Single LADIES and LADS. . .

Single LADIES and LADS. . .

Most of us have long given up even just the idea. The main issue is compatibility. If you can stand your partner's good and bad things, learn to forgive, respect each other and share at least 4 out of 10 common goals, then yes, you have a perfect r/ship. Then again it would be so boring not to have those arguments to fight over,coz believe me they make you know your partner even better. They also brings something new in a person and to the r/ship as well. Perfect r/ship.....I guess it all depends on your defination!
 
Mi sipo kwenye position ya kuchagua ila wakati nachagua nilizingatia hivi vigezo

1. Awe na mvuto umbo la wastani natural

2.Awe na good manners (sio umempakia kwenye gari anafunguo kioo anatupa barabarani maganda ya bazoka au chupa ya uhai) au analiona dust bin analiacha anatupa taka barabarani (akifanya hivyo tena kama first date bye bye)

3. Awe civilized ,Kwenye public asipende kuongea kwa nguvu kama ni wawili tunaongea basi aweke sauti chini (Sio unapokea simu kama unagombana, umekaa restaurant hadi meza ya kumi wanakusikia wewe, better aende kipembeni akaongee na simu yake, kama kwenye daladala ndio kabisa kama vipi asiipokee) (wapo walioshindwa huu mtihani nikawapiga chini) huwa sipendi unecessary attention.

4. Aweze ku mingle na watu wa aina tofauti

Hayo mambo ma 4 nilizingatia kuliko mengine kwakuwa yalikuwa yananipa taswira huyu mtu wa namna gani na nilifanikiwa :tongue:
 
Lizzy haya mbambo ya ndio au hapana kwenye ukoa au kuolewa mimi sipo kabisa, hebu mimi niambie hadithi ya zawadi imefikia wapi

Hahahaha mbona unanibania Ram?
Zawadi yupo kiasi, ngoja nikikamilisha sehemu inayofuata ntakushtua.
 
kumkabidhi mtu maisha yako yaliyobaki hapa duniani mara mda wa kufanya hivyo unapofika si jambo dogo.....kuna mambo mengi ya kuangalia....kwanza kwa mimi mwanaume lazima nijue je hili ni chaguo sahihi?..ameamua kwa dhati? au ameona wenzake wameingia huko nae akaingia? au ameshinikizwa? au umri umempita sasa ameona anaweza asiolewe ndo akaamua kuja na kunichagua mimi?

mawazao yake ni yapi? lazima awe na mawazo channya mwenye kujua kujenga hoja na kudadisi..lazima ajiamini, lazima apende kila mtu pasipo ubaguzi....


Lizzy, unajua mwili mmoja hauji kwa kusimama mbele ya padri/mchungaji au shehe.. mtumishi wa Mungu anapotamka ninyi ni mwili mmoja ule mwili huwa hauji mara moja pale...kuufikia mwili mmoja ni safari ndefu sana inayoanzia kwenye uchumba na hukamilishwa miaka mingi sana mkiwa ndani ya ndoa...

siku hizi kuna yale mahusiano yanaitwa ''cyber marriage'' ..we lizzy uko uko uliko na mimi niko huku niliko....mahusiano yotu yameunganishwa na mawasiano ya simu,internet,bbm,skype nk......hata tukikutana tunakutana kwa siku 1 au 2 then narudi baada ya mda tunaenda ndugu zangu wanakuja huko kwenu tunatoa mahali then sasa ndo tunaanza kuishi...hakika hapo tunaweza kuishi lakini kwa shida sana na inaweza kutuchukua mda mrefu kuwekana sawa..na ndio maana wengi hawaishi kulalamika na hatimae ndoa kuvunjika....hii idara ya ndoa ni pasua kichwa sana...ntarudi

Asante Ed kwa kutukumbusha mambo ya msingi kabisa. Nakuombea umpate wakuzeeka nae. . . .
 
Swala la vigezo huwa hakunaga, binadamu wote wapo spontaneous unaweza kukuta sista du anasema ,"mimi mwanaume mmfupi sipendi hata kusikia" kesho ukamkuta amefunga ndoa na emolo.

Wapo watu wanaojua wanachotaka na ndicho wanachotafuta mpaka kupata, na wapo watu wasiojua wanachotaka wenyewe wanabadili mawazo kuendana na wakati bila kusahau tamaa na faida binafsi.
 
Jamani mi nashindwa kusema kitu maana mi nilishaoa miaka 7 iliyopita
Ndoa inaendeleaje?

Ndiyo mamii, nina mpango wa kuolewa. Nina imani kubwa kuwa na familia ni jambo jema, hivyo inshallah Mola anijalie nipate mwenza yakinifu.

Kwakweli muda mwingine unaweza kuwa na vigezo usikutane navyo vyote ila si haba kuna vitakavyonivutia niweze funga pingu. Awe anajali kwao na kwetu, mpenda maendeleo, mcheshi, muwazi, mcha mungu(hata kama siyo mlokole) na kushirikishana mambo yote muhimu.

Ndoa inadumu kukiweko na upendo, heshima na uvumilivu..kuwasiliana kuwe msingi bora ili kuhakikisha tunaambiana yote muhimu mazuri na mabaya, kumpa kipaumbele mwenza yani nafasi ya mume/mke, kuwa marafiki zaidi tu ya mume/mke. Mume wangu atakuwa ni namba moja maana ndiye nitakae jenga nae familia na panapo majaliwa tuzeeke wote na kuzikana.

Miaka 30-39. Elimu iwepo na kazi awe nayo pia! maisha kusaidiana!

Ntakualika, tuombeane kheri Lizzy!

Asante BJ. . . vigezo naona vimetulia.

Hahahahaha. . . . Ntakuombea mpenzi niambulie pilau la sherehe na wewe mume wa ukweli.
 
Ahsante Mkasika!!

Maubdumula hongera sana kwa kufanikiwa, mzeeke pamoja Mungu akiwajalia uhai.
 
Una mpango wa kuoa/kuolewa?

Kama jibu ni HAPANA . . kwanini?
Kama ni NDIO. . . je ni VIGEZO gani ambavyo vikifikiwa na mkaka/mdada utashawishika/penda kuingia ndoani?
Na ni MASHARTI (usichukulie neno masharti kwa uzito wake, namaanisha vitu ambavyo ni muhimu kuzingatiwa) gani ambayo yakizingatiwa unaamini ndoa yako itadumu?

kwa ujinga gani nlionao mpaka nolewe?????????????
 
Una mpango wa kuoa/kuolewa?

Kama jibu ni HAPANA . . kwanini?
Kama ni NDIO. . . je ni VIGEZO gani ambavyo vikifikiwa na mkaka/mdada utashawishika/penda kuingia ndoani?
Na ni MASHARTI (usichukulie neno masharti kwa uzito wake, namaanisha vitu ambavyo ni muhimu kuzingatiwa) gani ambayo yakizingatiwa unaamini ndoa yako itadumu?

...ni kujitwisha kabati la matatizo.
...:A S-coffee:
 
Back
Top Bottom