Singularity microfinance

Joined
Mar 27, 2024
Posts
42
Reaction score
179
Wakuu..Hawa jamaa wa mkopo fasta wananidai balaa...kwa namna wanavonidai ningekuwa na hela ningewapa nimalizane nao waache kunitumia jumbe za vitisho na simu,..imefikia wakati wanataka kuwatumia ujumbe watu wangu wote wa kwenye phenebook yangu..walinipa 15000 saivi wananidai 21000.

Nimejaribu kiwaelekeze wanipe muda nipambane niwarudishie hela ...aisee jamaa Sio waelewa kabisa..kwa Hali nilionayo nimeamua waache tu wafanye wanachofanya Ila Bado nimepigika hela yao sijajipata na walinipatia siku nane tu.

Ulishawahi kukopa?je ulikabiliana nao vipi wakati unahali ngumu?
 
Hao ni pesa X. Unaogopa watu wasijue ulikopa 15000/
Kama huna kausha ukipata uwape Mie walitishia wee mwisho WA siku nlivopata nikawapa Ila baada ya kuacha kunidai na kunitumia msg za vitisho.
 
nakushauri ukipata wee walipe tu mana walisemaga dawa ya deni kulipa kama unaona kero kudaiwa.. vinginevyo utaishi kama digidigi.
 
bro dawa ya deni kulipa

pambana lipa hela ya watu
 
Thread + avatar vinachekesha

Lipa hela ya watu, acha kutia huruma mjomba.
 
Kuna mwenzako wanemfungulia group WhatsApp wameadd watu wake wa kazini na familia kama kumuumbua hivi, kama unaweza kulipa walipe tu mkuu, ntakuongezea hiyo 1,000 tafuta 20,000 ulipeπŸ™†β€β™‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…