Pre GE2025 Singida: Jesca Kishoa atumia wanafunzi kupitisha ajenda zake kugombea Ubunge

Pre GE2025 Singida: Jesca Kishoa atumia wanafunzi kupitisha ajenda zake kugombea Ubunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mgolobyo, Kijiji cha Mgolobyo Kata ya Miganga mkoani Singida wameelezea Furaha yao mara baada ya kupokea Taulo za kike ( Pads) kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa Wa Singida Mhe. Jesca Kishoa na kusaidia kuepukana na gharama za kununua taulo hizo za kike.

Wanafunzi hao wamemuomba Mbunge huyo kurudi tena Bungeni kutokana na namna ambavyo anajitolea kwa jamii.

Mhe kishoa alitoa taulo hizo za kike katika mkutano alioufanya February 16,2025 Katika kata ya Nkalakala ikiwa na lengo kuwasalimia na kutatua kero za wananchi.


Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pia soma
 
Amefanya kosa?
Amevunja sheria zipi za Tanzania?
 
Hilo jimbo mbunge wake wa sasa ni nani? au ndio Mwigulu Nchemba?
 
Ni upuuzi kugawa pads kana kwamba ni tatizo kubwa kwa wanawake wakati ni hali yao ya kimaumbile si lazima wanaume wajue kitu hicho ni aibu. Angegawa madaftari na kalamu ingetosha kuliko kugawa vitu vya siri kwa wasichana
 
Unawadhalilosha mabinti . Hizo Huwa zinatolewa kimya kimya bila camera za vyombo vya habari. Yeye mwenyewe akienda dukani kununua akikuta wanaume wamejazana anazuga mpaka waondoke. Vitoto ndio anavibebesha mbele ya camera?
 
Back
Top Bottom