Benki na taasisi nyingi za fedha zinatoa mikopo, lakini unatakiwa kuwa na TIN namba,leseni ya biashara akaunti ya benki husika,biashara isiyoamishika,yaani isiyo na kituo maalum.Masharti kwa benki nyingi yanaenda mbali zaidi kutaka uzungushe akaunti,yaani uwe unaweka na kutoa kwa kipindi fulani pesa katika akaunti yako.Hiyo hati ni dhamana tu na niya baba yako,siyo yako, itabidi huyo mzee akakudhamini kwa hati hiyo,kuna benki haziitaji biashara zinaweza kutoa mkopo lakini mengi kama nilivyoeleza.
Hitaji la mtaji wenyewe ni pesa kidogo hivyo km mwanachama mmoja alivyoeleza,unaweza kwenda finca,pride,advans bank,equity kwani wanakubali dhamana nyingine zaidi ya nyumba kwa kiasi hicho.Pia kuna mikopo wa vikundi hii haitaji dhamana yako, bali wanchama wanajidhamini wenyewe.