Pole, ila kesi yako kidogo nyepesi kwani una ushahidi wa mambo , na kama waswahili wasemavyo kikulacho kinguoni mwako.ila inaonekana una moyo wa subira na uvumilivu kwani mtu mwingine angesha mwaga mboga hapo, alichokifanya mumeo sio jambo la busara hata kidogo kama kuna mapungufu kutoka kwako alipaswa kukuweka chini na kukueleza mkarekebishana japo inawezekana pia hakuna anachokikosa kwako ila ni uendawazimu wake tu.
Nini chakufanya sasa.
Mweke chini mume wako ninyi wawili mzungumze si kwa ugomvi jaribu kutulia kabisa, umweleze the whole issue na kwamba umeshajua kinachoendelea baina yake na huyo rafikiyo, lakini pia jaribu kumuuliza kama angejisikia vema wewe kufanya alichokifanya yeye, zungumzeni muyamalize kwa amani kuachana sio solution, kama ni mume mwelewe atakuelewa lakini pia tumia staha ya kike katika kuzungumza nae, zungumza toka moyoni, akileta kiburi shirikisha wazazi.
Kwa rafikiyo huyo nae, ukishamalizana na mume wako mkayamaliza nae mwite siku moja kwa lunch nyumbani kwako wakati mumeo hayupo mweleze ulichokigundua lakini pia mweleze jinsi ulivyojisikia na jinsi gani hukupendezwa na tukio hilo najua ni vigumu ku control emotions sometimes ila jaribu utaweza, ila inategemea pia ni rafikiyo kwa level gani, siwezi kuandika kila neno ila naamini mtayamaliza kwa amani, wala huna haja ya kuanzisha vurumai mpaka majirani wakajua kinachoendelea.
Sio kwamba natetea uovu walio ufanya HAPANA; ila tumia busara kumaliza tatizo atakuheshimu kama ni mwanaume kweli na utaona mabadiliko, ILA KATIKA YOTE HAYO MTANGULIZE MUNGU:
Bye.