RUKUKU BOY
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 1,516
- 1,775
Wakuu pole na shughuli za kila siku, Mimi ni kijana nafanya kazi kwenye kampuni moja ya kimataifa apa Tanzania.
Kutokana kuwa kampuni kuwa ya kimataifa uwa wanaletwa wafanyakazi kutoka maeneo tofauti duniani. mwezi wa pili mwaka Jana kuna dada aliletwa ni mzungu, basi alipangwa kwenye kitengo ambacho nipo mimi.
Baada ya muda tulizoeana na yule dada yaani me ndo nilikuwa rafiki yake na kama ndugu, huyu dada alikuwa kapanga nyumba nzima apa Dar, baada ya muda mazoea yalizidi tulijikuta tushakuwa wapenzi, kwa kweli alinipenda na mimi nikampenda, inshort tulienjoy na tukapeana promise kibao.
Mwezi wa 8 mwaka huu alipata safari ya kikazi akaniachia kila kitu ili niwe naviangalia aliniachia nyumba yake pamoja na gari, usiku wa tarehe 17 mwezi wa10 sitausahau kwani aliniambia ukweli kuwa ameamishwa kikazi na amepelekwa Lisbon-Ureno, aliniambia aliogopa kuniambia akiwa TZ eti ningeumia sana na huenda ningemfanyia ujuma ili asihame, nilipo muuliza Manager akaniambia kuwa yele dada ameamishiwa ureno na harudi tena bongo.
Yaani nimeumia saaaaaaana, yule dada akaniambia kila kitu alichoacha nichukue ameacha vitu vingi Kama Gari, nguo zake unaweza jaza Lori, na vitu vya ndani, fridge, computer, n. k na kuniambia nimwambie baba mwenye nyumba kuwa mpangaji wake harudi tena, kwakweli nimemjibu kuwa nilikupenda wewe hvyo vitu vyako sivipendi.
NB. Wanaume tusikurupuke na wasichana wa kizungu.
......................................................... ..
UPDATES
walinifata watu wengi kuhusu hii mada, ila huyu dada nimeachana nae mazima, tarehe 26 mwezi uliopita aliolewa mazima. Too painful, sitaki tena kusikia mwanamke