Sina wa kumlaumu, niilijipoteza mwenyewe- CHID BENZ

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Sina wa kumlaumu, niilijipoteza mwenyewe, Kwa sehemu kubwa Jamii hainitazami tena kwa jicho la Usaidizi, Jamii inanitazama kama Mlevi au Teja, Lakini pengine Mimi ni Mfano hai unaoweza kutumika kusaidia kizazi kingine kinachoteketea kimya kimya.
1750261012220.jpg

Nilikuwa Msanii Pekee wa Hip Hop niliyekuwa Hot kiasi kwamba nikashirikishwa mpaka kwenye nyimbo za Boling na Taarab, kumbuka FM Academia na Mzee Yusuph!…haikuwa ajabu Mimi kufanya Show India Jukwaa moja na P Square, Haikuwa ajabu Katika Fiesta Concert tour Mimi kuwa na Msafara wangu Binafsi wa Magari wakati wasanii wengine wote wakiwa kwenye Isuzu journey na Costa.
1750260937151.jpg

Hayo yote ninayozungumza si kwa Lengo la kujisifu la hasha!...watu watasema mengi lakini naumia kuona nipo hivi leo..naumia kwa Ulevi niliouingia, ulevi ambao mara kadhaa nimejaribu kuuacha. Ulevi huu ni Pingu, leo King Kong Mwili Jumba nimebaki na Mwili huu? niseme tu wazi sisi kama wasanii hujaribu vilevi vingi hasa pale tunapokuwa Hot na fedha inaingia.
1750260966248.jpg

Kumbuka wasanii muda wote ni watu wa safari na show, wengi tunashindwa kuji-manage na Starehe, pamoja na maisha yanayotuzunguka hutulevya, maisha ya vilevi na wapambe.
1750260983398.jpg

Mimi nimewahi kulipiwa Mamilioni na watu mbalimbali kwa upendo tu ili kupata Rahabilitation kutoka katika kifungo hiki lakini nikabaki kwenye ulevi ule ule. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2015 siku moja wakati nipo Maisha Club Basement alikuja Mtu Mmoja nisiyemjua akaniambia "Chidy hii si sawa...Chidy umekwisha, Mimi ni Mshabiki wako..Afya yako inatisha...tafadhali chukua hii namba kesho nipigie nione namna ya kukusaidia" Basi kesho yake nikampigia simu yule jamaa, alichofanya ni kunichukua na kunipeleka Sober House (Pemba) akalipa Gharama zote.
1750261012220.jpg

Sasa wakati nipo Pemba kuna pesa zangu za kazi ya Muziki ziliingia ilikuwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu Millions of Money kwa kweli ilitaka sana Moyo kwa mtu mwenye Addiction kama mimi kuvumilia kukaa Sober House while huko nje kuna Milioni zangu kadhaa.
1750260937151.jpg

Nikaondoka Rehab kwa lazima hii ilikuwa sawa na mgonjwa anatoroka Dozi hospitali nikarudi Jijini Dar es Salaam nikakutana na Mamilioni yangu, Washkaji, Vileo na Wapambe nikaanza bata nikarejea kwenye ulevi wa vilevi vyote kikiwemo kile kikuu kinachoniangamiza home sikukaa, nilikaa hotel nikatumia kiasi cha fedha nilipeleka kwenye Ujenzi ambao haukufika mbali.
1750260966248.jpg

Leo nazungumza hapa zimekwisha zote maisha haya sio sifa bali ni utumwa, utumwa ambao sishauri mtu mwingine kujaribu kujiingiza, Brother hata wewe usije ukajaribu kamwe, huu ni utumwa mkuu kuliko Minyororo ya Mjerumani.
1750260983398.jpg

Mimi ni Muhanga mmoja hadharani lakini kuna maelfu wako Gizani. Nyinyi mmepata Fursa ya kuniona Mimi Chidy kwa sababu nilikuwa maarufu na mwenye impact ktk sanaa na Jamii. Je vipi kuhusu wale wasijulikana, wasio maarufu na wanahitaji Msaada?
1750261012220.jpg

Narudia, kipo kizazi kinachoendelea kuteketea kimya kimya bila Awareness yeyote, na lipo daraja linalonufaika na hali hiyo'- Chidy Benz (Katika Mahojiano na Saint Pio).

Credit: Pio Pius
 
BADO ANA NAFASI JAMAA ANAJUA NA KICHWA KINA AKILI , ATULIZE FUVU YATAPITA
 
Sina wa kumlaumu, niilijipoteza mwenyewe, Kwa sehemu kubwa Jamii hainitazami tena kwa jicho la Usaidizi, Jamii inanitazama kama Mlevi au Teja, Lakini pengine Mimi ni Mfano hai unaoweza kutumika kusaidia kizazi kingine kinachoteketea kimya kimya.
View attachment 3375012
Nilikuwa Msanii Pekee wa Hip Hop niliyekuwa Hot kiasi kwamba nikashirikishwa mpaka kwenye nyimbo za Boling na Taarab, kumbuka FM Academia na Mzee Yusuph!…haikuwa ajabu Mimi kufanya Show India Jukwaa moja na P Square, Haikuwa ajabu Katika Fiesta Concert tour Mimi kuwa na Msafara wangu Binafsi wa Magari wakati wasanii wengine wote wakiwa kwenye Isuzu journey na Costa.
View attachment 3375015
Hayo yote ninayozungumza si kwa Lengo la kujisifu la hasha!...watu watasema mengi lakini naumia kuona nipo hivi leo..naumia kwa Ulevi niliouingia, ulevi ambao mara kadhaa nimejaribu kuuacha. Ulevi huu ni Pingu, leo King Kong Mwili Jumba nimebaki na Mwili huu? niseme tu wazi sisi kama wasanii hujaribu vilevi vingi hasa pale tunapokuwa Hot na fedha inaingia.
View attachment 3375014
Kumbuka wasanii muda wote ni watu wa safari na show, wengi tunashindwa kuji-manage na Starehe, pamoja na maisha yanayotuzunguka hutulevya, maisha ya vilevi na wapambe.
View attachment 3375013
Mimi nimewahi kulipiwa Mamilioni na watu mbalimbali kwa upendo tu ili kupata Rahabilitation kutoka katika kifungo hiki lakini nikabaki kwenye ulevi ule ule. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2015 siku moja wakati nipo Maisha Club Basement alikuja Mtu Mmoja nisiyemjua akaniambia "Chidy hii si sawa...Chidy umekwisha, Mimi ni Mshabiki wako..Afya yako inatisha...tafadhali chukua hii namba kesho nipigie nione namna ya kukusaidia" Basi kesho yake nikampigia simu yule jamaa, alichofanya ni kunichukua na kunipeleka Sober House (Pemba) akalipa Gharama zote.
View attachment 3375012
Sasa wakati nipo Pemba kuna pesa zangu za kazi ya Muziki ziliingia ilikuwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu Millions of Money kwa kweli ilitaka sana Moyo kwa mtu mwenye Addiction kama mimi kuvumilia kukaa Sober House while huko nje kuna Milioni zangu kadhaa.
View attachment 3375015
Nikaondoka Rehab kwa lazima hii ilikuwa sawa na mgonjwa anatoroka Dozi hospitali nikarudi Jijini Dar es Salaam nikakutana na Mamilioni yangu, Washkaji, Vileo na Wapambe nikaanza bata nikarejea kwenye ulevi wa vilevi vyote kikiwemo kile kikuu kinachoniangamiza home sikukaa, nilikaa hotel nikatumia kiasi cha fedha nilipeleka kwenye Ujenzi ambao haukufika mbali.
View attachment 3375014
Leo nazungumza hapa zimekwisha zote maisha haya sio sifa bali ni utumwa, utumwa ambao sishauri mtu mwingine kujaribu kujiingiza, Brother hata wewe usije ukajaribu kamwe, huu ni utumwa mkuu kuliko Minyororo ya Mjerumani.
View attachment 3375013
Mimi ni Muhanga mmoja hadharani lakini kuna maelfu wako Gizani. Nyinyi mmepata Fursa ya kuniona Mimi Chidy kwa sababu nilikuwa maarufu na mwenye impact ktk sanaa na Jamii. Je vipi kuhusu wale wasijulikana, wasio maarufu na wanahitaji Msaada?
View attachment 3375012
Narudia, kipo kizazi kinachoendelea kuteketea kimya kimya bila Awareness yeyote, na lipo daraja linalonufaika na hali hiyo'- Chidy Benz (Katika Mahojiano na Saint Pio).

Credit: Pio Pius
Wakati anaingiza pesa, wakati anaheat kwenye media na nyimbo zake zinawin anakuwa sawa na Kada wa ccm aliyeteuliwa humwambii kitu. Hafikiri kesho.

Ni sawa na demu mzuri akiwa na miaka 23 mweupe mwenye tako. Prado na Benz zinamgombania. Huwezi kumshauri kuhusu Ukimwi akakuelewa.

Mpaka baadaeee!! Akianza kuharisha. A kutapika, mwili hauna hamu ya kula wala kunywa na vidonda visivyopona mdomoni.

Sisi hatuna cha kumshauri tunamwangalia tu na kusema Pole sana Chid Benz
 
Back
Top Bottom