Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

Ushirikina na uganga ndo umelifukarisha bara la afrika
 
Wa meshsjigundulia mbwa hawa
 
Moja ya kitu ulichoshindwa kukifuata katika simulizi yako ni utaratibu, yaani umechemsha kwelikweli Daraja la miti yaani umeanza vizuri, baadaye umechanganya soda, energy drink na gambe humo humo nadhani maji yatakuwa chini 😷!.
Storry inaeleweka mbona labda wew ndo husomi kwa utaratibu...may be kuna mada umeziruka
 
so mkuu mpaka leo hujapata ndagu la kukufanya utoboe
 
Wengine ushirikiana na wezi kwa kuwapa matumaini feki ya kutokamatwa.Tushawatembezea kipondo waganga kama watatu hivi na kuwaunganisha na kesi za wizi.
mmewaunganishaje
 
Moja ya kitu ulichoshindwa kukifuata katika simulizi yako ni utaratibu, yaani umechemsha kwelikweli Daraja la miti yaani umeanza vizuri, baadaye umechanganya soda, energy drink na gambe humo humo nadhani maji yatakuwa chini [emoji40]!.
Sio kweli. Labda kichwa chako ndio kina shida. Hii story imetulia na inafundisha.
 
Inaendelea....
Mwenye Uzi anazinguaaa, haya someni kisa changu hiki cha Mganga.

Nilienda kwa mganga ili kupata kinga ya mwili dhidi ya wachawi na wanga. Nilipofika kwa mganga akanipokea vizuri. Nikamweleza shida yangu akaniambia sawa haina shida, nikamwuliza shilling ngapi akasema tsh 30,000/-.

Cha Kwanza akanielekeza chumba fulani nikaoge, yale maji yana mixer ya madudu mengi kidgo yalikuwa kwenye mtungi na yamefunikwa, nilikuwa mdadisi niliweza kuona mawe ya baharini, konokono wa bahari na fuvu la mnyama. Alinisisitiza nikiwa naoga ninywe hayo maji kidogo kama nayaonja hivi. Nilipomaliza kuoga nikamwita, mana aliniambia nimstue, akaja na mkia wake nahisi ni wa nyumbu au ng'ombe. Ni mpana na mweusi tii.
Alinipiga nao ule mkia na kuupitisha katikati ya miguu, Mara mikono Kama anafunga kamba kwenye mzigo wa kuni au furushi huku akizungumza na kuwataja watu(kwakuwa tunashea kabila machache nikimwelewa) alikuwa anataja majina ya viongozi wa koo mbalimbali za makabila ya ukanda ninakoishi.

Baadae akaniamuru niende kwenye chumba anachofanyia uganga, Mana anafanyia nyumbani kwake ana nyumba bora tu hata simtank analo, na katika maongezi niligundua kuwa ana trekta kwa ajili ya shughuli zake za kilimo. Kwenye hicho chumba nikakuta zana zake, mizizi mingi na makopo yenye unga wa miti na mbegu za miti, mafuta... Yaani makorokoroko kibao nikakaa kwenye kigoda. Yule mzee akanambia uganga wake Ni wa msumbiji na amerudi siku si nyingi kuchukua dawa mpya, kinga zake yeye Ni hatari sana na yeyote atakayejipiga kwangu nimpe taarifa kwani atamwagua yeye kwa kutoa kiasi cha laki3 Kama Mimi nitaridhia kumgeuza. Alinambia yeyote atakayechota nyayo, mkojo, mate, kivuli, kucha, nywele zangu nk.. kwa nia ovu, atakuwa RIP.

Akamtuma kijana niliyefatana naye akanunue sindano za kushonea nguo kwa mkono, aliporudi akazitwaa zile sindano akaanza kuuchanganya unga wa miti Toka kwenye makopo mbalimbali. Baadae ule unga uliochanganywa akaanza kunipaka sehem mbalimbali za mwili, paji la uso, kichwan kwenye utosi, magotini, kifuani had nyayoni. Akachukua mafuta flani mazito akanipaka mlemle alimopaka dawa ya unga.

Kisha akachukua zile sindano, akaanza kunitoboa sehem zote zilizopakwa dawa ili iingie mwilini. Nilipata maumivu makali hasa kichwan kwenye utosi, huyu hatumii nyembe kupiga chale. Ni sindano inatumika. Kisha akamaliza mwili ukiwa unachemka kwa maumivu.

Akachukua kibiriti, na chupa Kama ya beer hivi ipo tupu. Akaiwasha njiti moja ikiwa na moto akaiweka kichwani mwangu utosini penye ile dawa na mafuta, akachukuwa chupa akaukandamizia ule moto kichwani, Hadi Moto ukazimikia hapohapo, maumivu yake yalikuwa makali sana na yale mafuta yenye mchanganyiko na dawa, yakaanza kutiririka Hadi puani, shughuli hizo zote mganga alikuwa anazungumza tu maneno ya kiganga. Alipomaliza akasema ile dawa imekolea vizuri sana.

Kisha akanipa dawa ya kuoga siku 7 nyumbani, akaniambia toka dakika ile Jambo lolote baya nitakuwa naarifiwa, hata chakula chenye sumu kitamwagika kabla sijala.
Wanga wakikaribia home nitaamshwa.
Nikarudi zangu home kiukweli niliexperience utofauti sana siku za mwanzo, nilikuwa nastuka sana kutoka usingizini hata mchana nikikaa sebuleni usingizi ukianza kunishika tu naweza kuhisi mtu ananitingisha miguu kwa nguvu ili niamke, au nasikia kifaa kizito Kama nyundo kinagonga kichwani paaaa!!Mara moja naamka na pengine naitwa jina langu la kwanza, Mana Sasa Nina watoto naitwa kwa majina yao au jina la ukoo( Kama urio, sanga, massawe, Magufuli) lakini hiyo sauti inaniita jina langu la kwanza alafu naamka na kukosa usingizi tena.

Hali hii kwa sasa huwa inatokea mara chache usiku wa manane na nikiamka huwa ni saa7 au saa8 usiku nikicheki saa yangu.
Sijajua Kama Kuna watu wanapata kikwazo kuniwangia ila nilienda kupata kinga tu dhidi ya wanga na walozi. Sikufata utajiri Wala kufanikiwa kibiashara.

Nimeona Mwenye Uzi huu kakimbiaa
Nimeuchangamsha kidogo.
 

Hivi kushtuka mida ya kuanzia saa7-10 asubuhi hasa saa8 na 9 usiku, ina maana yoyote kiimani??
 
Kwa wale wavivu:

Part I: Page no 1 (Post #1)

Part II: Page no 3 (Post #58)

Part III, IV, V: Page no 6 (Post kuanzia #84)

Part VI: Page no 6 (Post #104)
 
Huwezi kuelewa ninacho maanisha na sihitaji kukujibu kwa jazba, NIDHAMU na ADILI navipa nafasi.
Unetisha sana mkuu, sasa huoni kama ndo umejipa shida zaidi maana bongo wanga ni daily usiku na mchana hahahaaa
 
Azabu tosha kahaa moto kwenye utosi
 
Hataree sanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…