MwafrikaHalisi
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 1,741
- 511
Ahsante MammaMia. . .
Nimefurahi kua umegusia swala la mama wa kambo. Binafsi pale ambapo mama anaweza(kimatendo-hali na mali, kifikra,matakwa) kuwalea watoto ambao ni chini ya angalau miaka 8 basi waachwe kwa mama. Yani pamoja na kwamba mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kwamba bado wapo wanawake wenye mioyo ya kibinaadamu linapokuja swala la mama wa kambo, bado siko tayari kumwachia mwanamke mwingine ambae sio ndugu wala rafiki yangu ninaemwamini anilelee mtoto ambae hawezi kushtaki wala kujitetea pale anapoonewa.
Ila inapotokea mwanamke anakua hana mapenzi na wanae basi baba awe karibu sana na watoto kuhakikisha kwamba mwenzi wake mpya au hata dada wa kazi hafanyi zaidi ya anavyotegemea yeye.
Experienced and wise. Me likey likey