KERO Singida: Wakazi wa Unyakumi tunateseka na ubovu wa barabara. Ahadi zimekuwa nyingi bila utekelezaji

KERO Singida: Wakazi wa Unyakumi tunateseka na ubovu wa barabara. Ahadi zimekuwa nyingi bila utekelezaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Bado Hujasema

Member
Joined
Dec 1, 2024
Posts
12
Reaction score
14
Wakazi wa Mtaa wa Ginery maeneo ya Singida Sekondari tunaomba tusaidiwe barabara. Hali ni mbaya sana hasa msimu huu wa mvua. Watoto wanaenda shule kwa tabu maji na matope ya kutosha.

Wanakwenda na School bus zinaishia mbali kwasababu ya ubovu wa barabara. Ahadi zimekuwa nyingi bila utekelezaji.

Mbunge wetu Mussa Sima tunaomba kabla hujamaliza Ubunge tutengenezee barabara angalau ipitike kidogo.


20250130_070336.jpg
20250130_070154.jpg
20250130_070306.jpg

Pia soma ~ Singida: Barabara ya Unyakumi yaanza kurekebishwa baada ya malalamiko kuwa inawatesa watumiaji
 
Sima yupi wa kukusaidia?hapo hatuna mbunge,Yeye na CCM take hamna kitu,Singida barabara nyingi ni mbovu ukianzia hio inayokwenda kwa mkuu wa Mkoa,Veta,Sababsaba,Uwanja wa Ndege nk,Kifupi Singida inahitaji mabadiliko makubwa sana
 
Aibu ni barabara ya kwenda uwanja wa ndege, anzia kanisa la kkkt na chuo cha utumishi haina lami ni mashimo matupu. Fikiria rais ashuke na ndege uwanjani ataendaje ikulu wakati barabara ni mbovu kiasi hicho? Watasema wanatengeneza barabara ya unyankhae kwa lami, na hiyo ni baada ya kupigiwa kelele ndio wakajititimua kujenga. Kuna barabara ya karakana mpaka unyamikumbi ni kero tupu kwa wananchi, muda wa mbunge unaisha haijulikani atakuja mbunge gani mwenye maono mapya kujenga barabara ndani ya mji wa singida na viunga vyake
 
Back
Top Bottom