Singida: Halmashauri ya Mkalama yafafanua madai ya baadhi ya Maafisa Utumishi na Mkurugenzi kuchelewesha vibali vya Uhamisho

Singida: Halmashauri ya Mkalama yafafanua madai ya baadhi ya Maafisa Utumishi na Mkurugenzi kuchelewesha vibali vya Uhamisho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuandika Baadhi ya Maafisa Utumishi na Mkurugenzi wanashikilia vibali vya Uhamisho vinavyotoka kwa Katibu Mkuu Utumishi au TAMISEMI Halmashauri imetoa ufafanuzi kuhusu hoja hiyo...

WhatsApp Image 2025-06-11 at 16.18.57_e4a9b371.jpg

TAARIFA KWA UMMA​

YAH: UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU INAYOSAMBAA MTANDAONI KUHUSU SUALA LA UHAMISHO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kufuatia taarifa potofu zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uendeshaji wa mchakato wa uhamisho wa watumishi katika Halmashauri ya Mkalama kwa ufafanuzi ufuatao:-

1. UENDESHAJI WA MCHAKATO WA UHAMISHO.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inatekeleza mchakato wa uhamisho wa watumishi kwa mujibu wa taratibu na kanuni za utumishi wa umma, kupitia mfumo rasmi wa maombi ya uhamisho (Employee Self Service ESS). Hakuna mtumishi yeyote mwenye sifa ambaye ameomba uhamisho kupitia mfumo huu na kunyimwa haki yake kwa misingi isiyo ya haki.

2. KUHUSU WATUMISHI WANAOHAMA KUFUATA WENZA WAO.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara ya mwisho imepokea barua mwezi Mei, 2025 za watumishi walio omba kuhama kwa ajili ya kuungana na wenza wao. Barua zote za Watumishi waliokidhi vigezo zimepitishwa na wahusika wamekabidhiwa kwa ajili ya utekelezaji.

3. WITO KWA WATUMUSHI WENGINE.
Tunawakumbusha na kuwasihi watumishi wote wenye nia ya kuhama kuhakikisha w anazingatia taratibu zilizowekwa, na kuwasilisha maombi yao kwa kutumia mfumo wa ESS. Uwazi na uwajibikaji ni nguzo kuu katika utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA.
 
Kuna Halmashauri wakurugenzi wanazingua. Yaani mkuu wa Idara kashapitisha maombi ya mtumishi kuhama lakini yakifika kwa mkurugenzi yanastuck
 
Sijawaelewa kwa hiyo kuna baadhi vibali vya uhamisho wa watumishi vimetolewa na utumishi or tamisemi ila wahusika hawajapatiwa kutokana hawajakidhi vigezo?
Wangetakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu hao ambao hawajakidhi vigezo kwamba imekuaje utumishi au tamisemi watoe vibali vya kuhama kwa watumishi wasio na vigezo vya kuhama.
Na hivyo vigezo ni vipi?
Kwa hiyo barua inaonyesha kwenye hiyo halashauri kuna tatizo
 
Back
Top Bottom