Sina kazi nashinda na simu muda wote

Ungemueleza unafanyaje fanyaje HUYO KIJANA nafikiri angejifunza sana
 
Hongera sana kwa kuchagua maisha mepesi wala usijitese mdogo wangu maisha yenyewe haya mafupi we cheza magame, hela ya bando si unapewa lakin?
 
ndo kazi yenyewe sasa

wengine pia hawapati muda huo wa kukaa na simu wanakuwa na kazi nyingine
 
Vua aibu uweke pembeni, hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako mwenyewe, siyo kwa wazazi, ndugu au rafiki zako. Vile utakavyoamua kuwa ndivyo utakavyokuwa
If you do not know where you're going any road will take you there
 
KAZI zipo, ajira ndio hazipo.

Weka pembeni vyeti, tumia nguvu na akili Mungu aliyokujalia kufanya KAZI m alimbali katika mazingira uliopo upate kipato.

Uza hata maji Kwa kutumia guta la kukodi.

Baada ya miezi kadhaa, utapata mtaji wa kuanza kuzifikia ndoto zako Pole pole

Ubarikiwe.
 
Unashinda na simu muda wote na hujui kuhusu online business zipo nyingi sana ama hyo simu unashinda nayo xvideo
 
Sina kazi nashinda na simu muda wote
Nipo nipo tu sina muelekeo wowote
Nimemaliza Chuo mwaka Jana
Lakini mpaka sasa hata Senti Moja Sina
Ungekuwa unakaa nyumbani kwangu, haki ya nani ungeenda shamba kwa lazima. Na ungegoma kwenda, ningekutimua au kukunyima chakula.
 
Sina kazi nashinda na simu muda wote
Nipo nipo tu sina muelekeo wowote
Nimemaliza Chuo mwaka Jana
Lakini mpaka sasa hata Senti Moja Sina
Ngoja nikusanue uza sm kanunue mayai trei tano kila siku asubuhi Chemsha trei mbili ingia mtaani kwenye mkusanyiko wawatu uza kwenye mabar, vituo vya usafiri hakikisha unakata mitaa, ikifika jioni rudi nyumbani komaa upate pesa ya kununua kingamuzi cha azam na TV ukipata hivyo vitu, tafuta vijana wawili wape wauze mayai wewe anzisha kijiwe uswahilini cha kuuza maziwa fresh, uji wa ulezi na karanga hiyo TV na kingamuzi cha azam iwepo hapo wale wazee na vijana wasiopenda pombe kitakuwa kijiwe chao wanapiga soga uku unafanya biashara ukikomaa na imani kwa siku hutokosa faida elfu 20 na mtaji upo haya elfu ishirini mara 30 sawa na laki sita anza malengo ma kuwanza mambo makubwa zaidi kama kuanzisha kibanda cha chakula nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…