[FONT=times
new roman] Waheshimiwa wana JF Nimeleta taarifa hii ambayo
chanzo chake ni WAPO FM inayosema kwamba hapo jana mnamo majira ya saa
kumi jioni maeneo ya Kinondoni Mkwajuni Bondeni kulitokea mauaji. Tukio
hilo linasema chanzo ni mzozo uliojitokeza kati ya jamaa mmoja mwenye
asili ya Asia (Singasinga) ambapo wakati wakiwa katika vyombo vyao vya
usafiri Singasinga akiwa kwenye pikipiki na mtu mwingine ambaye sasa
hivi ni marehemu akiwa katika gari aina ya Toyota Carina.
Inasemakana singasinga huyu alitaka kulipita gari lililokuwa
limeharibika mbele yake na kwa bahati mbaya akaanguka barabarani na
katika harakati za kumkwepa huyo jamaa ambaye ni marehemu akabamiza gari
lake kwenye kingo za barabara na kupasuka gurudumu. Alimwendea ili
kumdai amlipe kwa kusababisha ajali ile hususani gurudumu kupasuka.
Singasinga yule aliinuka akiwa na chupa ya kilevi aina ya wine akiwa
anakunywa, ubishi ulipokolea alichomoa bastola yake na kumpiga kichwani
yule mwenye Carina na kupanda pikipiki yake na kutoweka. Wananchi
walioshuhudia tukio hilo kwa bahati mbaya hawakuweza kuchukua namba za
pikipiki ile.
Kupitia JF nikiamini ni mtandao mkubwa ningeomba tujitahidi
kutafuta taarifa na mwenye usahihi wa namba au kumfahamu huyo Singasinga
atoe vyote hapa JF na bila shaka makachero wa polisi ambao ni wanachama
wa JF watashughulikia.
Nawasilisha.
Asanteni.
[/FONT]