Singida: Watu 14 wafariki na watatu kujeruhiwa ajali ya Lori na hiace

Singida: Watu 14 wafariki na watatu kujeruhiwa ajali ya Lori na hiace

Emmanuel Robinson

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
1,856
Reaction score
1,793
Haya maisha haya tuendelee kumuomba Mungu anatulinda sana hapa nimetoka kushuhudia ajali mbaya hapa Singida, Hiace na semi trailler. Hiace hautamani kuitazama mara mbili. Yaani polisi ndiyo wanawapanga barabarani mimi nimeshuhudia miili sita dah huzuni maisha ya watu🙆🏿‍♂️😭😭😭. Mimi napita tu basi so msiniombe picha.

======
Singida.jpg

Ajali ya Lori aina ya Scania na Hiace imeacha watu 14 wakifariki dunia na watatu majeruhi. Ajali hiyo imetokea Kijiji cha Mkiwa wilaya ya Ikungi majira ya saa 9:30 Alasiri.

Dereva wa Hiace alitaka kulipita 'overtake' gari la mbele yake bila mafanikio na kukumbana na lori uso kwa uso.

Majeruhi watatu wanatibiwa hospitali ya wilaya ya Manyoni.
 
Duh...Mwisho Wa mwaka huu!!

Pole kwa ndugu na majamaa
 
Haya maisha haya tuendelee kumuomba Mungu anatulinda sana hapa nimetoka kushuhudia ajali mbaya hapa singida Hiace na semi trailler. Hiace hautamani kuitazama mara mbili. Yaani polisi ndiyo wanawapanga bararani mimi nimeshuhudia miili sita dah huzuni maisha ya watu🙆🏿‍♂️😭😭😭. Mimi napita tu basi so msiniombe picha
HAKUNA AJALI NZURI, kwahiyo huu msemo AJALI MBAYA UONDOENI.
Bora umefanya hivyo kutoweka picha,
 
Haya maisha haya tuendelee kumuomba Mungu anatulinda sana hapa nimetoka kushuhudia ajali mbaya hapa singida Hiace na semi trailler. Hiace hautamani kuitazama mara mbili. Yaani polisi ndiyo wanawapanga bararani mimi nimeshuhudia miili sita dah huzuni maisha ya watu🙆🏿‍♂️😭😭😭. Mimi napita tu basi so msiniombe picha
Mungu awatangulie….
 
Saw mkuu kwa habari, marehemu wapumzike pepa peponi.
 
Dah mwisho wa mwaka huu😥😥
Mungu awape imani, uvumilivu na utulivu wafiwa
Pole kwa majeruhi
Marehemu walale salama
 
Back
Top Bottom