Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Leomosho ni sehem gan rombo au marangu.... na vp ile crater katikat pale ulipaoona..? How many minutes ulikaa Hapo summit
...?

Sent using Jamii Forums mobile app
Lemosho route tulitoka na gari hadi Londorosi gate; ndio tukaanza kupanda...
hiyo crater sikumbuki kuiona; ila nikikipa kibao cha summit mgongo, upande wa kushoto lipo lile bonde kubwa na kwa mbali kinaonekana kilele cha Mawenzi na upande wa kulia mbele kiasi kulikuwa na yale mabarafu makubwa.
Pale summit sisi tulikaa kati ya dkk 20 na nusu saa hivi tukipiga picha. Guide wetu alituambie tusikae muda mrefu zaidi kwa sababu ya hali ya hewa sio rafiki kwa afya na pia kupisha watu wengine nao wapate fursa ya kupiga picha kwenye Kibao
 
Samahani wakuu, hivi na wazungu hua wakuandika sentensi moja kwa kiingereza, wanachanganya na kiswahili kidogo?? Mpanda mlima sijapenda huko kuchanganya lugha.

Yule mama mzungu alofiwa mmewe alikua analia na kuongea kiingereza, ila wewe ukamkalili kwa kiswahili!! Nazani ulifanya hivyo ili hata tusiojua kiingereza tuelewe maneno ya mama mzungu.

Lakini cha ajabu umeandika kiswakinge bila kututafsria kama ulivyo fanya kwa mama mzungu.

Hongera kwa kupanda mlima. Pia niambie ule utaratibu wa kuvaa nguo safi zote hadi soksi na chupi hukupata sababu za kufanya hvyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmetamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh yani mimi sijaona faida yoyote uliyopata hapo......huko ni ku-jila tunasema jeshini
 
Daah we ni muandishi mzuri pia,NimeEnjoy sana utazan na Mimi nlikuepo kwenye safari....ASANTE SANA


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna njia ngapi za kupanda mlima kilimanjaro,na njia ipi ni nyepesi isiyokuwa na changamoto nyingi na pia njia ambayo ina vivutio zaidi kama hiyo hali ya kubusu jiwe sijui uliyoisema.?! Natamani nami siku moja nifike juu kilimanjaro
Kuna njia sita,marangu route,machame route,rongai route,shira route,lemosho route na umbwe route.
Njia nyepesi kuna marangu,ila watu wengi hawafikagi kileleni kwa sababu ya kutojianda vya kutosha kwa kusikika kwake kuwa ni rahisi hupelekea watu kupuuzia,pia hali yake ya hewa ni Pasua kichwa kupua kwa shida coz oxygen hupungua.
Machame,60% ya watalii wanaopanda kwa kutumia hii njia hufika kileleni,pia inavivutio kama shira platue,lava,baranco wall,na hapo jiwe la kubusu.
Rongai,hii kama marangu.
Lemosho na umbwe,hizi ndo njia ngumu zaidi sio za kitoto.
Vivutio kwa ujumla,kuna watu mbalimbali walioweka rekodi zao,kuna zonational of mountain Kilimanjaro from the bottom to the peak,unavyokwenda juu ndo umbali kutoka usawa wa bahari unaongezeka.
Changamoto,kwanza kwa wewe unayetaka kwenda kupanda mlima kutokufanya mazoezi ya kutosha, mfano kutokupanda mlima wa majaribio,waongoza watalii/guides baadhi yao hawapo makini,pia kitengo cha uokoaji sio makini.
 
Badala ya kuwa INSPIRED nimetishika. Kibonge mimi najiona kabisa ningeishia karibu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Hongera kwa kufika kilele cha mlima maana si jambo rahisi.
Ngoja niendelee kuomba Mungu inshallah nitapata nguvu za kwenda huko. Na nilivyo sipendi shida nikifika huko mambo yakibadilika nikimuwaza mwanangu naweza katisha safari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…