Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Na Fundi madirisha,
Nawasalimu sana ndugu zangu wananchi wa jimbo la Singida Magharibi. Mwafanga naa! Amuchii!
Kwa ufupi ndugu zangu wa jimbo la Singida Magharibi hasa wapiga kura za maoni nataka niwadokezee kidogo, mna mtu mmoja mpambanaji na ni mtu wa kazi sana anaitwa HAMISI LISSU MAHANJU, huyu ni msomi wa chuo kikuu mwenye mipango yenye mafanikio makubwa katika taifa hili.
Huyu bwana ni mtia nia jimbo lenu la Singida Magharibi, huyu mtu namtazama kwa jicho la mbali anataka kulisaidia taifa hili na wananchi kwa ujumla kama mwakilihi wao. Huyu kwa maoni yangu ni mtu sahihi pengine kuliko watangulizi waliowahi kua wabunge katika jimbo hilo. Hiki kichwa ni balaa, nina kifahamu tangu tukiwa sekondari, Chuo cha Ualimu Mkwawa, JKT, UDSM na mpaka kwenye majukumu akiwa baraza la mitihani, mkaguzi mkuu wa shule kanda na Afisa Elimu wa mikoa ya Mara na Dar es Salaam, hakika kila alikopita aliacha alama kubwa sana. Ninyi Watani zangu hamlijui hili nisikilizeni mimi ambaye namjua kwa undani na hata yeye hanijui mimi kama ninavyomfahamu ingawa tumekua wote kwenye majukumu ya kujenga nchi.
Nataka niwaambie Watani zangu, mnaweza kuhisi ninapigia mtu kampeni lakini mimi natoa ya moyoni mwangu baada ya kusikia huyu bwana anagombea ubunge katika jimbo hilo, nimesisimkwa nikatamani angependa kugombea mkoani kwetu Mara maana huko pia aliacha alama akiwa kama Afisa Elimu wa mkoa kwa kuutoa kutoka kufanya vibaya hadi kua mkoa bora kielimu kitaifa kabla hajahamishiwa kuokoa jahazi Dar es Salaam.
Huyu bwana yawezekana hata hanijumbuki kwakua nilikua chini ya idara zake alizopitia lakini mimi ninamfahamu vizuri sana ndio maana nikaamua kutumia fursa hii kuwaeleza Watani zangu msiachie LULU hii. Sina sababu ya kumpigia kampeni ispokua natamani sana awawakilishe awasaidie kwa sababu ya uwezo wake mkubwa sana kiakili na kiuongozi.
Ninawatakia kila lakheri katika chaguzi zenu za kura za maoni lakini nina imani mmenielewa Watani zangu.Mungu awabariki sana.
Fundi Madirisha,
madirishafundi@gmail.com