Sintah alikwama sana kwa Juma Nature

Sintah alikwama sana kwa Juma Nature

Juma Kassim Kiroboto ( Juma Nature) Mtoto wa Kurasini Kijiji Cha Wavuvi alikuwa Na Usela Mwingi Sana Na ndio maana waliotajirika kwa Jina Lake Ni wengi Sana

Yule Binti alikuwa anapenda kudanga Na Watu Maarufu Na ndio sababu miongoni mwa Fimbo alizokula zilikuwa Za Kijana huyo Mla ndumu

Enzi hizo Bongo record ya PFunky ilikuwa Kama Sebule ya TMK
Kabisa
 
Miaka ya 2000 huko ilizuka ghafla couple ya nguvu iliyobustiwa na magazeti ya udaku. Nature na Sintah..

Okei. Mapenzi huota kokote lakini hii combo mpaka leo siisomi ilikaaje kaaje.

Sintah alikuwa mtoto wa mjini. Mdangaji kwa lugha ya kisasa ambaye alibahatika kupata exposure mapema ya ujanja ujanja wa hapa na pale. Ilifikia hatua akawa anaitwa Jennifer Lopez 'JLo' wa Bongo. Very classic!

Nature yeye alikuwa supastaa kutoka uswahilini huko Temeke. Jina kubwa kuliko uwezo. Uwezo wa kutengeneza maisha na kuishi kinyota. Kibongobongo alipeta lakini hakuwa mjanja. Well, alikuwa mjanja wa kishamba.

Ni kudanga? Labda. Zile story za kwenye Inaniuma sana na Sitaki demu zinaweza kuchora picha halisi ya jamaa alivyokuwa anatumika bila kujua maana drama za mahusiano yao zilikuwa dili kwa magazeti. Enzi hizo Sintah ndio queen wa maskendo hakauiki magazetini kabla hajaja kurithiwa na Wema Sepetu.

Swali la mshangao: Kama Sintah alikuwa akicheza league za vigogo wakiwemo akina Cool J, Dkt. Machache na the co., Meddy MP na ma-don wengine wa enzi hizo, kwa Kiroboto alikwama wapi?

Ustaa? Alikuwa nao.
Pesa? Ipi.
Mapenzi? Asingemfanyia masinema.

Pisi ilikwama sana. Muda umeongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuliwahi kumfuata kiroboto kumpa dili la kuzunguka na sisi mikoa ya kusini kuelimisha umma maswala ya afya-Nikiwa nafanya kazi na NGO ya masuala ya Afya. Sasa kwenye bei meneja anataja bei za ajabu (500 milioni) kwa matamasha mawili tu bei utadhani tunamualika 50 cent. Tukampiga chini kumfuata Inspekta Harun nae anazingua. Ndo nilipoelewa kuwa waswahili aisee si mchezo
 
Tuliwahi kumfuata kiroboto kumpa dili la kuzunguka na sisi mikoa ya kusini kuelimisha umma maswala ya afya-Nikiwa nafanya kazi na NGO ya masuala ya Afya. Sasa kwenye bei meneja anataja bei za ajabu (500 milioni) kwa matamasha mawili tu bei utadhani tunamualika 50 cent. Tukampiga chini kumfuata Inspekta Harun nae anazingua. Ndo nilipoelewa kuwa waswahili aisee si mchezo
Labda ilikuwa ni namna ya kukataa kwa sababu walikuwa over booked?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati alienda kutangaza Radio Clouds Mwanza,pale jengo la CCM round about...akiwa na mtangazaji wa Clouds ya Mwanza ambapo kuanzia saa 9 wanajiunga na Clouds Mwanza na Dsm hawasikiki,huyu jamaa wa Mwanza jina limenitoka kidogo.

Alipofika Mwanza,kuna bwanamdogo mshamba tu alikuwa anaitwa Jose Masamaki akambeba Sinta,enzi hizo anamiliki mitumbwi na samaki inakufa sana ziwani.Alikuwa anakula bata pale Deluxe Hotel barabara ya Uhuru karibu na Salma Corn.Pale Delux ilikuwa kijiwe cha wahuni wa kutoka Migodini Geita na vijana wa Samaki Mwanza.

Kulikuwa kuna Malaya wanajiuza toka Rwanda ila wanajidai ni Wanyambo wa Karagwe...Kuna jamaa yangu tumeenda Mwanza akalala hapo Deluxe na mtoto wa Kigali,asubuhi akakuta hata suti aliyotundika ukutani kuvaa kaa ajili ya semina imetunguliwa.
Alikuwa anaitwa ALBERT G SENGO
 
Uligoma kunywa...
Ulikuwa unashangaa ukatili gani wa kupora drip za maji ya wagonjwa Muhimbili tunaenda kunywa mitaani?

Hatuna huruma!!
Nilikuwa na ufahamu wa IV fluids?
Halafu Muhimbili siijui...wa mikoani tunapata tabu sana.
 
In Other way ilikua ni Tusu kubwa sana kwa Kibla Juma Kaasim Nature Kiroboto labda ile album Bora ya Muda wote "ugali" isinge fanya Vyema kiasi kile. Mungu ana njia zake za kumpa mtu umatemate.
 
PILI nae akashia kumletea kisosi tu ajisugue ila qibla huyu
 
Back
Top Bottom