Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ndiyo maana nikamuuliza ametembea nchi ngapi na kuona maisha gani tofauti tofauti?Usilazimishe fikra zako kwa wengine.
Njoo Japan au Korea Kusini. Kuna wanaume na wanawake wengi tu ambao hawataki kuoa au kuolewa.
Serikali inataka watu wazae zaidi na kuwapa kila aina ya misamaha ya kodi lakini wao wamekomaa na single life.
Hapa mwanamke ana elimu yake, ana kazi ya maana, ana mchumba, gari na nyumba yake. Huyu amekamilika kuliko yule anayeolewa kwa ajili ya sababu za kiuchumi.
Wanataka kufanya kazi na kustarehe tu. Harusi siyo muhimu kabisa kwake.
Ukienda nchi za magharibi kama Sweden au Uholanzi utawakuta watu wengi tu wanaishi pamoja na kuzaa lakini hawajaona.
Hiyo mikaratasi ya ndoa ni utamaduni tu. Kwako hajakamilika kama hajaoa/ hajaolewa, kwake maisha yanakwenda kwa raha kama kawaida.
Usifananishe utamaduni wako na jamii nyingine. Tofauti ya elimu, jamii na uchumi inahusika sana na maamuzi yao ya kuishi bila ndoa.
Siyo anakariri habari za kijijini kwao na kufikiri dunia nzima iko hivyo.