KERO Singida: Baadhi ya mitaa gari la taka halipiti kwa wakati, wiki ya 3 uchafu umezagaa mitaani

KERO Singida: Baadhi ya mitaa gari la taka halipiti kwa wakati, wiki ya 3 uchafu umezagaa mitaani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari.

Kuna kero moja Manispaa ya Singida, kumekuwa na tabia ya uchelewaji wa kuchukua taka katika baadhi ya maeneo hasa Ginery.

Wananchi wanatoa taka nje siku ya kubeba hawaji kuchukua. Hii ni wiki ya tatu taka zimezagaa kwenye mitaa tu.

Na ni tatizo limeanza toka mwezi wa 12 Mwaka jana (2024). Huko mitaani taka zinatupwa ovyo sababu watu wameshajaza vifaa vyao vya kuwekea taka.

1000615811.jpg

Hii picha chinii ni karibu na Chuo cha Uhasibu barabara ya kwenda Ginery.
WhatsApp Image 2025-02-10 at 12.43.54_e238e8f9.jpg



Pia soma ~ Hatimaye gari la taka lapita kukusanya takataka mitaa ya Singida
 
Back
Top Bottom