Habari zenu marafiki... Kwa kifupi ninawazo la kufanya biashara japo mkononi sina pesa za kutosha. Nilipo mueleza baba leo amenipa hati ya nyumba yake nitafute mkopo benki. Sijui hata nianzie wapi. Nina laki 9 mkononi na nina hitaji japo milioni 4 au 5 wazo langu litimie. Naombeni ushauri kwa mwenye ufahamu wa kutosha juu ya hili.
. AsanteMwanangu, jaribu kwenda kwenye Banks mbali mbali na uwaulize watakupa ushauri wakutosha kabisa
Nina hakika kama nyumba iko kwenye hali nzuri na inathamani kiasi BANK WATAKUPATIA MKOPO
NAKUTAKIA KILA HERI NA BARAKA TELE NA MSHUKURU MZAZI WAKO
Mkuu kwa thamani ya nyumba yako hata kama iko utete rufiji? ukaiweke rehani kwa mahitaji ya 4m? inakuingia akilini?
ww nenda finca, pride au ccm(wana anzisha mikopo kwa vikundi vya vijana) watakupa hiyo 4m ukifwata mashariti yao
Jaribu kuwaona Equity Bank
Niuzie hiyo nyumba.
Benki na taasisi nyingi za fedha zinatoa mikopo, lakini unatakiwa kuwa na TIN namba,leseni ya biashara akaunti ya benki husika,biashara isiyoamishika,yaani isiyo na kituo maalum.Masharti kwa benki nyingi yanaenda mbali zaidi kutaka uzungushe akaunti,yaani uwe unaweka na kutoa kwa kipindi fulani pesa katika akaunti yako.Hiyo hati ni dhamana tu na niya baba yako,siyo yako, itabidi huyo mzee akakudhamini kwa hati hiyo,kuna benki haziitaji biashara zinaweza kutoa mkopo lakini mengi kama nilivyoeleza.
Hitaji la mtaji wenyewe ni pesa kidogo hivyo km mwanachama mmoja alivyoeleza,unaweza kwenda finca,pride,advans bank,equity kwani wanakubali dhamana nyingine zaidi ya nyumba kwa kiasi hicho.Pia kuna mikopo wa vikundi hii haitaji dhamana yako, bali wanchama wanajidhamini wenyewe.