mastory
Member
- Dec 5, 2018
- 18
- 10
SIMULIZI:...............................UVUMILIVU BASI.
MTUNZI;..............................RAJA SAIDY.
WHATSAPP..........................0756920739. SMS;......................................0621047841.
YOUTUBE;..........................SIMULIZI ZA KWELI.
FACEBOOK PAGE;..................SIMULIZI ZA KWELI.
Utaratibu muhimu.
Hakikisha kabla ya kuanza kusoma simulizi hii ilike,baada ya kuwa umemaliza kusoma ndipo utoe maoni hii inasaidia katika kurekebisha nilipokosea.Like yako na maoni yako ni muhimu kwangu na nisapoti tosha sio uisome simulizi hii na upite mbali bila ya kulike wala kutoa maoni utakuwa hujanipa sapoti yoyote ile.
SEHEMU YA KWANZA ( 1 )
******
Mimi ni kijana wa kwanza katika familia ya Mzee Gasper,nimejaliwa kuwa na maendeleo makubwa katika familia yetu tofauti na ndugu zangu wengine.
Nilibahatika kujenga nyumba nzuri na ya kifahari nchini Tanzania.
Kazi yangu ya utangazaji katika Radio Maisha nayo ilinifanya nikawa na sifa nzuri huko nchini kenya.Siku zilizidikwenda nikaona ni vyema nitafute kazi nchini mwangu tanzania nikabahatika katika kufanya kazi katika shirika la utangazaji yani Tbc.
Hakika nilikuwa na maendeleo makubwa ila kitu ambacho sikujaliwa ni kuwa na Mke au Mpenzi,nikaona ni vyema kuoa kwani karibia familia yangu nzima walianza kelele za kunisihi niweze kutafuta Mke kwani umri wangu ulikuwa ukizidi kwenda.
Kauli zao ziliniweka katika wakati mgumu kwani sikutarajia kama ipo siku nitakuwa na Mke,kiukweli maisha yangu na Mke vilikuwa ni vitu viwili tofauti kwani niliona endapo nikioa hamna faida yeyote nitakayoipata.
Kama kawaida yangu katika swala la kuwaudhi wazazi sikuwahi kufikiria pia hata kuwaudhi wadogo zangu,hivyo nikaamua kuoa kwa kutafutiwa mshichana na rafiki yangu Yohana ili nipunguze kero zilizokuwa zikidi kila kukicha kutoka katika familia yangu.
Zilipita siku chache tayari nikawa nimeshapata Mke wa kuoa kiukweli Mke wangu alikuwa mzuri na kiufupi zaidi nilikuwa nikimpenda kwani muda wote alikuwa akitabasamu,pia akuacha kuonyesha vishimo shimo mashavuni mwake.
Ndoa ilifanyika bila kikwazo chochote nikapokea baraka zote kutoka kwa wazazi wangu pamoja na wadogo zangu,kwakuwa nilikuwa na nyumba hivyo haikuwa ngumu katika kufikiria nitamuweka wapi Mke wangu.
Mke wangu alikuwa anaitwa Sophia,kiukweli alikuwa ni mzuri sio siri alinifanya nikaanza kujilaumu yakuwa kwanini sikufanya uchaguzi mapema katika swala la kutafuta Mke.
Asemaye yakuwa kufanya kitu bila ya kufikiria hakusema uongo alikuwa sahihi,ni kweli kabisa siku zilivyozidi kwenda ndivyo visa vya ajabu vilianza ndani ya nyumba.
Nilipomuoa Mke wangu Sophia kila nilivyokuwa natoka kazini alikuwa akinipokea na kunipiga busu mashavuni,kisha anachukua mkoti wangu na kunipeleka hadi kwenye meza ya chakula.Baada ya kumaliza chakula alikuwa akinipeleka hadi bafuni na kuanza kuniongesha kama mtoto mdogo lakini kwa kipindi hicho ilikuwa tofauti sana kwani nilivyokuwa natoka kazini alikuwa akinitazama kwa jicho la dharau.Na nilipojaribu kuuliza kwanini hayo yote yanatokea lakini sikuweza kujibiwa chochote tofauti na kuzidi kuangaliwa kwa jicho la kejeli.
Hakika nilipiga simu nyumbani na kuwaomba ushari juu maisha ya kindoa,lakini jibu alionipa Mama lilinishangaza kwa kuhisi labda mimi nakosea.
"Mwanangu hayo ndio maisha ya ndoa pia mwanangu huyo ni Mke wako hofu yanini.."
Baada ya kusikia ushauri mzuri kutoka kwa Mama tabasamu lilinijia na kujikuta nakuwa na furaha ya ghafla japokuwa Mke wangu bado alizidikuwa katili.
****
Kuna siku niliwahi kurudi nyumbani kutokana na kichwa kuniuma kwa muda mrefu hivyo nikaona ni vyema kurudi nyumbani na kuamua kujipumzisha.
Nilipokuwa napiga hatua za kuingia ndani kiuweli hali ya nyumbani ilinishangaza kidogo kwani nilikuta nguo za Sophia alizokuwa amezivaa asubuhi zikiwa sebuleni pamoja na kandambili zake na nguo za kiume ikiwa ni suruali pamoja na mkoti huku vikiwa sebuleni.
Maumivu ya kichwa yalizidi maradufu lakini sikukata tamaa nilielekea hadi chumbani kwa kujihakikishia kilichokuwa kinaendelea kwani maisha yangu yalianza kuwa magumu kutokana na kuteswa na Mke wangu kwa kufanya vitu vilivyokuwa vikizidi kunishangaza kila siku baada ya siku.
Nilianza kwa kunyata huku moyoni nikimuomba mungu nisije kukutana na kitu chochote kibaya.Nilifika nje ya chumba ambacho nilikuwa nalala na Mke wangu,hakika nilishindwa kuvumilia kwani hali ya chumbani humo ilifanya mapigo ya moyo kwenda mbio.Nilianza kusikia miguno ya kimapenzi huku Mke wangu akiwa anazidi mumsifia mwanamume aliyekuwa anafanyanaye mapenzi.
"Baby wewe ni bora napenda unavyonipaga raha kila siku."
Hapo hapo nilidondoka kama mzigo na kujikuta napoteza fahamu.
******
Nilishtuka huku nikiwa sehemu nisioifahamu,nilianza kwa kuangaza pembeni yangu na kumkuta Mama yangu huku akiwa anabubujikwa na machozi ya furaha,pia niligeuka upande wa kulia kwangu na kumkuta Mke wangu akiwa anatizama chini na kushindwa kunitazama usoni mwangu.
Hasira zilinijia na kujikuta naanza kusimama kwa ajili ya kurudi nyumbani lakini kila nilipojaribu kuamka kuna kitu kilikuwa kikinizuia nilipojaribu kutazama kilichokuwa kinanizuia na kumkuta ni Mke wangu Sophia huku akiwa amenishika mkono.
"Mume wangu usiondoke kwani hali yako bado sio nzuri.."
"Niache malaya mkubwa wewe."
Nilimjibu jibu liliofanya aanze kulia kama mtoto mchanga huku akizungumza na Mama kwa hasira na jazba.
"Mama leo hii mwanao ananiona malaya ananiona sifai mimi."
Mama alianza kuzungumza na mimi huku akilia.
"Mwanangu punguza hasira bila Mkeo ungekufa mwanangu kwani amekukuta nje ya nyumba umeanguka na kupoteza fahamu.."
"Mama sio kweli huyu ni mala......."
Kabla sijamalizia chochote Sophia alinipigia magoti huku akinisihi nisiseme nachohitaji kusema.
Kwakuwa nilikuwa nampenda Sophia hivyo sikuendelea kuongea na kumtazama Mama kwa jicho la furaha.
"Mama muite Daktari aniondolee hii dripu."
Mama alitoka nje haraka haraka na kwenda kumuita Daktari kisha akaja naye.
"Pole sana kijana maana hali yako kwa sasa sio nzuri,umepata mshtuko wa moyo uliokupelekea kidogo upotezee maisha ila kama unataka hali hii isije ikatokea tena punguzo msongo wa mawazo jaribu kula matunda kwa wingi na tumia muda wako mwingi katika kupumzika ili tatizo lisije kuzua balaa jingine.."
Daktari alizungumza huku akizidi kuniodolea dripu.
"Kijana kwa sasa jaribu kuwa muangarifu ili hali hii isipate kujirudia tena."
"Sawa Daktari."
Nilitoka nje ya hospitali hiyo huku nikiambatana pamoja na Mama na Mke wangu.
Nilitoka mpaka nje ya hospitali hiyo kisha Mke wangu akakimbilia gari alilokuja nalo ili nipate kuingia lakini sikutaka kuambata na Mke,nilimomba kwa wakati huo ampeleke Mama nyumbani kwake nami atanikuta nyumbani.
Kisha nikapanda daladala na kuelekea nyumbani kwangu,nilivyofika nyumbani moja kwa moja nilielekea hadi chumbani mwangu na kujirusha hadi kutandani,nikiwa nimelala nilihisi nimekalia kitu kigumu gumu nilichoshindwa kujua kinahusiana na nini,nilianza kupapasa na kukishika kitu hicho.
"Mama yangu."
Nilizungumza kwa upole kwani sikuamini baada kuokota kidoge cha ARV na kujisemea moyoni.
"Mke wangu ana ukimwi..!!!!!"
Je,nini kitaendelea.............
Kama unataka muendelezo njoo whatsapp namba 0756920739 au sms namba 0621047841.
Sent using Jamii Forums mobile app