LGE2024 Singida: Polisi wanamsaka Katibu Mwenezi CCM kwa kumjeruhi Katibu wa CHADEMA kwa kisu

LGE2024 Singida: Polisi wanamsaka Katibu Mwenezi CCM kwa kumjeruhi Katibu wa CHADEMA kwa kisu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Huu uchaguzi ni balaa!

======

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamtafuta Joseph Shila, Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Mitunduruni, Wilaya ya Singida kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kisu kwenye bega la kushoto Hamisi Nkua, (52) Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Singida.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Tukio hilo linadaiwa kutokea Novemba 27,2024 majira ya saa 8:00 mchana katika eneo la uwanja wa maonesho Mandewa baada ya kutokea mzozo baina ya wanachama wa CCM na CHADEMA. Majeruhi alipata matibabu hospitali na kuruhusiwa.

Imetolewa na;
Amon D. Kakwale - SACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida.

1732724775999.png

Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
 
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linamtafuta Joseph Shila, Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Mitunduruni, Wilaya ya Singida kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kisu kwenye bega la kushoto Hamisi Nkua, (52) Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Singida.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Novemba 27,2024 majira ya saa 8:00 mchana katika eneo la uwanja wa maonesho Mandewa baada ya kutokea mzozo baina ya wanachama wa CCM na CHADEMA. Majeruhi alipata matibabu hospitali na kuruhusiwa.

Imetolewa na;
Amon D. Kakwale - SACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida.

1732726057319.jpeg
 
Huyo hawezi kumpata asilani
 
Back
Top Bottom