Wakazi wa Mtaa wa Ginery maeneo ya Singida Sekondari tunaomba tusaidiwe barabara. Hali ni mbaya sana hasa msimu huu wa mvua. Watoto wanaenda shule kwa tabu maji na matope ya kutosha.
Wanakwenda na School bus zinaishia mbali kwasababu ya ubovu wa barabara. Ahadi zimekuwa nyingi bila utekelezaji.
Sima yupi wa kukusaidia?hapo hatuna mbunge,Yeye na CCM take hamna kitu,Singida barabara nyingi ni mbovu ukianzia hio inayokwenda kwa mkuu wa Mkoa,Veta,Sababsaba,Uwanja wa Ndege nk,Kifupi Singida inahitaji mabadiliko makubwa sana
Aibu ni barabara ya kwenda uwanja wa ndege, anzia kanisa la kkkt na chuo cha utumishi haina lami ni mashimo matupu. Fikiria rais ashuke na ndege uwanjani ataendaje ikulu wakati barabara ni mbovu kiasi hicho? Watasema wanatengeneza barabara ya unyankhae kwa lami, na hiyo ni baada ya kupigiwa kelele ndio wakajititimua kujenga. Kuna barabara ya karakana mpaka unyamikumbi ni kero tupu kwa wananchi, muda wa mbunge unaisha haijulikani atakuja mbunge gani mwenye maono mapya kujenga barabara ndani ya mji wa singida na viunga vyake