Sindano ya chanjo begani yamtoa jipu mtoto.

Sindano ya chanjo begani yamtoa jipu mtoto.

mpita-njia

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2010
Posts
1,734
Reaction score
1,616
Habari wataalam, mwanangu ana miezi mi 3, alichomwa sindano begani akiwa hajafikisha mwezi.

Siku zinavyozidi kwenda ndo kinundu kinaongezeka pale alipochomwa sindano. Na kumeanza kuwa kama jipu na unjano wa usaha unaonekana.

Je hii ni kawaida au kuna tatizo?
Mtoto wangu wa kwanza hali hiyo haikumtokea.
 
Pole sana Mkuu.

Nendeni Hospital haraka lakini pia hizo
sindano kwa watoto wengine huwatoa
majipu ni vzr kuwaona wataalam ambao
pia wataona hali halisi ya mtoto.
 
Pole sana Mkuu.

Nendeni Hospital haraka lakini pia hizo
sindano kwa watoto wengine huwatoa
majipu ni vzr kuwaona wataalam ambao
pia wataona hali halisi ya mtoto.

Thanks
Itabidi J3 nimpeleke clinic alipochomwa.
 
mimi wa kwangu kwa sasa ana miezi sita na hiyo hali ilimkuta nilikuwa kila nikipagusa panakuwa pagumu sana.nilifikiri ni kawaida.ndipo siku moja mama mtoto akaniambia panatoa usaha kama ule wa jipu,,,nlichofanya niliukamua na ulikuwa mwingi sana. Mpaka sasa yupo shwari sema pana kaugumu flani lakini syo kama ule wa mwanzo. Mm nlifanya hivyo ila kama una muda nenda hospital..
 
Hiyo hali mara nyingi inawakuta watoto...hata wangu wa kiume ilimtokea hali kama hiyo ila kilikuja kuisha chenyewe. ....ni vizuri ukampeleka hosp ili ujiridhishe maana mtoto haongei
 
Nashukuru sana waungwana kwa ushauri. Hofu imepungua
 
Jipu limepasuka lenyewe usaha mwingi umetoka, nikakamua kidogo hadi damu ikaanza kutoka.
Kesho still Clinic.
 
Mkuu hiki sio kitu kigeni, huwa kinawatokea watoto, ingawa sio wote. Cha muhimu mpeleke Hospital!
 
Jipu limepasuka lenyewe usaha mwingi umetoka, nikakamua kidogo hadi damu ikaanza kutoka.
Kesho still Clinic.

mpita-njia hii huwatokea watoto wengi mi mama alinambia ndo inavyokuwa baada ya kumwona mtoto wa jirani akiwa hivyo siku nimeenda kliniki nikasikia nesi anawaambia hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, Nadhani inawezakuwa aliyemchoma sindano alimchoma sehemu mbaya au alirudia eneo 1. Ilikuwa sindano ya chanjo gani?.
 
Mkuu, Nadhani inawezakuwa aliyemchoma sindano alimchoma sehemu mbaya au alirudia eneo 1. Ilikuwa sindano ya chanjo gani?.

Huwa ni BCG ya kifua kikuu wengi huita ndui na kama haijaacha kovu baada ya miezi mitatu inarudiwa
 
Mambo hayo ya kumdunga mtoto sindano ya kifua kikuu akiwa na miezi 3 ndiyo huwa siyapendi kabisa. Hivi ndui ni lazima eti?
Huwa ni BCG ya kifua kikuu wengi huita ndui na kama haijaacha kovu baada ya miezi mitatu inarudiwa
 
Back
Top Bottom