Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

Simulizi yangu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi

Tukashuka chini tukakubaliana twende na moto wa kuni tukapanda nao,tukaichoma dawa ikawaka na kuteketea wakati nainama kuchukua majivu,akatokea nyoka mweusi mkubwa akawa anatoka upande mmoja akawa kama anatufuata ,niliinuka ghafla nikawa nataka kurudi kwa nyuma nilistuka sana lakini yule msaidizi wa mganga alinishika mkono kwa nguvu na kunizuia kutoka eneo lile.

Nyoka alitupita kwa karibu sana akawa anaelekea chini ya mlima,nikazoa majivu tukashuka nayo,tukafika kwa mganga,mganga akamuuliza yule msaidizi je,
nyoka alitokea,msaidizi wake akajibu ndiyo...nilibaki na mshangao.

Mganga akaendeleza uganga wake akanipa majivu na madawa mengine aliyoyafunga pamoja akaniambia niende kuyafukia kwenye kaburi,kaburi LA MTU mzima mwenye umri zaidi ya miaka hamsini na awe amezikwa zaidi ya miaka kumi na nifukie kabla ya SAA saba mchana,nikishindwa kwa Siku hiyo nifanye kesho yake muda huo huo.

Nikaondoka nikaenda kutafuta kaburi lenye sifa.
Nilitafuta kaburi pale mjini kuanzia makaburi ya Mfaranyaki,Ruvuma,Mkuzo nikaenda hadi kwenye makaburi yaliyo karibu na Chuo cha ualimu Songea Matogoro lakini kote huko nilikuta watu kibao,jambo langu
lilikuwa haliwezi kufanyika.
Ikabidi nitoke nje ya mji nikapata makaburi yaliyokuwa yamejitenga na yaliyokuwa na miti mingi kwahiyo kulikuwa na Giza kidogo.
Nikaanza kupita kusoma tarehe za kuzaliwa na tarehe za kuzikwa nikapata moja lililokuwa limejengewa lakini lilibomolewa na mizizi mikubwa ya mti iliyokuwa imepita kwenye kaburi.

Nikaanza kuchimba shimo katikati ya kaburi udongo ulikuwa umetitia ardhi ilikuwa ngumu sana kuchimba lakini nikatumia kipande cha mti nikafanikiwa kuchimba shimo dogo nikafukia dawa nikaondoka zangu.
Hela hazikurudi ila baada ya miaka kama mitatu yule tajiri nilikutana naye Madaba anafanya kazi ya kupakia magunia ya tangawizi kwenye roli.

Itaendelea.
Imebakia kwa mganga mmoja na stori za kutengeneza radi na kuita na kufukuza mvua.
 
Nikamwambia sawa endelea akaanza kujaza tyubu ikawa inajaa mwishowe mpira ukapasuka mganga akaniambia tushaua,nilistuka nikamuuliza unasemaje akarudia tushaua kwa sababu Mpira ulivyopasuka na matumbo ya wezi nayo yatakuwa yamepasuka,nikamuuliza sasa tunafanyaje akaniambia ondoka urudi kesho nikamwambia sawa,nikarudi getoni huku nawaza naanza tena kununua vitu.

Nikafika geto nikawasimulia jamaa zangu kilichotokea,walichukia sana nilipowaeleza sikwenda kwa binti Ndembo lengo lao lilikuwa kusikilizia kama binti Ndembo ni mganga kweli au la.
Wale vijana sikuwahi kuwaona tens.

Jamaa walikuwa magijwi wa kuzunguka kwa waganga, walikuwa wanaenda Msumbiji, Congo kufuata waganga.

Niliendelea kufanya biashara yangu ya mahindi wakati huo Mdigo alikuwa kaenda Msumbiji kununua magari mabovu na kuyaleta Tanzania na kutatengeneza kisha kuyauza,huyu Mdigo walikuwa na uwezo mkubwa wa kutambua fursa mapema ingawa naye alikuwa bingwa kwenye mambo ya ushirikina.

Baada ya Mdigo kuondoka na Mimi nilihama kwenye zile nyumba nikaenda kupanga kwenye nyumba moja ipo mtaa wa Mahenge,nilihama kwa sababu jamaa nilikuwa siendani nao pia biashara yao chafu ingeweza kusababisha tusombwe nyumba nzima.

Sababu nyingine ya kuhama nilikuwa nimepata demu mmoja anaitwa Y myao kutoka Tunduru alikuwa anakatika kuliko panga boi,alikuwa fundi kweli kweli,ningempeleka pale kwa jamaa zangu wangembeba tu,maana wao kuchangia demu kwao ilikuwa kitu cha kawaida.Pamoja na ufundi wake Y alikuwa mkorofi sana Mara kwa Mara tulikuwa tunagombana kwa sababu za kipuuzi na Mimi nilikuwa siyo mnyonge akizingua nilikuwa namzingua Mara mbili yake,Y akapata mimba,usiku wa SAA 4 anaweza akakuagiza ukamnunulie Coca cola,nilikuwa kijana Mdogo sijui lolote akiagiza hivyo lazima nimwambie maneno ya kijeuri ambayo alikuwa anachukia sana.

Ugomvi ukawa unaendelea mwishowe akaniambia naenda kutoa mimba yako nikamwambia nenda,nikampa elfu 30 akaenda kutoa,usiku akaja geto kulala lakini Siku hiyo hatukulala tumbo lilikuwa linamuuma akawa anajinyonga nyonga usiku kucha,sababu ya kuumwa ni kuna vitu walivisahau kuvitoa,Siku ile nilijua atakufa,SAA Tisa usiku nikazima taa zote za nje na ndani nikatoka nje ,pale nyumbani kwa nyuma kulikuwa na korongo kubwa nikawa naenda kuangalia njia nitakayoitumia kwenda kutupa maiti ya Y ikitokea amekufa.

Y hakufa lakini kama ningefanya vile ungekuwa uamuzi wa kipumbavu sana maana MTU wa kwanza kukamatwa ingekuwa mimi,watu wengi waliujua uhusiano wetu.
Nikarudi ndani Y alikuwa anaendelea kuugulia maumivu makali sana huku anajinyonga nyonga nilimuonea huruma sana.Nilikuwa sijaenda kanisani miaka mingi lakini Siku ile nilijikuta nasali sala zote,nilipiga magoti ,nilinyanyuka nikawa natembea huku naomba kama Walokole.

SAA 11 asubuhi Y bado alikuwa anaugulia maumivu makali nikapiga simu kuita boda boda ikaja ikampeleka kwa Daktari aliyemtoa mimba.
Mchana akawa amepona baada ya kwenda kutolewa vitu vilivyosahaulika.
Ukorofi uliendelea tukaachana.

Siku moja nilikuwa geto nikapigiwa simu kuna tajiri anataka mzigo nikaenda kumuona alikuwa kijana mmoja kutoka Njombe jamaa zangu waliniunganishia nikaenda nikamkuta kijana Mdogo mwenye mwili mdogo,walikuwa wanakunywa na kufanya maongezi na Mimi nikajiunga nao.
Nikafanya maongezi na tajiri tukakubaliana kesho yake atapakia mzigo na kulipa fedha zote,tajiri alikuwa anawanunulia pombe jamaa zangu lakini hela alikuwa anazitoa kwenye diary, nilijiuliza maswali mengi sana,alikuwa anafunua diary na kutoa fedha,hela zilikuwa haziishi wala diary haionekani kutuna.

Kesho yake muda wa SAA mbili usiku tajiri akalipa fedha milioni nane nikazichukua nikaenda nazo geto nikafunga mlango nikaziweka kwenye begi wala sikutoka Siku ile.
Asubuhi hakukuwa hata na buku,begi halijafunguliwa mlango umefungwa lakini fedha hazipo.Nilichanganyikiwa.
Nikaenda kijiweni kwa jamaa zangu nikawaeleza majanga ya
liyonikuta walisikitika sana wakasema itakuwa tajiri kazivuta.
Nikarudi geto huku nimechanganyikiwa nilijiuliza maswali mengi sana nakumbuka machozi yalinitoka.
Jioni nikaona namba ngeni inaingia kwenye simu yangu mtandao wa MCEL wa Msumbiji alikuwa Mdigo akaniambia Msomi nasikia wamekupiga,aliendelea kusema na ukiendelea na usomi wako watakupiga sana.Ingawa nilikuwa naenda kwa waganga lakini sikuwa nakubali
sana mambo hayo mazingira tu yalinilazimisha.
Siku ile niligundua naishi kwenye Dunia ya ushirikina ,nikatamani niajiriwe yaani nianze kuhangaika kutafuta ajira, nikakumbuka ajira walizokuwa wanafanya niliomaliza nao chuo, lakini nikikumbuka mishahara yao ya laki sita nikasema wacha niendelee kuishi kama wanavyotaka, yaani niendeleze ushirikina.

Kule machimboni Chunya kuna dogo mmoja nilipomaliza shule ya msingi nilimuacha madarasa manne,yeye alianza kuchimba zamani kwahiyo alibahatika kupata hela. Siku moja tuligombana aliniambia braza wewe umenizidi elimu na umri tu...Yalikuwa maneno ya ukweli ila yaliniuma.Kila nikiyakumbuka Yale maneno huwa nazidi kupata hasira niliapa ipo Siku nitamzidi elimu,umri na fedha.

Nikapanda pikipiki nikaelekea kwa mganga alikuwa anaishi kijiji kimoja kabla hujafika Namatuhi barabara ya kwenda Msumbiji.
Nilishaanza kuwa gwiji kwenye mambo hayo.Nilifika kwa mganga asubuhi sana nilienda kwa masuala mawili tu nizipate fedha zangu na nisiibiwe tena kizembe.

Itaendelea.
Pole sana mwamba
 
Pale madaba ulivyokutana na Yule Tajiri mwizi mbeba tangawizi ulichukua hatua gani ?
 
Back
Top Bottom