Singida Black Stars yasema imemlipa Mwenda Tsh. 140m yamtaka aripoti mazoezini

Singida Black Stars yasema imemlipa Mwenda Tsh. 140m yamtaka aripoti mazoezini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinsta.app_457496365_18039965720009355_6572213316159394366_n_1080.jpg

Snapinsta.app_458064769_18039965723009355_8936854412246807283_n_1080.jpg

Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars unapenda kuwajulisha wadau na mashabiki wetu kuwa tumeona taarifa zinazosambaa kuhusu maslahi ya mchezaji wetu Israel Patrick Mwenda tuliyemsajili msimu huu 2024/2025 kwa Ada ya TZS 200m.

Makubaliano ya mkataba yaliweka kiasi cha pesa kinachotakiwa kulipwa kabla ya mchezaji kusaini ni TZS 140m ambacho klabu ilimlipa kama mkataba ulivyotaka, kiasi kingine kilichobaki TZS 60m kinatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili.

Huu ni utaratibu wetu kama Klabu na wapo wachezaji wengine waliopewa malipo ya utangulizi kabla ya kusaini na malipo mengine wanaendelea kupokea wakiwa wanaendelea na Ligi.

Kuna wachezaji wamepokea malipo ya awali 20%, wengine 40% wengine 50%. Israel Mwenda amepokea 140m kama kiambatisho kinavyoonesha na anadai 60m. Yeye amechagua kusubiri mpaka alipwe kwanza ndio ajiunge na timu tofauti na wenzake ambao wanalipwa huku wakiwa kazini kama ilivyo kwenye vilabu vingi hapa nchini.

Klabu itaendelea kufanyia kazi maslahi yake kwa mujibu wa makubaliano kwa kumalizia sehemu ya ada yake ya uhamisho iliyobaki ambayo inatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili wake na mchezaji kujiunga rasmi na timu yetu.

Uongozi wa klabu unamtaka mchezaji kuripoti kambini haraka kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayoendelea kwa kuwa mahitaji yaliyobaki hayakuwa takwa la mkataba kuwa alipwe kwanza ndio aungane na timu kambini.

Soma Pia: Israel Mwenda arudisha pesa zote Simba SC na kusepa klabuni hapo
 
Kukopwa ndio tatizo.Kungekuwa na uweledi kungekuwa hamna tatizo.Timu nyingi zimeripotiwa FIFA kwa usanii huu wa kukopa na kulipa kwa installment halafu kukaushia baadaye mchezaji akianza kucheza.
 
Bongo uswahili mwingi hamna nidhamu, ndiyo maana soka letu halipigi hatua kwa nmna inavyotakiwa
Huyo dogo nae ana ujinga mwingi, huko Simba alichukua hela, harafu anaomba aachwe, akakaziwa arudishe hela. Haya mambo ya kizamani haya.
 
Duh! Kwenda 200M ? Ebana mpira uheshimiwe,ukalipa ile mbaya
 
huyo anaakisi akili za wachezaji wengi. kuwakilishwa hawataki wanaona ubahili. wachezaji hujakaa nao asilimia 90 ni majingamajinga kichwani
Na hata sheria zenyewe zina mapungufu, sijasikia hata siku moja mchezaji anayekiuka mkataba anaadhibiwa tofauti na timu.
 
Kwa hiyo wametuletea sisi kesi?

Si wa mwandikie barua yeye na akigoma wamfikishe kamati ya katiba na sheria TFF?
 
Nyie wajinga kweli mlivyokua mnakubaliana mlitushirikisha Sasa hivi mmeona mmepigwa 140m na mchezaji hajawasili ndio mnaleta hapa si mlikua mnafanya Siri na hili fanyeni Siri
 
Back
Top Bottom