Singida Out, iwe fundisho siku nyingine

Kolo Unaweweseka sana! Ungejikita zaidi kwenye kushauri makolo wenzio. Kuhusu maamuzi ya refa, ni taira pekee ndiye anaweza kukubaliana na ujinga ule.
Mleta mada asichojua ni kwamba kupoteza muda kwenye futbol ni advantage pia kwa timu inayoongoza.
 
kipa aliudakia nje
 
"kipa kaenda kudakia mpira nje then anarudi ndani, alitakiwa kuuacha. KONA NI HALALI NA GOLI NI HALALI"

Yaani unakubali kabisa kipa kadakia mpira nje. Sijui unapinga nini sasa?!

Ushabiki wa bila kutumia akili mimi niliukataa mapema sana iwe kwa timu yangu Yanga au Simba ukweli utabaki kuwa ukweli tu.
 

Angebaki nje
 
Kipa hafundishwi kuacha mpira uano elekea golini kwake hata awe anajua umetoka au ni offside sababu unaweza achaia muamuzi aka amua vingine ndio maana hua unaona makipa hata mpira unao toka nje lazima ajiridhishe

Angalia vema mstar
 
Refa awe ameongeza dakika au hajaongeza simalumu bali nawalaumu Singida kwa ujinga waliofanya. Singida walishawakamata Simba kila kona na walikuwa wanaongoza goli moja. Huku Simba wakiwa wamepaniki wamepoteana kabisa na benchi lao la ufundi limechanganyikiwa. Singida badala ya kutulia na kufunga goli mbili za haraka haraka na uwezo huo walikuwa nao wa kuimaliza mechi wakaanza ujinga wa kujilinda na kupoteza muda wakati dakika bado nyingi. Wajifunze siku nyingine kumaliza mechi kama zile kikatili mapema sana. Nina hakika Singida angekuwa anaoongoza goli tatu hata refa angeongeza dakika 20 bado Simba wasingerudisha.
 
Kipa mwenye akili timamu hawezi hangaika kwenda kudaka mpira ambao umetoka wakati yeye ndie mwenye advantage anaongoza goli na dakika zimeisha....

Ningependa kujua kwa nini kipa alienda kudaka mpira nje?
Alitaka aonyeshe sifa kuwa anajua kudaka
Mwisho wa picha ikala kwake na ikumbukwe mpira ni mchezo wa kimakosa,
Ukikosea unaadhibiwa hata kama maumivu ya adhabu atasikia nduguyo
Inakuwa imeisha hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…