Singida Big Stars tumecheza mechi ya kirafiki na Arusha City FC

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Jioni ya leo tulicheza mechi ya kirafiki na klabu ya Arusha City FC ya hapa hapa jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mazoezi yetu katika kipindi hiki ambacho bado tupo kambini tukijiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu.

Mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2

Ulikuwa mchezo mzuri sana wa kirafiki. Benchi letu la Ufundi leo llijikita zaidi kuangalia uwezo wa kikosi na muunganiko wa wachezaji wetu, haukuwa mchezo wa ushindani kusaka matokeo ndio sababu tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia makusudi.

Jumapili tutacheza na Mbuni FC kuendelea kutazama maendeleo ya kikosi chetu.

IMG_0745.JPG
IMG_0772.JPG
IMG_0785.JPG

Taarifa na iwafikie!
 
Attachments

  • IMG_0789.JPG
    IMG_0789.JPG
    628.7 KB · Views: 7
  • IMG_0806.JPG
    IMG_0806.JPG
    663.9 KB · Views: 6
  • IMG_0814.JPG
    IMG_0814.JPG
    467.7 KB · Views: 6
Hizo mbili hakuna wafungaji? Toa taarifa kamili boss
 
Mke naomba kazi ya kuosha viatu vya tambwe mpachika magoli
 
mimi najitolea nitakuwa nikiangalia mechi zenu halafu nashauri PM tu pale penye ubovu kwa jicho la mshabiki. mimi najua mengi ya mpira nikiifuatilia timu. Wachezaji wenu waige Yanga slogan kila mechi ni fainali kuanzia mechi ya kwanza hadi mwisho.

Siku mkicheza na Simba, Yanga au Azam msikubali wachezaji watafute sifa ya kuonesha viwango wataiga mpira wa mpinzani, watapiga chenga nyingi zisizo na lazima , wachezaji watakaa kaa na mpira na kuzunguka zunguka ovyo na kupoteza sana mipira hiyo wanayo hasa viungo.

Mcheze nao kusaka ushindi tu mchezaji apewe mwisho sekunde 3 kukaa na mpira na wasijifanye wanamiliki sana na kupoteza muda mwingi kutandaza soka upande wao badala ya kupeleka mpira mbele kushambulia.
 
Asante sana mkuu Zuga. Tutafurahi kupokea tathmini zako baada ya mechi.
 
Ushauri wangu;
Anzisha special thread kwa ajili ya Singida big star.
Hii itakusaidia kuwa na mapendekezo, ushauri na updates katika page moja.

Hii itakupa mtiririko mzuri wa watu kufuatilia timu yenu pia wewe utakuwa unafanya reference kirahisi sana
 
Ushauri mzuri. Asante sana. Nitaangalia namna ya kuufanyia kazi.
 
Hao mbuni muwaangalie sana wana faulo za hovyo sana hao
 
Back
Top Bottom