Sina hela kabisa kodi inasubiri bado watoto wanaumwa, watu wa karibu wamenikimbia

Sina hela kabisa kodi inasubiri bado watoto wanaumwa, watu wa karibu wamenikimbia

Pole kamanda ila maisha ni vita, pigano moja uliloshindwa haliamui hatma ya wakati ujao, simama futa makalio nyanyua Anza safari kwa nguvu mpya
 
Pole.sana Mkuu!!

Pesa zako zipo Bado kidogo zitakufikia!

Hebu nenda sehemu tulivu sana!mwambie Muumba akupe fungu lako katika kipindi hiki!!

Mlilie machozi akuonyeshe mwelekeo,mara nyingi huwa tunategemea akili zetu pekee,hebu nenda kwake kama mtu usie na plan ili akupe namna Kwa maana yeye haishiwi namna!!

Mungu akubariki!
 
Habari wanaJF !
Tuendelee kupeana moyo kiukweli ni faraj kwa watu wenye matatizo
  1. Kama huna ajira rasmi au umejiajiri lakini mambo yamebana sana, fikiria kubadili mazingira. Usikaze shingo mjini wakati gharama zinakukandamiza. Nenda kijijini ambako maisha ni nafuu, hata kwa muda wa miaka miwili tu. Baada ya hapo unaweza kurudi mjini ukiwa umepumua kidogo.
  2. Mfano mzuri ni maeneo kama Tukuyu. Huko utapata maisha ya aina mbili—ya kijiji na ya mji mdogo. Chakula bei yake ni rahisi sana, watoto hawatakosa lishe, na huduma muhimu zipo kama shule za msingi, sekondari na hata vyuo.
  3. Wengi hupoteza nguvu kwa kung’ang’ania maisha mjini ilhali kuna sehemu ambako gharama za maisha ni nafuu na unaweza kupanga upya maisha yako. Usione aibu kubadili goli, maana hiyo ndiyo mbinu ya kuokoa hali yako na familia yako.
  4. Napendekeza achana kabisa na kuwafikiria watu wako wa karibu waliosepa kwenye maisha yako. Zama tulizopo inatakiwa upambane kivyako kwelikweli. Ujamaa unatajwa tu lakini haupo. Pambana, pambana, pambanaaaa

N'yadikwa
 
Pole.sana Mkuu!!

Pesa zako zipo Bado kidogo zitakufikia!

Hebu nenda sehemu tulivu sana!mwambie Muumba akupe fungu lako katika kipindi hiki!!

Mlilie machozi akuonyeshe mwelekeo,mara nyingi huwa tunategemea akili zetu pekee,hebu nenda kwake kama mtu usie na plan ili akupe namna Kwa maana yeye haishiwi namna!!

Mungu akubariki!
🙏🏽🙏🏽
 
Back
Top Bottom