GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Tuliaminishwa Kipa Jefferson Luis ni bonge la Kipa mara ghafla akalazimishwa ajifanye kaumia ili aachwe na achukue hela yake ya bure ya Tsh. 150 milioni na wapigaji wachukue Tsh. 250 milioni na ikaishia hapo.
Simba Day tukatambulishwa Kipa Abel ambaye alishafungwa na Simba SC goli 6 au 7 alipokuwa na Timu yake Prisons FC kama sijakosea.
Tukiaminishwa kuwa ni Bonge la Kipa kumbe Kocha Mkuu kamtizama na hata tajiri nae akatonywa na Wakala mmoja wa Wachezaji wa Tanzania kuwa hakuna Kipa hapo na aachwe lakini wanaona aibu kumuacha kwani wataonekana ni Waswahili na wapuuzi wakati tokea zamani wenye akili akina GENTAMYCINE tulishawaona wako hivyo.
Mara tena tajiri nae (kama kawaida yake) kwa kupenda kukurupuka kaenda kumleta Kipa mwingine Ayoub wakati akijua kikosini tuna lundo la makipa na wengine wanatakiwa kutolewa kwa mkopo ili wakajiimarishe zaidi.
GENTAMYCINE namalizia kwa kuwaacha na swali je, tuliwezaje kutumia muda mrefu kuwasajili akina Onana, Chamalone na Miquissone na tukasahau kuanza na kwa kipa ambaye ndiyo msingi mkuu na mhimili wa mafanikio ya klabu yoyote kiufundi?
Hata kama tumechukua Ubingwa wa Community Shield Cup hivi majuzi tena mbele ya watani zetu kule Tanga ila GENTAMYCINE sitoacha au kuona aibu kuwasema kwa mapungufu yenu yanayokera ambayo nayaona, yanakera na hayavumiliki.