LGE2024 Singida: Mwigulu apanga foleni kupiga kura. Maigizo yanaendelea

LGE2024 Singida: Mwigulu apanga foleni kupiga kura. Maigizo yanaendelea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

1732704527186.png

Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), leo Novemba 27, 2024, ameungana na wananchi wa jimbo lake katika zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Dkt. Nchemba amepiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, aliwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi ya Kikatiba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.

"Uchaguzi huu ni wa haki na demokrasia. Tumeshuhudia zoezi likiendeshwa kwa uhuru kabisa. Naomba wananchi wote ambao bado hawajapiga kura wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo, kwani ni haki yao ya msingi," alisema Dkt. Nchemba.

Aliongeza kuwa uchaguzi ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleo na uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.

"Nimetimiza wajibu wangu wa kupiga kura, na niwaombe wananchi kote nchini kufanya hivyo kwa maslahi makubwa ya Taifa letu," alisisitiza.

Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo la upigaji kura.
 
Wakuu,

View attachment 3163211

Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), leo Novemba 27, 2024, ameungana na wananchi wa jimbo lake katika zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.​

Dkt. Nchemba amepiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.​

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, aliwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi ya Kikatiba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.​

"Uchaguzi huu ni wa haki na demokrasia. Tumeshuhudia zoezi likiendeshwa kwa uhuru kabisa. Naomba wananchi wote ambao bado hawajapiga kura wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo, kwani ni haki yao ya msingi," alisema Dkt. Nchemba.​

Aliongeza kuwa uchaguzi ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleo na uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.​

"Nimetimiza wajibu wangu wa kupiga kura, na niwaombe wananchi kote nchini kufanya hivyo kwa maslahi makubwa ya Taifa letu," alisisitiza.​

Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo la upigaji kura.​

Dduuuu basi sawaaa....kumbe wadunguaji huwa wameoa ???
 
Back
Top Bottom