Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

Watu wengi uenda kwa waganga lakini still mbona bado wanapigika na matatizo
 
Kuchimba madini sio mchezo, ni ulimwengu wa roho. Damu ya mtu wa karibu isikosekane.
 
Inaendelea

Nawashukuru mlionielekeza jinsi ya kuipost lakini baadhi ya vifaa sina na nipo ugenini kwahiyo tuendelee kwa mtindo huu huu.

Nilivyofika majini nikasimama kuitii ile sauti,sikumbuki kilitokea nini maana nilijikuta nipo ufukweni na mganga hakuwepo ila nguo zake zilikuwepo,sitaki kusema nilipoteza fahamu ila sijui nini kilitokea mmoja ya wale jamaa nilioenda nao ziwani aliniambia nilitoka majini mwenyewe na nilitembea kisha nilivyofika ufukweni nililala baada ya kuamka ndiyo nikaanza kuwaongelesha.Niliwauliza alipo mganga lakini hawakunipa ushirikiano walikuwa muda mwingi wanaongea kilugha kwahiyo mawasiliano kati yangu na wao yalikuwa magumu.Mmoja ndiyo alikuwa anajibu kwa kiswahili yule mwingine alikuwa haongei kabisa kiswahili.Kwa kifupi ile safari ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana na Mtanzania mtu mzima lakini hajui kuongea kiswahili.Tuliondoka kwa kupandisha milima hadi nyumbani kwa mganga ila nguo zake tuliziacha pale ufukweni, tulifika saa kumi na mbili asubuhi tulivyofika nyumbani kwa mganga kwa mshangao mkubwa nilimkuta mganga amekaa jikoni anaota moto akiwa amevaa nguo zile zile alizoziacha ufukweni akaniambia kaa hapo uote moto maji ya ziwani yalikuwa ya baridi sana.Kitu kingine kilichonishangaza ni wale wenzangu wao hawakuonyesha mshangao wowote kumkuta mganga pale kwake walivyofika wakawasha tumbaku wakawa wanavuta hawakuwa na wasiwasi wowote.

Muda wote tuliokaa kuota moto nilikuwa namuangalia mganga kwa makini ili kuhakikisha kama ni yeye mwenyewe au la,lakini alikuwa ni mwenyewe,nilibaki nimepigwa na mshangao nilishangaa sana nilijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu,alifikaje fikaje pale kwa sababu kwa umri wake wa zaidi ya miaka sitini isingekuwa rahisi kwa yeye kufika kabla yetu.

Kulipokucha aliwaagiza wasaidizi wake wamletee chura ,akaletwa chura baada ya kama nusu saa yule mganga alimchuna yule chura akiwa hai akachukua ngozi yake na kuichanganya na madawa mengine na kuichoma kisha alichukua majivu na kuyachanganya na madawa mengine na kuifunga kwenye mfuko mdogo,mfuko wa nguo ilikuwa kama hirizi lakini hakuishona aliifunga tu kwa uzi mgumu aliniambia niwe naingia nayo kwenye machimbio akanipa dawa nyingine ya kuoga kwa siku saba lakini nioge usiku tu njia panda.

Niliondoka nikarudi machimboni kama kawa niliona mabadiliko ila hayakuwa makubwa ingawa sina uhakika kama yalisababishwa na ile dawa au la.Baada ya muda nikaamua nika i boost lakini safari hii nilienda nchini Malawi.

Mganga wa Malawi

Nilifunga safari kwenda Malawi kwa kupitia mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela mkoa wa Mbeya,nchi zote za kusini mwa Afrika kuna uchawi na uganga unaofanana hauna tofauti,nilifika Malawi eneo lililo karibu na geti la Iponga nikashuka kwenye gari dogo nikiwa pamoja na Watanzania wafanyabishara wa kubadilisha fedha wa Kasumulu wote tulikuwa tunaenda kwa mganga.Nilifika nyumbani kwa mganga na kukaribishwa na wasaidizi wake na kupewa kiti kilichokuwa chini ya mti mkubwa wenye kivuli cha kutosha,Zamu yangu ilivyofika nikaingia kwa Mtaalam hakuwa kijana wala mzee nilimueleza shida yangu akanisikiliza na kunipa masharti ya kumpelekea kitovu cha mtoto mchanga kilichokatika na kumpelekea siku siku hiyo hiyo ,nikamwambia sawa nikaondoka kurudi Mbeya huku nikiwaza nitakipata wapi kitovu na kwa nani maana ili nikipate na kumpelekea kwa siku hiyo hiyo ilitakiwa niwe maeneo yale yale ya Malawi,Kasumulu,Kyela au Mbeya na kote huko sikuwa mwenyeji na ili nikipate ni lazima niwashirikishe watu ambao siwafahamu...yaani kitovu kidondoke au kikatike na kukipeleka siku hiyo hiyo ulikuwa mtihani.

Ulikuwa mtihani mkubwa pia kipindi hiko Mbeya kulikuwa na mambo ya kupiga watu nondo,mtu anapigwa nondo halafu nondo yenye damu inapelekwa kwa mganga,ningeanza kutafuta kitovu watu wangenihusisha na makundi yaliyokuwa yanapiga watu nondo na nilishuhudia mwenye mtu anapigwa nondo.Nilikuwa karibu na uwanja wa ndege wa zamani wa Mbeya kama unaenda shule ya msingi Pambogo nilikuwa na watu wachache kwenye bar moja ndogo ya mtaani muda wa saa mbili usiku nilisikia sauti ya mtu inaita mamaaa,,mwanamme mtu mzima alipigwa nondo mpaka akamkumbuka mama yake.Cha kushangaza kila mtu alikimbia hakuna aliyeenda kutoa msaada.

Niliamua niachane na mambo ya kutafuta kitovu na kurudi zangu kuendelea na shughuli zangu lakini niliamua kulala Mbeya mjini lakini kuna jambo ambalo mpaka leo lilinishangaza sana nilifika eneo linaloitwa Pambogo kwa ndugu yangu ni eneo nililokuwa nalifahamu kwa muda mrefu lakini siku ile nilipotea.Na kabla ya kwenda Malawi nililala pale lakini usiku ule niliitafuta ile nyumba kwa muda wa zaidi ya masaa matatu ....simu ilizima chaji na nyumba zote zina ua kwahiyo hakuna mtu wa kumuuulizia kila mtu alikuwa nyumbani kwake na ndiyo kulikuwa na mambo ya kupigana nondo kila mtu alikuwa muoga ,nilikuwa nazunguka tu kutafuta nyumba mtaa wote niliumaliza mwishowe nilikutana na vijana watatu walikuwa wanaenda kumsindikiza mwenzao ambaye walikuwa wanasoma wote hao ndiyo walinisaidia,nikawaulizia jina la mwenyeji wangu wale vijana walinicheka sana maana walinizungusha nyuma ya nyumba yao tu na nikawa nimefika kwa mwenyeji wangu.

Mganga wa Songea
Songea nilimfuata rafiki yangu tulikuwa tunamuita Mdigo huyu alikuwa anafanya biashara za matukio kwenye madini yupo,mahindi yupo ,kwenye ununuzi wa kahawa yupo ni mmoja kati ya binadamu wenye roho nzuri sana niliyepata kukutana naye.

Kuna mwaka mahindi yalipanda bei sana kwa sababu yalikuwa yanauzwa nje ya nchi kwa wingi Mdigo yeye aliuotea ule msimu akatukimbia mgodini akaenda kwa jamaa zake Songea kufanya biashara ya mahindi alipata sana hela msimu ule msimu uliofuata nikamfuata na mimi.

Huko nilikutana na majanga ya kupoteza kimaajabu milioni nane.

Itaendelea

kesho inaisha wamebaki waganga watatu.
 
Back
Top Bottom