Sina mzuka na mamito wangu...


1. Unafikiri ni kitu gani kinakufanya uwe karibu na mama mkubwa wako au baba mdogo wako?
2. Ni quality gani walizo nazo hao ulo karibu nao zinakufanya uwe huru nao?

Nitakuja kwenye angle ya 'usomi' baadaye.
 
1. Unafikiri ni kitu gani kinakufanya uwe karibu na mama mkubwa wako au baba mdogo wako?
2. Ni quality gani walizo nazo hao ulo karibu nao zinakufanya uwe huru nao?

Nitakuja kwenye angle ya 'usomi' baadaye.

1. nishajibu kwa pm
2.nilitokea kumpenda tu ba mdg angu mara tu baada ya baba kufariki ye pia ananipenda sana, na ndo nikiwa na shida yoyote ile nafeel huru kumuelezea hata kama inahusu mahusiano
 
Ni mama angu ndio, amenilea na hadi leo bado nipo kwake!!!!!!!
hata mi sina amani na hii na nahisi hata ye anajua sina mzuka nae

Oh! pole sana my sister!
Suluhisho la hilo tatizo ni KUISHI MBALI NAE! Hii haitakuwa na maana kama usiwasiliane nae, usimtembelee au huhitaji msaada wake.
Note: Uwe na hoja ya msingi ya kuishi mbali nae, eg: kuolewa au kuishi na ndugu zako wengine ukilindwa na sababu kama vile, kuishi nao kunaboresha au kurahisisha kazi au masomo.
Kuna maneno wazazi wetu huongea bila kuzingatia yatakavyopokewa, for them wanahisi mtu akisoma anakua MKAMILIFU. Thus why anashangaa kuona msomi anakosea kitu ambacho yeye mso elimu anajua how to do!
It seems we mwenyewe uko direct, unajiamini sana na (unapenda kulipiza kisasi - may be).
Hayo ni maoni yangu tu...!
Sorry kama nimekukwaza.
 

Ahsante kwa ushauri, mi naishi mbali nae ila kwa sasa nimekuja likizo na soon
nitarudi kwangu...
hapana mi si mtu wa kisasi hata kidogo, na hata ningekuwa na kisasi siwezi kumfanyia mama angu!!!!!
 
Kila nafsi itaonja umauti,kama ikifika zamu ya mama yako(siombei hivyo) ndipo utakapouona umuhimu wa mama duniani....
 
Ahsante kwa ushauri, mi naishi mbali nae ila kwa sasa nimekuja likizo na soon
nitarudi kwangu...
hapana mi si mtu wa kisasi hata kidogo, na hata ningekuwa na kisasi siwezi kumfanyia mama angu!!!!!

Thanx kwa kunielewa...
Nakutakia kila la heri... (NANI KAMA MAma!).
 
My dear, natamani kukuuliza umri wako. Lakini kadri unavyokua mkubwa ndipo ukaribu na mama utakuja naturally. Unless one of you is a character. Kuna issues ukikutana nazo utatamani sana kushare na utamuamini mama pekee. Mie ni mtoto wa baba, lakini niamini; ukubwa ulinifanya niwe karibu na mama automatikale.
Ushauri wangu...jitahidi kumpenda na kumthamini wakati yupo. Kuna siku utaamka nae atakuwa hayupo. Appreciate at least she is keeping your home(ukirudi home ukakuta hakuna aliefagia na kila kitu kiko misplaced utahuzunika mno!). Usijilazimishe kumuambia i love you, na usiamini wanaoandika fb 'i love mom' sijui na nini! Wengi wanaandika tu na hawawaambii mama zao hayo maneno. Telax, you are normal!
 

Kwa majibu haya naweza kusema kwamba wewe, unahubiriwa na nafsi yako kwamba mama yako anakuonea na hata imefikia kwamba inakuambia kwamba hakupendi. Nafsi yako huwa inakusemezesha haya ikitaka akili yako isimame na mwili na hisia zako ndizo zikuongoze.

sijui wengine kama akina Kaunga watakuwa wamelionaje lakini kinachokusumbua ma dearest ni ushuhuda mbaya unaopewa na nafsi yako, thats why hata mama yako akikugombeza unaona vibaya na anapojirudi kukuomba samahan unaoana kawaida tu. kwangu mimi ningeumia sana mama akinibembeleza niachilie moyo, ama pia anaponigombeza manake definately nitajua kwamba nimekosea mahali and she wants me to change.

Jambo la kufanya hebu achilia kila kitu, ondoa uchungu, wimbo wa uonevu, akili ya kutengwa nadani yako. Kisha anza kujifunza kuona mema ya mama yako. hebu fikiria kwamba anagekubana mlangoni usigekuwa hai leo hii, hebu fuikiria kwamba angekuachia moto ungekuwa kilema leo hii. hebu fikiria jins ambavyo ulimsumbua kwa kulia usiku, akawa na sleepless nights, ukamkojolea wala hakujali, pengine kuna muda ulimliza kwasababu tu ya kushindwa kutimiza mataakwa yako, yakumbuke haya ili uone sasa unalazimika kuwa na upendo nae.

sijui nisemeje ila kama kweli huna mzuka nae pengine ukizaa unaweza kuja manake ukipata karaha za kichanga lazima utakubali kwamba mama yako anahitaj upendo wako.
 
Last edited by a moderator:

Kwenye thread hii, na mie ninaomba niwe mwanafunzi maana................................ Da Mkubwa Kaunga na wengine please help
 
Last edited by a moderator:

Wala hata sisemi naonewa, wala kugombezwa kwangu sio ishu na nnapenda nikikosea niambiwe
ila basi tu mi huwa sina mzuka na maza yani ile kumfeel huwa sina mbali na hapo sina tatizo....
na nnatambua bila yeye nisingekuwa mie na ndo maana nataka solution niondokane na hii hali!!!
 

Ahsante am 24 years old!!!!!!
nitajitahidi kujenga huo mzuka, make sio kuwa simpendi kumpenda nampenda....
 
Kila nafsi itaonja umauti,kama ikifika zamu ya mama yako(siombei hivyo) ndipo utakapouona umuhimu wa mama duniani....

Nahitaji ushauri jinsi ya kujenga ukaribu na maza angu
sio maneno ya kuzidi kuniumiza, hii situation nilonayo inatosha kuniumiza
ahsante.
 
Evelyn Salt, Pole sana mwaya kwa yalokukuta. Kwanza jitahidi kumuomba Mungu aondoe hicho kizingiti kilichopo moyoni mwako, then jitahidi kufanya mawasiliano ya kila mara, hata kwa kuweka alamu kama mchangiaji alivyosema. ingekuwa upo under 18 ningesema akili bado haijakomaa. Lakini tambua Mungu atakusaidia
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye red, uapokosa unaonyesha ishara gani ya mama kukwazika? unajua kipindi hichi tofauti na kipindi chao maybe kuna vitu anavyo-relate na zama nyuma kuwa wasomi walikuaje.
 
Just ni-pm. Nitakupa ushauri.
 

Ahsante sana awp...
nitafanya hivo
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye red, uapokosa unaonyesha ishara gani ya mama kukwazika? unajua kipindi hichi tofauti na kipindi chao maybe kuna vitu anavyo-relate na zama nyuma kuwa wasomi walikuaje.

mi huwa nanyamaza tu siwezi kumjibu mami angu hata kuargue nae sijawahi asee!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…