KERO Singida: Wakazi wa Sabasaba Singida Hatuna maji wiki ya pili sasa

KERO Singida: Wakazi wa Sabasaba Singida Hatuna maji wiki ya pili sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Habarini wanajukwaa...
Takribani wiki ya pili sasa Tarura walikuja kutifua barabara kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizopo eneo la Sabasaba Manispaa ya Singida.

Kama wananchi hatupingani na shughuli za maendeleo zinazoletwa na Serikali ya mkoa shida ni kwamba wazee wa kazi walivyokuja kutufua barabara hawakutoa taarifa kuwa watakata na mabomba.

Tangu shughuli iyo.ifanyoke Septemba 19 2024 hawajarudi tena wala hatujui nini kinaendela. Kinachotutesa na kutuumiza ni kukosa maji kwa takriban wiki mbili sasa kwakuwa mabomba yote yamekatwa kwa jina la 'natengenezo ya barabara '

Tunaomba Mamlaka husika zitusaidie tupate huduma hii muhimu.
Snapchat-79028772.jpg
Snapchat-384665891.jpg
Snapchat-2099445782.jpg
Pia soma ~ Mamlaka ya Maji Singida (SUWASA) mnatuumiza sana Wananchi, bili mnazoleta haziendani na uhalisia
 
Back
Top Bottom