Sina uhakika kama diadora ndo watengezaji wa jezi za Simba

Sisi wa bongo wengi wetu uwa tunaingia chaka ki urahisi sana, Kama ulifuatilia zile ahadi za ule mkataba na uka zi tafakari, mtu makini lazima upate wasiwasi kwakua hazitekelezeki kwa Mazingira yetu ki u uwekezaji au katika biashara ya kawaida.
 
Kwani Mkuu kwa hii misimu mitatu iliyopita ni lini Simba walikuwa na Jezi nzuri? Kumbuka ile timu imejaa makanjanja almaarufu wazee wa 10% kwenye kila idara kwahiyo wanachozingatia ni maslahi binafsi kwanza kisha timu baadaye.
Kwa kifupi kwasasa Simba ipo mikononi mwa madalali wabobevu
 
Kuna wale wengine wameamua kubana matumizi kwa kushona sare zitakazovaliwa kwenye mechi na vikao vya chama.
 
Jezi ya Chelsea ya home msimu uliopita na msimu huu ya away ni jezi kali sana.
 
Ukiondoa quality ya picha, kama kweli hizo zilizovuja ni jezi mpya za Simba, basi ni jezi kali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…