Single Parenthood


Experienced and wise. Me likey likey
 
Kwangu mimi haijalishi ni kijana au la, kama swala la divorce limelazimika ntatulia kulea watoto wangu mpaka hapo watakapokuwa na kujitemea, mwili kunisumbua ni rahisi kuuhudumia bila kuathiri ufahamu wa watoto kuliko kuwaletea Baba/Mama ambaye hatawajali kama ni sehemu ya maisha yake na hivyo kuwaharibia kila kitu ktk maisha yao.
 


Thanks Mama Tuli kwa ku-share nasi japo kidogo na pole sana kwa situation nzima
 
Wacha kusema ndoa za siku hizi mbona sisi tumeoa na hatuna matatizo, mnao waza mambo ya kuwachana kwanini mlioa??

Hivi mtu anaoa kwa sababu gani??

Sijawahi kusikia ndoa zikafananishwa na ujio wa Yesu, naona wewe unataka kukufuru sasa :cool2:
temea mate chini Fazaa, una muda gani kwenye ndoa yako?
 
Asha,hapo kwenye red naomba nikuulize,hivi kwanini wazungu wanasainishana 'prenuptial' na kwa nini wanawake wa kiswahili wanajenga majumba bila waume zao kujua (na ni wengi hawa)? naomba jibu ndo niendelee.....
 
come on mamaT,stop here and relax,ka vipi hama kwenye hii thread,i can see your tears!
 
Easily said than done my dear Lizzy, i have been through the entire mchakato kuoa,kuzaa,divorce,remarry, kuzaa ,divorce and eventually u single father. Nashukuru Mungu wanangu nimeweza kuwa pull through (mdogo yuko secondary,wakubwa wamemaliza college). Lizzy,God willing siku moja nitakupa full tamthilia ya hekaya za Bishanga!
 
 

Bishanga thanks for your contributions,could you please PM me one day so that we can share more of your experiences and how you went through with those traumas of divorcing and remarrying.
 
Bishanga kumbe hata wewe ni muathirika wa hii kitu?
Pole aise, ila mimi nilijifunza mambo mengi sana baada ya kudivorce, jamii ilininyooshea kidole na kuona kwamba nimeshindwa kuilinda ndoa yangu, nilionekana mimi ni mkosefu na kweli from my heart hiki kitu kiliniumiza sana sana sana, sana tu lakini nawaambieni jamani acheni Mungu aitwe Mungu, ukimtegemea na kumwamini katika maisha hakuna kitakachoharibika. Tuliachana mtoto alikuwa pre-unit nw yuko std 4, bado naamini Mungu atanifanikisha nimfikishe pale ninapotamani afikie kielimu


 

Pole sana ram,keep going nothing will stop you unless you decide to be stopped
 
Reactions: ram
Asha,hapo kwenye red naomba nikuulize,hivi kwanini wazungu wanasainishana 'prenuptial' na kwa nini wanawake wa kiswahili wanajenga majumba bila waume zao kujua (na ni wengi hawa)? naomba jibu ndo niendelee.....

Hio Prenuptial agreement ni kuweka mazingira ya kuhakikisha kua mali ya mmoja wa spouse (hasa mwenye pesa nyingi) inabaki kua ni place in cases of emergency... Hio ya wanawake kujenga nyumba, I believe ni more of a safety net pale ambapo mume anakua ana ku mistreat na una hakika na future yako hapo.
 
Haaaa haaaa, nomba nicheke kwanza ndo niendelee kusoma, eti ujio wa yesu haaa haaa, my dear kama una watoto wako,kaa kwanza vuta muda kidogo laa sivyo kama ulitoka kwenyemahusiano au ndoa ngumu, ukikimbilia ndoa tena, kuangukia pua kwa mara nyingine tena hua ni rahisi zadi.

Hakuna raha kama kuishi mwenyewe na watoto au mtoto wako, mradi uwe na uwezo tu wa kuwatunza, Japo kweli wanahitaji malezi ya wazazi wawili, lakini kama imetokea bahati mbaya, basi wakati ukimuomba mweyezi Mungu akupatie anaekufaa bila hofu yeyote, Kama ukiwa ni mwanaume jitahidi kuwapa malezi bora watoto na kuhakikisha unafukiafukia matuta ya vitu alivyofanya mama yao kama mapenzi kuyazidisha.

Hali kadharika hata mama, unahitaji kufanya yale yote na zaidi alokua akiyafanya babayao, kama elim wapatiwe, wapate muda wa kucheza maadili mema tena ya ki Mungu, zawadi za hapa na pale bila kuwadekeza na kuwafanya wajinga hilo ndo la muhim. Zaidi ya hapo Mumea au Mke hutoka kwa Mungu.
 

Ram, Mungu wetu ni mwaminifu sana, tena walokua wakikunyooshea vidole, watafute sasa hivi kama wengine bado wako kwenye hizo ndoa. Cha muhim ni kumshukuru Mungu tu kwa makuu anayokutendea, kwani pengine hata kazidi kukufungulia milango. Mungu ni mwema sana.
 

Thanx Mamushka,am humbled t5o share these with you.Thanks again
 

Kweli umeongea mwaya.
 
Asha,hapo kwenye red naomba nikuulize,hivi kwanini wazungu wanasainishana 'prenuptial' na kwa nini wanawake wa kiswahili wanajenga majumba bila waume zao kujua (na ni wengi hawa)? naomba jibu ndo niendelee.....

AshaDii, watu hua hawaachani bila kutafuta suluhu hata siku moja. Naomba ufikiri kidogo , mfano umetafuta suluhu kwa muda wa zaidi ya mika mpaka suluhu zote mkazimaliza, kama ni washauri, viongozi wa dini, wazazi, mkaamua mambo yenu muwe mnayamaliza wenyewe bado tu yasiishe, mkaachana na kupeana muda kidogo, mkarudiana bado kitu kiko palepale, kinachofuatia hapo itakua ni nini? nadhani jibu pekee ni kwamba tulipendana sana lakini ndoa imeshindikana. Huo hua ni uamuzi mgumu kuliko chochote nikama kujilipua tu lakini ukishaamua maisha hua yanaenda tena kwa amani sana, kuliko maisha ya kulia kila siku kwa jina la ndoa NO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…