbatia mwenyewe. Shenaiza hakuwepo tena, nikageuka huku na kule, hakukuwa na mtu mwingine yeyote kwenye lile treni, nilibaki peke yangu huku mwanga wa ile taa iliyokuwa ndani ya behewa nililokaa ukizidi kufifia, muda mfupi baadaye giza nene likatanda kila mahali.
“Jamal! Jamal! Jamal!” nilishtuka baada ya kuisikia tena ile sauti nzito ya kutetemeka, iliyoniita kwa mara ya kwanza kabisa, ikiniita tena, ikafuatiwa na vicheko vya kutisha vya watu wengi, nikawa nageuka huku na kule lakini sikuona chochote zaidi ya giza nene, hofu kubwa ikatanda moyoni mwangu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 26:
ILIPOISHIA:
“Jamal! Jamal! Jamal!” nilishtuka baada ya kuisikia tena ile sauti nzito ya kutetemeka, iliyoniita kwa mara ya kwanza kabisa, ikiniita tena, ikafuatiwa na vicheko vya kutisha vya watu wengi, nikawa nageuka huku na kule lakini sikuona chochote zaidi ya giza nene, hofu kubwa ikatanda moyoni mwangu.
SASA ENDELEA…
“Hujafika hapa kwa bahati mbaya Jamal, ilikuwa ni lazima uje huku ili ufunuliwe haya mambo ambayo kwa akili ya kawaida usingeweza kuyajua, hebu nifuate,” ilisikika ile sauti nzito ya kutetemeka na kutisha, nikiwa sielewi ni nani aliyekuwa akizungumza nami na alikuwa anataka nimfuate wapi, nilishtukia nikishikwa mkono.
Kufumba na kufumbua, tulitokezea sehemu ambayo kulikuwa na watu wengi wa kila aina wamekusanyika. Wengine walikuwa wamekaa, wengine wamesimama, wengine wamejiinamia na wengine wamelala.
Walikuwa wengi mno, wakubwa kwa wadogo, vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake. Cha ajabu, licha ya wingi wao, wote walikuwa kimya kabisa, hakuna aliyekuwa anazungumza chochote, sauti pekee zilizokuwa zinasikika zilikuwa ni za watu wachache waliokuwa wakigugumia kuonesha wapo kwenye maumivu makali.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Hapa ni wapi na hawa ni akina nani?” niliuliza lakini hakukuwa na mtu wa kunijibu, yule mtu aliyenileta sikumuona tena, nilijikuta nikiwa peke yangu lakini kukawa na nguvu fulani iliyokuwa inaniongoza sehemu ya kwenda.
Niliendelea kujipenyeza ndani ya lile kundi la watu, nikawa makini kuwatazama wale watu usoni nikiamini naweza kukutana na ninaowafahamu lakini sura nyingi zilikuwa ngeni kwangu. Nikiwa naendelea kushangaashangaa, nilimuona mtu ambaye nilikuwa namfahamu vizuri lakini nilishangaa iweje nikutane naye?
Hakuwa mwingine bali Mzee Muyombe, huyu alikuwa dereva wa halmashauri na nilimkumbuka vizuri kwa sababu mwanaye, Mathayo, tulisoma naye darasa moja tukiwa shule ya msingi na alikuwa rafiki yangu kipenzi. Kilichonishangaza, ni kwamba ilikuwa imepita karibu miaka tisa tangu mzee huyu afariki!
Alipoteza maisha kwenye ajali mbaya ya gari baada ya gari alilokuwa anaendesha kugonganga uso kwa uso na gari dogo lililokuwa linaendeshwa na kijana mmoja wa palepale mtaani. Nakumbuka hata siku ya mazishi yake nilikuwepo na nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanamfariji Mathayo kwa kuondokewa na baba yake.
Kumbe wakati nikiendelea kutafakari hivyo, na yeye alinikumbuka ingawa alionekana ni kama ananifananisha, akawa ananitazama kwa kunikazia macho. Kiukweli niliogopa sana maana kwa tafsiri nyepesi, yule hakuwa binadamu wa kawaida bali mzimu kwa sababu mwenyewe alishakufa siku nyingi zilizopita.
Tuliendelea kutazamana kwa muda, akaanza kunionesha ishara kama ya kunikataza jambo ambalo sikulielewa, akawa anatumia mikono yake kunizuia, nikiwa naendelea kujaribu kutuliza kichwa ili nielewe alikuwa akimaanisha nini, nilishangaa ameyeyuka na kupotea kwenye upeo wa macho yangu.
Nilifikicha macho na kutazama tena pale alipokuwepo, hakuwepo. Nikabaki na maswali mengi yaliyokosa majibu. Nilijikuta nikiendelea na safari, nikazidi kupenya kwenye ule umati huku nikimtazama kila mmoja usoni, kwa mara nyingine nikajikuta nikishtuka mno baada ya kumuona mtu ambaye nilikuwa namfahamu.
Huyu hakuwa mwingine bali Hezron, tuliyekuwa tukicheza naye enzi za utoto ambaye naye kama ilivyokuwa kwa mzee Muyombe, alikuwa amefariki dunia miaka mingi iliyopita. Nakikumbuka vizuri kifo chake, alipoteza maisha baada ya kuzama baharini wakati akiogelea na ndugu zake, akazidiwa na mawimbi yaliyomvutia baharini na baadaye mwili wake kuokotwa ukiwa ufukweni, akiwa tayari amefariki dunia.
Nilishangaa imekuwaje nikutane na mtu mwingine ambaye naye alikuwa amepoteza maisha? Kingine kilichonishangaza, wakati anapoteza maisha, Hezron bado alikuwa kijana mdogo lakini siku hiyo, naye alionekana kuwa mkubwa, akiwa analinganalingana na mimi.
*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Sikuwahi kusikia wala kusoma mahali popote kwamba mtu akifa akiwa mtoto, anaendelea kukua huko kwenye maisha yake mengine mpaka hatua ya kufikia utu uzima, nilibaki nimepigwa na bumbuwazi. Cha ajabu, naye alikuwa akinioneshea ishara kama ya kunikataza jambo, sikuelewa pia ni jambo gani alilokuwa akinikataza.
Nilipoendelea kumtazama, naye aliyeyuka, nikaendelea kusonga mbele ambapo sasa nilianza kukutana na watu wengi niliokuwa nawafahamu. Miongoni mwao, wote walishatangulia mbele za haki kwa maana kwamba walishakufa. Kadiri nilivyokuwa nazidi kukutana nao ndivyo hofu ilivyokuwa inazidi kupungua ndani ya moyo wangu.
Kati ya yote, ilionesha watu wote niliokuwa nafahamiana nao walikuwa wakinikataza jambo ambalo bado sikuwa nimelielewa ni nini. Nikiwa naendelea kushangaashangaa, nilisikia mlio wa kengele ya ajabu, ikalia mfululizo kisha nikawaona watu wote wakiinamisha vichwa vyao chini, giza nene likaanza kutanda.
“Tuondoke, muda huu haufai kabisa wewe kuwepo huku, unaweza kupitiliza moja kwa moja,” niliisikia ile sauti kisha nikahisi nikishikwa kwa nguvu, kufumba na kufumbua nilikuwa nimerejea tena kule kwenye giza nilikokuwepo awali lakini bado niliendelea kuisikia ile sauti ya kengele ikilia.
Sikukumbuka nimeshuka saa ngapi kwenye treni na limeelekea wapi ila nilijikuta tu nikiwa nimesimama. Mlio wa ile kengele ulipokoma, nilianza kusikia sauti za watu wengi wakilia kwa sauti za ajabuajabu, wakionesha kwamba wapo kwenye maumivu makali.
“Mbona unaonesha kuwa na hofu kubwa moyoni mwako?” niliisikia ile sauti ikiniuliza, nikashindwa cha kujibu zaidi ya kujiinamia. Wale watu niliowaona kule, walinifanya nijawe na huzuni kubwa kwenye moyo wangu. Kumbukumbu ya misiba mingi niliyohudhuria tangu nikiwa mdogo ilianza kujirudia kichwani mwangu.
Kwa mbali nikaanza kuamini maneno ya Shenaiza kwamba huenda ni kweli nilikuwa nimekufa. Nilijisikia uchungu mkali sana ndani ya moyo wangu, nilitamani nirudi kwenye maisha yangu ya kawaida kwa sababu bado sikuwa nimekamilisha mambo mengi sana kwenye ulimwengu wa kawaida.
Kama kweli huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yangu, tafsiri yake ni kwamba ingekuwa sawa na kusema kwamba sijafanya chochote maishani mwangu, yaani nimezaliwa, nikaishi kisha nikafa bila kufanya jambo lolote la maana maishani mwangu, jambo ambalo liliniumiza sana.
“Najua unavyojisikia ndani ya moyo wako, nalijua hitaji la moyo wako na ndiyo maana nataka nikuoneshe kilichofanya uletwe huku. Kama nilivyosema, hukuletwa huku kwa bahati mbaya bali kuna kazi ambayo unatakiwa kwenda kuifanya.
“Kuna mamia ya watu wanaendelea kuwa wahanga kwa sababu ya tamaa za watu wachache. Maisha yako yalikuwa yamefikia mwisho lakini umshukuru Mungu wako kwa kupata nafasi hii, huwa siyo kila mtu anaipata.
“Tabia yako njema uliyoionesha katika maisha yako tangu ulipopata akili, ikiwemo kushika ibada, kufuata maandiko kwa kuacha kufanya yale yaliyokatazwa na kuishi katika misingi ambayo ndiyo hasa binadamu anayotakiwa kuishi, ni miongoni mwa sababu zilizofanya upate hii nafasi ya kurudi tena duniani.
“Ukirudi duniani, ukawe balozi mzuri wa kuwahamasisha binadamu wenzako ambao bado wapo hai juu ya kumuabudu Mungu, kuwapenda binadamu wenzao na kuwatendea mambo mema, kuacha kufanya maovu na maasi na kubwa zaidi, kwenda kuikomesha kazi inayofanywa na baba yake Shenaiza na watu wake, maelezo mengine utakuwa unaletewa hukohuko,” ilisikika ile sauti nzito ya kutisha.
Sikuelewa aliyekuwa anayasema hayo ni nani na pale nilikuwa wapi maana nilimsikia akizungumzia kuhusu kurejea duniani, akimaanisha kwamba pale hapakuwa duniani. “Umenielewaa?” ilihoji ile sauti na kusababisha ngurumo nyingi zianze kusikika kutoka kila upande, zikiambatana na upepo mkali uliokuwa ukivuma kwa kasi kubwa.
“Ndiyooo!” nilijibu kwa sauti iliyojaa hofu kubwa, iliyokuwa ikitetemeka ambayo kama nilivyoeleza kuanzia mwanzo, ilikuwa ikitokea moyoni na siyo mdomoni, nikasikia radi kubwa ikipiga jirani kabisa na pale nilipokuwepo, sikuelewa tena kilichoendelea.
Nilipokuja kushtuka, nilijikuta nikiwa nimelala kitandani, mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida, nikiwa nimeunganishwa mashine ya kunisaidia kupumua huku mwili wangu ukiwa umeunganishwa na vifaa vingi vya kitabibu, milio ya mashine mbalimbali ikisikika ndani ya chumba kile ambacho hata bila kuuliza, niligundua kwamba ni wodini.
“Amefumbua macho! Dokta… amefumbua macho! Njooni haraka!”
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 27;


Nilipokuja kushtuka, nilijikuta nikiwa nimelala kitandani, mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida, nikiwa nimeunganishwa mashine ya kunisaidia kupumua huku mwili wangu ukiwa umeunganishwa na vifaa vingi vya kitabibu, milio ya mashine mbalimbali ikisikika ndani ya chumba kile ambacho hata bila kuuliza, niligundua kwamba ni wodini.
“Amefumbua macho! Dokta… amefumbua macho! Njooni haraka!”
SASA ENDELEA…
Harakaharaka madaktari wengi waliingia ndani ya kile chumba na kuzunguka kitanda changu, kwa mbali nikawa nawatazama mmoja baada ya mwingine, wote wakionekana kukiinamia kitanda changu. Macho yangu yalikuwa na ukungu, hali iliyonifanya nisiwe na uangavu wa kutosha machoni kuwaona ingawa bado nilikuwa na uwezo wa kutambua sura zao.
“Unaendeleaje Jamal?” nilisikia daktari mmoja akiniuliza. Kwa jinsi sauti yake ilivyokuwa ikisikika, ilikuwa mithili ya inayotoka kwenye redio mbovu. Nilijaribu kufumbua mdomo lakini nilishindwa kwani nilikuwa nimeunganishwa na mabomba mengi, mdomoni na puani, nikawa natingisha tu kichwa kuashiria kwamba najisikia vizuri.
Jopo la madaktari waliendelea kunizunguka pale, nikamuona mwingine akinipima kwa kutumia kifaa maalum kusikiliza mapigo ya moyo wangu, mwingine akaniweka ‘thermometer’ kwapani kwa lengo la kunipima joto huku mwingine akiwa bize kufuatilia maandishi yaliyokuwa yanaonekana kwenye mashine inayofanana na kompyuta, iliyokuwa ikipiga kelele kwa kutoa milio ya ‘kubipu’ kila mara.
“He is recovering! His heartbeats are stabilizing, blood sugar is coming to normal and the wound is healing!” alisema daktari mmoja wakati akiwaambia wenzake, kwa kuwa Kiingereza hakikuwa kikinipiga chenga, niliweza kuelewa vizuri kwamba alikuwa akiwaambia wenzake kwamba nimeanza kupata nafuu, mapigo yangu ya moyo yanaimarika, kiwango cha sukari kinarudi kwenye hali ya kawaida na jeraha langu linapona.
Niliwaona wote wakitabasamu na kunitazama usoni, kila mmoja akawa ananipongeza kwamba eti nimepigania vizuri maisha yangu kwa sababu nilikuwa na hali mbaya sana. Daktari mwingine ambaye kiumri alikuwa kijana mdogo, alinitania kwamba eti mimi ndiye binadamu wa kwanza niliyeweza kwenda kuzimu na kurudi, wenzake wote wakacheka.
Japokuwa mwenyewe alizungumza kama utani na wenzake nao wakacheka wakichukulia utani, kile alichokisema hakikuwa utani ingawa siwezi kusema kwamba kule nilikofika ndiyo kuzimu kwenyewe au la lakini ukweli ni kwamba nilikuwa nimefika mahali ambako sidhani kama kuna binadamu aliye hai amewahi kufika.
Kuna muda nilihisi huenda bado nipo kwenye ile hali ya kuuona mwili wangu wakati mwenyewe nikiwa pembeni lakini haikuwa hivyo, ni kweli nilikuwa nimerejewa na fahamu na kila kilichokuwa kinaendelea kilikuwa kikitokea kwenye ulimwengu halisi.
Unajua namna nyepesi ya kujigundua kwamba unaishi kwenye ulimwengu wa kawaida unapoona upo kwenye mazingira ambayo huelewielewi kama upo ndotoni au la, ni kujaribu kupepesa macho, kukunja vidole vya mikono au kuigusa ngozi ya mwili wako kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Ukiona umeweza kupepesa macho, kukunja vidole au umesikia maumivu baada ya kujifinya au kujichoma na kitu chenye ncha kali, basi ujue kwamba haupo ndotoni au kwenye ulimwengu wa tofauti bali upo kwenye ulimwengu halisi. Hicho ndicho nilichokifanya mimi na kweli majibu yalionesha kwamba nilikuwa nimerejea kwenye ulimwengu wa kawaida.
Madaktari waliendelea kujadiliana na mwisho walifikia muafaka wa kuamua kunipunguza baadhi ya vifaa mwilini mwangu, ikiwemo mirija ya kunisaidia kula pamoja na ile ya kutolea haja ndogo kwani kwa kipindi chote nilichokuwa sina fahamu, kila kitu kilikuwa kikifanyika kwa msaada wa mirija.
Hilo lilifanyika, kitu pekee kilichoachwa mwilini mwangu ilikuwa ni mashine ya kunisaidia kupumua ambayo nayo walikubaliana kwamba niendelee kuitumia kwa muda lakini nitakapofikia hatua ya kuweza kupumua mwenyewe vizuri, wataitoa.
Niliwaona madaktari wote wakiwa na nyuso za furaha sana mle ndani ya wodi yangu, tofauti kabisa na kipindi nilipokuwa nikiwatazama kutokea pembeni kabla sijarejewa na fahamu ambapo kila mmoja alikuwa akionesha sura ya kukata tamaa.
“Vipi Jamal, unajisikiaje?” nesi mmoja wa kike aliniuliza kwa sauti ya upole wakati akinisafisha mwili wangu kwa kutumia kitambaa laini kilichokuwa kimewekwa kwenye kopo lenye maji ya uvuguvugu.
Nikamjibu kwa sauti ya chini kwamba nilikuwa najisikia vizuri, akaendelea kunifutafuta uso wangu, hasa kwenye yale maeneo niliyokuwa nimebandikwa bandeji za kushikilia ile mirija iliyotolewa. Yule nesi aliendelea kunipigisha stori za hapa na pale, huku mara kwa mara akiingizia utani ambao nilielewa kwamba ulikuwa ni kwa lengo la kunichangamsha.
Unajua jambo ambalo watu wengi hawalijui, madaktari, manesi na wauguzi, huwa wanafundishwa saikolojia ya namna ya kucheza na akili za mgonjwa na kumfanya ajisikie amani ndani ya moyo wake na kuamsha upya matumaini ya kupona, hata kama alikuwa mahututi.
Ndiyo maana ni nadra sana kumuona daktari aliyesomea vizuri kazi yake na kuhitimu, akimfokea mgonjwa au kuzungumza naye kwa lugha isiyo rafiki. Fuatilia kwa makini, madaktari karibu wote, wa hospitali za binafsi na za serikali, huwa wanakuwa wapole sana wanapozungumza na wagonjwa wao, hata kama una tatizo kubwa, atakupa maneno laini ya kishujaa yatakayokufanya uamini kwamba lazima utapona.
Hata manesi wale waliofundishwa vizuri na kuelewa, huwa wapole sana kwa wagonjwa kwa sababu wamefundishwa hivyo. Ukiona nesi anawabwatukia wagonjwa wake, anawatolea lugha chafu na za matusi, wengi wanakuwa ni wale ambao wameingia kwenye fani hiyo kwa njia za kiujanjaujanja, pengine wamefoji vyeti au vyuoni walifeli lakini wameingizwa kwa migongo ya ndugu zao au kwa kutoa rushwa.
Basi yule nesi aliendelea kunipa maneno matamu, eti akawa ananisifia kwamba japokuwa nilikuwa nimepoteza fahamu kwa muda mrefu, eti bado nilikuwa naonekana ‘handsome’, nikashindwa kujizuia na kuachia tabasamu hafifu.
Akaniambia eti kama angekuwa hana aibu za kikekike, angenitongoza ili nimuoe, nikazidi kuachia tabasamu pana kwani sijawahi kusikia eti mwanamke anamtongoza mwanaume amuoe, japokuwa anaweza tu kumrahisishia mazingira ya kumpata, nikajikuta nikivutiwa naye kwani ukiachilia mbali masihara yake, pia alikuwa na sura nzuri ya kuvutia na umbile lililokaa kikekike haswaa!
“Yaani sikomi tu, tamaa za wasichana warembo na huruma zangu ndiyo iliyonifanya niingie kwenye mtego wa Shenaiza, hata kupona vizuri bado nimeanza kumzimikia nesi,” nilijisemea mwenyewe moyoni na kuzidi kutabasamu.
Alizidi kunipigisha stori mpaka nikaona ile mashine ya kunisaidia kupumua kama inaninyima uhuru, nikamuomba aitoe ili nijaribu kupumua mwenyewe, akafanya hivyo na kwa bahati nzuri, tayari nilikuwa na uwezo wa kupumua mwenyewe vizuri, madaktari wakazidi kufurahi na kushauri kwamba kwa kuwa nilikuwa na hali nzuri, nihamishiwe kwenye wodi za kawaida kwa sababu kwa muda wote huo, bado nilikuwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).
Mipango ilianza kuandaliwa na hatimaye nilihamishiwa kwenye wodi ya wanaume ambapo nilipoingizwa tu, ndugu, jamaa na marafiki walianza kufurika kwa wingi kuja kuniona kwani fursa hiyo waliikosa nilipokuwa ICU kwa sababu kule huwa ndugu hawaruhusiwi kumuona mgonjwa ambaye yupo kwenye hali mbaya kama niliyokuwa nayo mimi, labda kama kuna sababu maalum.
Miongoni mwa watu wa mwanzomwanzo kabisa kuja kuniona, alikuwa ni Raya ambaye hakuamini kabisa aliponiona nikiwa nimefumbua macho, akanikumbatia kwa nguvu pale kitandani bila kujali dripu niliyokuwa nimeunganishwa, akawa ananibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu huku akiangua kilio kwa nguvu.
“Nilijua nimekupoteza mpenzi wangu, ooh ahsante Mungu! Ahsante Mungu,” alisema Raya, ikabidi niinue ule mkono ambao haukuwa na dripu nikaupitisha mgongoni kwake na kumkumbatia, nikambusu shavuni, kitendo ambacho kwa kiasi kikubwa kilimfariji sana.
Japokuwa mwili wangu haukuwa na nguvu, ilikuwa ni lazima nifanye hivyo kwa sababu kusema ukweli, tangu nipatwe na matatizo, Raya alionekana kuguswa pengine kuliko mtu mwingine yeyote.
Niliamini uchungu ambao alikuwa nao msichana huyo, ungekuwa sawa na wa mama yangu endapo angefahamu kilichokuwa kimenitokea mwanaye lakini kwa kuwa wazazi wangu hawakuwa wakijua chochote kutokana na mazingira ambayo mimi mwenyewe ndiye niliyeyatengeneza (nitafafanua kuhusu hili baadaye), Raya ndiye aliyesimama kwenye nafasi ya mama yangu.
Kingine nilichojifunza, ni kuacha kuhukumu watu wote kwambe eti siku hizi duniani hakuna tena mapenzi ya kweli! Siyo sahihi kabisa, kuna watu wana mapenzi mpaka shetani mwenyewe anayaogopa, mmoja wapo akiwa ni Raya.
Niliendelea kumkumbatia msichana huyo huku marafiki na jamaa zangu wengine wakiwa pembeni wakitutazama, tukiwa kwenye hali hiyo, nilisikia mlango wa wodi ukifunguliwa na mtu akaingia mbiombio mpaka pale kitandani kwangu, nikashtuka na kumuachia Raya, Raya naye akainua uso wake, watu wote tukawa tunamtazama kwa mshangao mtu yule aliyeingia, tukiwa ni kama hatuamini.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 29;

ILIPOISHIA:
Niliendelea kumkumbatia msichana huyo huku marafiki na jamaa zangu wengine wakiwa pembeni wakitutazama, tukiwa kwenye hali hiyo, nilisikia mlango wa wodi ukifunguliwa na mtu akaingia mbiombio mpaka pale kitandani kwangu, nikashtuka na kumuachia Raya, Raya naye akainua uso wake, watu wote tukawa tunamtazama kwa mshangao mtu yule aliyeingia, tukiwa ni kama hatuamini.
SASA ENDELEA…
Hakuwa mwingine, bali Shenaiza ambaye alikuwa amevaamavazi ya hospitalini hapo kuonesha kwamba alikuwa amelazwa, mkononi akiwa na sindano iliyofungwa na plasta, nafikiri kwa ajili ya kumuingizia dawa au kumtundikia dripu, nikawa namtazama usoni, naye akawa ananitazama.
“Jama! Kumbe ni kweli hujafa?” alisema Shenaiza kwa sauti ya kukwamakwama, wote tukatazamana tena kisha nikageuka na kumtazama Shenaiza, alionesha kabisa kwamba hakuwa sawa, nikawa najiuliza maswali mengi kichwani ambayo sikuwa na majibu yake.
>>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilikumbuka kwamba kuna muda mimi na Shenaiza tulikuwa tumnekaa siti moja kwenye treni la ajabu, tukielekea kusikojulikana, giza likiwa limetanda kila sehemu. Kama mimi nilikuwa kitandani, wodini, na Shenaiza naye alikuwa hospitalini hapo akiwa amelazwa, ina maana kwamba mimi na yeye tulikutana wapi?
Nilikumbuka pia kwamba yeye mwenyewe aliniambia kwamba ameamua kuyakatisha maisha yake kwa kujiovadozi dawa ya usingizi, na kwamba aliamua kufanya hivyo kama njia ya kupumzika na mateso aliyokuwa anayapata, sasa Shenaiza aliyejiua ni nani na huyo aliyekuwa amesimama mbele yangu ni nani?
Nilihisi kama kichwa kinapata moto kwa sababu ya utata wa kilichokuwa kinaendelea, hata hivyo nilipoemndelea kutuliza kichwa changu, nilianza kupata baadhi ya majibu.
“Kumbe kweli hukufa?” Shenaiza aliniuliza tena swali lile ambalo lilinizindua kutoka kwenye lindi la mawazo.
“Hebu naomba mtupishe kidogo nizungumze na Shenaiza,” niliwaambia watu wote waliokuwa wamenizunguka pale wodini lakini Raya alikataakatakata.
“jamal! Are you out of your mind?” (Jamal umechanganyikiwa) alisema raya kwa sauti ya juu. Akaendelea kuniambia kwamba Shenaiza ndiye aliyekuwa chanzo cha mimi kutaka kupoteza maisha, iweje leo nimuone yeye ndiyo wa maana kiasi c ha kuwataka watu wote watoke nje?
>>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Kama amekuja kwa lengo la kukumalizia je? Mimi siendi popote, nitakaa hapahapa kukulinda,” alisema Raya huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara, nikashindwa cha kufanya.
Wale watu wengine wote walitoka lakini kama Raya alivyosema, hakutaka kuinuka pale pembeni ya kitanda changu alipokuwa amekaa na mimi sikuona sababu yoyote ya kumlazimisha.
Bado tulikuwa tukiendelea kutazamana na Shenaiza, kadiri nilivyokuwa nazidi kumtazama ndivyo nilivyokuwa naendelea kukumbuka mambo mengi yaliyotokea kwenye ulimwengu usio wa kawaida na kwenye ulimwengu wa kawaida.
“Haya sema shida yako iliyokuleta,” Raya alivunja ukimya, Shenaiza akashusha pumzi ndefu na kusogea kwenye kitanda nilichokuwa nimelazwa.
‘Samahani dada wala mimi sijaja hapa kwa nia mbaya, kwanza nimejikaza tu kwani bado naumwa sana, nimetoroka tu wodini baada ya kusikia Jamal yupo hapa,” alisema Shenaiza kwa sauti ya chini, nikamuona Raya naye akishusha pumzi kwani alishajiandaa kwa shari lakini msichana huyo akaonesha kwamba hakuwa amekuja kisharishari.
“Nilisikia kwamba umekufa na mimi nilithibitisha hilo,” alisema Shenaiza kwa upole, nikamuliza amesikia wapi na amethibitishaje hilo?
“Niliambiwa na daktari mmoja kati ya wale waliokuwa wanakutibu, akaniambiakwamba ulishakata roho lakini walikuwa wamekuunganisha kwenye mashineya kusaidia moyo wako uendelee kudunda, akanihakikishia kwamba saa chache baadaye watakutoa kwenye mashine hiyo.
“Mh! Sikuelewi! Raya wewe unamuelewa anachokisema huyu?”
“Mimi namuelewa, ni kweli hata mimi daktari aliniambia kwamba huwezi kupona,” alisema Raya na kunifanya nikose cha kujibu, nikawa nawatazama mmoja baada ya mwingine usoni kwa zamu. Unajua miongoni mwa mambo ambayo sikuwa nataka kuyasikia, ni kwamba eti watu wote walikuwa wanajua kwamba nimekufa.
“Halafu kuna mambo yananichanganya sana kichwa changu, sijui ni ndoto, maruweruwe au uchawi hata sielewi. Mbona nakumbuka kama mimina wewe kuna sehemu tulikutana halafu tukaongea mambo mengi tu? Na kubwa zaidi mbona nakumbuka kama na mimi nilikufa?”
Swali hilo la Shenaiza liliunga kabisa na kile nilichokuwa nakifiria kichwani mwangu muda wote. Ni kweli hata mimi nilikuwa najua kwamba kuna sehemu mimina Shenaiza kuna sehemu tulikuwa pamoja na tukazungumza mambo mengi tu pamoja, tena tukiwa tumekaa kwenye siti moja kwenye treni la ajabu.
“Utakuwa ulikuwa unaota, ulikutana wapi na Jamal wakati tangu siku ile ulipomsababishia atake kufa hajainuka kitandani na leo ndiyo amefumbua macho?” Raya aliingilia mazungumzo yale, sote tukawa tunamtazama kwa sababu hakuwa akijua chochote.
“Mh! Inawezekana kweli nilikuwa naota, kwa sababu katika maisha yangu sijawahi kupanda treni hata siku moja lakini nakumbuka eti tulikuwa tumekaa kwenye siti mojaya treni,” alisema Shenaiza na kuzidi kunihakikishia kwamba kumbe kile kilichotokea kilikuwa ni jambo halisi, Raya akazidi kubisha.
“Sasa mtu yupo kitandani anaumwa hoi hajitambui atapandaje treni? Dada ulikuwa unaota na sidhani kama Jamal anahitaji kusikia ndoto zako, kama hicho ndicho kilichokuleta naomba uondoke, mgonjwa anahitaji kupumzika,” alisema Raya kwa msisitizo.
“Basi tuachane na hayo, Jamal nimekuja kukuomba msamaha!”
“Msamaha wa nini Shenaiza?”
“Kwa yote niliyokufanyia. Haikuwa kusudioa langu kukuingiza kwenye matatizo, najua wewe na watu wako wote wa karibu mnanichukia sana.”
>>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Msamaha wako una maana gani leo? Kama angekuwa amekufa ungemuomba nani msamaha? Dada hebu nakuomba uondoke,” Raya alijibu kwa ukali, nikamuona Shenaiza akijiinamia na kuanza kuangua kilio.
“Wewe! Kwa nini unatusumbua kukutafuta? Kwa nini unatoka wodini bila taarifa wakati unajua hali yako siyo nzuri? Unatusababishia matatizo kwa ndugu zako,” manesi wawili waliingia mbiombio mle wodini, akawamshika Shenaiza huku an kule na kumtoa msobemsobe huku mwenyewe akiendelea kuangua kilio. Mimi na Raya tukatazamana!
“Inaonesha mnafahamiana kuliko hata mimi ninavyojua, huyu si mmekutana juzijuzi tu hapo, mbona inaonesha kama kuna kinachoendelea nyuma ya pazia?” Raya aliniuliza, akionesha dhahiri kuwa na wivu mkali ndani ya moyo wake, nikashindwa cha kumjibu.
“Jamal, nakupenda sana mpenzi wangu, nakuomba uamini ninachokisema. Sijawahi kumpenda mtu yeyote katika maisha yangu na wewe mweyewe ni shahidi kwamba umenikuta nikiwa simjui mwanaume yeyote.
“Niliamua kukupa zawadi ya kuwa mtu wa kwanza kunijua na nataka uwe wa mwisho kwangu, nataka unioe tuishi pamoja milele Jamal,” alisema Raya huku machozi yakimlengalenga.
Kiukweli na mimi nilikuwa nimetokea kumpenda Raya baada ya kuwa nimeutezsa moyo wake kwa kipindi kirefu na kweli nilishaanza kuweka mnalengo ya maisha yangu ya baadaye nikiwa naye lakini niliona kama huo siyo muda muafaka wa kuzungumzia mapenzi.
Ndiyo kwanza nilikuwa nimerejea kwenye ulimwengu wa kawaida, bado kuna maswali mengi ambayo sikuwa nimeyapatia majibu, kuhusu mimi mwenyewe na pia kumhusu Shenaiza na familia yake.
Hata hivyo, sikutaka Raya ajisikie vibaya kwa namna yoyote, mwenyewe nilishajiwekea nadhiri moyoni kwamba nitakuwa sehemu ya furaha ya raya, hasa baada ya kugundua ni kwa kiasi gani alikuwa akinipenda.
Nikamkumbatia na kubusu kwenye paji lake la uso, nikamwambia hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Shenaiza isipokuwa ilikuwa ni lazima niendelee kuwa naye karibu kwa sababu kuna mambo muhimu ilikuwa ni lazima niyajue, hasa kuhusu baba yake Shenaiza.
“Kuna kazi nimepewa ya kuhakikisha namzuia baba yake Shenaiza hicho anachokifanya, na ni lazima nitimize.”
“Kazi? Nani aliyekupa hiyo kazi? Halafu umzuie kwani anafanya nini na wewe umejuaje?” Raya alinibana kwa maswali, nikawa nashindwa hata namna ya kumjibu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 29;

“Kuna kazi nimepewa ya kuhakikisha namzuia baba yake Shenaiza hicho anachokifanya, na ni lazima nitimize.”
“Kazi? Nani aliyekupa hiyo kazi? Halafu umzuie kwani anafanya nini na wewe umejuaje?” Raya alinibana kwa maswali, nikawa nashindwa hata namna ya kumjibu.
SASA ENDELEA...
“Si naongea na wewe Jamal!”
“Aah! Unajua ni stori ndefu kidogo na... na... ni...” nilijikuta nikishikwa na kigugumizi, Raya alikuwa akinitazama huku amenikazia macho. Nadhani kuna mambo alianza kuhisi kama hayaendi sawa.
Nilichokifanya ilikuwa ni kumzugazuga na kubadilisha mada, nikamhakikishia kwamba nitakapokaa na kutulia nitamueleza kwa kirefu kila kitu kilichokuwa kinaendelea. Bado Raya alionesha kutoridhishwa na maelezo yangu na kikubwa kilichokuwa kikimsumbua ilikuwa ni wivu.
Kwa sababu kihistoria alishajenga mawazo akilini mwake kwamba mimi simpendi isipokuwa yeye ndiyo analazimisha mapenzi, alikuwa akiteseka sana ndani ya moyo wake akiamini kwamba akitokea mwanamke ambaye nitampenda, kama alivyokuwa akihisi kwa Shenaiza, nitamuacha jumla, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea.
“Halafu kuna mambo yananichanganya sana kichwa changu, sijui ni ndoto, maruweruwe au uchawi hata sielewi. Mbona nakumbuka kama mimi na wewe kuna sehemu tulikutana halafu tukaongea mambo mengi tu? Na kubwa zaidi mbona nakumbuka kama na mimi nilikufa?” kauli aliyoitoa Shenaiza muda mfupi uliopita ilijirudia ndani ya kichwa changu, nikawa natazama juu darini nikitafuta majibu ya maswali yangu.
Alichokisema Shenaiza ndicho kilichokuwa ndani ya akili yangu, ni kweli mimi na yeye kuna sehemu tulikutana na tukaongea mambo mengi tu, akanieleza kwamba ameamua kujiua kwa kujiovadozi madawa ya kulevya, akanihakikishia na mimi kwamba nilikuwa nimekufa lakini nikawa nambishia.
Shauku ya kutaka kufahamu zaidi kuhusu kilichotokea, ilinisukuma kuweka nadhiri ndani ya moyo wangu kwamba lazima nimtafute tena Shenaiza ili tuzungumze kwa kina, huenda mwenzangu alikuwa anaelewa kilichotokea kwa ufasaha zaidi.
Raya aliendelea kunisemesha mambo mengi lakini nikiri kwamba akili yangu haikuwa pale wodini, nilikuwa nikimfikiria Shenaiza na yote yaliyotokea. Naomba nieleweke kwamba hiyo haikumaanisha kwamba sikuwa nampenda Raya, nilishaamua kuwa naye baada ya kugundua kuwa ananipenda sana lakini kila nilipomfikiria Shenaiza, nilijikuta mwili wangu ukisisimka mno.
Bado kuna swali kubwa halikuwa limepata majibu akilini mwangu, haya yote yaliyokuwa yakitokea kwenye maisha yangu, kuanzia Shenaiza kunipigia simu na baadaye kunieleza kwamba amekosea namba, akaniganda kwamba hata kama amekosea anaomba nimsaidie na yote yaliyofuatia mpaka muda huo niliokuwa wodini.
“Hivi kama Mungu angeamua kuyachukua maisha yangu jumla, ningekufa nikiwa gizani kabisa, nikiwa sielewi chochote kilichosababisha mpaka nikafikwa na mauti? Mimi ni mtu wa ajabu eeh!” nilijikuta nikimuuliza Raya swali hilo, akashusha pumzi ndefu na kunitazama.
“Kwa hiyo kumbe muda wote nilikuwa naongea peke yangu?” alisema Raya huku akionesha kukasirishwa na kitendo cha mimi kuzungumza kitu ambacho hakikuwa na uhusiano wowote na kile alichokuwa akiniongelesha.
Niligundua kwamba nimekosea na kwa kuwa sikutaka kumuudhi Raya, ilibidi nimdanganye kwamba tangu nimerejewa na fahamu zangu, nahisi kichwa changu hakipo sawa kwa hiyo asinielewe vibaya, nikamuona akishusha tena pumzi na kunisogelea, akanibusu na kuninong’oneza:
“Nakupenda sana mpenzi wangu, nakuombea upone kabisa ili tuendelee na maisha yetu,” akanibusu na lipsi zake laini kwenye midomo yangu, akanibusu tena kwenye paji la uso kisha akaniambia kwamba anaenda kuniandalia chakula.
Alipofungua mlango na kutoka, ndugu na marafiki zangu waliokuwa wakisubiri nje, waliingia wodini na kukaa pembeni yangu, tukaendelea na stori za hapa na pale, wengi wakinipa pole kwa kilichotokea. Japokuwa hali yangu ilikuwa ikizidi kuimarika kwa kasi, lakini niliwaona watu wote wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua nini hasa kilichotokea.
Sikuwa tayari kueleza kila kitu, nikawa nafupisha tu kwamba nilivamiwa na majambazi walionijeruhi vibaya na kunifanya ninuse kaburi. Nilikuwa na sababu maalum za kutoeleza kila kitu kilichotokea, bado nilikuwa na kazi kubwa ya kuifanya.
Muda wa kuona wagonjwa ulipoisha, watu wote waliondoka na kuniacha nikiwa na nesi aliyekuwa akinihudumia tu, huku nikiendelea kumsubiri Raya ambaye aliahidi kwamba ndiyo atakayeniuguza mpaka nipone na kuruhusiwa kutoka wodini.
Kwa kuwa ndiyo kwanza alikuwa ametoka na kwenda kuniandalia chakula kama mwenyewe alivyosema, niliona huo ndiyo muda muafaka wa kumtafuta Shenaiza ili anieleze ukweli wa mambo mengi niliyokuwa nahitaji kuyajua.
“Nesi samahani naomba nikuulize,” nilimuuliza yule nesi mchangamfu aliyekuwa akipenda kunitania.
“Niulize tu honey wangu, nakupenda lakini mume mwenyewe una wanawake kibao, hujui najisikia wivu?” alisema huku akinisogelea, nikajikuta nikicheka kwa sauti. Nilimuuliza kuhusu Shenaiza kama anafahamu wodi aliyolazwa.
Alinipa majibu ambayo yalinishangaza sana, aliniambia kwamba msichana huyo alikuwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa wa akili na kwamba kuna muda ilikuwa ni lazima wamfunge kamba kwa jinsi alivyokuwa akiwasumbua madaktari na wagonjwa wenzake.
Kiukweli nilishangazwa sana na maelezo hayo kwa sababu muda mfupi uliopita, nilikuwa nimezungumza naye na hakuonesha dalili zozote za kuchanganyikiwa mpaka alipokuja kuchukuliwa kwa nguvu na wale manesi.
Nilimuomba anielekeze vizuri wodi aliyokuwa amelazwa kwa sababu nilikuwa na mazungumzo muhimu naye, akaniambia kwamba utaratibu wa hospitalini hapo hauruhusu. Ilibidi niendelee kumbembeleza ambapo aliniambia atanisaidia kwa sababu ananipenda, akanisaidia kuinuka pale kitandani, tukaongozana kuelekea kwa Shenaiza kama nilivyomuomba.
Njia nzima yule nesi alikuwa akiendelea kunitania kuhusu mambo ya kimapenzi mpaka ikafika kipindi nikawa na wasiwasi kama kile alichokuwa anakisema ni utani au ananifikishia ujumbe kwa njia ya utani! Ukarimu na ucheshi wake, achilia mbali uzuri wa kipekee wa sura na umbo aliojaliwa, vilinifanya nimzoee haraka.
Alinipeleka mpaka kwenye wodi hiyo lakini kutokana na mazingira ya mle ndani, aliniambia nimsubiri hapohapo nje, akaingia na kwenda kuzungumza na manesi wenzake na muda mfupi baadaye, alitoka akiwa na Shenaiza ambaye aliponiona tu, alinikimbilia na kunikumbatia.
“Eti wameamua kunipakazia kwamba mimi ni mgonjwa wa akili. Jamal, eti mimi naongea kama mtu aliyechanganyikiwa?” aliniuliza Shenaiza huku akilia kwa uchungu, nikamuomba yule nesi atuache kidogo ili tuzungumze wawili tu, akanitazama kwa macho yake mazuri ya kurembua kisha akatingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichomwambia.
“Nakupa dakika tano tu, nakusubiri pale pembeni,” alisema, nikamshukuru na kumshika mkono Shenaiza, tukakaa kwenye benchi lililokuwa pembeni.
“Akina nani wanaokupakazia kwamba wewe ni mgonjwa wa akili?”
“Baba na watu wake, wanataka kuniziba mdomo maana nimetishia kwamba nitaueleza ulimwengu wote ukweli wa wanachokifanya, naomba unisaidie,” alisema Shenaiza huku akilia, akanikumbatia kwa nguvu huku machozi mengi yakinichirizikia mwilini.
Kitu ambacho lazima nikikiri hapa, japokuwa nilikuwa nimeamua kumchagua Raya kuwa mke wangu mtarajiwa, nilipokuwa nikimtazama Shenaiza au kukaa naye karibu, moyo wangu ulikuwa ukisuuzika mno. Nadhani hata yeye alikuwa analijua hilo ndiyo maana kila tunapokaa pamoja, ilikuwa ni lazima anishike mkono, aniegamie au anikumbatie.
“Sasa nakusaidiaje Shenaiza mbona unazidi kuniweka kwenye wakati mgumu?”
“Unataka kuwajua watu waliokuwa nyuma ya tukio lako la kunusurika kuuawa?”
“Ndiyo, hata sasa hivi nataka kuwajua. Bado nina maswali mengi kichwani ambayo hayana majibu.”
“Najua, majibu ya maswali yako yote ninayo na kwa hali ilipofikia, nipo tayari kukueleza kila kitu kabla hawa mashetani hawajaniharibu kumbukumbu zangu maana najua haya madawa ya wagonjwa wa akili wanayolazimisha nichomwe, huwa yanaenda kuvuruga kabisa ubongo,” alisema Shenaiza kisha akanibusu kwenye paji la uso.
“Nenda Kisutu, Mtaa wa Mama Zayumba, nyumba namba 203, muulize mtu anaitwa Firyaal, ni mdogo wangu wa kuzaliwa na nilishampa maelekezo, kuna bahasha atakupa na hiyo ndiyo yenye majibu ya maswali unayoyahitaji,” alisema Shenaiza huku akinitazama kwa macho ya upole.
“Narudia tena kukuomba msamaha kwa yote yaliyotokea Jamal, naomba unisamehe. Nahitaji ukaribu wako na msaada wako katika kipindi hiki kigumu ninachopitia,” alisema Shenaiza huku macho yake yakiwa yamebeba ujumbe mzito zaidi, tukatazamana kama sekunde tano mfululizo, nikamuona akiachia tabasamu hafifu lililofanya uzuri wake wa asili uonekane vizuri.
“Ukikamilisha kazi nitakupa zawadi ya ushindi,” alisema Shenaiza huku akinifinyia kijicho kimoja, nilishaelewa alimaanisha nini. Nikasimama na kumshukuru, nikambusu kwenye paji la uso wake na kugeuka nyuma ili nirudi kule wodini kwangu.
Sijui Raya alikuwa amefika muda gani eneo hilo kwani nilipogeuka tu, macho yangu na yake yaligongana, japokuwa alikuwa umbali wa mita kadhaa, niliweza kuona hali aliyokuwa nayo. Ilionesha hata kitendo cha mimi kumbusu Shenaiza alikiona kwa macho yake, nikamuona akianza kububujikwa na machozi.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 30;


ILIPOISHIA:
“Ukikamilisha kazi nitakupa zawadi ya ushindi,” alisema Shenaiza huku akinifinyia kijicho kimoja, nilishaelewa alimaanisha nini. Nikasimama na kumshukuru, nikambusu kwenye paji la uso wake na kugeuka nyuma ili nirudi kule wodini kwangu.
SASA ENDELEA…
Sijui Raya alikuwa amefika muda gani eneo hilo kwani nilipogeuka tu, macho yangu na yake yaligongana, japokuwa alikuwa umbali wa mita kadhaa, niliweza kuona hali aliyokuwa nayo. Ilionesha hata kitendo cha mimi kumbusu Shenaiza alikiona kwa macho yake, nikamuona akianza kububujikwa na machozi.
Nilijikuta mwili wangu ukipigwa na ganzi, nikabaki nimesimama nikihisi hata miguu ilikuwa mizito kuinyanyua. Raya alipoona nimemuona, aligeuka na kuanza kutembea harakaharaka huku akiendelea kulia. Niljihisi kuwa na hatia kubwa sana ndani ya moyo wangu.
Japokuwa mimi na Shenaiza hatukuwa tumebusiana kwa nia mbaya, nilijaribu kujiweka kwenye nafasi ya Raya na kuhisi maumivu ambayo alikuwa anayahisi kwa wakati huo. Kwa wale ambao wamewahi kupitia maumivu ya mapenzi watakuwa wanaelewa vizuri ninachomaanisha!
Ukimpenda mtu halafu ukasikia au ukahisi mtu mwingine pia anampenda, ukiwaona pamoja lazima moyo uume sana, na hapo ni ukiwaona kawaida tu, iwe wameongozana barabarani au wamekaa sehemu! Raya alishajua kwamba kuna kitu kipo kati yangu na Shenaiza na kama hakipo basi kinakuja lakini kibaya zaidi, alikuwa amenifuma laivu nikimbusu msichana huyo!
>>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Uso wangu ulinishuka kwa haya, sikujua nitatumia maneno gani kumlainisha Raya, nikawa nazidi kuongeza mwendo kumfuata lakini ghafla nikahisi kitu kikinipasua pale kwenye jeraha langu kifuani ambalo japokuwa nilikuwa na nafuu kubwa, bado halikuwa limepona kabisa.
Licha ya maumivu niliyoyasikia, sikutaka kurudi nyuma, nilijikaza kisabuni na kuendelea kujikokota kumfuata Raya ambaye naye alizidi kuongeza mwendo, akiwa hataki hata kugeuka nyuma kunitazama. Nilivuka kwenye mlango wa kuingia kwenye ile wodi niliyokuwa nimelazwa, nikawa naendelea kumfuatilia Raya aliyekuwa akielekea kwenye geti la kutokea kwa kasi.
Hatua chache mbele nilishindwa kuendelea kumfuatilia baada ya kuhisi maumivu yakizidi pale kifuani kwenye jeraha, nikainama kidogo ule upande wenye jeraha, katika hali ambayo sikuitegemea, nilishtuka mno kugundua kuwa kumbe damu zilikuwa zikinitoka pale kwenye jeraha kiasi cha kulowanisha shati nililokuwa nimevaa.
Nilipogeuka nyuma, niliona michirizi sakafuni kuonesha kuwa kumbe damu ilianza kunitoka pale nilipohisi kitu kikinipasua kifuani, hofu kubwa ikatanda moyoni mwangu. Nikawa nahaha kutaka kujifuta damu na kuzifuta sakafuni kabla mtu yeyote hajaona maana ningeonekana mzembe nisiyejijali afya yangu na huenda madaktari wangenifokea sana lakini sikuwa na nguvu ya kufanya hivyo.
Niligeuka huku na kule kutazama kama kuna mtu alikuwa akiniangalia, pande zote hakukuwa na mtu yeyote zaidi ya Raya aliyekuwa akiishia kwa mbali, lakini nilipotazama kwenye mlango wa ile wodi niliyokuwa nimelazwa, macho yangu yaligongana na ya yule nesi ambaye kumbe muda wote alikuwa akitazama kila kilichokuwa kikiendelea, akiwa ametulia tuli.
>>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Nilishindwa cha kujibu zaidi ya kuendelea kuhaha huku na kule, yule nesi aliendelea kunitazama huku akitingisha kichwa kwa masikitiko. Maumivu yalinizidi, ikabidi niegemee kweye ukuta wa korido huku nikipumua kwa shida.
Harakaharaka yule nesi alikuja mpaka pale nilipokuwa nimeegemea ukuta lakini tofauti na nyakati zote, safari hii hakuwa akicheka wala kutabasamu, kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa ‘serious’.
“Help me please!” (Nisaidie tafadhali) nilisema huku nikiendelea kupumua kwa shida, hakunijibu kitu zaidi ya kunipa ishara kwamba nimshike begani, nikafanya hivyo, akapitisha mkono wake mmoja kiunoni kwangu, wa kwangu nikaupitisha kwenye bega lake, akanisaidia kutembea kuelekea wodini huku damu zikiendelea kunitoka.
Yule nesi alinipeleka mpaka kitandani kwangu, akanisaidia kupanda na harakaharaka akanivua lile shati nililokuwa nimevaa, akatoka mbiombio na muda mfupi baadaye alirejea akiwa na kisinia kilichokuwa na vifaa vingi vya tiba.
Kimyakimya akaanza kunisafisha pale kweye jeraha, akanifungua bandeji iliyokuwa imeachia, akanipaka dawa ya kuzuia damu kutoka, akanifunga plasta na bandeji nyingine kisha akanipa dawa za kutuliza maumivu. Akachukua lile shati lililokuwa limeloa kwa damu na kutoka nalo.
Muda mfupi baadaye alirudi akiwa na fulana nyeupe, akanipa nivae huku pia akiwa na vifaa vya kupigia deki, wakati navaa ile fulana kwa umakini ili nisijiumize tena, yeye alikuwa akifuta damu harakaharaka pale chini ya kitanda changu, akaendelea kufuta mpaka kule koridoni nilikokuwa nimechafua.
Yaani hata kama ulikuwa unaumwa vipi, ukikutana na nesi wa namna hii, lazima upone, nilijihisi kuwa na bahati ya kipekee kuhudumiwa naye. Ile fulana aliyonipa nivae ambayo hata sikujua ameipata wapi, ilikuwa imepuliziwa manukato mazuri yaliyofanana na yale aliyokuwa amejipulizia mwilini mwake, nikajisikia raha fulani ndani ya moyo wangu, nikabaki sina la kusema zaidi ya kumshukuru ingawa mwenyewe wala hakunijibu chochote.
Aliendelea kusafisha mpaka nje, aliporudi wodini, niligundua kwamba kumbe wakati akinisaidia kuniingiza wodini, nilimchafua gauni lake jeupe kwa damu, nikazidi kujihisi kua na hatia kubwa. Kumbe na yeye alishagundua kwamba nimemchafua, bila kuzungumza chochote alienda mpaka kwenye chumba cha manesi na kubadilisha gauni, akarudi akiwa amevaa gauni jingine safi.
Kama ilivyokuwa mwanzo, hakutabasamu wala kucheka, hata yale masihara yake hayakuwepo tena, nikahisi nimemkwaza sana kwa nilichokifanya. Alinisogelea pale kitandani, akanipima joto la mwili wangu kisha nikamsikia akishusha pumzi ndefu.
>>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
Bila kuzungumza chochote, alienda kukaa kwenye meza iliyokuwa inatazamana na mlango, nikamuona akifunua mafaili mengi, akawa anajaza vitu ambavyo sikujua ni nini, nilihisi ni katika kutimiza majukumu yake ya kazi. Aliendelea kuwa kimya huku mara kwa mara akinitazama kwa kunikazia macho, nikimtazama anakwepesha macho yake na kujifanya hakuwa ananitazama, na mimi nikawa najifanya kama simuoni.
Japokuwa alikuwa ameamua ‘kunichunia’, moyoni nilishukuru kwa msaada alionipa kwani muda mfupi baadaye, yale maumivu yalitoweka kabisa na zile damu nazo zikaacha kutoka, moyoni nikajiapiza kwamba sitainuka tena kitandani mpaka kidonda kikauke kabisa.
Nikiwa pale kitandani, nilizama kwenye dimbwi la mawazo kuhusu mfululizo wa matukio yale yaliyonitokea maishani mwangu mpaka wakati huo, nilikuwa na shauku kubwa ya kupona haraka ili niende kule nilikoelekezwa na Shenaiza kwamba nitakutana na mdogo wake atakayenipa bahasha yenye maelezo ya nilichokuwa nakitafuta.
Hata hivyo, niliamua kujipa muda kidogo ili nipone kidogo na mwili wangu upate nguvu, mawazo mengi yakawa yanaendelea kukizunguka kichwa changu. Niliendelea kujiuliza maswali mengi kuhusu ule ulimwengu mwingine niliouona na maajabu yake, pia jinsi nilivyokuwa naweza kutoka kwenye mwili wangu halisi na kukaa pembeni kisha nikaanza kujitazama mwenyewe.
Ndani ya kipindi kifupi tu nilikuwa nimetokewa na matukio mengi ya kutisha na kustaajabisha ambayo hakuna ambaye angeweza kuniamini endapo ningemsimulia na ndiyo maana mwenyewe niliamua kubaki nayo moyoni, mtu pekee ambaye nilitaka nipate muda wa kutosha kuzungumza naye, alikuwa ni Shenaiza ambaye naye alionesha kutokewa na hali kama na iliyokuwa nayo mimi.
“Umefahamiana vipi na yule dada aliyelazwa kwenye wodi ya vichaa?” aliniuliza swali yule nesi lililonizindua kutoka kwenye lindi la mawazo, nilipogeuka na kumtazama, alionekana kuwa bize na simu yake ya kisasa, nikashusha pumzi ndefu na kuendelea kumtazama.
“Si naongea na wewe Jamal?” alisema, nikashtuka zaidi alipolitaja jina langu kwa ufasaha mno, kama vile linavyotakiwa kuitwa, tofauti na watu wengi waliokuwa wakilikosea.
“Ni rafiki yangu tu.”
“Baba yake unamjua?” aliniuliza swali lingine ambalo liliufanya moyo wangu ulipuke paah! Tayari alikuwa amesimama na kunisogelea pale kitandani, ule ‘u-serious’ wake ukawa umepungua kiasi. Alionesha kama kuna jambo muhimu anataka kuniambia kuhusu Shenaiza na baba yake ingawa sikujua ni jambo gani.
“Ha..pa…na! Hapana!” nilijibu kwa kubabaika huku nikiwa makini kutaka kusikia ataniambia nini.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 31:

ILIPOISHIA:
Alionesha kama kuna jambo muhimu anataka kuniambia kuhusu Shenaiza na baba yake ingawa sikujua ni jambo gani.
“Ha..pa…na! Hapana!” nilijibu kwa kubabaika huku nikiwa makini kutaka kusikia ataniambia nini.
SASA ENDELEA…
“Kuwa makini, baba yake siyo mtu mzuri,” alisema nesi huyo ambaye baadaye nilikuja kugundua kwamba anaitwa Shamila.
“Unamaanisha nini?” nilimuuliza kwa sauti ya chini, akanisogelea zaidi na kukaa pembeni ya kitanda changu.
“Kuwa tu makini, nakupenda na sitaki jambo lolote baya likutokee,” alisema huku akinitazama kwa macho yake mazuri, macho yetu yakagongana. Tulitazamana kwa sekunde kadhaa, akakwepesha macho yake huku aibu za kikekike zikiwa zimetawala uso wake.
“Ahsante kwa kunisaidia kunifunga upya jeraha langu,” nilimwambia tena, nikamuona akitabasamu kisha akanishika mkono wangu.
“Usijali, hiyo ni kazi yangu ila inabidi uijali afya yako. Hata kama angekuwa ni mgonjwa mwingine, ningemsaidia kama nilivyokusaidia wewe.”
“Ahsante pia kwa fulana uliyonipa, ni nzuri na inanukia vizuri,” nilimwambia kwa sauti ya chini, akatabasamu tena na kuniambia:
“Nilijinunulia hiyo fulana kama zawadi siku ya Valentine Day.”
>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Kwa nini ujinunulie mwenyewe zawadi katika siku muhimu kama hiyo? Kwani shemeji hakukupa zawadi?”
“Shemeji? Shemeji gani? Niliamua kujionesha upendo mwenyewe.
“Unataka kusema msichana mrembo kama wewe unaweza kuwa huna mtu?”
“Huwezi kuamini, sina mtu yeyote karibia mwaka unaelekea kuisha sasa. Niliyekuwa naye aliniumiza sana moyo wangu na kunifanya niyachukie mapenzi,” alisema Shamila kwa sauti ya upole, nikawa namtazama usoni alivyokuwa anaongea.
“Mbona unaniangalia sana usoni? Mi nasikia aibu bwana,” alisema huku akiniachia mkono wake na kusimama, aibu zikiendelea kutawala uso wake.
“You are so beautiful Shamila!” (Wewe ni mrembo sana Shamila) nilimwambia, akacheka sana na kurudi tena kukaa pale pembeni ya kitanda changu, akaniambia zimepita siku nyingi hajasikia kauli kama hiyo kutoka kwenye kinywa cha mwanaume mzuri kama mimi, wote tukacheka na kugongesheana mikono.
Kuna jambo kubwa lilikuwa limebadilika maishani mwangu, kwa kipindi kirefu sikuwa na mazoea ya kukaa karibu na wasichana wala kupiga nao stori.
Mtu pekee niliyekuwa nimezoeana naye alikuwa ni Raya ambaye hata hivyo mara kwa mara nilikuwa nikimkwepa lakini cha ajabu, katika siku za karibuni, nilijikuta nikivutiwa na wasichana wawili, Shenaiza na sasa Shamila, achilia mbali Raya ambaye tayari tulishaanza naye uhusiano wa kimapenzi.
Hata ujasiri wa kuzungumza pia ulikuwa umeongezeka. Nikaendelea kupiga stori za hapa na pale na Shamila, nikawa namchangamsha kwa sababu nilijua kuna jambo nilikuwa nimemkera lakini pia nilitaka kumuingia ili nipate habari kumhusu Shenaiza na baba yake kwani ilionesha kwamba nesi huyo anawajua vizuri.
“Hujaniambia ubaya wa baba yake Shenaiza, kwani amefanya nini?”
“Tuachane na hayo, usije ukaenda kumwambia binti yake bure, inaonesha unampenda sana. Hivi nikuulize, kwani wewe una wapenzi wangapi?”
“Nijibu kwanza swali langu na mimi nitakujibu la kwako. Ubaya wa baba yake Shenaiza ni upi?” nilimkomalia Shamila, akashusha pumzi ndefu na kugeuka huku na kule kama anayehakikisha kwamba hakuna mtu aliyekuwa akitusikiliza.
“Anafanya biashara za hatari sana, siyo mtu mzuri hata kidogo.”
“Biashara za hatari ndiyo biashara gani? Anauza madawa ya kulevya?”
“Si bora hata angekuwa anauza madawa ya kulevya! We elewa kwamba anafanya biashara za hatari sana, kama huamini endelea kumchunguza taratibu.”
“Nitamchunguza vipi wakati hata simfahamu?”
>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Humfahamu?” aliniuliza Shamila kwa mshangao, nikamhakikishia kwamba simfahamu kabisa. Aliniambia inawezekanaje nikawa na ukaribu na Shenaiza lakini nisimfahamu baba yake? Sikuwa na cha kumjibu lakini ukweli ni kwamba sikuwa nimewahi kumuona zaidi ya kusikia tu habari zake.
Akaniambia kuwa muda mwingi huwa hakai nchini na hata akija, huwa haonekani kwa urahisi. Nikamuuliza yeye amemfahamia wapi? Akanijibu kwamba huwa anakuja mara kwa mara hospitalini hapo kwa sababu ana marafiki wengi ambao ni madaktari.
“Kwani na yeye ni daktari?”
“Hapana.”
“Sasa iweje awe na marafiki madaktari?” nilimuuliza, akashusha pumzi ndefu na kuniambia kwamba ana urafiki nao kwa sababu huwa anashirikiana na baadhi yao wasio waaminifu kwenye hizo biashara zake.
Nilijaribu kumbana aniambie ni biashara ya namna gani anayofanya na madaktari lakini hakuwa tayari kuniambia chochote kwa maelezo kwamba anahofia maisha yake. Nilimbana sana lakini alikataa katakata kuniambia zaidi ya kunitaka niendelee kufuatilia mwenyewe nitaujua ukweli.
Kiukweli alinichanganya kichwa lakini alinipa mwanga. Ukichanganya na yale maelezo ya Shenaiza, tayari nilikuwa na sehemu ya kuanzia, nikajiapiza ndani ya moyo wangu kwamba ni lazima nitaujua ukweli na nitafanya kazi niliyotumwa, ya kumzuia kuendelea kufanya alichokuwa anakifanya japokuwa sikujua ni kitu gani.
Ni kazi ambayo nilipewa nikiwa kule kwenye ulimwengu mwingine kama masharti ya kurejea kwenye ulimwengu wa kawaida. Sikujua nitafanya nini lakini nilichojiapiza ni kwamba ilikuwa ni lazima nifanikiwe kumzuia alichokuwa anakifanya.
“Mbona kama umezama kwenye dimbwi la mawazo?” Shamila aliniuliza na kunizindua kutoka kwenye mawazo mazito, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni.
“Haya na wewe nijibu maswali yangu!” alisema Shamila huku tabasamu likianza kuchanua kwenye uso wake. Jambo ambalo sikuwa na uhakika nalo, ni juu ya uchangamfu wa Shamila. Sikujua huwa anachangamka hivyohivyo akiwa na watu wengine au ni kwangu tu.
“Nimekuuliza una wapenzi wangapi?”
“Mmoja tu, anaitwa Raya, yule niliyekuwa namkimbilia muda ule.”
“Muongo wewe, na Shenaiza?”
“Shenaiza siyo mpenzi wangu, ni rafiki yangu tu.”
“Rafiki yako ndiyo mna-kiss? Yaani hamjifichi kabisa, inaonesha ni mpenzi wako.
“Siyo mpenzi wangu, kweli tena,” nilimwambia Shamila lakini akaendelea kukataa, akaniambia hata Shenaiza mwenyewe alikuwa akiwaambia manesi kwamba mimi ndiyo mpenzi wake na tuna mipango ya kuja kufunga ndoa, kauli iliyonishangaza sana.
Shamila aliendelea kunishutumu kwamba sijatulia, naonesha nina wanawake wengine wengi na ndiyo maana nashindwa kuwathamini watu wanaonipenda kwa dhati. Sikuelewa msingi wa lawama zake ni nini kwa sababu mimi na yeye ndiyo kwanza tulikuwa tumejuana, akaendelea kuniambia kwamba kwa sababu sijatulia nitakosa vitu vizuri.
Akaonesha kususa na kutoka wodini kwa hasira, akaniacha nikiwa na maswali mengi yaliyokosa majibu, wakati anatoka mlangoni, alipishana na Raya aliyekuwa akiingia akiwa na kikapu ambacho hata bila kuuliza nilijua kwamba kina chakula. Nilipomtazama usono, macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kuonesha kwamba alikuwa amelia kwa muda mrefu, hata ule uchangamfu wake haukuwepo tena. Macho yake yakatua kwenye fulana niliyokuwa nimevaa, akanikazia macho.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 32

ILIPOISHIA:
Nilipomtazama usoni, macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kuonesha kwamba alikuwa amelia kwa muda mrefu, hata ule uchangamfu wake haukuwepo tena. Macho yake yakatua kwenye fulana niliyokuwa nimevaa, akanikazia macho.
SASA ENDELEA…
“Umebadilisha nguo saa ngapi? Na hiyo fulana umeipata wapi mbona inanukia pafyumu ya kike?” alinihoji Raya uso akiwa ameukunja, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni, huku nikiuvaa ujasiri wa kiume.
“Yaani hiyo ndiyo salamu? Ama kweli mapenzi yamepungua, kwa hiyo hata nikifa huwezi kujali tena?” ilibidi nimgeuzie kibao Raya. Moyoni nilikuwa najua kwamba nakosea lakini ilikuwa ni lazima nifanye hivyo ili kutuliza hali ya mambo.
“Wewe ndiyo wa kunitamkia mimi maneno hayo? Nikupende vipi Jamal, kwa nini unautesa moyo wangu?” alisema Raya na kuanza kuangua kilio. Kauli yangu ni kama ilikuwa imeenda kutonesha donda ndani ya nafsi yake.
Nilijisikia vibaya lakini ikabidi niendelee ‘kumkazia’, nikamwambia wakati anaondoka kwa kususa, nilikuwa nikimfuata lakini kwa bahati mbaya nikaanguka na kusababisha jeraha langu lifumuke na kuanza kumwaga damu.
“Huoni kwamba nimefungwa plasta na bandeji upya? Kama huamini muulize yule nesi, amenisaidia sana, huenda sasa hivi ungekuja na kukuta stori nyingine,” nilimwambia Raya, kauli ambayo ilionesha kumshtua mno.
>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Mungu wangu, kwani ilikuwaje?” alisema Raya huku akikaa pembeni ya kitanda changu, akawa anajifuta machozi huku akionesha kushtushwa mno na nilichomweleza, nikamwambia shati langu lilikuwa halitamaniki kwa damu na kwamba hiyo fulana nilikuwa nimesaidiwa tu na msamaria mwema.
Maskini Raya! Alianza kujihisi kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wake, ule moto aliokuja nao ukazimika, akaanza kunipa pole na kuniomba msamaha kama ameniudhi! Yaani japokuwa mimi ndiyo nilikuwa na makosa, yeye ndiyo alikuwa akiniomba msamaha!
Nilimkubalia na kumuomba apunguze wivu kwa sababu nampenda yeye peke yake na ukaribu wangu na Shenaiza ulikuwa ni kwa sababu maalum tu. Hakutaka tena kuendelea kulizungumzia suala hilo, akili yake yote akaielekeza kwangu kuhakikisha nakula vizuri chakula alichokuwa ameniandalia.
Nilikifurahia chakula alichokuwa ameniandalia, nikala vizuri na kumfanya na yeye afurahi, nikamshukuru kisha akatoa vyombo na kuvirudisha kwenye kikapu chake, akasafisha kila kitu pale kitandani kwangu kisha akakaa tena pembeni yangu, mkono wake mmoja ukiwa kwenye mwili wangu, mara kwa mara akawa ananibusu kwa mahaba mazito.
“Niambie kama kweli unanipenda Jamal!”
“Nakupenda sana Raya na kwangu wewe si tu mpenzi, bali mke mtarajiwa, namshukuru Mungu kwa kukuleta karibu yangu,” nilimwambia, nikamuona akitabasamu.
Maneno yangu matamu yalienda kumaliza kila kitu, nikaendelea kumpamba, akawa anacheka kwa furaha utafikiri siyo yule aliyeingia macho yakiwa yamemvimba na kuwa mekundu kwa kulia. Nikawa nimefanikiwa kabisa kumsahaulisha mabaya yote.
Mpaka muda wa kuondoka unafika, Raya alikuwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake, akaniaga kwa kunimwagia mvua ya mabusu na kuniambia kwamba anatamani angelala na mimi wodini lakini kwa kuwa sheria haziruhusu, tutaonana asubuhi ya siku inayofuatia, akaondoka zake.
“Huyo ndiyo Raya?”
“Ndiyo! Vipi kwani mbona umeniuliza hivyo?”
“Aah, nilitaka tu kumjua vizuri,” nesi Shamila aliongea huku akionesha kabisa kuwa na kinyongo ndani ya moyo wake. Kumbe muda wote wakati nikizungumza na Raya, alikuwa kwenye ofisi ya manesi akitusikiliza kila kitu kwa mbali, akajikausha kama hayupo mpaka Raya alipoondoka.
“Kumbe hanizidi kwa uzuri, tena isitoshe mimi tayari nina kazi, naishi kwangu na kuendesha maisha yangu bila tatizo lolote. Mwanaume atakayenioa atafaidi sana,” Shamila alijipigia debe, nikawa nimeshamuelewa kwa nini anasema vile, nikakosa hata cha kumjibu.
“Si naongea na wewe mbona hunijibu?”
“Sasa nitakujibu nini Shamila? Ndiyo maana nimebaki kimya,” nilimwambia kwa upole. Sikutaka kumuudhi kwa sababu naye alikuwa na umuhimu mkubwa kwenye maisha yangu, katika kipindi hicho nilichokuwa hospitalini hapo chini ya uangalizi wake.
Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale, mara kwa mara akimtoa kasoro Raya na kujisifia, nikawa namuunga mkono kwa sababu kama nilivyosema sikutaka kumuudhi na kubwa zaidi, nilikuwa nataka kumtumia kufahamu mambo mengi zaidi kuhusu baba yake Shenaiza.
“Hivi ukiniangalia unahisi nitaruhusiwa lini kutoka?”
>>Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi
“Mh! Yaani wewe unafikiria kutoka? Unajiona umeshapona siyo? Unajua wewe unashangaza sana!”
“Nashangaza kivipi?”
“Hivi unajua tangu ulipoletwa hapa hospitalini na kulazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, ulikaa siku ngapi bila kurudiwa na fahamu zako?” Shamila aliniuliza.
“Sasa kwani kuna uhusiano gani kati ya nilichokuuliza na hayo unayoyasema?”
“Nakuona una mambo mengi sana. Ndiyo kwanza umerudiwa na fahamu zako lakini hutulii, mara uinuke kitandani, mara umkimbilie huyo Raya wako, mara uende wodini kwa Shenaiza na sasa hivi unaulizia siku ya kutoka,” alisema Shamila, nikaona ni kama alikuwa amenipania.
Nilijua nini kilichokuwa kikimsumbua ndani ya moyo wake. Ni kweli sikuwa na muda mrefu tangu nirejewe na fahamu lakini kwa kuwa mwili wangu ulikuwa na nguvu, sikuona sababu ya kuendelea kupoteza muda, hasa ukizingatia kwamba kuna kazi kubwa ilikuwa inanisubiri.
“Hata madaktari wenyewe nikiwaeleza hizo hekaheka ulizonazo, watashauri uwe unachomwa sindano za usingizi muda wote ili uendelee kupumzika, sijawahi kuona mgonjwa msumbufu kama wewe,” Shamila alizidi kunishukia.
Nisingeweza kuendelea kusubiri wodini hapo eti mpaka niruhusiwe na madaktari, kitu pekee nilichoona ni kikwazo kwangu kufanya kazi niliyotumwa, niliona ni lile jeraha la kifuani tu ambalo nilikuwa nimelitonesha.
Hayo mambo ya kupoteza fahamu hayakuniingia akilini kwa sababu kwanza siyo kweli kwamba nilipoteza fahamu na kulala tu kitandani nikiwa sielewi kinachoendelea bali kilichokuwa kimetokea ilikuwa ni kama tu kuhama kutoka ulimwengu mmoja mpaka mwingine.
Jambo ambalo kwa mtu mwenye akili alipaswa kujiuliza, hivi inawezekana vipi mtu aliyekuwa amepoteza fahamu, awe na pilikapilika nyingi muda mfupi baada ya kurejewa fahamu hizo kama mimi?
Yaani mtu umetolewa leo kwenye mashine ya kukusaidia kupumua ukiwa mahututi halafu saa chache baadaye unaweza kusimama na kutembea mwenyewe kutoka wodi moja hadi nyingine? Kulikuwa na siri kubwa iliyojificha ndani ya moyo wangu.
Kwa jinsi Shamila alivyoanza kunibadilikia kwa sababu ya wivu wake wa kimapenzi, niliona njia nyepesi ya mimi kupata kile nilichokuwa nakitaka, ni kumuingiza kwenye mtego wa mapenzi, kwamba nijifanye nampenda sana yeye kuliko Raya, nimuaminishe kwamba atakuwa mpenzi wangu ili nimtumie vizuri kupata kile nilichokuwa nakitaka.
Ilikuwa ni lazima kesho yake niende kule nilikoelekezwa na Shenaiza kukutana na mdogo wake anipe hiyo bahasha yenye maelezo yote kuhusu kilichokuwa kinafanywa na baba yake lakini hilo lingewezekana tu kama ningekula njama na Shamila, ikabidi nianze kucheza na akili yake.
“Lakini Shamila, kwa nini unaongea na mimi kwa ukali kiasi hicho? Au nimekosea kukuonesha hisia zangu kwamba nakupenda?” nilimwambia, nikamuona akishtuka kuliko kawaida, akanitazama kwa macho yake mazuri.
“Kwani umewahi kuwa na hisia za kunipenda Jamal?” alinihoji, safari hii kwa sauti ya chini na ya upole, akawa ananisogelea pale kitandani huku akinitazama kwa macho yaliyobeba hisia nzito.
“Nakuapia kama ningekutana na wewe kabla ya Raya, huenda wewe ndiyo ungekuwa mpenzi wangu na si ajabu ningeshakuwa nimekuoa, naogopa kukueleza ukweli wa moyo wangu kwa sababu mtu mwenyewe unakuwa mkali kwangu,” nilizidi kumseti kwa maneno matamu, akashindwa kujizuia na kuniinamia pale kitandani, akanibusu kwa hisia za hali ya juu na kunikumbatia bila kujali kwamba anaweza kunitonesha tena jeraha langu la kifuani.
Je, nini kitafuatia? Usikose next
 
SEHEMU YA 34


ILIPOISHIA:
“Nakuapia kama ningekutana na wewe kabla ya Raya, huenda wewe ndiyo ungekuwa mpenzi wangu na si ajabu ningeshakuwa nimekuoa, naogopa kukueleza ukweli wa moyo wangu kwa sababu mtu mwenyewe unakuwa mkali kwangu,” nilizidi kumseti kwa maneno matamu, akashindwa kujizuia na kuniinamia pale kitandani, akanibusu kwa hisia za hali ya juu na kunikumbatia bila kujali kwamba anaweza kunitonesha tena jeraha langu la kifuani.
SASA ENDELEA…
“Hata mimi nakupenda sana Jamal lakini nilikuwa nashindwa namna ya kukufikishia ujumbe, ahsante kwa kuzielewa hisia zangu,” alisema Shamila huku akiwa amenikumbatia, akaendelea kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu.
Niliona jinsi kitendo changu cha kuingiza masuala ya mapenzi kilivyomfurahisha, tukaendelea kupiga stori mbalimbali huku mara kwa mara akinikumbatia na kunibusu, na mimi nikawa nazidi kumsifia kwani miongoni mwa ‘maradhi’ ya wanawake, ni kupenda kusifiwa! Dalili za kutimia kwa nilichokuwa nakitaka zikaanza kuonekana waziwazi.
Hatukuwa nesi na mgonjwa kama ilivyokuwa awali, sasa tukawa zaidi ya hapo, nikamuona Shamila akizidi kuninyenyekea, kunipa huduma bora zaidi na muda mwingi akiwa pembeni ya kitanda changu.
Sikujihisi tena kama niko hospitali, ungeweza kusema nipo tu nyumbani. Japokuwa siku hiyo Shamila alikuwa na ‘shift’ ya kutoka saa kumi na mbili jioni, hakutaka kuondoka, akaniambia kwamba ataenda kuongea na kiongozi wao ambadilishie zamu, alale tena kazini mpaka kesho yake ndiyo arudi nyumbani.
“Nimechoka kukaa hospitali mpenzi wangu, naona kama kuna mambo ya muhimu yanazidi kuchelewa, sijui utanisaidieaje?” nilimwambia Shamila, akiwa amekaa pembeni yangu, muda wote mikono yake ikiwa mwilini mwangu.
“Kwani unataka kwenda kufanya nini Jamal, mi nakuonea huruma bado hujapona vizuri. Kuna kazi ya muhimu inatakiwa nikaifanye.”
“Kwa nini usiniagize mimi nikakufanyie?”
“Hapana, ni lazima niifanye mimi mwenyewe labda kama utanisindikiza tu.”
“Lakini bado hujapona.”
“Kwani haiwezekani nikatoka asubuhi halafu baadaye nikarudi?”
“Sasa madaktari wakipita ‘raundi’ na kukukosa wodini itakuwaje? Si unajua wewe bado unatakiwa kuwa chini ya uangalizi maalum na ndiyo maana umeletwa huku kwenye wodi ya peke yako mpenzi?” alisema Shamila.
Kimsingi hakukuwa na uwezekano wowote wa mimi kutoka kirahisi hospitalini lakini nikaona niendelee kumbembeleza Shamila. Kwa kuwa sasa nilikuwa mpenzi wake na nilishaanza kumpa ahadi kemkemu kuhusu maisha yetu ya kimapenzi yatakavyokuwa, nilifanikiwa kumteka akili.
“Basi kesho inabidi mimi asubuhi nisiondoke mapema, nitasubiri mpaka madaktari wakishapita raundi wodini tu, tutaondoka wote mpaka nje ya hospitali. Nitawaambia walinzi umeandikiwa vipimo ambavyo hapa hospitalini havipo,” alisema Shamila, nikaachia tabasamu pana.
Waliosema mapenzi yana nguvu hawakukosea. Shamila alikuwa tayari kuhatarisha kazi yake kwa sababu ya kutetea penzi! Basi tulifikia muafaka, ukaribu wa mimi na Shamila ukazidi kuongezeka utafikiri tulifahamiana miaka mingi iliyopita.
Hata yale masihara aliyokuwa ananiletea awali, nikaona yamepungua sana, muda mwingi akawa anapenda tuzungumzie kuhusu penzi letu. Unajua wanaume wengi huwa wanafanya makosa sana kushindwa kufahamu namna ya kuishi na mwanamke ambaye anaonesha hisia za kukupenda.
Tofauti na wanaume ambao akimpenda mtu huweza kumwambia moja kwa moja kwa ujasiri, wanawake huwa hawana ujasiri huo labda wachache. Kama mwanamke anakupenda, kuna baadhi ya dalili atakuwa anakuonesha akiamini ukiziona, utajiongeza mwenyewe kichwani.
Ukishaziona dalili hizo, hata kama huna malengo ya kuanzisha naye uhusiano wa kimapenzi, kuna namna ya kumuonesha kwamba umemuelewa hata kabla hajatamka chochote na kwamba unaziheshimu hisia zake.
Ikitokea anakuonesha dalili fulani lakini wewe unaendelea kujifanya kipofu, kihulka wanawake ni wepesi sana wa kujisikia vibaya, atahisi umemdharau, ataamini hajakuvutia ndiyo maana umeshindwa kuelewa hisia zake na mwisho utashangaa anaanza kujitenga mbali na wewe na kukujengea chuki.
Kwangu mimi niliamua kupiga ndege wawili kwa mpigo kwa Shamila, japokuwa kiukweli hakuwepo kwenye mawazo yangu kwa sababu tayari nilishaamua kumkabidhi moyo wangu Raya, niliamua kumuonesha kwamba nampenda sana kwa sababu mbili; kwanza sikutaka ajisikie vibaya kwamba ananionesha ishara kwamba ananipenda lakini nampuuza lakini kubwa, nilitaka anisaidie kwenye ile kazi kubwa iliyokuwa inanisubiri.
Malengo yangu yalianza kutimia haraka kuliko hata nilivyotegemea kwa sababu tayari jambo moja muhimu lilikuwa likienda kutimia; kwenda kuonana na Firyaal, mdogo wake Shenaiza ambaye angenipa bahasha yenye taarifa kuhusu baba yao na biashara hatari alizokuwa anazifanya.
Usiku huo Shamila wala hakwenda kukaa kwenye chumba cha manesi kama utaratibu ulivyo, muda wote alikuwa na mimi wodini na hata muda wa kulala ulipofika, alisogeza kitanda tupu kilichokuwa pembeni karibu kabisa na kitanda changu, akajilaza juu yake huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale mpaka nilipopitiwa na usingizi.
Kesho yake asubuhi, Shamila aliwahi kuamka na kuniamsha na mimi, akanisaidia kubadilisha shuka pale kwenye kitanda changu, akaniandalia mswaki na taulo na kuniambia inatakiwa nikaoge ili nipate nguvu. Akanisisitiza kwamba nihakikishe maji hayagusi kwenye jeraha langu.
Nilijikaza na kuamka, nikaenda bafuni ambako nilioga kwa mara ya kwanza tangu nirudiwe na fahamu zangu, nikajisikia mwili ukipata nguvu kubwa, nikarudi wodini ambako nilikuta Shamila akiandaa kahawa, niliporudi kitandani tukakaa pamoja na kuanza kunywa, sote tukachangamka.
Baadaye madaktari walipita kwa ajili ya kutazama maendeleo yangu, wakafurahishwa sana na jinsi nilivyokuwa nikipona haraka, wakawa wanampongeza Shamila kwamba amefanya kazi yake ipasavyo ndiyo maana nilikuwa napona haraka, wote tukafurahi.
“Bila shaka sasa unaweza kutusimulia kuzimu kulivyo maana naamini ulifika na kukutana na mtoa roho ila akaamua kukusamehe tu,” alisema yule daktari kijana aliyezoea kunitania, wote tukacheka.
Nikaandikiwa dawa nyingine za kukausha jeraha langu kisha wakaondoka na kuendelea kuwatembelea wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye wodi nyingine, Shamila akanitazama, macho yetu yakagongana, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kunisogelea huku akitabasamu.
“Sasa itabidi uwe makini sana, mtu yeyote akituuliza tunaelekea wapi utamjibu kwamba nakufanyisha mazoezi, sawa?” Shamila aliniambia kwa sauti ya mamlaka, nikatingisha kichwa kuonesha kukubaliana naye.
Tukajiandaa kisha akachukua mkoba wake, tukatoka taratibu huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale. Kwa kuwa Shamila alikuwa akifahamika hospitalini hapo, hatukupata usumbufu wowote, tukatoka mpaka nje kabisa ya geti bila kuulizwa chochote na mtu yeyote.
Tukaenda mpaka kwenye maegesho ya teksi, madereva wakatudaka juujuu na kuanza kutukaribisha, tukaingia kwenye teksi moja kisha Shamila akanigeukia.
“Tunaanzia nyumbani kwangu, sawa?”
“Hapana, naomba kwanza twende Kurasini halafu ndiyo tutaenda kwako, niko chini ya miguu yako nakuomba,” nilimwambia, akanitazama kwa macho yake mazuri na kutingisha kichwa kuonesha kukubaliana na nilichokisema.
“Naomba tupeleke kwenye Mtaa wa Mama Zayumba, Kurasini,” Shamila alimwambia dereva huyo. Alishakuwa anaujua mpaka mtaa kwa sababu aliniuliza na nikamuelekeza kama na mimi nilivyokuwa nimeelekezwa na Shenaiza, safari ikaanza.
Safari iliendelea na hatimaye tukawasili kwenye mtaa huo ambao ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika, tukafuata ramani aliyonipa Shenaiza na hatimaye tukatokezea kwenye jengo la kisasa la ghorofa tatu, likiwa na geti kubwa lililozungushiwa nyaya zinazopitisha umeme upande wa juu huku kukiwa na mlinzi mwenye silaha.
Tukasogea na teksi mpaka jirani kabisa na lile geti, yule mlinzi akamuonesha dereva ishara ya kusimama kisha akatusogelea na kutusabahi,mimi nidyo nikawa mzungumzaji mkuu.
“Nikajitambulisha kwamba ni rafiki yake Shenaiza na kuna kitu alikuwa amenituma kuja kukichukua kwa mdogo wake, Firyaal. Kwa jinsi nilivyompa maelezo, wala hakututilia mashaka, hasa alipomuona pia Shamila akiwa amevaa nguo zake za kazini, akajua tumetoka kuonana na Shenaiza hospitalini.
Nikamuona akiingia kwenye chumba cha walinzi na kushika mkonga wa simu, akawa anazungumza na upande wa pili kisha akarudi pale tulipokuwa tumepaki gari na kutuambia tusubiri hapohapo. Tulikaa kwa zaidi ya dakika tatu, tukaona mlango mdogo uliokuwa pembeni ya geti ukifunguliwa, wote tukakazia macho kutaka kuangalia ni nani aliyekuwa anatoka.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 35

Harakaharaka tukatoka na kuingia ndani ya teksi, safari ya kurudi hospitalini ikaanza huku muda wote Shamila akiwa na furaha ya ajabu, akawa ananimwagia mvua ya mabusu. Dakika kadhaa baadaye, tuliwasili hospitalini lakini mazingira ya pale yalinishtua mno, hofu kubwa ikaukumba moyo wangu tulipofika kwenye maegesho ya magari.
SASA ENDELEA…
Gari jeusi lililokuwa na vioo vya rangi nyeusi (tinted), Isuzu Bighorn lilikuwa limepaki kwenye maegesho hayo huku milango ya upande mmoja ikiwa wazi. Kumbukumbu zangu zilionesha kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kuliona gari hilo machoni mwangu, nikawa najaribu kukumbuka ni wapi?
Shamila alimlipa dereva teksi na kutaka kushuka lakini nikamzuia, akabaki anashangaa. Niliendelea kulitazama lile gari na kwa makini, ghafla kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu baada ya kumuona mmoja kati ya watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
Alikuwa ni kijana mmoja mwenye asili ya Bara la Asia, ambaye rangi ya ngozi yake ilikuwa ikifanana sana na ya Shenaiza pamoja na mdogo wake, kuonesha kwamba walikuwa na aina fulani ya unasaba kati yao. Nilipozidi kumtazama, nilimkumbuka kwamba mimi na yeye tulikutana kwenye matukio mawili tofauti, tena yote ya hatari yakimhusisha Shenaiza.
Tukio la kwanza lilikuwa ni siku nilipokuwa najaribu kumtorosha Shenaiza hospitalini, kipindi hicho wakati ndiyo kwanza tumeanza kufahamiana. Tukio la pili, ambalo liliyafanya mapigo ya moyo wangu yaniende kasi kuliko kawaida.
Lilikuwa ni tukio ambalo almanusra liukatishe uhai wangu baada ya kuvamiwa na watu nisiowafahamu kwenye foleni, maeneo ya Magomeni Mataa ambao walinishambulia vikali na kunijeruhi vibaya na kitu chenye ncha kali kifuani.
“Ni yeye! Ni mwenyewe…” nilijikuta nikitamka kwa nguvu, Shamila na yule dereva teksi wakabaki kunishangaa, wakiwa hawaelewi nilichokuwa namaanisha.
“Upo sawa kweli? Kama kuna tatizo si uniambie mpenzi?” alisema Shamila huku na yeye akiwa makini kutazama kule nilikokuwa naangalia, ghafla nikamuona amekazia macho pale kwenye lile gari, naye akawa ni kama ameona kitu.
Kwa bahati nzuri, ile teksi tuliyopanda ilikuwa pia na vioo vyenye tinted kwa hiyo haikuwa rahisi kwa watu waliokuwa nje kutuona. Tulitulia kwa dakika kadhaa, wote tukiwa tunawatazama wale vijana ambao walionekana kama wanajadiliana kitu huku macho yao yote yakiwa upande zilipokuwepo wodi, hasa ile niliyokuwa nimelazwa mimi.
“Unawafahamu?”
“Ndiyo, wana ukaribu na Shenaiza na ndiyo waliohusika kwenye jaribio la kutaka kuyakatisha maisha yangu.”
“Sasa hapa watakuwa wamefuata nini?”
“Kuna mawili, wanaweza kuwa wamemfuata Shenaiza au wamenifuata mimi.”
“Wakufuate wewe? Kwa kipi hasa?”
“Nimeshakwambia kuwa ni hawa ndiyo walioshiriki kwenye jaribio la kutaka kuyakatisha maisha yangu, yule mmoja namkumbuka vizuri kabisa.”
“Basi kama ni hivyo kwa nini tusiwapigie simu walinzi wa hospitali wawasiliane na polisi na kuwakamata? Mimi nina namba za mlinzi wetu wa kule getini,” alisema Shamila huku akitoa simu yake lakini nikamzuia.
Yule dereva teksi aliendelea kutulia kama haelewi chochote kinachoendelea, tukaendelea kujadiliana mle ndani ya teksi kwa muda mrefu huku nikiwa nimekosa kabisa amani.
Hakuna kitu kibaya maishani kama kuwaona wabaya wako lakini ukawa huna namna ya kulipa kisasi, nikaamua kufuata ule usemi maarufu ambao Waingereza hupenda kuutumia; ‘dont hunt what you can’t kill’ wakimaanisha usiwinde usichoweza kukiua!
Tukiwa bado tumetulia pale kwenye gari, ghafla kwa mbali tulimuona mtu aliyekuwa amevalia mavazi ya kidaktari akitoka kwenye wodi niliyokuwa nimelazwa, akatazama huku na kule kama anayetafuta kitu kisha akatembea harakaharaka mpaka pale kwenye lile gari, akawa anazungumza na wale watu waliokuwa mle ndani ya lile gari huku mara kwa mara wakigeuka kutazama kama kuna mtu aliyekuwa akiwatazama.
“Mungu wangu, nini kinachoendelea hapa? Mbona huyu aliyevaa kama daktari siyo mfanyakazi hapa hospitalini?”
“Siyo daktari? Kivipi? Na kama siyo daktari mbona amevaa nguo za kidaktari na ameingia hadi wodini?”
“Niamini ninachokwambia, madaktari wote wa hapa nawafahamu, huyu siyo mfanyakazi,” alisema Shamila kwa kujiamini, nikaiona hatari kubwa iliyokuwa mbele yangu. Kwa tafsiri nyepesi, mtu huyo alikuwa akishirikiana na wale watu waliokuwa ndani ya gari.
Kilichozidi kunishangaza, aliwezaje kuingia mpaka ndani ya wodi niliyokuwa nimelazwa bila kugunduliwa na walinzi wa hospitali hiyo? Kama angekuwa na nia ya kunidhuru ingekuwaje?” nilijikuta kijasho chembamba kikinitoka.
Waliendelea kujadiliana pale kwenye gari kisha tukamuona yule aliyejifanya daktari akivua koti lake jeupe na kuliweka kwenye siti za nyuma za gari, akaingia kwenye gari, milango ikafungwa na gari hilo ambalo muda wote lilikuwa likinguruma taratibu bila kuzimwa (silencer), likaanza kurudi nyuma likitafuta upenyo wa kutoka kwenye maegesho hayo.
Muda mfupi baadaye, liliondoka kwa kasi kubwa huku likitimua vumbi bila kujali kwamba eneo hilo lilikuwa ni hospitali na kulikuwa na wagonjwa waliokuwa wakihitaji utulivu, nikashusha pumzi ndefu na kuegamia kwenye siti niliyokuwa nimekaa, Shamila naye akafanya hivyohivyo.
“Sasa itakuwaje?”
“Sipo tayari kuendelea kulazwa kwenye hii hospitali, ni bora nikafie mbele ya safari, hapa si sehemu salama tena,” nilimjibu Shamila, akawa anatingisha kichwa kuonesha kuniunga mkono kwa kile nilichokuwa nakisema.
Tukiwa bado ndani ya teksi ile, nilishtuka sana baada ya kumuona Raya akifungua mlango na kutoka kwenye ile wodi niliyokuwa nimelazwa, mkononi akiwa amebeba kikapu kilichokuwa na chakula, akionesha kuwa na huzuni kubwa ndani ya moyo wake.
Baada ya kutoka wodini, alikaa kwenye benchi lililokuwa pale nje na kuweka kikapu chake chini, akawa anatazama huku na kule huku akionesha kuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wake. Kwa kumtazama tu, japo nilikuwa kwa mbali, nilielewa kilichokuwa kikipita ndani ya kichwa chake, nikajikuta nikimuonea huruma sana.
Kumbe wakati nikimtazama Raya kwa huruma, Shamila naye alikuwa akinitazama usoni! Haya mambo ya mapenzi hatari sana, akashikwa na wivu mkali, akanizindua kwa kunigeuza kule nilikokuwa natazama na kunigeuzia kwake.
>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Uko sawa?” aliniuliza huku hisia kali za wivu zikijionesha waziwazi kwenye uso wake.
“Nitakuwaje sawa katika mazingira kama haya? Naomba unisaidie jambo, kamuulize Raya yule daktari feki alipoingia wodini amesemaje?” nilimwambia Shamila, akaendelea kunitazama machoni huku akionesha dhahiri kwamba kuna jambo alikuwa anataka kuniambia.
Kwa shingo upande alishuka na kutuacha mimi na dereva teksi ndani ya ile teksi, aliposhuka tu, nilimwambia dereva aloki milango, tukawa tunamtazama Shamila anavyotembea kwa maringo kuelekea kule nje ya wodi alikokuwa amekaa Raya.
“Vipi kaka ndiyo unakaa hapa nini?” aliniuliza yule dereva teksi kwa lugha za vijana, akimaanisha kama mimi ndiye niliyekuwa nikitoka kimapenzi na Shamila, nikashindwa cha kumjibu kwani kwa muda huo akili yangu ilikuwa ikienda ‘resi’ sana, akaendelea:
“Duh! Si mchezo, utakuwa unafaidi sana, bonge la kifaa, ningekuwa mimi ningetangaza ndoa kabisa!”
Alikuwa na haki ya kusema hivyo kwa sababu kama nilivyoeleza awali, Shamila alikuwa mwanamke aliyejaaliwa uzuri wa kipekee mno, ukichanganya na umbile lake lililojazia kwa nyuma, hakuna mwanaume ambaye amekamilika angeweza kupishana naye bila kugeuka mara mbilimbili.
Japokuwa alikuwa amevaa nguo zake za kazini, uzuri wake haukuweza kujificha, nikajikuta kwenye wakati mgumu kwani Raya nilikuwa nampenda na alikuwa na mapenzi ya dhati kwangu, ukichanganya pia kwamba mimi ndiye niliyekuwa mwanaume wake wa kwanza maishani, nilijihisi kuwa sehemu ya maisha yake!
Niliendelea kutulia mle ndani ya teksi, Shamila akaenda mpaka pale Raya alipokuwa amekaa huku amejiinamia, alipomuona Shamila tu, harakaharaka alisimama na kumsogelea, akawa anamuuliza jambo ambalo japokuwa sikuwa nasikia, nilitambua kwamba ananiulizia mahali nilipokuwa mimi ‘mgonjwa wake’.
Tofauti kabisa na tulivyokubaliana, nilishangaa Shamila akimuonesha kwa kidole kwenye ile teksi niliyokuwemo, nikamuona Raya akiacha kila kitu palepale na kuanza kutimua mbio kuja kwenye ile teksi, Shamila akawa amesimama akimtazama. Nilijua wazi kwamba amefanya hivyo kwa sababu ya wivu.
Ghafla akiwa anakuja mbio, lile gari lilitokeza tena na kuja kwa kasi pale lilipokuwa limepaki awali, nikashtuka kugundua kuwa kumbe wale watu hawakuwa wameondoka, nikajua lazima watashtukia mahali nilipo kutokana na jinsi Raya alivyokuwa anakuja kwa kasi.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 36


ILIPOISHIA:
Ghafla akiwa anakuja mbio, lile gari lilitokeza tena na kuja kwa kasi pale lilipokuwa limepaki awali, nikashtuka kugundua kuwa kumbe wale watu hawakuwa wameondoka, nikajua lazima watashtukia mahali nilipo kutokana na jinsi Raya alivyokuwa anakuja kwa kasi.
SASA ENDELEA…
“Naomba unisaidie kitu, huyu dada akifika hapa kuniulizia mwambie nimeshashuka kwenye gari nimeelekea upande wa wodi za wanaume, nikishuka funga huu mlango haraka,” nilimwambia dereva teksi ambaye alibaki ameduwaa, akiwa haelewi kinachoendelea.
Harakaharaka nikafungua mlango wa upande wa pili, nikashuka kwa kasi na kubingirika mpaka chini ya ile teksi, nikatulia huku mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio kuliko kawaida. Nilimuona Raya akikimbia mpaka pale kwenye ile teksi, nikajikausha kimya.
“Kaka samahani, nimeelekezwa kuwa mgonjwa wangu yupo ndani ya hili gari, yuko wapi?” nilimsikia Raya akimuuliza yule dereva teksi huku akihema.
“Alikuwepo lakini ameshuka ameelekea kule kwenye wodi za wanaume,” yule dereva teksi alijibu kama nilivyomuelekeza. Nikasikia Raya akiguna akiwa ni kama haamini, mara nikaliona lile gari limekuja na kupaki palepale lilipokuwa limepaki mara ya kwanza, nikaiona miguu ya watu wakishuka na kusogea pale Raya alipokuwa amesimama akizungumza na dereva teksi.
Yaani kama mtu angepata wazo la kuchungulia chini ya ile teksi, basi huenda siku hiyo ndiyo ingekuwa mwisho wangu.
“Habari yako kaka,” nilimsikia mmoja kati ya wale wanaume walioshuka kwenye lile gari, Isuzu Bighorn.
“Safi!”
>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Kuna mtu tunamtafuta, tunahisi yupo ndani ya hili gari lako,” alisema mwingine kwa sauti nzito, bila kusubiri kujibiwa, nikawasikia wakifungua milango ya teksi hiyo, yule dereva na Raya wakawa wanashangaa.
“Kwani nyie ni akina nani?” nilimsikia Raya akiwauliza lakini hakuna aliyemjibu, nikasikia wakibamiza milango ya teksi hiyo kwa nguvu, nadhani ni baada ya kufungua na kunikosa.
Nikawaona wakiondoka kwenye teksi hiyo bila kusema kitu, wakaelekea kwenye gari lao, wakapanda kisha nikaona gari likirudi nyuma na kuondoka tena.
“Kwani wale ni akina nani? Mbona wamekuja kisharishari namna hiyo?” nilimsikia Raya akimuuliza yule dereva teksi lakini hakuwa na majibu. Baada ya kuhakikisha wameshaondoka na gari lao, nilibingirika na kutoka uvunguni mwa gari.
Kwa bahati nzuri, pale kwenye maegesho ya magari palikuwa na lami kwa hiyo sikuchafuka sana, Raya akapigwa na butwaa kuniona nikitoka uvunguni mwa gari.
“Jamal! Ooh maskini pole mpenzi wangu, wale ni akina nani wanaokusaka kama jambazi?” alisema Raya huku akinisogelea na kunikumbatia huku akinimwagia mvua ya mabusu.
“Na muda wote huo ulikuwa umeenda wapi? Mbona nimekuja muda mrefu tu kukuletea chakula lakini haukuwepo?” Raya alizidi kunihoji, nikamwambia atulie kwanza nitamueleza kila kitu vizuri.
Yule dereva teksi akawa ananitazama kwa macho yaliyoonesha kuwa na maswali mengi yasiyo na majibu.
“Yule daktari alikuwa anasemaje kule wodini?” nilimuuliza Raya kimitego, akanijibu kwamba alikuwa akiniulizia kwa madai kwamba kuna kipimo inatakiwa nikafanyiwe nje ya hospitali, akawa anashangaa kwa nini sikuwepo wodini.
“Kwani wewe ulikuwa wapi mpaka madaktari wanakutafuta?” Raya aliniuliza tena, nikaendelea kumjibu vilevile kwamba atulie, nitamueleza kila kitu baadaye.
“Basi twende ukale nimekuletea chakula unachokipendaga,” alisema Raya, nikamjibu kwamba hospitalini hapo hapakuwa sehemu salama tena kwangu. Sikutaka kumuudhi Raya lakini pia sikutaka afahamu kwamba nilikuwa nimetoka nyumbani kwa Shamila na tayari mimi na yeye tulishaanzisha uhusiano wa kimapenzi.
“Naomba hicho chakula kaniletee kwenye gari, nichukulie na vitu vyangu mle wodini,” nilimwambia, akaondoka harakaharaka huku akigeuka huku na kule.
“Kaka kwani nini kinaendelea? Mbona sielewielewi?” alisema yule dereva teksi, naye nikamjibu tu kwa kifupi kwamba mambo yalikuwa magumu.
“Hawa jamaa mbona wamekuja kibabe sana halafu yule mmoja anaonekana kama ana mashine kwenye koti?” alisema yule dereva, nikashtuka sana kusikia kwamba kumbe mmoja kati yao alikuwa na bunduki, nikahisi maisha yangu yako hatarini zaidi.
>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
“Au wanakudai?” yule dereva teksi alizidi kunihoji lakini bado sikumpa ushirikiano aliokuwa anautaka.
Akili yangu ilikuwa ikiwaza mambo tofauti kabisa, kwanza ilikuwa ni lazima nijue kuhusu biashara aliyokuwa akiifanya baba yake Shenaiza lakini pia ilitakiwa niwe makini kulinda maisha yangu kwani kwa ilivyoonesha, tayari walikuwa wameshtukia kwamba nawafuatilia.
Muda mfupi baadaye, Raya alirudi akiwa ameongozana na Shamila, wote wakaingia kwenye ile teksi, Raya akakaa pembeni yangu na Shamila akakaa siti ya pembeni ya dereva.
“Nimepata wazo, unajua hapa kuna wodi za ‘private’ ambazo zinalindwa, unaonaje tukikuhamishia huko maana hali imeshachafuka,” alisema Shamila, wazo ambalo kwa kiasi fulani niliona kama ni la msingi.
“Kwani huyu ni nani?” Raya aliuliza baada ya kumsikia Shamila.
“Huyu ndiyo nesi anayesimamia matibabu yangu lakini ameguswa na matatizo yangu na ndiyo maana ameamua kunisaidia kwa karibu. Shamila, kutana na Raya, mchumba wangu,” nilisema kwa kujiamini, nikamuona Shamila akitoa tabasamu la uongo.
Dereva teksi kwa kuwa alikuwa anajua mchezo unavyoenda, alijifanya yuko bize kurekebisharekebisha vitu pale kwenye ‘dashboard’ ya gari lake.
“Nimefurahi kukufahamu,” Raya alijibu kwa kifupi, Shamila akanyoosha mkono na kumpa, wakashikana kwa sekunde chache na kuachiana. Ilikuwa ni lazima nifanye vile na kusimama kama mwanaume kwani nilishaanza kumuona Raya akikosa raha.
“Unalionaje wazo alilolitoa nesi?” nilimuuliza Raya, naye akaliunga mkono.
“Basi tufanye hivyo haraka, wanaweza kurudi tena,” nilisema, wote tukashuka kwenye teksi harakaharaka na kuanza kumfuata Shamila ambaye ndiye aliyekuwa akituongoza.
“Usitembee haraka hivyo, utajiumiza tena kidonda,” alisema Raya huku akitaka kunipokea laptop niliyokuwa nimeing’ang’ania lakini nikamkatalia. Muda mfupi baadaye tayari tulikuwa kwenye lifti, tukapanda mpaka ghorofani kulikokuwa na wodi za private.
Mazxingira ya wodi hizo yalikuwa mazuri kwa sababu kwanza kulikuwa na walinzi wenye silaha koridoni, halafu milango ya wodi ilikuwa imara, kidogo nikawa na amani moyoni mwangu. Tulipoingia tu wodini, harakaharaka niliiwasha ile laptop na kuanza kuyaangalia yale mafaili machache niliyokopi kutoka kwenye ile ‘hard disk’.
“Hivyo ni vitu gani unavyoviangangalia kwenye hiyo laptop?” Raya aliniuliza wakati akiandaa chakula huku Shamila naye akiwa bize kuwekaweka vitu vyote vizuri ndani ya wodi hiyo, nikamdanganya Raya kwamba kuna kazi nilikuwa nimetumiwa kutoka kazini.
“Mh! Kutoka kazini? Nani anayeweza kukupa kazi wakati watu wote wanajua kwamba unaumwa? Isitoshe asubuhi nilipitia kule kazini na kila mtu akawa anakupa pole,” Raya alizidi kunibana, nikamwambia nitamfafanulia baadaye.
Niliendelea ‘kuperuzi’ yake mafaili, moja baada ya jingine. Kama nilivyokuwa nimeona awali, yalikuwa yamejaa taarifa za watu mbalimbali, wakubwa kwa wadogo, yakiwa na taarifa kuhusu hali zao za kiafya na viungo mbalimbali kwenye mwili, bado nikawa sielewi.
Niliendelea kuchimba kwa undani, taratibu nikaanza kugundua mambo ambayo ama kwa hakika yalinishangaza sana. Kwa jinsi ilivyoonesha, kulikuwa na mtandao mpana sana wa watu kutoka hapa nyumbani Tanzania, India, Marekani, Uingereza na nchi za kiarabu ambao ulikuwa ukihusisha hospitali kubwakubwa duniani.
Nilipoendelea kufuatilia kwenye mafaili yake, nikaanza kugundua kwamba kumbe kulikuwa na biashara ya viungo vya binadamu ilikuwa ikifanyika katika nchi mbalimbali, kwamba baba yake Shenaiza alikuwa akiwakusanya watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na kuwasafirisha kwenda kwenye hospitali kubwakubwa duniani kwa ajili ya kuchangia viungo mbalimbali vya miili yao.
Kilichonishangaza sana ni kugundua kuwa wengi walikuwa wakisafirishwa kutoka Tanzania, wakiwa hawajui chochote kinachoenda kuwatokea. Mbaya zaidi, kulikuwa na watu ambao wameandikwa kwamba wanaenda kuchangia moyo, ninavyofahamu mimi binadamu anakuwa na moyo mmoja tu, kwa hiyo akichangia inakuwaje?
Nikajiuliza pia kwamba kuna baadhi ya watu ilionesha kwamba wanaenda kuchangia ubongo, sasa ukichangia ubongo na wewe nini kinakutokea? Unawezaje kubaki ukiwa hai? Kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu, nikawa nahisi pengine nipo ndotoni.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 37

ILIPOISHIA:
Niliendelea ‘kuperuzi’ yake mafaili, moja baada ya jingine. Kama nilivyokuwa nimeona awali, yalikuwa yamejaa taarifa za watu mbalimbali, wakubwa kwa wadogo, yakiwa na taarifa kuhusu hali zao za kiafya na viungo mbalimbali kwenye mwili, bado nikawa sielewi. Niliendelea kuchimba kwa undani, taratibu nikaanza kugundua mambo ambayo ama kwa hakika yalinishangaza sana.
SASA ENDELEA…
Kwa jinsi ilivyoonesha, kulikuwa na mtandao mpana sana wa watu kutoka hapa nyumbani Tanzania, India, Marekani, Uingereza na nchi za Kiarabu ambao ulikuwa ukihusisha hospitali kubwakubwa duniani ambao walikuwa wakifanya biashara ambayo nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kuijua.
Nilipoendelea kufuatilia kwenye mafaili yake, niligundua kuwa kulikuwa na namba za mawasiliano za kila mtu ambaye taarifa zake zilikuwa zimeandikwa na kama hiyo haitoshi, pia kulikuwa na taarifa za mtu wa karibu (next of keen), nikawa nimepata pa kuanzia.
“Naomba ukaninunulie kalamu na daftari dogo kule nje ya hospitali,” nilimwambia Raya lakini akanikatalia na kuja juu.
“Ina maana unaona afya yako siyo muhimu kuliko hicho unachokifanya? Siendi popote mpaka ule kwanza,” alisema huku akinisogezea chakula, nikashusha pumzi ndefu na kuiweka laptop pembeni, nikanyoosha mikono nikiashiria aninawishe, nikaanza kula.
“Unaonekana kuwa na pilikapilika nyingi, kwa nini hujionei huruma mpenzi wangu? Inabidi upone kwanza, afya yako ni muhimu kuliko kitu kingine chochote,” Raya alisema kwa upole huku akinibembeleza nile, nikawa nakula huku mara kwa mara macho yangu yakigongana na ya nesi Shamila.
“Sawa nimekuelewa mpenzi wangu,” nilisema kwa upole. Jambo jingine ambalo sikuwa najua linatokea kwa sababu gani, ninapokuwa na Raya nilikuwa na kawaida ya kutulia sana, jambo ambalo hata Shamila alilitambua.
Kwa kawaida, unapokaa jirani na mtu mwenye tabia fulani kwa muda mrefu, kuna mambo mawili, wewe umbadilishe au yeye akubadilishe! Raya alikuwa na hulka ya upole na utulivu, nahisi kwa sababu ya kukaa naye karibu muda mwingi, na mimi alikuwa ameniambukiza tabia hizo ndiyo maana ninapokuwa karibu naye, nilikuwa nikitulia sana.
Tofauti na Raya, Shamila alikuwa mcheshi sana, anayependa masihara na mchangamfu, ambaye naye kila nilipokuwa nikipata muda wa kuwa naye karibu, nilikuwa nikibadilika na kuendana naye.
Nilikula harakaharaka, ili kumfurahisha Raya nilimaliza chakula chote, akanimiminia na juisi, nikaifuta yote, nikamuona akitabasamu, akaja kunibusu kwenye paji la uso wangu na kunishukuru kwa kula vizuri, na mimi nikamshukuru kwa kuniandalia chakula kizuri.
Akakusanya vyombo vyake na kuviweka kwenye kikapu, akataka kutoka kwenda kuninunulia vile nilivyomuagiza lakini kabla hajatoka, Shamila aliniletea karatasi kadhaa nyeupe zilizokuwa zimebanwa pamoja vizuri na kalamu, akanikabidhi. Nilimuona Raya akimtazama kwa jicho kali kama anayesema ‘mbona unajipendekeza sana’?
>>> Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Sikuwa na muda wa kupoteza, harakaharaka nilichukua tena laptop na kuanza kuzinakili namba za simu za wale watu wote pamoja na watu wao wa karibu. Namba zilikuwa nyingi mno lakini kwa kuanzia, niliandika namba hamsini, yaani za wahusika 25 na ndugu zao wa karibu 25.
“Kama unahitaji msaada wangu niambie mpenzi wangu, nipo kwa ajili yako,” alisema Raya, nikamwambia naomba akaninunulie vocha ya shilingi elfu kumi. Kabla Raya hajainuka, Shamila aliingilia kati:
“Kama unataka vocha usijali mgonjwa wangu, mimi nina pesa kwenye simu naweza kukuunganisha.”
“Tunashukuru kwa msaada wako, tukihitaji tutakwambia. Ngoja nikakununulie mume wangu,” alisema Raya kwa nyodo za kike, akanibusu tena kwenye paji la uso na kutoka huku akitembea kwa maringo, nikabaki kutingisha tu kichwa.
Kwa jinsi upepo ulivyokuwa ukielekea, nilijua kama nisipokuwa mkali kwa Shamila, muda si mrefu watavaana na Raya na kuleta picha mbaya kwani walishaanza kuchokozana.
“Kwa nini unafanya hivyo Shamila? Si tumekubaliana kwamba uhusiano wetu uwe wa siri kwanza? Kwa nini mnafanya mambo ya kitoto?” nilimwambia Shamila nikiwa nimevaa uso wa ‘usiriasi’.
“Hata kama… ndiyo awe anakubusubusu mbele yangu, na mimi nina moyo ujue, sina chuma. Asipoacha na mimi sitaacha,” alisema Shamila huku akionesha dhahiri alivyokuwa akiumia moyoni kwa sababu ya wivu. Japokuwa ndiyo kwanza tulikuwa tumeanza mapenzi yetu, Shamila alionesha ‘kukolea’ sana.
Muda mfupi baadaye, Raya alirudi akiwa na vocha, akakwangua mwenyewe na kuweka kwenye simu yake kisha akanipa. Nikamshukuru.
“Naombeni mnipe muda wa kuwa peke yangu kwa dakika kadhaa, kuna simu za muhimu nataka kuzungumza nazo,” niliwaambia, nikawaona wanatazamana kisha Raya akabeba kikapu chake na kuniaga kwamba atarudi baadaye.
“Sasa kuhusu simu yako?”
“Baki nayo tu mpenzi wangu, nitaichukua baadaye nikirudi, mtu yeyote akipiga pokea,” alisema Raya, nikaelewa kwa sababu gani amesema vile, akamtazama Shamila kuanzia juu mpaka chini kwa yale macho ambayo wenyewe wanaita ‘kunyali’, akatoka na kikapu chake na kuniacha mle wodini nikiwa na Shamila.
Ili kumfanya Raya awe na amani, nilimwambia Shamila naye atoke, kwa bahati nzuri alinitii, akamfuata Raya nje, sijui walienda kuzungumza nini huko nje, nikabaki peke yangu. Harakaharaka nilianza kupiga namba za simu za wale watu nilizozichukua.
Cha ajabu, katika namba zote ishirini na tano, hakuna hata moja iliyokuwa ikipatikana, ikabidi nianze kujaribu upande wa pili; namba za watu wao wa karibu. Nilipoanza ya kwanza tu, iliita, nikaiweka sikioni huku nikiwa makini kutaka kusikia nani atapokea.
“Haloo!”
“Haloo, habari yako dada.”
“Nzuri, nani?”
“Samahani mimi naitwa Jamal, najua hunijui lakini nilikuwa na shida na Simon Nyimbi, unamfahamu?”
“Ndiyo, ni mchumba wangu.”
“Ok, nampigia simu yake simpati, naweza kuzungumza naye?” nilimuuliza swali la mtego, akaingia mzimamzima kwenye ‘target’ yangu.
“Simon alisafiri kwenda kusoma India, huu ni mwezi wa kumi sasa tangu aondoke.”
“Ameenda kusomea nini na amedhaminiwa na serikali au nani?”
“Ameenda kusomea teknolojia ya mawasiliano (IT), alipata udhamini wa shirika moja liitwalo Black Heart.”
“Tangu aondoke umewahi kuwasiliana naye?”
“Hapana, sijawahi kuwasiliana naye hata mara moja ila kuna siku kuna mwanaume alinipigia simu na kunieleza kuwa yeye ni mwakilishi wa shirika la Black Heart nchini India, akaniambia nisiwe na wasiwasi mume wangu mtarajiwa yuko bize na masomo na atarudi baada ya miaka miwili kupita,” alisema yule msichana niliyekuwa nazungumza naye kwenye simu.
Kabla sijakata simu, nilimuuliza anaishi wapi ambapo aliniambia kwamba anaishi Kibaha, Pwani, nikamshukuru kwa ushirikiano kisha nikakata simu.
>>> Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi
Maelezo yake yalitosha kunipa mwanga wa kilichokuwa kinaendelea, harakaharaka nikachukua laptop yangu na kuingia kwenye mtandao, ‘nika-google’ shirika liitwalo Black Heart, mtandao ukafunguka, nikaanza kusoma kuhusu shirika hilo.
Kwa maelezo yaliyokuwa yameandikwa mtandaoni, shirika hilo lilikuwa likiwasaidia vijana weusi kuwalipia gharama za masomo nje ya nchi au kuwasaidia maskini wenye maradhi mbalimbali kwenda kutibiwa nje ya nchi. Nikachukua mawasiliano yao na kuyaandika pembeni, nikaendelea na ile kazi.
“Nilipiga namba ya pili, akapokea mwanaume. Nilijitambulisha kwa upole, nikamueleza yule mwanaume ambaye kwa jinsi alivyokuwa akizungumza alionesha kuwa ni mtu wa makamo, kwamba naitwa Jamal na nilikuwa namuulizia mtu aitwaye Tusekile Mwankenja, nikamdanganya kwamba tulisoma wote shule ya msingi.
“Mimi ni baba yake. Yupo nchini India kwa matibabu, alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya figo kwa muda mrefu, kwa bahati nzuri tukapata mdhamini ambaye alimgharamia kila kitu, hivi tunavyoongea yupo Apollo Hospital, Mumbai akiendelea kupatiwa matibabu.”
“Ooh! Poleni sana, alisafiri na nani kwa upande wa wanafamilia na mara ya mwisho mlizungumza naye lini?”
“Aliondoka peke yake kwa sababu tuliambiwa hilo shirika la wadhamini lina uwezo wa kumlipia mgonjwa pekee, kama tunataka mtu wa kwenda naye sisi familia ndiyo tumlipie kila kitu lakini tukashindwa kutokana na umaskini.”
“Mara ya mwisho mlizungumza naye lini?”
“Kiukweli tangu aondoke hatujawahi kuzungumza naye, wanasema hospitalini hawaruhusu kutumia simu,” alijibu mwanaume huyo, nikashusha pumzi ndefu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 38;


ILIPOISHIA:
“Mara ya mwisho mlizungumza naye lini?”
“Kiukweli tangu aondoke hatujawahi kuzungumza naye, wanasema hospitalini hawaruhusu kutumia simu,” alijibu mwanaume huyo, nikashusha pumzi ndefu.
SASA ENDELEA...
Majibu ya watu hao wawili tu yalitosha kunifanya nielewe kilichokuwa kinaendelea lakini ili kupata ushahidi mkubwa zaidi, niliendelea kuwapigia simu wengine. Wachache hawakuwa wakipatikana hewani lakini karibu watu 16 wote walikuwa wakipatikana na majibu yao hayakuwa yakitofautiana.
Wapo waliosema kwamba ndugu zao walichukuliwa kwenda kusoma nje ya nchi kwa msaada wa shirika hilo, wengine wakasema walipelekwa kwa matibabu lakini asilimia kubwa walisema kwamba ndugu zao walichukuliwa kwa ahadi ya kwenda kutafutiwa kazi nchi za Uarabuni, India, Marekani na nchi za Ulaya.
“Kwani binti yako ana elimu kiasi gani mpaka uamini kwamba anaenda kutafutiwa kazi nzuri huko anakokwenda?”
“Kiukweli wala hajasoma, aliishia darasa la saba tu lakini tukaambiwa kule kuna watu wanatafutwa kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani, na mshahara wake ni mkubwa kuliko hata mameneja wengi wa Tanzania, ndiyo maana tukamruhusu kwa shingo upande.
“Isitoshe kabla ya kuondoka, viongozi wa shirika hilo walitupa shilingi milioni moja kama shukrani tu na hapo ni nje ya mshahara wa binti yetu,” mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Akilimali, aliniambia wakati akizungumza nami kwenye simu.
“Uko bize sana na simu mpenzi wangu, kitaalamu simu huwa inatoa mionzi ambayo siyo mizuri kwa mtu kama wewe kwani inaweza kukuongezea matatizo mpenzi, au wewe hulioni hilo?” alisema Shamila baada ya kuingia wodini, ikiwa imepita takribani nusu saa tangu nilipomtaka yeye na Raya watoke na kunipisha.
Nilishindwa hata nimjibu nini, akanisogelea na kunibusu kwenye paji la uso wangu, akakiweka kitanda vizuri kisha akakaa pembeni yangu.
“Eti, unalijua shirika linaloitwa Black Heart?” nilimuuliza Shamila, akanitazama kwa macho ya mshangao kama anayejiuliza ‘umelijuaje?’.
“Jamal!” aliniita huku sauti yake ikionesha kuwa na hofu kubwa.
“Kumbe hicho ndicho ulichokuwa ukikihangaikia muda wote?”
“Ndiyo, kwani kuna tatizo?”
“Ni hatari mpenzi wangu, nakupenda sana na sitaki kuona ukipatwa na jambo lolote baya.”
“Kivipi? Mbona sikuelewi Shamila?” nilimuuliza, akashusha pumzi ndefu na kunitazama usoni.
“Kuna siku uliniuliza kuhusu yule mgonjwa anayeitwa Shenaiza, nikakueleza kwa kifupi kwamba baba yake siyo mtu mzuri hata kidogo.”
“Ndiyo nakumbuka, sasa kwani kuna uhusiano gani na hiki nilichokuuliza?” nilimtega Shamila kwani ilionesha kuna mambo mengi anayajua lakini anaogopa kuniambia.
“Usinifanye mimi mjinga Jamal, najua kila kitu kuhusu unachokifanya tangu mwanzo, najua kwamba unachimba kutaka kujua baba yake Shenaiza anashughulika na nini lakini nakuomba sana, achana na hicho unachokifanya.
“Watu wengi wameshapotea kwa sababu ya kumfuatilia huyo mzee! Jamal, mwenzio nakupenda na sitaki kuona ukipotea ndiyo maana nakwambia achana na hayo mambo.”
“Hapana, ni lazima niikamilishe hii kazi Shamila, nimerudi duniani kwa ajili ya kazi hii, sitaogopa chochote wala sitarudi nyuma,” nilimwambia kwa msisitizo, akanitazama tena machoni na kushusha pumzi ndefu kwa mara nyingine, akatazama huku na kule kuhakikisha hakuna mtu anayetusikiliza.
“Mhusika mkuu wa hiyo Black Heart ni baba yake Shenaiza.”
“Ni shirika la nini?”
“Kwa nje linajitambulisha kama shirika la kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali, kuwasafirisha wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, kuwalipia gharama za masomo watoto na vijana kutoka kwenye familia maskini pamoja na kuwatafutia kazi nzuri wananchi nje ya nchi.”
“Umesema kwa nje, vipi kwa ndani?”
“Jamal, unajua mpaka nafikia hatua ya kuufungua mdomo wangu kukwambia masuala haya ninayahatarisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa kwa sababu ikija kufahamika kwamba mimi ndiyo niliyekwambia nitauawa mwenzako,” alisema Shamila kwa hofu kubwa. Sikuelewa hasa hofu yake ilikuwa ikisababishwa na nini. Nikamtoa wasiwasi kwamba nitamlinda, akaniambia kuwa sina uwezo wa kumlinda kwa sababu hata mimi mwenyewe nilikuwa nahitaji kulindwa ndiyo maana nilishindwa kujitetea siku nilipovamiwa na kutaka kuuawa.
Ni kweli alizungumza pointi lakini nilijivisha roho ya kiume, nikaendelea kumtoa wasiwasi na kujitutumua kwamba siku hiyo walinibahatisha tu, akakubali kunieleza kwa upana.
Aliniambia kwamba licha ya shirika hilo kujinadi kwa sura hiyo ya nje, likijifanya linasaidia jamii ya watu maskini, ukweli ni kwamba lilikuwa likifanya biashara haramu ya viungo vya binadamu. Akaendelea kuniambia kwamba shirika lilikuwa na mtandao mpana, likiwagusa viongozi kadhaa wa ngazi za juu serikalini pamoja na watu wengine wenye taaluma mbalimbali, wakiwemo madaktari.
Aliniambia kwamba watu wote waliokuwa wakisafirishwa kwenda nje ya nchi na shirika hilo, walikuwa wakienda kutolewa viungo vyao muhimu, kama moyo, mapafu, figo na vingine vingi, vikitolewa na kupandikizwa kwa watu waliokuwa wakivihitaji.
Akaniambia kwamba kwenye nchi zilizoendelea, kuna watu wengi wanaojiweza kifedha lakini wanakuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya kiasi kwamba fedha zao haziwasaidii kupona kwa kutumia madawa mbalimbali ya hospitalini. Ni hao ndiyo waliokuwa wateja wakubwa wa viungo hivyo vya binadamu.
Akanifafanulia kwamba; kwa mfano kama kuna tajiri ana matatizo ya figo au ini na ameshatumia madawa yote bila kupata nafuu, njia nyepesi ya kumrudishia afya bora ilikuwa ni kupandikizwa viungo vingine kutoka kwa mtu asiye na matatizo.
Akasema kwa kuwa uhitaji ni mkubwa siku hizi kutokana na mtindo wa maisha, hasa kwa nchi zilizoendelea, njia nyepesi iliyokuwa inatumiwa na baba yake Shenaiza na wenzake, ilikuwa ni kuwasafirisha watu kutoka nchi za kimaskini na kwenda kuwauza kwa bei ghali kwa ajili ya kutolewa viungo vyote muhimu ambavyo huwekewa watu wanaojiweza kiuchumi.
Maelezo yake yalinishangaza na kunishtua sana, akanihakikishia kwamba tangu shirika hilo lianze kufanya kazi miaka kadhaa iliyopita, hakukuwa na hata mtu mmoja ambaye aliondoka na kurejea nyumbani salama, wengi walikuwa wakirejeshwa wakiwa maiti na wengine hawakuwa wakirejeshwa kabisa.
Ndugu zao wanapowaulizia, hutulizwa kwa kupewa fedha na kuambiwa wapo salama na ipo siku watarejea nchini.
“Ina maana serikali kupitia kwa vyombo vya usalama hawajui kuhusu hiki kinachoendelea?”
“Watu wanajua sana, lakini nimeshakwambia huu ni mradi wa vigogo wakubwa serikalini, hakuna anayeweza kufumbua mdomo wake na ukijaribu tu, basi ujue kifo kinakuita.”
Japokuwa mle wodini mlikuwa na kipupwe, nilijikuta nikitokwa na kijasho chembamba, mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio kuliko kawaida. Ni hapo ndipo nilipoelewa kwa nini Shamila alikuwa akinikataza kujihusisha na mambo yale.
Akaendelea kuniambia kwamba Shenaiza alikuwa akifahamu kinachofanywa na baba yake na kwa sababu ilifika hatua akawa amechoshwa na ukatili huo, alimtishia baba yake kuwa atatoa siri, jambo lililosababisha ateswe sana, ikawa mtu yeyote akionekana kuwa karibu naye, baba yake anahisi anaweza kupewa siri hiyo hivyo anauawa haraka kabla hajafumbua mdomo wake.
“Kumbe ndiyo maana na mimi wananiwinda kutaka kuniua?” nilijikuta nikisema kwa sauti kubwa.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 39

ILIPOISHIA:
Akaendelea kuniambia kwamba Shenaiza alikuwa akifahamu kinachofanywa na baba yake na kwa sababu ilifika hatua akawa amechoshwa na ukatili huo, alimtishia baba yake kuwa atatoa siri, jambo lililosababisha ateswe sana, ikawa mtu yeyote akionekana kuwa karibu naye, baba yake anahisi anaweza kupewa siri hiyo hivyo anauawa haraka kabla hajafumbua mdomo wake.
“Kumbe ndiyo maana na mimi wananiwinda kutaka kuniua?” nilijikuta nikisema kwa sauti kubwa.
SASA ENDELEA...
“Na bado wataendelea kukuwinda mpaka watakapoyakatisha maisha yako, unapaswa kuwa makini sana mpenzi wangu,” alisema Shamila lakini alichokisema ni kama hakikuingia akilini mwangu.
Akili yangu ilianza kunienda mbio kuliko kawaida, nikawa naunganisha matukio, kuanzia siku Shenaiza aliponipigia simu na kuniambia kwamba ana tatizo kubwa na anahitaji nimsaidie, baada ya awali kuwa amekosea namba.
“Lazima nikazungumze na Shenaiza, atakuwa anajua mambo mengi zaidi,” nilisema huku nikijaribu kuinuka, Shamila akanizuia na kuniuliza kama ninakumbuka kilichotokea muda mfupi uliopita kwenye maegesho ya magari.
Japokuwa nilikuwa na shauku ya kwenda kuonana na Shenaiza, maneno hayo ya Shamila yalinivunja nguvu kabisa. Nilikumbuka jinsi wale wanaume wenye asili kama ya Shenaiza walivyokuwa wakiniwinda kwa udi na uvumba.
“Kama usingepata akili ya kuingia kwenye wa ile teksi unafikiri nini kingetokea?” alisema Shamila huku akinibusu kwenye paji langu la uso.
Kitu ambacho ningependa kukieleza hapa, ndani ya muda mfupi tu tangu nifahamiane na Shamila na kujikuta nikianguka naye dhambini, dada huyo mrembo alionesha kuchanganyikiwa kabisa na penzi langu.
Kila mara alikuwa anapenda kunibusubusu, mara anishike hapa, mara anisafishe kucha, mara anidekeze basi ilimradi roho yake ifurahi! Moyoni nilikuwa najisikia raha sana kwa sababu siyo siri, sikuwa mzoefu wa mambo hayo ya kikubwa.
Unajua kwa nini wanaume wengine huwa wanafikia hatua ya kutelekeza familia zao? Unakuta katika maisha yako, hujawahi kukutana na mwanamke anayejua kukupetipeti kama ilivyokuwa kwa Shamila. Sasa ukishaangukia kwenye mikono yake, na wewe ni mgeni wa mambo hayo, lazima utelekeze mke na watoto na kuhamia kwake.
“Kwani Shamila wewe ni mtu wa wapi?”
“Mbona unaniuliza swali ambalo haliendani kabisa na mada tunayozungumza?” aliniuliza Shamila huku akinitazama kwa yale macho yake ambayo muda wote yapo kama yana usingizi!
Nikachekacheka pale na kupotezea mada, akaendelea kunisisitiza kwamba huo haukuwa muda muafaka wa mimi kutoka na kwenda kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Shenaiza, wala kuzungukazunguka kwa sababu ya usalama wangu.
“Lakini Shamila, kuna kazi ambayo ni lazima niikamilishe haraka iwezekanavyo, au wewe unaridhishwa na kinachofanywa na huyu mzee pamoja na kundi lake?”
“Siyo kwamba naridhishwa mpenzi wangu, Wazungu wanasema ‘dont hurt what you cant kill’ (usiwinde kitu ambacho hutaweza kukiua), hata ukifuatilia na kuujua ukweli, utafanya nini?”
Shamila alikuwa amenizidi kwa hoja, ikabidi nitulie tu wodini huku nikiendelea kutafakari nini cha kufanya kwa sababu ile hoja ya kwamba niache kufuatilia suala lile kwa sababu sikuwa na cha kufanya, sikuliona kama ni sahihi kwangu.
Baadaye, nilijifanya kama nimepitiwa na usingizi, lengo lilikuwa ni kumpumbaza Shamila, kweli aliponiona nimelala alikuja nakunifunika vizuri kisha akatoka na kwenda kuendelea na shughuli zake.
Nilisubiri kwa dakika kadhaa, nilipoona kumetulia kabisa, niliamka na kuvaa viatu, nikatazama huku na kule, niliporidhika kwamba Shamila hakuwepo, nilinyata hadi kwenye chumba cha manesi, nikachukua koti la kidaktari lililokuwa limetundikwa ukutani, nikalivaa na kusogea kwenye kioo kilichokuwa pembeni, nikajirekebisha vizuri.
Kama ungenitazama haraka, ungeweza kudhani na mimi ni muuguzi hospitalini hapo, niliamini hiyo ndiyo itakuwa njia nyepesi ya kwenda kuonana na Shenaiza kule wodini kwake bila kushtukiwa na mtu yeyote.
Harakaharaka nilitoka huku nikiwa makini jeraha langu la kifuani lisije kufumuka tena, nikaingia kwenye lifti na kushuka hadi ghorofa ya chini, nikashuka na kuanza kutembea harakaharaka kuelekea kule kwenye wodi ya wagonjwa wa akili, wanawake alikokuwa amelazwa Shenaiza.
Nilifanikiwa kufika kwenye wodi ya wagonjwa wa akili, kama ilivyokuwa kawaida ya wodi hiyo, nilipokelewa na vurugu na kelele za kila aina kutoka kwa wagonjwa, nikawa nawapita mmoja baada ya mwingine mpaka nilipofika kwenye kitanda cha Shenaiza.
Tofauti na nilivyotegemea kumkuta Shenaiza akiwa amekaa kitandani kwake akilalamika, nilishangaa kumkuta akiwa amelala tuli, akionesha kabisa kwamba hakuwa kwenye hali ya kawaida.
Nilisimama kwa sekunde kadhaa na kuanza kumtazama, kwa zile saa chache tu nilizokaa mbali naye, alikuwa amebadilika kabisa. Ngozi ya mwili wake, iliyokuwa na weupe wa kung’aa, ilikuwa imebadilika na kuwa na rangi kama ya kijivu hivi, macho yalikuwa yamefumbwa nusu na nusu yapo wazi, mdomo pia haukuwa umefumbwa, nikajikuta nikishindwa kujizuia kutokwa na machozi.
“Shenaiza! Shenaiza!” nilimuita lakini hakuitika, nilijaribu kumtingisha lakini hakutingishika, nikabaki nikihaha huku na kule, nikiwa sijui cha kufanya. Nilipotazama pembeni ya kitanda chake, kulikuwa na kichupa kidogo juu ya droo ya kitanda chake, kilichokuwa na maandishi yaliyosomeka Benzodiazepam.
Harakaharaka nilikichukua kichupa kile na kukiweka kwenye mfuko wa koti, nikatazama huku na kule kujaribu kuangalia kamakuna mtyu aliyekuwa akinitazama. Katika hali ambayo sikuitegemea, miongoni mwa wale wagonjwa wengi wa akili waliokuwa ndan ya wodi hiyo, kuna mmoja alikuwa ametulia, muda wote akinikodolea macho.
Kwa kumtazama tu, hakuonesha kwamba ni mwendawazimu kama wale wenzake kwa sababu macho yangu na yake yalipogongana tu, harakaharaka alikwepesha macho pembeni na kuvunga kama hakuwa akinitazama. Kitendo hicho tu kilitosha kunifanya niamini kwamba hakuwa mgonjwa kama wale wengine.
Niliendelea kumkazia macho, akawa ananitazama kwa wiziwizi, nikamsogelea pale kwenye kitanda alichokuwa amelala juu yake, nikashtuka kumuona akiwa na simu kubwa ya kisasa ambayo harakaharaka aliificha kwenye shuka.
“Wewe ni nani?” nilimuuliza kwa sauti ya chinichini, akanigeukia, tukatazamana.
“Kwani unataka nini?” naye aliniuliza kwa sauti iliyoonesha dhahiri kwamba ni mwanamke mjeuri sana na alikuwepo pale kwa kazi maalum.
“Naomba kuzungumza na wewe, unamfahamu Shenaiza?” nilimuuliza lakini badala ya kunijibu, alinitazama kuanzia juu mpaka chini kisha akageukia pembeni. Kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa changu, harakaharaka nikageuka na kuanza kutembea kuelekea kwenye mlango wa kutokea.
“Unahatarisha maisha yako, achana na mambo yasiyokuhusu,” alisema yule msichana, nikageuka na kumtazama, naye akawa ananitazama. Sikuelewa kwa sababu gani amezungumza maneno yale, nikaendelea kutembea harakaharaka na kutoka.
“Mungu wangu, mbona sielewi kinachoendelea?” nilisema huku nikiendelea kutembea kwa haraka, nikaenda mpaka kwenye lifti na kupanda, nikabonyeza namba ya ghorofa ilipokuwa wodi ya ‘private’ niliyokuwa nimelazwa, lifti ikaanza kupanda.
“Unatoka wapi?” Shamila aliniuliza nilipofungua mlango tu, kumbe alikuwa amerejea muda mrefu na akawa anahangaika kunitafuta.
“Nilitoka mara moja,” nilijitetea huku nikijisikia aibu ndani ya moyo wangu.
“Kwa nini hujihurumii mpenzi wangu? Mimi sitakwambia tena kuhusu suala la kuzingatia usalama wako,” alisema huku akinisaidia kuvua lile koti la kidaktari huku akiendelea kunitazama kwa macho ya mshangao.
“Samahani, eti hii ni dawa gani?” nilisema huku nikitoa kile kichupa nilichokichukua kwenye kitanda cha Shenaiza. Akakishika na kukitazama.
“Umekipata wapi?”
“Nimekikuta kwenye kitanda cha Shenaiza, na anaonekana kama hana fahamu, rangi ya ngozi yake imebadilika na kuwa ya kijivu,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu na kunitazama usoni.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 40

ILIPOISHIA:
“Nimekikuta kwenye kitanda cha Shenaiza, na anaonekana kama hana fahamu, rangi ya ngozi yake imebadilika na kuwa ya kijivu,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu na kunitazama usoni.
SASA ENDELEA...
“Benzodiazepam,” Shamila alisema kwa sauti ya juu, akitamka maneno yaliyokuwa yameandikwa kwenye kile kichupa nilichokikuta pembeni ya kitanda cha Shenaiza.
“Kwani ni dawa gani?”
“Mungu wangu! Wameamua kummalizia kabisa mdada wa watu. Hii ni dawa ya usingizi ambayo hairuhusiwi kutumika bila uangalizi wa kutosha wa daktari. Mtu anapotumia dozi kubwa, husababisha muda wote awe analala tu na kama hali hii ikiendelea kwa muda, husababisha mgonjwa kupoteza kumbukumbu na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.”
“Haa! Na siyo kwamba dawa hii hutumika kuwatibu wagonjwa wa akili?”
“Hapana Jamal, hii hutumika tu kuwatuliza watu wenye msongo mkali wa mawazo au stress kiasi kwamba wanakosa usingizi. Wakitumia dawa hii chini ya uangalizi wa daktari, huwasaidia kupata usingizi na kuwapunguzia msongo mkali au ‘stress’, lakini narudia tena, ni lazima itumiwe chini ya uangalizi mkali wa daktari.”
“Sasa kwa nini wanampa Shenaiza?”
“Jibu ni moja tu, wanataka watu wote waamini kwamba kweli amechanganyikiwa. Kama kwa siku chache tu alizokaa hapa hospitalini kichupa kimeshaisha, maana yake ni kwamba anapewa dozi kubwa sana ambayo ndani ya muda mfupi tu, itamfanya apoteze kumbukumbu na kuwa mwendawazimu.”
“Shamilaa! Cant we help her?” (Shamilaa! Hatuwezi kumsaidia?)
“Its none of our business Jamal.” (Hilo halituhusu Jamal)
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Nikukumbushe tu kwamba mambo yote hayo yanafanywa kwa maagizo ya baba yake mzazi. Unataka kusema wewe una uchungu na Shenaiza kuliko baba yake?” alisema Shamila na kunifanya nikose cha kujibu, nikajiinamia huku nikijisikia uchungu mkali sana ndani ya moyo wangu.
Ni hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwa nini Shenaiza alikuwa akihitaji sana msaada kutoka kwangu. Ni hapo pia ndipo nilipoelewa kwa nini alikuwa anashindwa kunieleza moja kwa moja ni msaada gani aliokuwa anauhitaji na alikuwa akisumbuliwa na tatizo gani. Nilishusha pumzi ndefu na kukaa vizuri pale kitandani.
“Utakapojaribu kutoka tena wodini na kwenda unakokujua mwenyewe, kitakachokupata mimi sitahusika maana naona hunielewi,” alisema Shamila huku akionesha kukasirishwa na kitendo changu cha kutoka wodini bila ruhusa yake, wakati nikijua kwamba nilikuwa nikisakwa na watu wenye nia ovu.
“Nisamehe Shamila, lakini muda mwingine nakuwa sina namna zaidi ya kuvunja sheria zako,” nilisema kwa upole, akanisogelea, tukawa tunatazama, nikambusu kwenye paji lake la uso.
“Kwa nini unaonekana kuguswa sana na matatizo ya Shenaiza?” Shamila aliniuliza huku akikaa vizuri, nikashusha tena pumzi ndefu nikitafakari nianzie wapi kumueleza. Kwa jinsi hali ilivyokuwa, kumsaidia Shenaiza peke yangu lilionekana kuwa suala gumu, ilikuwa ni lazima nimueleze Shenaiza ukweli ili kwa pamoja tujue namna ya kumsaidia.
Ilibidi nianze kumsimulia Shamila kila kitu kuhusu mimi na Shenaiza. Nilimueleza kilichotokea kuanzia siku ya kwanza msichana huyo alipopiga simu yangu na baadaye kuniambia kwamba alikuwa amekosea namba. Nilimueleza alivyoendelea kunisumbua akidai kwamba hata kama amekosea namba, anaamini mimi naweza kumsaidia kumtoa kwenye matatizo makubwa yaliyokuwa yanamkabili.
“Nilimueleza Shamila jinsi nilivyoendelea kuwasiliana na msichana huyo, jinsi tulivyoenda kukutana na kumkuta akiwa na hali mbaya hospitalini baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya. Sikumficha kitu, niliendelea kumueleza jinsi alivyonishawishi nimtoroshe hospitali na yote yaliyotokea baada ya hapo.
Shamila alikuwa kimya kabisa akinisikiliza, kadiri nilivyokuwa naendelea kumsimulia kuhusu sakata hilo la Shenaiza, taratibu nilianza kumuona na yeye akiguswa, nilimfafanulia kila kitu isipokuwa kilichotokea baada ya mimi kushambuliwa na kunusurika kufa, na kujikuta nikizinduka nikiwa kwenye ulimwengu mwingine.
Nilimficha kuhusu kipengele hicho kwa sababu maalum kwani nilijua hata nimueleze kwa lugha gani, hawezi kunielewa, sanasana atahisi labda na mimi nimeanza kuchanganyikiwa.
Nashukuru Mungu kwamba maelezo yangu kuhusu Shenaiza yalimuingia sana moyoni mwake, naye akaguswa kama nilivyokuwa nimeguswa mimi lakini kabla ya yote akanitahadharisha.
“Mara kwa mara nimemsikia Raya akilalamika kwamba wewe una uhusiano wa kimapenzi na Shenaiza,” alisema Shamila, kauli ambayo ilinishtua sana. Nikajua kwamba kumbe hata kabla sijaanzisha uhusiano naye wa siri, Shamila alikuwa akinifuatilia kwa karibu sana na tayari alikuwa anajua mambo yangu kadhaa.
Akaendelea: “Sasa isije kuwa mi nakusaidia kumuokoa Shamila kumbe nakurahisishia mpango wako wa kumuokoa mpenzi wako, nikija kujua kwamba ni kweli mna uhusiano naye wa kimapenzi nitafanya jambo hilo ambalo hutakuja kulisahau maishani mwako.”
“Siyo hivyo Shamila, wala sina uhusiano naye wa kimapenzi, ni kama nilivyokueleza na hakuna chochote zaidi ya hayo niliyokwambia.
“Ndiyo nimeshakwambia hivyo, kwa jinsi ninavyokupenda sitaki kuona mtu mwingine akikusogelea, hata huyo Raya naandaa mpango wa kumtoa kwenye maisha yako, nataka nibaki peke yangu, wewe ndiyo mume wangu mtarajiwa,” alisema Shamila na kunibusu na lipsi zake laini, mkondo wa raha za kipekee ukapita kwa kasi kwenye mishipa yangu ya damu, nikajikuta nikisisimka mno hasa nilipokumbuka asali aliyonilambisha.
“Nakuhakikishia, suala kama hilo haliwezi kutokea,” nilisema kwa kumnong’oneza sikioni, akaruka kidogo kwa msisimko na kunibusu tena, akaniambia kwamba ananipenda sana na anaamini mimi ndiyo baba mtarajiwa wa wanaye.
“Kwa hiyo utanisaidia kuhusu suala la Shenaiza,” nilimchombeza, akanihakikishia kwamba yupo tayari kunisaidia kwa chochote ambacho nakihitaji, hata kama kitayagharimu maisha yake.
Nilifurahishwa mno na majibu yake kwani kiukweli, naomba Mungu anisamehe! Hilo ndiyo lilikuwa lengo langu kubwa la kuanzisha naye uhusiano wa kimapenzi, nilitaka nimtumie kukamilisha baadhi ya mambo yangu!
Siyo jambo zuri hata kidogo kucheza na hisia za mtu anayekupenda, nawashauri watu wenye tabia hii waache mara moja kwa sababu mapenzi huwa hayajaribiwi, kama ambavyo ilitokea kwangu na Shamila, Raya na Shenaiza. Nitafafanua kwa kina baadaye jinsi ujanja wangu wa kucheza na hisia za wote watatu kwa wakati mmoja zilivyonigharimu.
Tulichokubaliana na Shamila ilikuwa ni kufanya kila kinachowezekana kwanza kumjua daktari aliyekuwa akisimamia matibabu yake, na ikiwezekana kumbadilishia dawa bila mwenyewe kujua, kwamba badala ya kuendelea kumpa sumu Shenaiza, ampe dawa zitakazomsaidia mwili wake kurudiwa na nguvu zake upya na akipata nafuu tu, tufanye utaratibu wa kumtorosha.
Tulijadiliana pia kwa kina juu ya nini cha kufanya baada ya kugundua mchezo haramu uliokuwa ukifanywa na baba yake Shenaiza kwa kutumia Shirika la Black Heart, wa kuwasafirisha watu na kwenda kuwauza kisha kuwaua na kuwatoa viungo muhimu miilini mwao, kwa kivuli cha kujifanya wanaenda kuwasomesha, kuwapatia matibabu au kuwatafutia kazi.
Kutokana na upana wa mtandao wa baba yake Shenaiza, Shamila alinishauri kwamba kwa sababu tayari nilikuwa nimeshapata pa kuanzia, niendelee kukusanya taarifa kimyakimya kisha nikishapata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitalini, ndiyo tukae tena na kuamua nini cha kufanya kuhakikisha tunamuangusha baba yake Shenaiza na kuokoa maisha ya watu wengi waliokuwa wakienda kutolewa kafara bila wenyewe kujua chochote.
“Lakini sitakiwi kuendelea kukaa hapa hospitalini zaidi, wanaweza kuja hata huku na kunichukua kiulaini, wakaenda kuniua au kunifanya chochote wanachotaka ili kuniziba mdomo,” nilimwambia Shamila, akaniondoa wasiwasi kwamba naye analijua hilo lakini hatutakiwi kufanya mambo kwa kukurupuka. Akanihakikishia kwamba kila kitu kitaenda vizuri, nimuachie yeye.
Wakati tukiendelea kuzungumza, Raya alifungua mlango na kuingia akiwa na kikapu cha chakula, mazungumzo yakakatika ghafla, Shamila akajifanya yuko bize kwenye meza ya dawa, akipangapanga vitu.
“Habari za saizi nesi,” Raya alimsalimia Shamila kwa unyenyekevu, jambo ambalo hakuwahi kulifanya kabla. Shamila naye akajibu kwa uchangamfu, nikabaki njia panda. Sikujua walizungumza nini muda ule mpaka wakamaliza tofauti zao. Raya akaja mpaka pale kitandani na kunibusu mdomoni, Shamila akageuka na kulishuhudia tukio hilo.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
SEHEMU YA 41


ILIPOISHIA:
“Habari za saizi nesi,” Raya alimsalimia Shamila kwa unyenyekevu, jambo ambalo hakuwahi kulifanya kabla. Shamila naye akajibu kwa uchangamfu, nikabaki njia panda. Sikujua walizungumza nini muda ule mpaka wakamaliza tofauti zao. Raya akaja mpaka pale kitandani na kunibusu mdomoni, Shamila akageuka na kulishuhudia tukio hilo.
SASA ENDELEA...
Alipogundua kwamba namtazama, harakaharaka Shamila alijifanya kama hakuwa ameona chochote.
“Leo nimekupikia chakula kizuuri, naamini utakipenda,” alisema Raya huku akianza kuniandalia chakula. Nikawa nimetulia pale kitandani huku akilini mwangu mawazo mengi yakipita. Nilikuwa nimeingia kwenye mtego hatari sana ambao sasa ilikuwa ni lazime nifanye kila kinachowezekana kujikomboa.
Njia pekee ambayo ingenisaidia, ilikuwa ni kuhakikisha baba yake Shenaiza na kundi lake lote wanafikishwa mbele ya sheria na mamia ya watu ambao maisha yao yalikuwa hatarini, wanaokolewa kutoka kwenye shimo la mauti.
Ni jambo hilo pekee ndiyo lingenifanya niwe na amani kwa sababu bila kumdhibiti baba yake Shenaiza, maana yake ni kwamba angeendelea kunisaka kwa lengo la kuniua, akiamini tayari kuna siri zake nyingi nazijua, lakini pia maana yake ni kwamba baada ya kunimaliza mimi, angefuatia Shenaiza na baada ya hapo, angeendelea na kazi yake haramu ya kuteketeza maisha ya watu bila huruma.
“Mbona unaonekana kama una mawazo mengi, nini kinakusumbua?” swali la Raya ndilo lililonizindua kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Akaacha kuandaa chakula na kunisogelea, akaniinamia pale kitandani na kunibusu kwenye paji la uso, akawa ananiuliza kwa upole kinachonisumbua.
Mpaka muda huo, Raya hakuwa akielewa chochote kilichokuwa kinaendelea, zaidi ya kufahamu tu kwamba nilikuwa hospitalini nimelazwa baada ya kuvamiwa na majambazi ambao almanusra wayakatishe maisha yangu. Hakuwa anajua ‘connection’ iliyokuwepo kati ya matukio yaliyokuwa yananitokea hata kidogo.
“Kuna jambo linanisumbua sana kichwa changu.”
“Jambo gani mpenzi wangu, si unajua sipendi kukuona ukikosa raha?”
“Najua mpenzi wangu, mambo yamenifika shingoni,” nilimwambia Raya, akazidi kunidadisi ambapo nilimwambia aniandalie kwanza chakula mengine tutaongea baadaye.
Kwa jinsi hali ilivyokuwa, sikuona sababu ya kuendelea kumficha Raya, nilitaka nimueleze ili naye akae akiwa anaelewa kuhusu kipindi kigumu nilichokuwa napitia ili kama kuna msaada wowote anaweza kunisaidia afanye hivyo.
Baada ya kumaliza kuandaa chakula, alinisogezea na kuanza kunibembeleza nile. Kwa jinsi alivyokuwa amepika chakula vizuri, nilikula chote mpaka nikamaliza, jambo ambalo lilimfurahisha sana.
“Enhee, haya niambie sasa,” alisema baada ya kumaliza kutoa vyombo, kama nilivyokuwa nimedhamiria kutoka ndani ya moyo wangu, nilianza kumueleza ukweli wa kila kitu. Jambo pekee ambalo sikumueleza, kama ilivyokuwa kwa Shamila, ni kile kilichonitokea baada ya kupoteza fahamu. Nilihisi naweza kumjaza woga moyoni akaanza kunitazama kwa macho yasiyo ya kawaida.
Nilimficha pia suala la mimi na Shamila kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, nikamwambia kwamba alitokea kuguswa na kilichonipata na kuamua kunisaidia kwa sababu hata yeye kuna ndugu yake amewahi kusafirishwa na shirika hilo na mpaka muda huo hawakuwa na mawasiliano naye. Niliamua kutumia uongo huo ili asishtuke mapema kwamba mimi na Shamila tulikuwa na uhusiano wa kimapenzi
Kiukweli Raya alishtuka sana nilipomueleza kilichokuwa kinaendelea, akawa hataki kuamini, akawa anahisi labda nimeamua kumtungia stori za kumtisha. Nilimhakikishia kwamba kila kitu nilichomwambia ni kweli na kama anataka kuthibitisha, ipo siku atajionea mwenyewe.
Nilimuona Raya akishusha pumzi ndefu, akainua shingo yake akiwa anatazama huku na kule kisha akanigeukia: “Kwa hiyo wewe ulikuwa umeamuaje?”
“Ni lazima nipambane nao.”
“Jamal, umechanganyikiwa nini? Unawezaje kupambana na watu hatari kama hao?”
“Ni lazima nifanye hivyo Raya, sipo tayari kufa kama kifaranga cha kuku mbele ya mwewe, ni lazima nipambane.”
‘Sidhani kama hilo ni jambo sahihi kwa sasa, isitoshe bado hata afya yako haijawa poa, kwa nini tusitafute sehemu nje ya Dar tukaenda kujificha huko na kuanzisha maisha yetu bila mtu yeyote kujua? Mimi nipo tayari hata sasa hivi na naamini nikiwaambia wazazi wangu watakuwa tayari kutusaidia,” alisema Raya, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama.
“Ni lazima nipambane Raya, siwezi kuwakimbia. Najua ni kazi ngumu lakini mwisho wa siku ni bora nife nikiwa napambana,” niliendelea kushikilia msimamo, raya akawa hana cha kuniambia tena.
Bado alikuwa na maswali mengi yaliyokosa majibu ndani ya kichwa chake, akawa ananiuliza kila alipokuwa anakumbuka. Aliniuliza kama watu hao ndiyo walioenda kuvunja nyumba yangu siku ile usiku, nikamjibu kwamba kwa ushahidi huo, inaonesha moja kwa moja kwamba ni wao.
Maswaliyalikuwa mengi mpaka ikabidi nimkatishe, nikamwambia anatakiwa kupeleka vyombo nyumbani ili na yeye apate muda wa kupumzika, nikamuona akisimama kwa shingo upande na kukusanya vitu vyake.
“Nimeongea na daktari, anasema naweza kuruhusiwa ndani ya siku hizi mbili kwa sababu naendelea vizuri.”
“Ooh! Itakuwa vizuri sana, sasa umepanga ukitoka ukaishi wapi?”
“Itakuwa ni siri yangu lakini kwa sasa sitakiwi kukaa pale kwangu kwa sababu najua watakuwa wananiwinda usiku na mchana.”
“Natamani sana tukaishi nyumbani kwetu, wazazi wangu wanakaribia kurudi lakini usijali ile nyumba ni kubwa, wanaweza kukupa hata vyumba vya uani, ukakaa hapo chini ya uangalizi wangu mpaka mambo yatakapotulia.”
“Ahsante sana mpenzi wangu, hivi kazini unaenda kweli wewe?”
“Kazini siendi, nimeomba ruhusa kwamba nakuuguza wewe, kwanza ukiwa kama mfanyakazi mwenzangu na pia ukiwa mume wangu mtarajiwa, kwa hiyo usijali,” alisema Raya huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, akakusanya vitu vyake, akaja kunibusu kisha akaniaga.
Akatoka na kufunga mlango, mara Shamila naye akaingia, ni kama alikuwa amekaa sehemu anasubiri aondoke tu ili na yeye aingie. Akaja uso akiwa ameukunja, nilishaelewa ni kwa sababu gani yupo kwenye hali hiyo.
“Vipi?”
“Mbona unapenda kunitesa Jamal, kwani huyo mwanamke wako huwezi kumkataza kukubusu mbele yangu?”
“Siyo hivyo mpenzi wangu, naomba kaa kwanza tuzungumze.”
“Sitaki, na kwa sababu yeye ameanza basi mimi namaliza,” alisema Shamila na kwenda kufunga mlango kwa funguo, akashusha na mapazia yote, nikawa sielewi alichokuwa anataka kukifanya.
“Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, nilishtuka kumuona akianza kufungua vifungo vya gauni lake la kazini, mara akalivua na kubaki na sidiria na nguo ya ndani tu, ukichanganya na jinsi alivyokuwa amegawanyika na kujaa sehemu za katikati, nilijikuta nikikosa cha kufanya.
“Una..ta..ka kufa...nya ni...ni,” sikumalizia kauli yangu, akawa tayari ameshafikapale kitandani, tukagusanisha ndimi zetu huku Shamila akionesha kweli kudhamiria kile alichokitaka. Hakuogopa kabisa kwamba pale ni wodini.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Back
Top Bottom