Sina uwezo wa kifedha kusoma chuo kikuu

Sina uwezo wa kifedha kusoma chuo kikuu

Finder boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
608
Reaction score
150
Napenda nianze kwa salaam, wakubwa shikamoni, wadogo habari zenu. Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mchepuo wa HKL, nimepata III ya 15 (HistoryE KiswahiliE LanguageE General Studies S).

Kwa kifupi baba yangu alifariki toka kitambo na ninaishi na mama yangu ambaye naye hajiwezi kiuchumi. Elimu yangu ya sekondari nilisaidiwa na jirani yangu ambaye naye kwa bahati mbaya kafariki mwezi machi mwaka huu. Nimejaribu kuulizia kwa wanachuo kuhusu uombaji mkopo chuo kikuu wakanambia naweza kuomba mkopo na nisipate au ata nikipata ni asilimia ndogo.

Hivyo kwa yeyote anayejua hatua za kufuata iliniweze kupata mkopo angalau asilimia 90% aweze kunisaidia. Nahitaji sana msaada wenu.

Asanteni na Mungu awabariki.
 
Penye nia pana njia. Usikate tamaa endelea najitihada zako utafanikiwa, kaonane na Wakuu wa Jumuiya mbali mbali jijini.

Hutatoka mtupu. Go ahead.
 
Mungu yu pamoja nawe,kajaribu sehemu mbali mbali naamin utafanikiwa maana Mungu hamtupi mja wake.
 
Pole sana cha muhimu ni kuomba coz za kipaumbele kwa bodi kama eductn itakufaa
 
Napenda nianze kwa salaam, wakubwa shikamoni, wadogo habari zenu. Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mchepuo wa HKL, nimepata III ya 15 (HistoryE KiswahiliE LanguageE General Studies S). Kwa kifupi baba yangu alifariki toka kitambo na ninaishi na mama yangu ambaye naye hajiwezi kiuchumi. Elimu yangu ya sekondari nilisaidiwa na jirani yangu ambaye naye kwa bahati mbaya kafariki mwezi machi mwaka huu. Nimejaribu kuulizia kwa wanachuo kuhusu uombaji mkopo chuo kikuu wakanambia naweza kuomba mkopo na nisipate au ata nikipata ni asilimia ndogo. Hivyo kwa yeyote anayejua hatua za kufuata iliniweze kupata mkopo angalau asilimia 90% aweze kunisaidia. Nahitaji sana msaada wenu. Asanteni na Mungu awabariki.
ndugu education ndo itakayokufaa ingawa unaweza usipate asilimia 100...
 
kuhusu mkopo usiogope...mkopo ni probability hivyo omba na utapata... but usiende kusomea usichokitaka kisa mkopo...unaweza kuchaguliwa na utakachopewa kikawa hakitoshelezi bado
 
kuhusu mkopo usiogope...mkopo ni probability hivyo omba na utapata... but usiende kusomea usichokitaka kisa mkopo...unaweza kuchaguliwa na utakachopewa kikawa hakitoshelezi bado

asante!
 
Kwanza hongera kwa kufaulu!

Pili kuhusu mkopo ucogope ata ukipata asilimia 50 hiyo nyingine utatoa kwenye boom ujazie hapo hzo 50 nyingine na maisha yataenda na chuo utamaliza.

Cha muhmu ujue umefuata nn chuo na c starehe sawa bwana mdogo! Pombe club na umalaya ni adui wa boom!
 
Apply haraka SAUT kuna scholarship degree ya tourism kama utapenda
 
Napenda nianze kwa salaam, wakubwa shikamoni, wadogo habari zenu. Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita mchepuo wa HKL, nimepata III ya 15 (HistoryE KiswahiliE LanguageE General Studies S). Kwa kifupi baba yangu alifariki toka kitambo na ninaishi na mama yangu ambaye naye hajiwezi kiuchumi. Elimu yangu ya sekondari nilisaidiwa na jirani yangu ambaye naye kwa bahati mbaya kafariki mwezi machi mwaka huu. Nimejaribu kuulizia kwa wanachuo kuhusu uombaji mkopo chuo kikuu wakanambia naweza kuomba mkopo na nisipate au ata nikipata ni asilimia ndogo. Hivyo kwa yeyote anayejua hatua za kufuata iliniweze kupata mkopo angalau asilimia 90% aweze kunisaidia. Nahitaji sana msaada wenu. Asanteni na Mungu awabariki.

Finder boy.

Kwanza hongera.

Pili nakushauri hivi. Tafuta cheti cha kifo cha mzee haraka iwezekanavyo ili umbatanishe na form za mkopo
sehemu ya mdhamini muweke mama kwenye fomu za mkopo, Kingine omba bachelor ambayo ina priority ya mkopo, mathalan unaweza kuchagua education mkopo utapata na ajira yake ipo wazi ...kama kweli una shida usijisikie vibaya kumbiwa unasoma education.

Be consistent and stay focus on your goals!
 
Pole sana, usikate tamaa. Nenda kwenye taasi za dini may be unaweza saidiwa.
 
Pole sana, nenda RITA kaandikishe death certificate ya baba yako ambatanisha cheti hicho HESLB ktk maombi ya mkopo. Ila usisahau kuwa B.A. Education ndio choice yako ya kwanza.
 
Finder boy,
Kwanza hongera
Pili nakushauri hivi...
Tafuta cheti cha kifo cha mzee haraka iwezekanavyo ili umbatanishe na form za mkopo
sehemu ya mdhamini muweke mama kwenye fomu za mkopo,
Kingine omba bachelor ambayo ina priority ya mkopo,
mathalan unaweza kuchagua education mkopo utapata na ajira yake ipo wazi ...kama kweli una shida usijisikie vibaya kumbiwa unasoma education!...be consistent and stay focus on your goals!
Amesema anataka kufundisha? Kwa ushauri huu haina haja kwa Serikali kuunda tume kujua sababu ya kwanini walimu hawatoshi shuleni hata baada ya kuongeza vyuo vikuuu vinavyotoa Education Course.
 
Back
Top Bottom