Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nakumbuka nilipokuwa mdogo, babu yetu alikuwa na utaratibu wa kuwakusanya wajukuu zake wote, na kuwasimulia hadithi mbalimbali; na masimulizi hayo yalikuwa yakifanyika huku tukiwa tunaota moto ili kuondoa baridi, huku yeye akipata kahawa iliyo chungu.
Kuna hadithi moja alitusimulia, inahusiano na machifu wa kizamani pamoja na maisha yao.
Kulikuwepo na chifu mmoja, ambaye alijaribu kulinda mila na desturi za kichifu, ilikuwa kila anapotembea, akijisikia kutema makohozi alikuwa hatemi chini; bali alimuita mpambe wake na kumuambia aachame mdomo na kumtemea.
Na alikuwa akifanya hivyo, akihofia kutema kwake chini makohozi, yangeweza kuibiwa na maadui zake au wachawi na hatimaye kuuwawa.
Alipokuja kufariki yule chifu, ilibidi azikwe na mpambe wake mmoja aliyekuwa hai ili aweze kumlinda humo ndani kaburini, ili mwili wa chifu usiweze kuibiwa; ingawa mpambe wake baada ya kufukiwa naye alikufa.
Hayo ndio yalikuwa maisha ya kale.
Tupe simulizi yako.