Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema (55), amesema ana msimamo na haogopi shinikizo la yeyote.
Werema amesema, Rais Jakaya Kikwete, anafahamu kuwa ana msimamo na pia waliowahi kufanya kazi na yeye wanatambua kuwa hafanyi uamuzi kwa kushinikizwa.
Bila shinikizo hakuna kazi, mimi ni mtu wa msimamo, aliyeniteua anajua msimamo wangu na hata waliowahi kufanya kazi nami wananijua sishinikizwi na mtu amesema Werema jana muda mfupi baada ya Rais Kikwete kumuapisha Ikulu, Dar es Salaam.
Werema anafahamu kuwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu inatuhumiwa kwa rushwa katika kuingia mikataba ya Serikali lakini yeye amesema ninaporidhika ndipo mikataba itatekelezwa sitaki kushinikizwa.
Amesema, hana taarifa rasmi kwamba, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inahusika kuingia katika mikataba mibovu.
Mimi sifahamu taarifa hizo nasoma kwenye magazeti hivyo nahitaji kufanya utafiti wa kutosha na kuwasiliana na taasisi nyingine za Serikali kupata taarifa kamili ndipo nijue kama nachukua hatua amesema.
Werema ana taaluma ya sheria ya biashara, namna ya kujadiliana katika mikataba na namna ya kufanya biashara ya umeme katika kubinafsisha nishati hiyo.
Amesema, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haina uhaba wa wataalamu wa mikataba na amebainisha kwamba, mikataba mingine wanalazimika kuingia bila kuwa na uwezo wa kujadili ikiwemo ya Benki ya Dunia.
Jaji Werema amewahi kuwa wakili wa Serikali kwa miaka 23 kuanzia mwaka 1984,na Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu kuanzia mwaka 2007.
Anachukua nafasi ialiyoiacha Johnson Mwanyika,yupo kwenye likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Mwanyika aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Desemba, mwaka 2005.
Rais Kikwete pia amemuapisha George Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Werema na Masaju waliteuliwa Jumanne, kabla ya uteuzi huo, Masaju alikuwa Mshauri wa Sheria wa Rais,Ikulu.
Rais Kikwete pia amewaapisha Makatibu wakuu wa Wizara za Serikali na maofisa wawili waandamizi wa Serikali. Rais aliwateua Jumatatu wiki hii.
Rais amemuapisha David Jairo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbarak M. Abdulwakil kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Amemuapisha pia Christopher Sayi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, na Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais.
Nakwenda kujifunza kwa nitakaowakuta na kushirikiana na wanasekta za habari, michezo na utamaduni amesema Kamuhanda.
Mbena, amesema, atamsaidia Rais Kikwete katika mambo mbalimbali yanayomkabili likiwemo tatizo la umeme, kuyumba kwa uchumi, usafirishaji, na uchaguzi mkuu mwakani.
Chanzo: Gazeti la HabariLeo