Mfalme_wa_Nyika
JF-Expert Member
- May 24, 2023
- 683
- 1,581
Jamani....
Leo napenda kuinama kwa heshima mbele ya wanawake hawa mashujaa — wamama wanaosimama peke yao katika jukumu zito la kulea, kufundisha, kulinda, na kupenda watoto wao kwa hali na mali, licha ya changamoto, upweke au hukumu za jamii...ambao jamii ya wahuni fulani fulani tu wanawaita "Single Mothers"
Single mother si jina la udhaifu naomba muelewe hovyo jamani, bali ni cheo cha heshima, ushupavu na kujitoa kupita mipaka....
Moyo wako Single Mother umebeba kazi ya watu wawili, huku ukitabasamu kama mama na kulinda kama simba.....
Kila siku unaamka mapema, unahakikisha watoto wanakula, wanavaa, wanapata elimu, hata kama roho yako imechoka...
Umejifunza kutotegemea makofi wala sifa, bali kutegemea neema ya Mungu na nguvu ya maombi yako ya kimya usiku....Oh Single Mother! Mungu aendelee kukuweka juu daima!
Mara nyingine, jamii hukunyoshea vidole, wengine huongea bila kujua vita unavyopigana ndani ya nyumba yako, lakini bado unasimama....
Mvua ikinyesha unakuwa paa, jua likichoma unakuwa kivuli. Wakati mwingine huna cha kula, lakini mtoto hapati shida. Hicho ni kiwango cha upendo kisichopimika kwa pesa wala sifa...